Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya sabaΒ
“Naomba niongee na Shayo haraka” Alisema Rais, mara mojaΒ Waziri Mkuu alipiga simu kwa mkuu wa kitengo cha Usalama waΒ Taifa ambaye hadi kufikia wakati huo hakujuwa Faudhia alikuwaΒ wapi, ni mzima au amekufa ila Faudhia alikuwa barabaraniΒ kuelekea Dar kwa ajili ya kuzuia mpango wa Mzee Shomari.Β
Mara moja simu ya Mzee Shayo ilipokelewa na maongezi kati yaΒ Mzee Shayo na Rais yalianza, Rais alisikika kwa kupoa sanaΒ tofauti na mwanzo ambapo alionesha hasira sana kwa Mzee ShayoΒ
“Shayo!!” Aliita RaisΒ
“Naam Mkuu” Aliitika Mzee Shayo . ENDELEAΒ
SEHEMU YA NANEΒ
“Wewe ni Mtu pekee ambaye unaweza ukadhibiti kila kitu naΒ kuleta sifa kwa Taifa hili, ruhusu Vijana wako waishambulieΒ Benki sasa hivi” Alisema Rais kisha mwisho alisema kwa kukazaΒ sauti tofauti na mwanzo alivyoanza.Β
“Mkuu, ndani ya Benki kuna Raia wasio na hatia, shambulioΒ lolote lile tutakalo lifanya litasababisha madhara makubwaΒ sana. Hiyo siyo suluhu ya jambo hili Mkuu, busara niΒ kuhakikisha Mateka wote wanatoka salama” Alijibu Mzee ShayoΒ
“Mimi ndiye Rais wa Nchi hii nataka uamrishe walengaji wakoΒ waishambulie Benki haraka iwezekanavyo” Alisema tena Rais kwaΒ sauti ya kufoka huku akijuwa fika kuwa Mzee Shayo haweziΒ kukubaliana na wazo hilo.
Β Β
“Hilo haliwezekani Mkuu, tuvute subra kwa masaa kadhaaΒ nitakuja na mpango wa nini tufanye” Alisema tena Mzee ShayoΒ
“Shayo! Narudia tena Mimi ndiye Rais wa hii Nchi, hakuna RaisΒ mwingine wala amiri jeshi Mkuu. Kama utashindwa kufanya hivyoΒ nitatengua uteuzi wako haraka sana” Alisema Rais kwa sautiΒ ile ile ya kufokaΒ
“Mkuu siwezi kutoa amri hiyo kwa vijana wangu, hii kaziΒ inahitaji…”Β
“Shayo siwezi kukubembeleza” Alisema Rais kisha simuΒ ilikatika, Mzee Shayo alibakia akiwa njia panda, alijaribuΒ tena kuipiga simu ya Faudhia lakini haikuita kabisa,Β alijiuliza kama Faudhia atakuwa ameshakufa basi hakutokuwa naΒ jambo lolote la kuzuia amri ya Rais huyo, alichoka naΒ kujitupa Kitini huku akitafakari afanye kitu gani.Β
Mwendo wa Bakora huko Bagamoyo Road, Matilda aliendesha gariΒ kama dereva wa mshindano ya Formula one, ilikuwa ni safariΒ yenye matumaini, Bado Mzee Shayo aliendelea kumtafuta FaudhiaΒ huku Mzee Shomari akipewa taarifa kuwa Diana alikuwaΒ ameshauawa na mzigo ulikuwa umechukuliwa, taarifa hiyo ilimpaΒ wazimu sana Mzee Shomari, alimpigia tena Chogo na kumwambiaΒ kuwa wana chini ya masaa mawili kuhakikisha wanachomoka ndaniΒ ya Benki hiyo haraka sana, wakati huo huo baada ya kumalizaΒ kuongea na Chogo alipiga simu na kuagiza Helkopta isogeeΒ lilipo jengo la China plaza ili aweze kuondoka baada yaΒ kuhakikisha akina Chogo wanatoka salama.Β
Akiwa ofisini Mzee Shayo, ilikuwa ni baada ya saa moja kupitaΒ aliingia Mwanaume mmoja aliyejulikana kama Samuel Dinonga,Β alikuwa ni Mkuu wa jeshi la polisi, iliwapasa kumpa salamuΒ aliyostahili kisha Dinonga alimueleza Mzee Shayo kuwa yeyeΒ ndiye aliyepewa jukumu la kuongoza idara ya Usalama wa TaifaΒ kwa wakati huo, Mzee Shayo alipaswa kukiacha kitengo harakaΒ sana. Yalikuwa ndiyo maamuzi ya Rais, hakukuwa na namna, MzeeΒ Shayo aliacha kila kitu na kuondoka ofisini hapo.Β
Lengo la Rais lilikuwa ni kuishanbulia Benki hiyo bila kujaliΒ kuwa kulikuwa na Gavana na Mke wake pia kilikuwa naΒ wafanykazi wa Benki na wateja wa Benki hiyo ambao hawakuwa naΒ hatia yoyote ile, muda huo alilielekea gari lake ili awezeΒ kutimka eneo hilo la Makao makuu ya Kitengo cha Usalama waΒ Taifa, alipofika ndani ya gari simu yake iliita.Β
Aliitilia mashaka kidogo simu hiyo sababu ilipigwa kwa nambaΒ ambayo hakuifahamu kabisa, alisubiria kidogo kisha aliipokeaΒ
“Hello!” Alisema Mzee Shayo kwa umakini wa hali ya juu sana.
