Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (03)

    Mkeka Wa Leo Jumamosi 07/02/2026 | Mechi Za Over 1.5 Pekee

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (02)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (03)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (03)

    Hamza NgondoBy Hamza NgondoFebruary 7, 2026Updated:February 7, 2026No Comments10 Mins Read970 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia

    “Saida, si unaona? Yule siyo Kichaa na ukitaka kuamini jiulize kwanini  alienda kituo Cha Polisi?” aliniuliza Veronica akiwa amenishika bega, mara  alisimama yule Kichaa Kisha aligeuza shingo kutazama tulipokua 

    tumesimama. Nikamvuta Veronica tukajificha nyuma ya gari Moja lililokua  limepaki nje ya kituo Cha Polisi 

    Tukawa tunamchungulia, alitazama sana pale tulipokua tumesimama,  Kisha aliondoka zake akipitia upande mwingine ambao ulikua na geti la  kutokea, sisi tulikua upande wa geti la kuingilia pale kituo Cha Polisi. 

    “Mama yangu!” Nilisema huku nikishika Sehemu ulipo moyo Wangu,  nilikua nimeishiwa nguvu sababu ya Mshituko. Veronica akanyanyua  kichwa kumtazama akamwona akiondoka…  Hukusoma SEHEMU YA KWANZA Na  SEHEMU YA PILI? Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI  Kisha Endelea

    SEHEMU YA TATU 

    “Twende” alisema Veronica, Mimi nilikua naogopa lakini alinishika mkono  tukatembea kuelekea zilipo ngazi za kupandisha kuelekea mapokezi.  Palikua na Polisi kadhaa waliokua wamekaa kando, wengine wakiwa ndani  ya Kituo. Tulipitiliza Hadi eneo la mapokezi, Veronica akawa jasiri wa  kueleza kilichotuleta tena akaongezea kua Mtu aliyetupa vitisho ni Kichaa  aliyetoka muda sio mrefu. 

    “Unamaanisha aliyetoka sasa hivi?” 

    “Ndiyo aliyelekea upande ule wa kutokea” alisema Veronica. Yule Polisi  akacheka kidogo Kisha akamjibu. 

    “Mbona yule ni Mkuu wa kituo Cha Polisi hapa, Ina maana hujaziona zile  Sare?”  

    “Sare?” 

    “Ndiyo. Hebu njoo” alisema yule Polisi wa Kiume, akamshika mkono  Veronica. Nami nilifuata kwa nyuma, tukashusha ngazi Kisha tukasimama  karibu na geti la kutokea. 

    “Si mnamsema yule?” alimwonesha kidole yule Kichaa, alikua amesimama  kando ya gari ndogo nyeusi, nikalikumbuka lile gari lilikua ni lile lililokuja  kazini na kunipatia Karatasi kua Nina deni. 

    “Ndiyo, sasa yule ni Askari? Macho Yako yanaona vizuri? Yule ni Kichaa  huoni alivyovaa?” aliuliza Veronica, kiukweli tulipoangalia tena tulimwona  Askari mmoja Mtu mzima mwenye kitambi akiongea na simu.  

    Ilikua kama Mchezo wa kuigiza, yaani dakika hiyo hiyo Mtu yule alibadilika  na kua askari. Tulikaa kimya kwa Mshangao, kwa maana hiyo hata  tulichoenda kushitaki kilikua hakina maana tena. 

    “Si mmeona? Mko sawa kweli?” aliuliuliza huku akitutazama mmoja Hadi  mwingine, alikua askari mstaarabu anayezungumza Kizanzibari. Ilibidi  niitoe kwenye pochi ile karatasi ya vitisho niliyopewa ili nimpe yule askari, 

    nilipoitoa niliona pamechorwa mchoro wa kopa uliomaanisha Upendo,  sikutaka tena kumpa yule askari badala yake nikamshika mkono Veronica  tukaondoka pale kituoni haraka haraka kwa kutumia geti la kuingilia. 

    Tulitembea haraka haraka sana kama vile tulikua tumefukuzwa pale kituo  Cha Polisi, tulipofika nje ya Uzio tuliangalia huku na kule Kisha tulivuka  barabara. Tukatembea haraka haraka kurudi Kazini huku Kila mmoja  akiwa kimya mwenye uwoga sana.  

