Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » ZAINABU ( 01)
    Hadithi

    ZAINABU ( 01)

    Hamza NgondoBy Hamza NgondoMarch 23, 2026Updated:March 23, 20261 Comment7 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!! 

    Mimi ni Mtoto wa kwanza kati ya Watoto wanne, ni Mtoto wa  kike wa pekee katika Familia yetu, ndugu zangu wengine wote  ni Wanaume. Nimetokea katika familia masikini sana, lakini  yenye Mama mwemye upendo sana japo hakusoma sababu Babu yangu  hakuamini katika kusomesha Mtoto wa Kike, Mama yangu  aliipenda sana Elimu na alitamani kutuona Watoto wake  tukiipata elimu ambayo yeye aliikosa huko nyuma, Namshukuru  Mungu nilikuwa Mtoto mzuri na mwenye adabu ambaye nilimfanya  Mama yangu ajivunie. 

    Baba yangu hakuwa na utofauti na Baba wengine wa Afrika,  aliipenda sana familia yake na alihakikisha tunapata mahitaji  muhimu kama Chakula na mavazi, hakupenda nisome ila kwa  ushawishi wa Mama alikubali niende shule, Baba yangu hakuwa  na kazi nzuri sana alikuwa akifanya kazi ya kulima katika  Mashamba, familia yetu ilijengwa katika misingi ya Uislam 

    Kutokana na hali yetu kimaisha, shuleni sikuwa na vitabu wala  nguo nzuri za kuvaa lakini haikunifanya nikate tamaa  nilipigania ndoto yangu ili siku moja nije kuwa daktari wa  kwanza wa kike katika Mji wetu. Mji wetu haukuwa na huduma  nzuri za maji, elimu hata Madawa, Watu walikuwa wakifa kwa  kukosa huduma muhimu. 

    Nilikuwa na miaka 14 tu, lakini akili yangu ilikuwa ikiwaza  mambo makubwa tofauti na umri wangu, siku zote niliziweka  ndoto zangu mbele bila kujali wangapi walikuwa wakinicheka na  kunisema vibaya, tulikuwa Wasichana wachache tu katika darasa  letu sababu hakukuwa na mwamko mkubwa wa elimu, uwezo wangu  darasani ulinifanya nipendwe sana na Waalimu, walinifanya  Mimi kuwa wa mfano kwa Wanafunzi wengine huku Maisha yangu ya  kukosa mahitaji yalifanywa kuwa funzo shuleni kwani sikuwa na  vitu muhimu vya kujifunzia lakini nilikuwa nikifanya vizuri 

    “ZAINABU hana madaftari ya kutosha, hana Sare nzuri lakini  anafanya vizuri, hii iwe funzo kwenu nyie wenye vitabu na  mazingira mazuri, mkae chini mtafakari” Yalikuwa ni maneno ya  Mwalimu Ibrahim ambayo mara nyingi alikuwa akiyarudia, maneno  haya yaliwafanya wanafunzi wengi wa kike kunichukia na kuniona kama adui kwao, Mwanafunzi mmoja pekee aliyeitwa  Aminata alinichukulia kama rafiki kwake, alinipenda na  kunifanya nijione mwenye furaha shuleni. 

    Kipindi hicho tulikuwa tukijiandaa na mitihani ya kupanda  darasa, siku moja nikiwa nyumbani najisomea alikuja Mjomba  wangu aliyeitwa Suleiman, alikuja kumuona Baba akanikuta  nikiwa najisomea akanitazama kisha akatikisa kichwa chake,  nikamsikia akimwambia Baba kuwa 

    “Hee! bado unaendelea kumlisha msichana mkubwa kama huyu,  unapoteza pesa na muda wako ili asome? huyu anapaswa kuolewa”  Baba alimkata jicho kisha akasema kwa hasira 

    “Muache Mtoto asome, bado mdogo ndio kwanza ana miaka 14” 

    “Miaka 14 unasema nini wewe? Binti yangu ameolewa akiwa na  miaka 13 tuu, unapoteza chakula bure” Alijibu Mjomba Suleiman  bila woga wowote ule na kunifanya nijisikie vibaya sana,  ndoto yangu ilikuwa ni kusoma na kutimiza malengo yangu  niliyojiwekea. 