“Baba!!” Alisikia sauti ya Faudhia ikimuita, hakuaminiΒ masikio yake ni kama vile alisikia kitu kisichomuingiaΒ akiliniΒ
“Faudhia uko wapi?” Alihoji Mzee ShayoΒ
“Nipo Barabarani nakuja huko Baba, naomba unisikilize kwaΒ makini sana” Alisema FaudhiaΒ
“Ndio ndio”Β
“Ndani ya jengo la China plaza ndimo alipo Mkuu wa kikosiΒ hicho, si mwingine ni Mzee Shomari! Chukua askari nendaΒ kamdhibiti haraka sana mimi muda siyo mrefu nitakuwa Dar”Β Alisema Faudhia kwa umakini sanaΒ
“Kwasasa mimi siyo Mkuu wa Kitengo Faudhia, sina mamlaka yaΒ kuamrisha askari wa kitengo tena” Alisema Mzee ShayoΒ
“Oooh! Shit, basi jitahidi uwende mwenyewe maana ndani yaΒ hicho kitengo kuna Watu wanafanya kazi ya kukwamisha juhudi”Β Alisema FaudhiaΒ
“Sawa ngoja nisogee huko” alisema Mzee Shayo kisha simuΒ ilikatika, aliangalia kwenye gari yake aliona silaha aina yaΒ Bastola, hakujuwa uzito wa ulinzi wa huko ndani ya jengo laΒ china plaza ila aliamini Bastola hiyo itamsaidia, aliondoaΒ gari kitengo na kuelekea China plaza.Β
Mkuu mpya wa kitengo Bwana Dinonga alifuata maagizo ya RaisΒ wa Nchi, ilikuwa ni lazima aunganishe jeshi la polisi naΒ askari wa kitengo ambao walikuwa eneo la tukio kuifanya kaziΒ kwa pamoja. Aliondoa idadi kubwa ya Askari pale makao makuuΒ kwa ajili ya kuelekea Benki ili kuishambulia benki hiyo,Β lengo likiwa kuuwa kila aliye ndani ya jengo hilo ili siri yaΒ pesa zile iendelee kubakia wakiamini kuwa Chemba haikuwezaΒ kuonekana wakati chemba ya siri ilikuwa imeshafunguliwa.Β
Upande wa pili, Helkopta iliyoitwa kwa ajili ya kumchukuaΒ Mzee Shomari ilikuwa ikijongea taratibu kuelekea hapo, MzeeΒ Shayo naye akiwa ndani ya gari lake alikuwa akifikiria niΒ jinsi gani ataweza kukabiliana na Magaidi hao ndani ya jengoΒ la China plaza, safari ya kutoka Kigamboni hadi Mjini ilikuwaΒ fupi tu ukizingatia hakukuwa na shughuli zozote zilizokuwaΒ zikifanyika ndani ya Jiji hili la kibiashara, muda huoΒ Faudhia alikuwa akiingia Dar, mwendo wao haukuwa wa kawaida,Β walipofika Tegeta Matilda alimwambia Faudhia kuwa anahisiΒ kizunguzungu kutokana na spidi ya gari aliyokuwa nayo,Β ilimlazimu Faudhia amwambia Matilda kuwa asimamishe gariΒ
Β Β
haraka, Basi Matilda alifanya hivyo wakiwa maeneo ya kwaΒ Ndevu – TegetaΒ