    Jua lilikua linawaka kwa kiasi chake japo wingu zito lilikua linakuja na  kutoweka, tulipofika kazini tulisimama nje ya Ofisi. Kila mmoja akipumua  kwa uzito wa aina yake kama vile tulikuwa tumeshaikimbia ile hatari. 

    Nilimtazama Veronica nikamuuliza tufanye kitu gani ikiwa kwenda Polisi  kumeleta MAUZAUZA Yale? Akanitazama Kisha akaniambia 

    “Hapa nilipo naogopa sana Saida, unajua siyo jambo la kawaida Hili eeh?”  alisema akiwa anaonekana Koo yake kukauka mate kutokana na hofu  aliyonayo. Macho yalikua yamenitoka pima, Kila mara nilikua nikiangalia  huku na kule 

    “Tufanye nini sasa Jamani?” niliuliza huku nikiwa nakaribia kulia. Macho  yangu yalikua mepesi sana kutoa mchozi hasa ukizingatia aina hii ya  Maisha niliponea chupu chupu kule Rukwa 

    “Kuna Mtu ulimkosea huko nyuma Saida?” aliniuliza Veronica. Kiukweli  sikutaka kumsimulia chochote kuhusu Maisha yangu ya nyuma, sikutaka  ajuwe chochote kile. Nikatikisa kichwa changu kumkatalia japo nilikua  nasema Uwongo lakini ni Bora ibaki kua Siri yangu. 

    Mara Meneja alituona tukiwa tunaongea akaja moja kwa moja na kutuuliza  kama tulifanikiwa tulichoenda kufanya kule Polisi. Tulitazamana kwa  kutegeana, hakuna ambaye alikua tayari kusema kwa Meneja, nikajikuta  nikiropoka 

    “Ndiyo, Kila kitu kimeenda sawa” nilisema huku macho yangu  yakimtazama Veronica kuona kama alikua akiniunga mkono, naye akasema 

    “Dunia imeharibika sana Meneja, kwenda Polisi lilikua chaguo Bora zaidi”  alisema kwa sauti ya Uwongo, nilipepesa kope zangu kwa hofu huku  nikisubiria neno kutoka kwa Meneja.  

    “Basi sawa kama ni hivyo, nawaruhusu kwa Leo murudi nyumbani, kesho  Mje kazini mapema” alisema Kisha aliondoka, sote tulishusha pumzi nzito  kwa maana haikua kazi rahisi kusema Uwongo mbele ya Meneja. 

    Veronica aliendelea kusisitiza kua tunapaswa kuujua mzizi wa jambo lile,  tuliagana Kila mmoja alichukua vitu vyake na kurudi anapoishi. Nilitembea  taratibu sana Hadi nafika nyumbani, kwanza nilisimama mbele ya nyumba  yetu nikifikiria namna ya kuingia ndani peke yangu. 

    Japo ilikua mchana lakini nilikua naogopa sana, niliamua kukaa kwanza  nje huku nikifikiria ile Kauli ya yule Kichaa kua watakuja kunichukua  kwasababu Nina deni kwao, moyo ulinienda mbio sana. Nikatoa kitambaa  changu na kujifuta jasho huku nikifikiria nifanye kitu gani. 

    “Nani ana deni na Mimi?” nijiuliza ndani ya nafsi yangu, nilianza kuamini  kua Hilo deni Ndiyo sababu ya mauza uza yote, nikarudisha kumbu kumbu  zangu nyuma ili kuona kama nilikua nadaiwa na yoyote yule, kumbukumbu  zangu hazikunipa majibu niliyoyataka. 

    Nilikaa pale nje Hadi jioni ilipoingia, wazo la kuingia ndani nililikwepa  sana sababu nilikua naogopa mno. Ule wasiwasi wa zamani ulikua  umenirudia tena, nilikaa kwa muda mrefu Hadi Mama mmoja jirani  alipokuja kuniuliza ni kwanini nimekaa hapo nje kwa muda mrefu badala  ya kuingia ndani? 

    Ilikua ni kawaida kwa majirani kuniangalia mara kwa mara sababu ya  mambo yaliyotokea kwenye Maisha yangu, ukizingatia nilikua naishi peke  yangu halafu jirani huyu alikua rafiki mkubwa wa Marehemu Mama yangu. 

    “Kuna Mtu namsuburia Hapa Mama Amida” nilijibu huku nikimtazama  usoni yule Mama, akaguna tu Kisha akaniambia 

    “Haya, Mimi nipo ndani” alisema Kisha aliingia nyumbani kwake,  nikatazama huku na kule nikaona ni Bora niondoke pale nyumbani,  nikaitazama tena nyumba yetu Kisha nikazunguka Upenyoni halafu  nikaondoka bila hata kufungua mlango. 