    Baba akamsogelea Mjomba Suleiman kisha akamuuliza “Hiki ndicho kilichokuleta hapa?” 

    “Aaah! hapana, nimekuja kuazima Reki yako nitairudisha kesho  asubuhi” Baba hakujibu chochote akaenda kuchukua Reki  akampatia, Mjomba aliondoka bila kuongeza neno lolote lile,  nilijawa na faraja sana kuona Baba yangu ananipigania na  kuhitaji kuniona nikifika mbali kielimu. 

    Katika Mji wetu ilikuwa ni kawaida sana Wazazi kuwaoza Binti  zao wakiwa wadogo, nilimshukuru Mungu sababu Wazazi wangu  hawakuwa kama Wazazi wengine wasio thamini elimu na haki ya  Mtoto kusoma. Tulifanya Mtihani, nilifanya vizuri na kufaulu,  ni Mimi na Aminata pekee ndio tuliofaulu kwa upande wa  Wasichana, wengine wazazi wao walifanya jitihada za kuhonga  kuhakikisha wanapanda darasa. Ilikuwa ni kawaida sana kuona  Wazazi wanatumia pesa ili Watoto wafaulu. 

    Nilifika hatua kubwa ya elimu ambayo Wasichana hawakuwahi  kufika katika Mji wetu, kwa muda mchache niliweza kuzungumza  Kiingereza vizuri, hata Anko Suleiman alipokuja alinikuta  nikizungumza Kiingereza vizuri 

    “Huna lolote unajifanya kuongea kiingereza ili uonekana ni  Mtu mweupe?” Alisema lakini Baba alisimama upande wangu kitu  ambacho kilimkasirisha sana Anko Suleiman.

    Maisha yangu ya Shule yaliendelea japo Wasichana wengine  walifanya niione shule chungu kwa maneno yao ya kejeri na  dharau, tulipofunga shule nilibakia nyumbani kwa ajili ya  kusubiria Mwaka ujao niweze kuingia kitado cha kwanza, Maisha  yalianza kubadilika kwa upande wa Baba, alikosa kazi katika  Mashamba, tulianza kuishi maisha magumu hata kula yetu  ilikuwa ni mara moja tu kwa siku kitu ambacho kilimuumiza  sana Baba yangu. Mdogo wangu Akeem alianza kuumwa, Mama  alijitahidi kumpa dawa za mitishamba ambazo zilimsaidia kwa  kiwango kidogo sana huku hali ikizidi kuwa mbaya, hofu  ikatanda mioyoni mwetu kuwa Hakeem anaweza kufa muda wowote  ule. 

    “Baba ni lazima tumpeleke Akeem Mjini kwa ajili ya Matibabu  vinginevyo tunaweza kumpoteza” Nilisema kwa huzuni sana huku  macho yangu yakitiririsha chozi lililobubujika hadi kwemye  mashavu yangu 

    “Upo sahihi Zainabu lakini matibabu yanahitaji pesa na Mimi  hapa sina pesa kabisa” Alijibu Baba kisha aliinamia chini 

    “Oooh Mungu msaidie Mwanangu apone” Ilisikika sauti ya Mama  akiwa analia, kilikuwa ni kipindi kigumu sana 

    “Baba Zainabu kwanini usiende kukopa pesa kwa Alhaji Usman?”  Mama aliuliza akiwa anajifuta mchozi, Alhaji Usman alikuwa  tajiri sana katika Kijiji chetu, alikuwa akikopesha pesa. 

    “Huwezi amini Mke wangu nilisahau kabisa kuhusu hilo jambo,  wacha niende mara moja” Alisema Baba kisha aliondoka haraka. 

    Yalipita masaa Matatu ndipo Baba aliporejea nyumbani lakini  akionekana kutokuwa na furaha kabisa japo alipatiwa mkopo wa  pesa, jambo hili lilitushangaza sana, Mama akamuuliza 

    “Baba Zainabu mbona unaonekana kama hauna raha kulikoni?” 

