Ilipoishia
“Saida, si unaona? Yule siyo Kichaa na ukitaka kuamini jiulize kwanini alienda kituo Cha Polisi?” aliniuliza Veronica akiwa amenishika bega, mara alisimama yule Kichaa Kisha aligeuza shingo kutazama tulipokua
tumesimama. Nikamvuta Veronica tukajificha nyuma ya gari Moja lililokua limepaki nje ya kituo Cha Polisi
Tukawa tunamchungulia, alitazama sana pale tulipokua tumesimama, Kisha aliondoka zake akipitia upande mwingine ambao ulikua na geti la kutokea, sisi tulikua upande wa geti la kuingilia pale kituo Cha Polisi.
“Mama yangu!” Nilisema huku nikishika Sehemu ulipo moyo Wangu, nilikua nimeishiwa nguvu sababu ya Mshituko. Veronica akanyanyua kichwa kumtazama akamwona akiondoka… Hukusoma SEHEMU YA KWANZA Na SEHEMU YA PILI? Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI Kisha Endelea
SEHEMU YA TATU
“Twende” alisema Veronica, Mimi nilikua naogopa lakini alinishika mkono tukatembea kuelekea zilipo ngazi za kupandisha kuelekea mapokezi. Palikua na Polisi kadhaa waliokua wamekaa kando, wengine wakiwa ndani ya Kituo. Tulipitiliza Hadi eneo la mapokezi, Veronica akawa jasiri wa kueleza kilichotuleta tena akaongezea kua Mtu aliyetupa vitisho ni Kichaa aliyetoka muda sio mrefu.
“Unamaanisha aliyetoka sasa hivi?”
“Ndiyo aliyelekea upande ule wa kutokea” alisema Veronica. Yule Polisi akacheka kidogo Kisha akamjibu.
“Mbona yule ni Mkuu wa kituo Cha Polisi hapa, Ina maana hujaziona zile Sare?”
“Sare?”
“Ndiyo. Hebu njoo” alisema yule Polisi wa Kiume, akamshika mkono Veronica. Nami nilifuata kwa nyuma, tukashusha ngazi Kisha tukasimama karibu na geti la kutokea.
“Si mnamsema yule?” alimwonesha kidole yule Kichaa, alikua amesimama kando ya gari ndogo nyeusi, nikalikumbuka lile gari lilikua ni lile lililokuja kazini na kunipatia Karatasi kua Nina deni.
“Ndiyo, sasa yule ni Askari? Macho Yako yanaona vizuri? Yule ni Kichaa huoni alivyovaa?” aliuliza Veronica, kiukweli tulipoangalia tena tulimwona Askari mmoja Mtu mzima mwenye kitambi akiongea na simu.
Ilikua kama Mchezo wa kuigiza, yaani dakika hiyo hiyo Mtu yule alibadilika na kua askari. Tulikaa kimya kwa Mshangao, kwa maana hiyo hata tulichoenda kushitaki kilikua hakina maana tena.
“Si mmeona? Mko sawa kweli?” aliuliuliza huku akitutazama mmoja Hadi mwingine, alikua askari mstaarabu anayezungumza Kizanzibari. Ilibidi niitoe kwenye pochi ile karatasi ya vitisho niliyopewa ili nimpe yule askari,
nilipoitoa niliona pamechorwa mchoro wa kopa uliomaanisha Upendo, sikutaka tena kumpa yule askari badala yake nikamshika mkono Veronica tukaondoka pale kituoni haraka haraka kwa kutumia geti la kuingilia.
Tulitembea haraka haraka sana kama vile tulikua tumefukuzwa pale kituo Cha Polisi, tulipofika nje ya Uzio tuliangalia huku na kule Kisha tulivuka barabara. Tukatembea haraka haraka kurudi Kazini huku Kila mmoja akiwa kimya mwenye uwoga sana.
Jua lilikua linawaka kwa kiasi chake japo wingu zito lilikua linakuja na kutoweka, tulipofika kazini tulisimama nje ya Ofisi. Kila mmoja akipumua kwa uzito wa aina yake kama vile tulikuwa tumeshaikimbia ile hatari.
