Ilipoishia
Niliitazama tena ile Pete huku chozi lilikaribia kunitoka, sikujua ni kwanini nilipaswa kuivaa ile Pete, ni Mikoba gani ambayo nilipaswa kukabidhiwa? Nilijiuliza yote huku nafsi yangu ikiniambia niichukue Pete ili kuokoa Maisha ya Watu wengine ndani ya basi.
Wala haikuchukua hata dakika Moja ukatokea mtikisiko mwingine mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo, hata abiria wengine walianza kupiga kelele, lakini dereva aliliweka tena gari Barabarani, nilijua lilikua onyo kwangu na pengine sasa pasingelikua na onyo jingine
Niliiokota ile Pete Kisha niliivaa bila kusita, Pete ilizima. Hali ya utulivu ilipatikana ndani ya Basi, pakawa kimya safari ikiwa inaendelea kuelekea Dar-es-salaam. Sikuhisi chochote kile mwilini mwangu, ilikua kama vile nilikua nimevaa Pete ya kawaida tu.
Hukusoma SEHEMU ZILIZOPITA? Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI , SEHEMU YA TATU , SEHEMU YA NNE , SEHEMU YA TANO , SEHEMU YA SITA Kisha Endelea
SEHEMU YA SABA
“Kwanini nimelazimishwa kuivaa hii Pete, Ina nini?” Nilijiuliza swali hili huku nikiwa ninaingalia mara kwa mara. Mwishowe nilikosa majibu nikaona nitulie
Safari ilizidi kuendelea kwa utulivu wa Hali ya juu sana, hapakua na Mtikisiko wa aina yoyote ule. Saa ya kwenye basi ilionesha ilikua ni saa Nne na nusu usiku, nilifikiria kujipumzisha kidogo. Basi nilijiegesha kimagutu.
Usingizi haukuwa na hiyana ulikuja, tena ulikuja Usingizi mzito sana kiasi kwamba ilikua ngumu kuelewa kua nilikua napitia wakati mgumu sana.
**
Baada ya kitambo Cha kulala ndani ya Basi, nilianza kuhisi upepo mkali ukiwa unanipiga hasa kwenye paji langu la Uso, upepo ule uliniamsha kutoka Usingizini. Sikujua hata ulitokea wapi lakini nilipoamka haukuwepo tena
Bado safari ilikua ikiendelea, nilisimama ili kuangalia saa ya kwenye Basi, muda ulikua ni saa 5:55 Usiku. Wakati nataka kukaa nilihisi kuona kitu Cha ajabu sana, nilihisi Nina wenge la Usingizi lakini kiuhalisia halikua wenge la Usingizi.
Yes‼ nilichokiona kulinifanya nishangae kuliko wakati wowote ambao niliishi juu ya Uso wa Dunia. Niligundua Watu wote ndani ya Basi walikua wafu waliobakiwa mifupa tupu.
Kabla hata sijashangaa zaidi, basi lilisimama katikati ya Msitu, taa za Basi ziliniambia kua haikua Barabara kuu ya kawaida isipokua Barabara ya vumbi isiyo salama.
Nilitamani kulia, lakini halikua chaguo langu. Nilizidi kuhema kwa Kasi sana, nilianza kusikia sauti za Watu wakiimba, sauti hizi zilikua zikisikika nje ya Basi.
Nilitamani kuchungulia nje, taratibu nilisogea nikiwa ninatetemeka ili niangalie nje ya Basi. Niliwaona Watu waliovalia mavazi meusi, Watu hao walikua wengi lakini walikua wamefunika vichwa vyao kwa vitambaa vyeusi.
Nilijiuliza nifanye nini, au Ndiyo ulikua mwisho wangu? Basi nikawaona Watu wawili wakiingia ndani ya Basi, taa za ndani ya Basi zilikua zimewashwa.
Niliwaona vyema Watu wale, waliovalia mavazi meupe tofauti na wale wengine waliovalia mavazi meusi. Hawa walio ingia ndani ya Basi niliwaona Hadi sura zao. Walipofika nilipo mmoja akaniambia
“Fuatana nasi” Wala hakuongeza neno, mmoja akasogea mbele na mwingine akaja kusimama nyuma ya Siti yangu. Miguu ilikua inatetemeka na sikuweza hata kupiga hatua vizuri, mdomo Wangu ulikua mzito sikuweza hata kuzungumza neno Moja. Nilijilazimisha kupiga hatua huku chozi likinibubujika kwa Kasi sana, nilikua kama ‘zezeta’
Nilipiga hatua ndogo ndogo nikimfuata yule wa mbele wakati huo yule mwingine akija nyuma yangu, hawakuni harakisha. Walitembea kwa kufuata hatua zangu Hadi tunafika chini ya Basi, zile kelele za kuimba zilikoma.