“Pole sana, Asante pia” Alisema Faudhia, Matilda alishindwaΒ hata kumjibu Faudhia alipoteza fahamu akiwa ameshikiliaΒ usukani. Faudhia alishuka na kuielekea pikipiki iliyokuwaΒ imesimama kando ya Barabara, aliiwasha na kuondoka eneo hilo.Β
Ukimya ulikuwa mkubwa sana alipofika maeneo ya Mnazi mmoja,Β alilazimika kushuka na kutembea kwa mguu kuelekea ChinaΒ plaza, japo alikuwa Mzee lakini hakusahau mbinu zakeΒ zilizompa umaarufu miaka ya 90, Mzee Shayo alikuwa ni zaidiΒ ya komando wa vita, alisogea kwa kasi ya ajabu kwa kutumiaΒ njia za ndani kama anaelekea Shimoni kariakoo, alijuwa fikaΒ kuwa kama ni kweli magaidi hapo ndipo walipoweka kambi yaoΒ basi ulinzi wake utakuwa mkubwa sana. Alikuwa ndani ya sutiΒ ya kijivu iliyomkaa vizuri, alivua koti akabakiwa na shatiΒ jeupe litakaloweza kumpa urahisi wa kuifanya kazi yake.Β Alikuwa akitembea huku akiangalia saa yake aliyoweka mudaΒ maalum wa kufika eneo husika kabla kitengo cha Usalama waΒ Taifa hakijashambulia Benki na kuuwa Watu wasio na hatia,Β alikuwa na nusu saa tuu iliyobakia, muda huu alikuwaΒ ameshazunguka hadi Msimbazi polisi, alikuwa sasa eneo laΒ Msikiti wa Shekh Idrisa, alikuwa makini kuliko wakati wowoteΒ katika Maisha yake, alijuwa hiyo ndiyo nafasi pekee naΒ pengine ingelikuwa kazi yake ya mwisho kutokana na umri wakeΒ na pia kuondolewa kwake kwenye kitengo na Rais.Β
Kwa mbali asikia sauti ya Helkopta ambayo ilikuwa ikielekeaΒ China plaza kwa ajili ya kumchukua Mzee Shomari, muda huoΒ Faudhia alikuwa ameshafika upanga kwenye msikiti wa MaamurΒ ili kuingia kwenye hiyo chemba itakayotumika kutorosha pesaΒ kutoka Benki kuu. Alipofika hapo aliona Watu watatu wenyeΒ asili ya kiarabu wakiwa wamekaa kwa nje, aliwatazama kwaΒ jicho la kijasusi aligundua Watu hao ambao ni wanaumeΒ walikuwa na silaha walizozificha kwenye viuno vyao, FaudhiaΒ alifikiria atumie njia gani kufika pale, alifikiria kwa zaidiΒ ya dakika mbili huku ile presha kuwa muda unaisha ilizidiΒ kumjaa aliona ni bora aamuwe kufanya kitu kimoja.Β
Alisogea hadi kwenye ukuta kimya kimya pasipo wale WanaumeΒ kushtuka huku wanaume hao wakionekana kusoma vitabu ya dini,Β alijuwa ulikuwa mtego ili watu wasishtuke chochote, alionaΒ pia baadhi ya Watu wakitoka na kuingia Msikitini hapo,Β ilikuwa ngumu kwake kujuwa kuwa Watu hao walikuwa wema auΒ maadui. Pembezoni aliona nguo zilizokuwa zinetundikwa naΒ zilikuwa ni za kiume, haraka Faudhia alizichukua na kuzivaa.