Nilimtazama Veronica nikamuuliza tufanye kitu gani ikiwa kwenda Polisi kumeleta MAUZAUZA Yale? Akanitazama Kisha akaniambia
“Hapa nilipo naogopa sana Saida, unajua siyo jambo la kawaida Hili eeh?” alisema akiwa anaonekana Koo yake kukauka mate kutokana na hofu aliyonayo. Macho yalikua yamenitoka pima, Kila mara nilikua nikiangalia huku na kule
“Tufanye nini sasa Jamani?” niliuliza huku nikiwa nakaribia kulia. Macho yangu yalikua mepesi sana kutoa mchozi hasa ukizingatia aina hii ya Maisha niliponea chupu chupu kule Rukwa
“Kuna Mtu ulimkosea huko nyuma Saida?” aliniuliza Veronica. Kiukweli sikutaka kumsimulia chochote kuhusu Maisha yangu ya nyuma, sikutaka ajuwe chochote kile. Nikatikisa kichwa changu kumkatalia japo nilikua nasema Uwongo lakini ni Bora ibaki kua Siri yangu.
Mara Meneja alituona tukiwa tunaongea akaja moja kwa moja na kutuuliza kama tulifanikiwa tulichoenda kufanya kule Polisi. Tulitazamana kwa kutegeana, hakuna ambaye alikua tayari kusema kwa Meneja, nikajikuta nikiropoka
“Ndiyo, Kila kitu kimeenda sawa” nilisema huku macho yangu yakimtazama Veronica kuona kama alikua akiniunga mkono, naye akasema
“Dunia imeharibika sana Meneja, kwenda Polisi lilikua chaguo Bora zaidi” alisema kwa sauti ya Uwongo, nilipepesa kope zangu kwa hofu huku nikisubiria neno kutoka kwa Meneja.
“Basi sawa kama ni hivyo, nawaruhusu kwa Leo murudi nyumbani, kesho Mje kazini mapema” alisema Kisha aliondoka, sote tulishusha pumzi nzito kwa maana haikua kazi rahisi kusema Uwongo mbele ya Meneja.
Veronica aliendelea kusisitiza kua tunapaswa kuujua mzizi wa jambo lile, tuliagana Kila mmoja alichukua vitu vyake na kurudi anapoishi. Nilitembea taratibu sana Hadi nafika nyumbani, kwanza nilisimama mbele ya nyumba yetu nikifikiria namna ya kuingia ndani peke yangu.
Japo ilikua mchana lakini nilikua naogopa sana, niliamua kukaa kwanza nje huku nikifikiria ile Kauli ya yule Kichaa kua watakuja kunichukua kwasababu Nina deni kwao, moyo ulinienda mbio sana. Nikatoa kitambaa changu na kujifuta jasho huku nikifikiria nifanye kitu gani.
“Nani ana deni na Mimi?” nijiuliza ndani ya nafsi yangu, nilianza kuamini kua Hilo deni Ndiyo sababu ya mauza uza yote, nikarudisha kumbu kumbu zangu nyuma ili kuona kama nilikua nadaiwa na yoyote yule, kumbukumbu zangu hazikunipa majibu niliyoyataka.
Nilikaa pale nje Hadi jioni ilipoingia, wazo la kuingia ndani nililikwepa sana sababu nilikua naogopa mno. Ule wasiwasi wa zamani ulikua umenirudia tena, nilikaa kwa muda mrefu Hadi Mama mmoja jirani alipokuja kuniuliza ni kwanini nimekaa hapo nje kwa muda mrefu badala ya kuingia ndani?
Ilikua ni kawaida kwa majirani kuniangalia mara kwa mara sababu ya mambo yaliyotokea kwenye Maisha yangu, ukizingatia nilikua naishi peke yangu halafu jirani huyu alikua rafiki mkubwa wa Marehemu Mama yangu.