Palikua kimya sana, pale nje upande wa mbele palikua na gari jipya kabisa la kifahari.
“Tafadhali fuatana nasi” alisema tena yule Mtu, sikujua nilikua napelekwa wapi. Yule Mtu akaingia ndani ya lile gari huku nikioneshwa ishara kua nami napaswa kuingia ndani ya lile gari. Niligeuka kutazama huku na kule, hapakua na upepo wowote ule Hadi nilijiuliza Mbona Dunia ipo kimya sana?
Niliingia ndani ya lile gari taratibu sana, Kisha yule Mwingine akaja kukaa siti jirani na nilipokaa, yule Mwingine akalitoa lile gari la kifahari kutoka pale Msituni, Kisha tulitembea kidogo tukaingia barabara ya Lami. Kila gari tuliyopishana nayo ilikua gari ya kifahari Hadi nikajiuliza tupo Mji gani?
Nilitamani sana kuuliza walikua wananipeleka wapi lakini nilijawa na hofu sana. Sura zao zilikua na michoro ya ajabu ajabu sana, nakumbuka tulisafiri kwa umbali mrefu kidogo kabla ya gari kusimama nje ya jumba Moja la kifahari sana kando ya fukwe ya Bahari.
Geti lilifunguliwa Kisha gari likaingia ndani ya Uzio wa ile nyumba. Palikua kimya isipokua kelele za Maji ya Bahari yaliyokuja yakigonga Kingo za Bahari
Niliambiwa nishuke kwenye gari, mlango ulifunguliwa Kisha nami nikashuka nikiwa sielewi eneo lile lilikua ni wapi. Mara walikuja Watu wawili, mmoja wa kike na mwingine wa Kiume,.
Wote walikua wamefunga macho Yao kwa kutumia vitambaa vyekundu, wenyewe walivalia nguo nyeupe mfano wa magauni makubwa yanayoburuza Hadi chini. Nilikua natetemeka, palikua na Giza lakini angalau taa za ile nyumba zilinifanya nione bila shida yoyote ile.
Mwanamke alikua ameshikilia sahani yenye mshumaa unaowaka na Mwanaume alikua ameshikilia sahani yenye kikombe Cha Udongo, cheupe.
Nilikua natetemeka, hata walipofika hawakuzungumza chochote kile. Yule Mwanaume alichukua kikombe akanimwagia maziwa usoni kutoka kwenye kile kikombe. Nilitetemeka sababu yalikua ya Baridi sana, harufu na Radha kidogo iliyoniingia Mdomoni mwangu ilinifanya nigundue haraka kua yalikua maziwa.
“Aahh” Niligugumia kidogo Kisha chozi lilianza kunitoka, kusema ukweli sikua na Ujanja wowote ule maana hata nisingeliweza kukimbia. Halafu yule Mwanamke akachukua mshumaa na kuanza kuzungusha usoni pangu
Sijui aliwezaje kuona wakati alikua amefungwa kitambaa usoni, ni maajabu. Nilisubiria kuona baada ya kunifanyia vile kingefuata nini.
Hakuna aliyezungumza hata kukohoa, Kisha baada ya kumaliza alitoa ishara kwa wale Watu niliosafiri nao, alitingisha kichwa na wala sikujua aliwaambia nini, nikageuka kuwatazama maana walikua nyuma yangu
Mmoja wao akanishika mkono, alikua ni yule aliyekua amekaa siti Moja na Mimi nyuma ya gari. Akanionesha ishara ya Mkono kua nielekeze mbele ambako palikua ndiyo Kuna mlango wa kuingia ndani ya jumba Hilo la Kifahari sana
Nilitembea taratibu, hapakua na ‘kashkash’ yoyote ile kwangu, hawakuonekana kunilazimisha chochote kile.
Hapakua na umbali mrefu sana, tulilipita bwawa dogo la kuogelea ambalo lilikua linawaka taa za Bluu, Kisha Tulifika mlangoni. Mlango ulikua na michoro Mingi sana ya ajabu, nilisimama nikiiangalia Kisha nilisisitizwa kua niingie ndani.