    “Amekubali kutupatia pesa lakini amesema tusimrudishie”  Alisema Baba kwa Unyonge sana akiwa anakaa vizuri kwenye kiti 

    “Hizo ni Habari njema kwanini usifurahie?” Aliuliza tena Mama  huku tabasamu likiwa limenijaa usoni pangu 

    “Anacho kihitaji ni kikubwa zaidi” 

    “Unasemaje? hakuna kitu kikubwa katika kupigania uhai wa  Mtoto wetu”. Alisema Mama

    “Amesema anataka kumuowa Zainabu” Baba alisema kisha moyo  wangu ukawa kama umemwagiwa maji PWAAA, Nilihisi kulowa ndani  ya moyo wangu 

    “Mungu zuia hili jambo” Mama alipaza sauti yake kisha  alisimama, akaendelea kusema 

    “Mzee wa miaka 60 tena ana wake watano aje amuowe Binti yangu  Zainabu? hilo haliwezekani kabisa” 

    “Hebu tulia Fatma Mke wangu, unajua nampenda sana Binti yangu  lakini hakuna namna tunaweza kufanya, ameahidi kutupa pesa  zaidi na kubadilisha Maisha yetu, tukubali tu ili Usman awe  Mkwe wetu” Baba alisema , Nilibakiwa nikiwa nimepigwa  bumbuwazi huku nikiwa nawatazama Wazazi wangu wakiendelea  kurumbana kwasababu yangu kitu ambacho hakikuwahi kutokea,  Nilistaajabu sana Kuona Baba yangu anaanza kulegeza msimamo  wake aliokuwa akiukaza mwanzo kuwa nisome. 

    Hali ya Mdogo wangu ilizidi kuwa mbaya kitu ambacho  kiliniogopesha sana, amani ya moyo wangu iliondoka sababu  Mama na Baba hawakupatana kabisa, walinuniana kwasababu  yangu, hali ngumu ya Maisha iliendelea kutupiga, njaa  ilitumaliza nilitamani sana kuisaidia familia yangu hasa  Akeem ambaye alikuwa mgonjwa huku akikosa chakula.  Nilifikiria kuhusu elimu na ndoto zangu, sikutaka kabisa  kupoteza muelekeo katika Maisha yangu tena kwa Mwanaume Mzee  mwenye wake watano na watoto wakubwa walionizidi Umri, kila  nililolifikiria niliona linaenda kunivunja moyo wangu lakini  unafikiria ningefanyaje? 

    Siku moja Anko Suleiman alikuja nyumbani, namna sura yake  ilivyo nilijua tu kulikuwa na tatizo, nilimsalimia 

    “Shikamoo Anko Suleiman” Hakujibu badala yake aliniuliza “Mama yako yupo wapi?” 

    “Yupo ndani ngoja nimuite” Niliinuka na kwenda kumuita Mama,  siku hiyo Baba alikuwepo pia, walikaa na kuanza kuzungumza 

    “Fatma kwanini unataka kuiharibu hii Familia? kwanini wewe ni  Mama Mbaya sana” Aliuliza Anko Suleiman 

    “Mimi sio Mama mbaya na siwezi kuiharibi Familia yangu  mwenyewe, unasema nini Suleiman?” Mama alihoji 

    “funga bakuri lako, kwanza sikulaumu wewe kuwa hivyo bali  namlaumu Mume wako aliyekupa mamlaka ya kuwa na sauti hapa 

    nyumbani, Fatma unang’ang’ania elimu ili ije kumsaidia nini  Zainabu? unafikiri hata akisoma ndio hatoolewa?” 

    Nini Kitaendelea? USIKOSE SEHEMU YA PILI 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

     

    riwaya mpya Riwaya ya Goryanah Riwaya Ya Kisasi Changu Riwaya Ya Msala riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni soma riwaya bure

    1 Comment

    1. Ander on March 24, 2026 10:05 am

      Nice

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.