    Nikampigia simu Veronica kumuuliza kama alikua amefika salama,  akaniambia alikua amefika salama pia amemsimulia Mama yake  kilichotokea. Nikashtuka kidogo halafu nikataka kujua Mama yake alitoa  ushauri gani, akaniambia kua Mama yake amemshauri twende kwa Mganga 

    Moyo ulishtuka sana, nikahisi mwili ukisisimka. Nikamuuliza tena  akaniambia Mama yake amemshauri twende kwa Mganga, sikua na ajizi  nilikubali japo kwa shingo Upande, Veronica akaniambia kua kesho yake  twende kwa Mganga, tuombe ruhusa kazini. 

    Basi tukakubaliana twende kwa Mganga. Nilijikuta nikitembea tembea  mitaa ya Magomeni Hadi Giza lilipoingia, nikakaa Sehemu nikala chakula 

    lakini sikutaka kurudi nyumbani kulala peke yangu, niliendelea kuzunguka  zunguka huku nikihisi maumivu ya miguu 

    Nilipochoka nikatafuta Sehemu nikakaa huku nikiangalia pirika pirika za  Watu zilivyokua zikimalizikia. Muda ulikua unakimbia kuliko kawaida,  nikatafuta Sehemu nyingine ambayo Bado Watu walikua kwa wingi,  nikaenda kituo Cha daladala nikakaa hapo Hadi mishale ya Saa sita Usiku,  Watu walianza kupungua huku hofu ikizidi kuniingia. 

    Kila nilipofikiria kwenda niliona Watu walikua wakimalizikia, hatimaye  nikajikuta peke yangu nikitembea mtaani huku mgongoni nikiwa na Begi  langu dogo. Nikapata wazo la kuelekea Magomeni mikumi, nilitembea  taratibu Hadi Magomeni mikumi. 

    Saa yangu ya Mkononi iliniambia kua ilikua ni saa 7 kasoro Usiku. Nilikua  nimechoka kimwili na kiakili, nikakaa mbele ya fremu Moja hivi. Angalau  mahali hapo palikua salama kwangu pia palikua na Baa kando yangu, basi  nilikaa hapo nikiangalia namna walevi walivyokua wakijibizana. 

    Lilikua tukio la ajabu sana Maishani, kuikimbia nyumba yetu na kuiacha  peke yake lakini sikua na jinsi. Nililikumbatia Begi langu huku baridi Kali la  Usiku likiwa linanipiga mwilini, jambo Zuri ni kwamba nilikua nimevalia  Baibui hivyo nilikua nimepunguza kidogo ukali wa Baridi. 

    Nilitamani pakuche ili niwasiliane na Veronica twende kwa Mganga kama  alivyoshauri Mama yake, nilikua nageuka huku na kule. Ilipofika mishale ya  Saa 9 kasoro, pale Baa lilikuja gari Moja nyeusi, kutokana na lile Giza  sikuweza kulitambua vizuri lilikua gari gani. Sijui kwanini nilikua makini  sana kulitazama lakini nilijikuta nikiliangalia sana kama Mtu aliyepooza  hivi. 

    Akashuka Mwanaume mmoja aliyevalia Shati jeupe na Suruali nyeupe, hata  kiatu chake kilikua cheupe, mavazi Yale yalinifanya nianze kuogopa.  Nikamwona akimwita Mwanamke kutoka pale Baa Kisha akaongea naye  kwa sekunde kadhaa halafu kibaya zaidi aliyekua anaongea naye alionesha  kidole nilipokua nimekaa, nilishtuka nikahisi mwili Wangu kama ulikua  umepigwa shoti ya Umeme. 

    Nikajikuta nikiweka vizuri Miguu yangu huku macho yakiwa yamenitoka.  Yule Mwanaume akarudi kwenye gari, halafu yule Mwanamke akawa  anakuja nilipokua nimekaa Mimi, ilikua rahisi kugundua alikua akija  kwangu sababu alishaonesha kidole nilipo, nikaliweka Begi vizuri tayari  kwa ajili ya kukimbia.

    Yule Mwanamke wa Baa alikuja Moja kwa moja Hadi nilipo, hapo nilikua  tayari kwa ajili ya kukimbia. Moyo ulikuwa unadunda kama vile unataka  kupasuka.  