Niligeuka nyuma, wale Watu walikua nyuma yangu. Nami ndiye niliyekua mbele zaidi, basi niliutosa Mguu wangu ndani ya Nyumba hiyo, nilihisi kama vile nilikua nimepuliziwa marashi Fulani makali sana
Marashi ambayo sikuwahi kuyahisi Maishani mwangu. Tena sikufikiria kama ningeyahisi siku Moja, yalikua na harufu nzuri sana siwezi hata kuielezea. Nilihisi Ubaridi Fulani, Kisha wale Watu waliingia halafu mlango ukawa umefungwa
Jumba lilikua kimya sana halafu sakafu ilikua safi mno kama vile hua haikanyagwi na yeyote yule. Namna walivyo kua wakinitendea nilianza kuondoa hofu kidogo, nilioneshwa Sehemu ninayotakiwa kwenda, walinisogeza kupitia korido Hadi mlango ulioandikwa ‘MWISHO’
Niligeuka kuwatazama wale Watu, mmoja akatikisa kichwa kunipa ishara kua napaswa kuingia humo, kama ulivyo mlango wa kwanza hata huu pia ulikua na Michoro lakini huu niliweza kuukagua vizuri zaidi ya ule wa mwanzo.
Ulikua na michoro ya Watu walio Uchi wa Mnyama, wanawake kwa Wanaume. Nilivuta pumzi ili kujiandaa kuingia humo, Kisha pole pole niliingia kwa kuanza kutekenya kitasa ambacho kilinipokea kwa utulivu sana.
Yale Marashi yalikua mengi sana humo, chumba kilikua na kiti kimoja kikubwa. Nilipokiangalia niligundua kua kilikua kiti maalum kwa Mtu maalum, ndani ya chumba hapakua na yeyote yule isipokua Mimi na wasiwasi wangu.
“Kwanini nimeletwa hapa?” Nilijiuliza kwa sauti ya ndani. Niligeuka tena nyuma, nilikutana na Mlango uliofungwa
Nilishusha pumzi huku sauti ya ndani ikiniambia niwe mdadisi, nafsi yangu haikutaka kuridhika kabisa ikaniambia ni lazima nidadisi ni kwanini nipo ndani ya kile chumba Chenye kiti kama Cha kifalme hivi.
Hii haikua ndoto kwangu Mimi Saida, sikulala Bali nilikua macho nikishuhudia maajabu haya. Niliruhusu miguu yangu kutembea taratibu kukifuata kile kiti kilichokua katikati ya kile chumba.
Mapigo yangu ya Moyo yalizidi kwenda Mbio, jasho lilianza kunitoka licha ya Ubaridi uliokua ndani ya kile chumba, niligeuza macho huku na kule lakini sikung’amua chochote.
Nilikifikia kile kiti baada ya hatua kama saba hivi, hatua za taratibu mno. Nilipofika nilikigusa kile kiti, mara Pete ya Mkononi ilianza kuwaka na kutoa mwanga wa Kijani ambao ulikua mkali kuliko hata ile mara ya kwanza kule ndani ya Basi nilipoivaa kwa mara ya kwanza.
Nilishtuka nikarudisha mkono wangu nyuma.
Nilisikia sauti ya Kiume nzito sana ikiniambia
“Karibu Malkia Saida kwenye kiti Cha enzi” sauti hii ilitokea Kila kona ya kile chumba, ilikua sauti ya kutisha mithiri ya radi ipasuayo miamba.
Niliziba masikio yangu kuzuia sauti Kali isinipe kiwewe, sauti ile haikukoma hata licha ya kuziba masikio.
“Umechaguliwa kukalia kiti Cha enzi kama Malkia wa Enzi. Sasa una nguvu za Kichawi kutoka kwenye Pete, wewe ni Msaidizi wa Shetani na utafanya kazi za shetani” ilisema ile sauti, nilizidi kushangaza.
Ile sauti ilinifanya nitikise kichwa changu, nilihisi nachanganyikiwa sababu kilichosemwa hakikua kitu Cha Kawaida.
“Nani alikwambia Mimi nahitaji kumtumikia shetani?” nilipaza sauti kwa nguvu, nilishatoa mikono masikioni. Hasira ilinipanda sababu niliona nilikua naelekea kupoteza Kila kitu Maishani.
“Saida, wewe ulishakufa baada ya kuokolewa Msituni. Roho Yako iliondoka Usiku ule ambao ulitoroshwa kule kwenye ile nyumba Msituni. Kuishi kwako Hadi sasa ni kibali Cha Shetani hivyo unapaswa kumtumikia” ilisema sauti ile, nilizidi kuchanganyikiwa.
Yaani Mimi nilikufa? Chozi lilinibubujika. Sasa kama nilikufa iliwezekanaje nikawa na akili za Kibinadamu, kwanini Nilikutana tena na Salehe, Salehe ni Nani Hadi anipatie hiyo Pete inayodaiwa kua na nguvu za Kishetani?
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya NANE
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