“Kuna Mtu namsuburia Hapa Mama Amida” nilijibu huku nikimtazama usoni yule Mama, akaguna tu Kisha akaniambia
“Haya, Mimi nipo ndani” alisema Kisha aliingia nyumbani kwake, nikatazama huku na kule nikaona ni Bora niondoke pale nyumbani, nikaitazama tena nyumba yetu Kisha nikazunguka Upenyoni halafu nikaondoka bila hata kufungua mlango.
Nikampigia simu Veronica kumuuliza kama alikua amefika salama, akaniambia alikua amefika salama pia amemsimulia Mama yake kilichotokea. Nikashtuka kidogo halafu nikataka kujua Mama yake alitoa ushauri gani, akaniambia kua Mama yake amemshauri twende kwa Mganga
Moyo ulishtuka sana, nikahisi mwili ukisisimka. Nikamuuliza tena akaniambia Mama yake amemshauri twende kwa Mganga, sikua na ajizi nilikubali japo kwa shingo Upande, Veronica akaniambia kua kesho yake twende kwa Mganga, tuombe ruhusa kazini.
Basi tukakubaliana twende kwa Mganga. Nilijikuta nikitembea tembea mitaa ya Magomeni Hadi Giza lilipoingia, nikakaa Sehemu nikala chakula
lakini sikutaka kurudi nyumbani kulala peke yangu, niliendelea kuzunguka zunguka huku nikihisi maumivu ya miguu
Nilipochoka nikatafuta Sehemu nikakaa huku nikiangalia pirika pirika za Watu zilivyokua zikimalizikia. Muda ulikua unakimbia kuliko kawaida, nikatafuta Sehemu nyingine ambayo Bado Watu walikua kwa wingi, nikaenda kituo Cha daladala nikakaa hapo Hadi mishale ya Saa sita Usiku, Watu walianza kupungua huku hofu ikizidi kuniingia.
Kila nilipofikiria kwenda niliona Watu walikua wakimalizikia, hatimaye nikajikuta peke yangu nikitembea mtaani huku mgongoni nikiwa na Begi langu dogo. Nikapata wazo la kuelekea Magomeni mikumi, nilitembea taratibu Hadi Magomeni mikumi.
Saa yangu ya Mkononi iliniambia kua ilikua ni saa 7 kasoro Usiku. Nilikua nimechoka kimwili na kiakili, nikakaa mbele ya fremu Moja hivi. Angalau mahali hapo palikua salama kwangu pia palikua na Baa kando yangu, basi nilikaa hapo nikiangalia namna walevi walivyokua wakijibizana.
Lilikua tukio la ajabu sana Maishani, kuikimbia nyumba yetu na kuiacha peke yake lakini sikua na jinsi. Nililikumbatia Begi langu huku baridi Kali la Usiku likiwa linanipiga mwilini, jambo Zuri ni kwamba nilikua nimevalia Baibui hivyo nilikua nimepunguza kidogo ukali wa Baridi.
Nilitamani pakuche ili niwasiliane na Veronica twende kwa Mganga kama alivyoshauri Mama yake, nilikua nageuka huku na kule. Ilipofika mishale ya Saa 9 kasoro, pale Baa lilikuja gari Moja nyeusi, kutokana na lile Giza sikuweza kulitambua vizuri lilikua gari gani. Sijui kwanini nilikua makini sana kulitazama lakini nilijikuta nikiliangalia sana kama Mtu aliyepooza hivi.
Akashuka Mwanaume mmoja aliyevalia Shati jeupe na Suruali nyeupe, hata kiatu chake kilikua cheupe, mavazi Yale yalinifanya nianze kuogopa. Nikamwona akimwita Mwanamke kutoka pale Baa Kisha akaongea naye kwa sekunde kadhaa halafu kibaya zaidi aliyekua anaongea naye alionesha kidole nilipokua nimekaa, nilishtuka nikahisi mwili Wangu kama ulikua umepigwa shoti ya Umeme.
Nikajikuta nikiweka vizuri Miguu yangu huku macho yakiwa yamenitoka. Yule Mwanaume akarudi kwenye gari, halafu yule Mwanamke akawa anakuja nilipokua nimekaa Mimi, ilikua rahisi kugundua alikua akija kwangu sababu alishaonesha kidole nilipo, nikaliweka Begi vizuri tayari kwa ajili ya kukimbia.