Alihakikisha anaonekana kama Mwanaume, na kweli alifanikiwaΒ kwenye hilo, alivuta pumzi zake ili kujiondoa wasiwasi kishaΒ aliitoa bastola aliyoichukua baada ya kumuuwa Diana,Β aliangalia Bastola hiyo yenye risasi tatu pekee alionaΒ isingeliweza kumfaa ila ingelimsaidia kwa kiasi fulani,Β aliiweka sawa Bastola yake kisha aliingia barabara ya lamiΒ akawa anasogea, Wale Wanaume walipomuona Faudhia walionekanaΒ kumkagua kwa kutumia macho yao yaliyojaa wizi hukuΒ wakijifanya wengine kusoma na mwingine kuchezea tasbihi.Β Walipeana isharaka kisha mmoja akaingia ndani wawiliΒ wakabakia pale, Faudhia alisogea hadi lango la Msikiti.Β Mwanaume mmoja aliyekaa alimsalia Faudhia kwa Salam yaΒ KiislamΒ
“Asalaam Alaykum?” Alisalimia huku akimtazama Faudhia ambayeΒ alikuwa amevalia kiremba na kuificha sura yake kwa kuangaliaΒ pembeni, yule Mwanaume alimsalimia tena FaudhiaΒ
“Asalam Alaykum Shekh” Alisalimia bila wasiwasi, FaudhiaΒ alihema sana akijuwa kuwa jamaa huyu alikuwa ameshamshtukia,Β kisha Mwanaume huyo aliinuka na kumsogelea Faudhia ambayeΒ hakutaka kuonesha sura yake.Β
Sura ya Mwanaume huyo ilianza kubadilika na kuwa ya hasira,Β alikuwa tayari ameshamtilia Mashaka Faudhia. Alizidi kusogeaΒ kisha alimuuliza FaudhiaΒ
“Wewe ni nani?” Aliuliza kwa rafudhi ambayo ilionesha waziΒ kuwa Mwanaume huyo alijifunza kiswahili siku si nyingi,Β mapigo ya moyo ya Faudhia yalizidi kwenda mbio. Yule MwanaumeΒ akawa anasogea kuitazama sura ya Faudhia, endapo atagunduaΒ kuwa Faudhia si Mwanaume itakuwa shida kwa FaudhiaΒ
Yule Mwanaume alisogeza mkono ili amshike Faudhia amgeuze,Β Faudhia alifumba macho yake kuwa asingeliweza kufurukutaΒ hapo, ghafla kabla hata hajamgusa Faudhia liliingia gari laΒ kubebea maiti lililoleta maiti kwa ajili ya kuswaliwa.Β Purukushani za watu zikawa nyingi na kwakuwa walisimamaΒ katikati ya lango iliwapasa kulipisha gari hilo, FaudhiaΒ alibakia upande wa kulia na yule Mwanaume alirudi upande waΒ kushoto kisha gari ikapita katikati yao. Fumba na kufumbuaΒ Macho yule Mwanaume aligundua kuwa Faudhia ameshatoweka pale,Β haraka alipiga simu kwa wenzake kuwa eneo hilo si salamaΒ tena, aliwavuka Watu na kuelekea kwenye mlango wa kuzidiΒ kuzama ndani ya Msikiti huo.Β
Naam!! Sasa, Mzee Shayo alikuwa ameshafika chini ya Jengo laΒ China plaza, jengo hilo lilikuwa refu lenye vioo, Mzee ShayoΒ alipochungulia kwa mbele aliona kuna Watu waliokuwaΒ
wamesimama pembezoni, alijuwa tu Watu hao siyo watu salamaΒ kwake, muda huo Helkopta ilikuwa hewani juu ya Ghorofa hilo,Β alijuwa ndiyo wakati sahihi wa kuanza kukiwasha ili kuzuiaΒ Mzee huyo asitoweke eneo la tukio. Haraka alisogea mbele yaΒ jengo, alimvizia mlinzi wakwanza kisha alimnyonga kwa kutumiaΒ kamba ya kiatu chake, alimvuta hadi mahali ambako kulikuwa naΒ jenereta kubwa la kuzalisha umeme, huyu wa pili alikuwaΒ amempa mgongo Mzee Shayo hivyo ilikuwa ni rahisi kumalizanaΒ naye, alimpiga kiwiko eneo la shingo, alifanya kimya kimyaΒ kisha alimvuta na kumsogeza pembeni, alihakikisha anawasachiΒ na kuchukua silaha zao. Alikuwa ni Mtu makini sana ambayeΒ aliijuwa thamani ya kazi aliyokuwa akiifanya, alisogea hadiΒ mlango wa kuingilia, jengo lilikuwa kimya sana na hakukuwa naΒ dalili kuwa Kulikuwa na mitembeo ya Mtu zaidi ya sauti yaΒ Helkopta iliyokuwa juu ya Jengo, humo ndani Mzee ShomariΒ alidhamiria kuhakikisha kuwa anachukua kila kitu kabla yaΒ kutimka, alichotaka ni kuhakikisha Chogo anatoroka na pesaΒ hizo ndani ya benki kwanza kabla yeye hajaondoka sababuΒ alishajuwa ni wapi watakutana kwa ajili ya kugawana kiasiΒ hichoΒ
Alimpigia Chogo na kumwambia kuwa ni muda wa kuondoka, upandeΒ huo wa Benki tayari Chogo alikuwa na kiasi hicho cha pesaΒ ndani ya mabegi kilichobakia kilikuwa ni kuondoka tuu,Β aliwaambia vijana wake kuwaΒ
“Tunaenda kuwa Mamilionea leo” Alisema Chogo kwa tabasamu,Β aliamuru waifuate Chemba kwa ajili ya kuondoka, tayariΒ alikuwa ameshawaweka vijana huko wakawa wanachimba naΒ kuunganisha chemba hiyo ambayo hadi kufikia muda huo ilikuwaΒ tayari kilichobakia kilikuwa wao kuondoka tuu. AlipofikaΒ kwenye Korido alikumbuka kuna kitu amesahau kisha aliwaambiaΒ vijana wake kuwa wamsumbirie kwenye chemba, Chogo aliendaΒ kwenye Chumba ambacho alimuacha Selina. Huwezi amini ChogoΒ alikuwa ameshampenda Selina, alipofika alimtazama SelinaΒ ambaye alikuwa analia akiwa amekaa juu ya meza, chogo alijawaΒ na huruma huku simu yake ikiwa inazidi kuita, alikuwa ni MzeeΒ Shomari ndiye aliyekuwa akimpigia simu.Β
Upande mwingine ndani ya Msikitini, Mtafutano ulikuwa mkubwaΒ mno, Faudhia aliijuwa ramani ya ilipo chemba hiyo yaΒ utoroshwaji wa pesa ndani ya Benki, alijificha mahali ambapoΒ aliamini ingelikuwa rahisi kuwaona Wanaume hao, wanaumeΒ walipofika ndani waliufunga mlango huo ili kisisikikeΒ chochote kutokea humo na kwenda kule Msikitini ambakoΒ kulikuwa na harakati za kuanza ibada ya kuisalia Maiti.Β
Walifunga viwanbo vya kuzuia sauti kwenye Bastola zao iliΒ kuhakikisha hakuna kitakachosikika ili wasije haribu mpangoΒ wao. Faudhia alikuwa kwenye moja ya vyumba ambavyo vilikuwaΒ ndani ya Eneo hilo, wale wanaume waligawana Majukumu yaΒ kumsaka Faudhia.Β
Chumba alichojificha Faudhia kilikuwa kina dirisha la KiooΒ hivyo ilimpa urahisi wa kuona na kuonwa pia endapo adui yakeΒ atatazama kwenye kioo, mlango ulitekenywa huku Faudhia akiwaΒ amjibanza ukutani, bastola yake ilikuwa kiunoni sababuΒ aliamini matumizi ya Bastola yangelimfanya agundulike. WaleΒ magaidi waliambiana kuwa wanapaswa kuingia kwa pamoja kwenyeΒ vyumba na kutoka pamoja hivyo endapo mmoja hatotoka basiΒ chumba hicho ndicho ambacho adui yao atakuwa yumo.Β
Wakati kitasa kinatekenywa, Faudhia aliona Upanga kwenye konaΒ ya Chumba hicho, aliuchukua taratibu bila kupiga kelele yaΒ aina yoyote ile, alijiweka sana huku kioo kikiwa ndio msaadaΒ pekee kwake, yule Mwanaume alivyotokeza kichwa alikutana naΒ upanga ambao ulizama kichwani, haraka Faudhia alimvutaΒ Mwanaume huyo ndani kisha alichukua Bastola ya Mwanaume huyoΒ alafu akasikia sauti ya kwanza ikisemaΒ
“Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba kingineΒ ikisemaΒ
“Safi” wakimaanisha kuwa vyumba vyao vipo salama hapo ndipoΒ Faudhia aliposhtuka kuwa anapaswa kuwa nje ya chumba harakaΒ sana ili awawahi Wanaume hao, alifanya hivyo upesi sana hukuΒ akiwa ameelekeza Bastola yake mbele mahali ambako sauti hizoΒ zilitoka, wale wanaume hawakuisikia sauti ya tatu ya mwenzaoΒ ndipo walipotoka nje haraka ila walikuwa wamechelewa,Β walikutana na mishale ya risasi kutoka kwa Faudhia, MsichanaΒ kutoka Mbeya, aliwamaliza kimya kimya bila kusikika popoteΒ sababu bastola ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti .Β
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA TISA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β
12 Comments
Thanks alot kijiwen
But mnafanya niunge megabyte zangu always ili tyu kupata hii zaid ya story
Kubali Sanaa faudhia people ya green city
hatarii
hizi ndio tunataka sio za kichawi usiku hatulali
Hatar sqna kiongozi
Hiii story ni ya π₯π₯π₯ admin upo vzr
Iko pw ila inachelewa sana kupostiwa tupia inayofuata
Ni bongo la story hongera mtunzi
Story Nzuri Saana Ila Tunaomba Jaman Mnazichelewesha Saana Ni Inasisimua Saana Hiii
Daaah!! nzuri saaana, sehemu ya 9 tafadhari naisubiria kwa hamu.
f8qmc5
Good ππ
Tunaomba mwendelezoππ
i2ibrt