    Akasimama mbele yangu, nilikua kimya sana lakini mwenye vita kubwa ya  hofu ndani yangu, upepo ulikua ukiendelea kukoreza baridi Kali lakini  nilihisi joto Kali sana.  

    “Habari Yako?” alinisalimia yule Mwanamke, nikapata kigugumizi kumjibu. “Nzuri” 

    “Unaitwa kwenye lile gari” alisema yule Mwanamke, nilipeleka macho  kwenye lile gari Kisha nikameza funda zito la mate. 

    “Ananiita kivipi?” nilimuuliza huku nikiwa nimeshajiweka sawa kukimbia. 

    “Anasema anakudai anataka ukalipe deni” aliposema hivi nilihisi  kuchanganikiwa, nikajua ni Yale mauza uza yaliyonifanya niikimbie  nyumba yetu, nikamtazama yule Mdada Kisha nikaanza kukimbia kurudi  mitaa ya nyumbani kwetu. Wakati nakimbia lile gari likawa kinakuja kwa  nyuma upande wa Barabara kubwa inayorudi Magomeni kanisani. 

    Nilizidi kukimbia bila hata kujali kwamba nilikua nimeshadondosha viatu  vyangu, sikujali hata kama ningekanyaga Msumari lakini ningekimbia tu.  Kibaya zaidi Watu walikua wachache sana Barabarani tena wengi wao  walikua wale ambao hawana makazi 

    Nikaona kama nitakimbia usawa wa Barabara nitakamatwa kirahisi,  nikaona ni Bora niingie uchochoroni, haraka nikaingia uchochoroni. Kibaya  zaidi huko kulikua na Giza nene pia hapakua na Watu kabisa lakini ilikua  njia ya mkato kufika nyumbani. 

    Nilikimbia kama mwehu aliyesikia Kuna jalala jipya mahali, sijui hata  niliwezaje kukatiza pale kwa Kasi ile. Nilipita uchochoroni kwa Kasi sana  hata kama ningelikutana na Mtu Angekua ni mwenye kujiuliza nakimbia  nini. 

    Nilikimbia Hadi nilipotokezea eneo la Wazi ambalo lilikua na Uwanja  Mdogo wa kuchezea Mpira Watoto, hapo nikapunguza kidogo mwendo  maana nilikua tayari mtaani halafu pia nilikua karibu zaidi kufika  nyumbani maana kutoka hapo ni mtaa wa pili kufika nyumbani. 

    Mbwa walianza kubweka kwa nguvu sana, niliangaza huku na kule lakini  sikuona Mtu yoyote yule, sikuwaogopa wale mbwa isipokua niliogopa 

    kukamatwa na Mtu anayesema ananidai. Kwa hakika kabisa Mtu yule  alikua akinifwatilia Kila mahali nilipokua naenda 

    Angalau eneo Hilo lilikua na taa, nilitembea haraka haraka Hadi nilipofika  nyumbani, ila nilikua naogopa sana kuingia ndani, nikapata wazo la  kumuamsha Mama Amida nimuombe nilale nyumbani kwake Hadi  Asubuhi. 

    Niligonga mlango wake kwa nguvu huku nikimtaka anifungulie haraka,  chozi lilianza kunitoka. Nilikua nageuka huku na kule, mara haraka Mama  Amida alinifungulia, nilimsukuma nikaingia Hadi ndani Kisha  nikamwambia aufunge mlango haraka, akafanya hivyo haraka bila kujua ni  kwanini nilimtaka aufunge mlango, Kisha akanigeukia 

    “Saida, Kuna tatizo gani?” aliniuliza, chozi lilikua linanibubujika tu.  Akanishika mkono na kunipeleka chumbani kwake Kisha akaniambia nikae  kwenye kiti. 

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA NNE Sasa ( Comments ziwe nyingi) 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx  Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

    Msala Msala Kijiweni riwaya mpya Riwaya ya Goryanah Riwaya Ya Kisasi Changu Riwaya Ya Msala riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni soma riwaya bure
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Hadithi February 7, 2026

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (03)

    Ilipoishia “Saida, si unaona? Yule siyo Kichaa na ukitaka kuamini jiulize kwanini  alienda kituo Cha…

    Mkeka Wa Leo Jumamosi 07/02/2026 | Mechi Za Over 1.5 Pekee

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (02)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (01)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.