Yule Mwanamke wa Baa alikuja Moja kwa moja Hadi nilipo, hapo nilikua tayari kwa ajili ya kukimbia. Moyo ulikuwa unadunda kama vile unataka kupasuka.
Akasimama mbele yangu, nilikua kimya sana lakini mwenye vita kubwa ya hofu ndani yangu, upepo ulikua ukiendelea kukoreza baridi Kali lakini nilihisi joto Kali sana.
“Habari Yako?” alinisalimia yule Mwanamke, nikapata kigugumizi kumjibu. “Nzuri”
“Unaitwa kwenye lile gari” alisema yule Mwanamke, nilipeleka macho kwenye lile gari Kisha nikameza funda zito la mate.
“Ananiita kivipi?” nilimuuliza huku nikiwa nimeshajiweka sawa kukimbia.
“Anasema anakudai anataka ukalipe deni” aliposema hivi nilihisi kuchanganikiwa, nikajua ni Yale mauza uza yaliyonifanya niikimbie nyumba yetu, nikamtazama yule Mdada Kisha nikaanza kukimbia kurudi mitaa ya nyumbani kwetu. Wakati nakimbia lile gari likawa kinakuja kwa nyuma upande wa Barabara kubwa inayorudi Magomeni kanisani.
Nilizidi kukimbia bila hata kujali kwamba nilikua nimeshadondosha viatu vyangu, sikujali hata kama ningekanyaga Msumari lakini ningekimbia tu. Kibaya zaidi Watu walikua wachache sana Barabarani tena wengi wao walikua wale ambao hawana makazi
Nikaona kama nitakimbia usawa wa Barabara nitakamatwa kirahisi, nikaona ni Bora niingie uchochoroni, haraka nikaingia uchochoroni. Kibaya zaidi huko kulikua na Giza nene pia hapakua na Watu kabisa lakini ilikua njia ya mkato kufika nyumbani.
Nilikimbia kama mwehu aliyesikia Kuna jalala jipya mahali, sijui hata niliwezaje kukatiza pale kwa Kasi ile. Nilipita uchochoroni kwa Kasi sana hata kama ningelikutana na Mtu Angekua ni mwenye kujiuliza nakimbia nini.
Nilikimbia Hadi nilipotokezea eneo la Wazi ambalo lilikua na Uwanja Mdogo wa kuchezea Mpira Watoto, hapo nikapunguza kidogo mwendo maana nilikua tayari mtaani halafu pia nilikua karibu zaidi kufika nyumbani maana kutoka hapo ni mtaa wa pili kufika nyumbani.
Mbwa walianza kubweka kwa nguvu sana, niliangaza huku na kule lakini sikuona Mtu yoyote yule, sikuwaogopa wale mbwa isipokua niliogopa
kukamatwa na Mtu anayesema ananidai. Kwa hakika kabisa Mtu yule alikua akinifwatilia Kila mahali nilipokua naenda
Angalau eneo Hilo lilikua na taa, nilitembea haraka haraka Hadi nilipofika nyumbani, ila nilikua naogopa sana kuingia ndani, nikapata wazo la kumuamsha Mama Amida nimuombe nilale nyumbani kwake Hadi Asubuhi.
Niligonga mlango wake kwa nguvu huku nikimtaka anifungulie haraka, chozi lilianza kunitoka. Nilikua nageuka huku na kule, mara haraka Mama Amida alinifungulia, nilimsukuma nikaingia Hadi ndani Kisha nikamwambia aufunge mlango haraka, akafanya hivyo haraka bila kujua ni kwanini nilimtaka aufunge mlango, Kisha akanigeukia
“Saida, Kuna tatizo gani?” aliniuliza, chozi lilikua linanibubujika tu. Akanishika mkono na kunipeleka chumbani kwake Kisha akaniambia nikae kwenye kiti.
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA NNE Sasa ( Comments ziwe nyingi)
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx


