Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)
    Hadithi

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJune 6, 2025Updated:June 6, 20257 Comments12 Mins Read756 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya sabaย 

    “Naomba niongee na Shayo haraka” Alisema Rais, mara mojaย  Waziri Mkuu alipiga simu kwa mkuu wa kitengo cha Usalama waย  Taifa ambaye hadi kufikia wakati huo hakujuwa Faudhia alikuwaย  wapi, ni mzima au amekufa ila Faudhia alikuwa barabaraniย  kuelekea Dar kwa ajili ya kuzuia mpango wa Mzee Shomari.ย 

    Mara moja simu ya Mzee Shayo ilipokelewa na maongezi kati yaย  Mzee Shayo na Rais yalianza, Rais alisikika kwa kupoa sanaย  tofauti na mwanzo ambapo alionesha hasira sana kwa Mzee Shayoย 

    “Shayo!!” Aliita Raisย 

    “Naam Mkuu” Aliitika Mzee Shayo . ENDELEAย 

    SEHEMU YA NANEย 

    “Wewe ni Mtu pekee ambaye unaweza ukadhibiti kila kitu naย  kuleta sifa kwa Taifa hili, ruhusu Vijana wako waishambulieย  Benki sasa hivi” Alisema Rais kisha mwisho alisema kwa kukazaย  sauti tofauti na mwanzo alivyoanza.ย 

    “Mkuu, ndani ya Benki kuna Raia wasio na hatia, shambulioย  lolote lile tutakalo lifanya litasababisha madhara makubwaย  sana. Hiyo siyo suluhu ya jambo hili Mkuu, busara niย  kuhakikisha Mateka wote wanatoka salama” Alijibu Mzee Shayoย 

    “Mimi ndiye Rais wa Nchi hii nataka uamrishe walengaji wakoย  waishambulie Benki haraka iwezekanavyo” Alisema tena Rais kwaย  sauti ya kufoka huku akijuwa fika kuwa Mzee Shayo haweziย  kukubaliana na wazo hilo.

    ย ย 

    “Hilo haliwezekani Mkuu, tuvute subra kwa masaa kadhaaย  nitakuja na mpango wa nini tufanye” Alisema tena Mzee Shayoย 

    “Shayo! Narudia tena Mimi ndiye Rais wa hii Nchi, hakuna Raisย  mwingine wala amiri jeshi Mkuu. Kama utashindwa kufanya hivyoย  nitatengua uteuzi wako haraka sana” Alisema Rais kwa sautiย  ile ile ya kufokaย 

    “Mkuu siwezi kutoa amri hiyo kwa vijana wangu, hii kaziย  inahitaji…”ย 

    “Shayo siwezi kukubembeleza” Alisema Rais kisha simuย  ilikatika, Mzee Shayo alibakia akiwa njia panda, alijaribuย  tena kuipiga simu ya Faudhia lakini haikuita kabisa,ย  alijiuliza kama Faudhia atakuwa ameshakufa basi hakutokuwa naย  jambo lolote la kuzuia amri ya Rais huyo, alichoka naย  kujitupa Kitini huku akitafakari afanye kitu gani.ย 

    Mwendo wa Bakora huko Bagamoyo Road, Matilda aliendesha gariย  kama dereva wa mshindano ya Formula one, ilikuwa ni safariย  yenye matumaini, Bado Mzee Shayo aliendelea kumtafuta Faudhiaย  huku Mzee Shomari akipewa taarifa kuwa Diana alikuwaย  ameshauawa na mzigo ulikuwa umechukuliwa, taarifa hiyo ilimpaย  wazimu sana Mzee Shomari, alimpigia tena Chogo na kumwambiaย  kuwa wana chini ya masaa mawili kuhakikisha wanachomoka ndaniย  ya Benki hiyo haraka sana, wakati huo huo baada ya kumalizaย  kuongea na Chogo alipiga simu na kuagiza Helkopta isogeeย  lilipo jengo la China plaza ili aweze kuondoka baada yaย  kuhakikisha akina Chogo wanatoka salama.ย 

    Akiwa ofisini Mzee Shayo, ilikuwa ni baada ya saa moja kupitaย  aliingia Mwanaume mmoja aliyejulikana kama Samuel Dinonga,ย  alikuwa ni Mkuu wa jeshi la polisi, iliwapasa kumpa salamuย  aliyostahili kisha Dinonga alimueleza Mzee Shayo kuwa yeyeย  ndiye aliyepewa jukumu la kuongoza idara ya Usalama wa Taifaย  kwa wakati huo, Mzee Shayo alipaswa kukiacha kitengo harakaย  sana. Yalikuwa ndiyo maamuzi ya Rais, hakukuwa na namna, Mzeeย  Shayo aliacha kila kitu na kuondoka ofisini hapo.ย 

    Lengo la Rais lilikuwa ni kuishanbulia Benki hiyo bila kujaliย  kuwa kulikuwa na Gavana na Mke wake pia kilikuwa naย  wafanykazi wa Benki na wateja wa Benki hiyo ambao hawakuwa naย  hatia yoyote ile, muda huo alilielekea gari lake ili awezeย  kutimka eneo hilo la Makao makuu ya Kitengo cha Usalama waย  Taifa, alipofika ndani ya gari simu yake iliita.ย 

    Aliitilia mashaka kidogo simu hiyo sababu ilipigwa kwa nambaย  ambayo hakuifahamu kabisa, alisubiria kidogo kisha aliipokeaย 

    “Hello!” Alisema Mzee Shayo kwa umakini wa hali ya juu sana.

    “Baba!!” Alisikia sauti ya Faudhia ikimuita, hakuaminiย  masikio yake ni kama vile alisikia kitu kisichomuingiaย  akiliniย 

    “Faudhia uko wapi?” Alihoji Mzee Shayoย 

    “Nipo Barabarani nakuja huko Baba, naomba unisikilize kwaย  makini sana” Alisema Faudhiaย 

    “Ndio ndio”ย 

    “Ndani ya jengo la China plaza ndimo alipo Mkuu wa kikosiย  hicho, si mwingine ni Mzee Shomari! Chukua askari nendaย  kamdhibiti haraka sana mimi muda siyo mrefu nitakuwa Dar”ย  Alisema Faudhia kwa umakini sanaย 

    “Kwasasa mimi siyo Mkuu wa Kitengo Faudhia, sina mamlaka yaย  kuamrisha askari wa kitengo tena” Alisema Mzee Shayoย 

    “Oooh! Shit, basi jitahidi uwende mwenyewe maana ndani yaย  hicho kitengo kuna Watu wanafanya kazi ya kukwamisha juhudi”ย  Alisema Faudhiaย 

    “Sawa ngoja nisogee huko” alisema Mzee Shayo kisha simuย  ilikatika, aliangalia kwenye gari yake aliona silaha aina yaย  Bastola, hakujuwa uzito wa ulinzi wa huko ndani ya jengo laย  china plaza ila aliamini Bastola hiyo itamsaidia, aliondoaย  gari kitengo na kuelekea China plaza.ย 

    Mkuu mpya wa kitengo Bwana Dinonga alifuata maagizo ya Raisย  wa Nchi, ilikuwa ni lazima aunganishe jeshi la polisi naย  askari wa kitengo ambao walikuwa eneo la tukio kuifanya kaziย  kwa pamoja. Aliondoa idadi kubwa ya Askari pale makao makuuย  kwa ajili ya kuelekea Benki ili kuishambulia benki hiyo,ย  lengo likiwa kuuwa kila aliye ndani ya jengo hilo ili siri yaย  pesa zile iendelee kubakia wakiamini kuwa Chemba haikuwezaย  kuonekana wakati chemba ya siri ilikuwa imeshafunguliwa.ย 

    Upande wa pili, Helkopta iliyoitwa kwa ajili ya kumchukuaย  Mzee Shomari ilikuwa ikijongea taratibu kuelekea hapo, Mzeeย  Shayo naye akiwa ndani ya gari lake alikuwa akifikiria niย  jinsi gani ataweza kukabiliana na Magaidi hao ndani ya jengoย  la China plaza, safari ya kutoka Kigamboni hadi Mjini ilikuwaย  fupi tu ukizingatia hakukuwa na shughuli zozote zilizokuwaย  zikifanyika ndani ya Jiji hili la kibiashara, muda huoย  Faudhia alikuwa akiingia Dar, mwendo wao haukuwa wa kawaida,ย  walipofika Tegeta Matilda alimwambia Faudhia kuwa anahisiย  kizunguzungu kutokana na spidi ya gari aliyokuwa nayo,ย  ilimlazimu Faudhia amwambia Matilda kuwa asimamishe gariย 

    ย ย 

    haraka, Basi Matilda alifanya hivyo wakiwa maeneo ya kwaย  Ndevu – Tegetaย 

    “Pole sana, Asante pia” Alisema Faudhia, Matilda alishindwaย  hata kumjibu Faudhia alipoteza fahamu akiwa ameshikiliaย  usukani. Faudhia alishuka na kuielekea pikipiki iliyokuwaย  imesimama kando ya Barabara, aliiwasha na kuondoka eneo hilo.ย 

    Ukimya ulikuwa mkubwa sana alipofika maeneo ya Mnazi mmoja,ย  alilazimika kushuka na kutembea kwa mguu kuelekea Chinaย  plaza, japo alikuwa Mzee lakini hakusahau mbinu zakeย  zilizompa umaarufu miaka ya 90, Mzee Shayo alikuwa ni zaidiย  ya komando wa vita, alisogea kwa kasi ya ajabu kwa kutumiaย  njia za ndani kama anaelekea Shimoni kariakoo, alijuwa fikaย  kuwa kama ni kweli magaidi hapo ndipo walipoweka kambi yaoย  basi ulinzi wake utakuwa mkubwa sana. Alikuwa ndani ya sutiย  ya kijivu iliyomkaa vizuri, alivua koti akabakiwa na shatiย  jeupe litakaloweza kumpa urahisi wa kuifanya kazi yake.ย  Alikuwa akitembea huku akiangalia saa yake aliyoweka mudaย  maalum wa kufika eneo husika kabla kitengo cha Usalama waย  Taifa hakijashambulia Benki na kuuwa Watu wasio na hatia,ย  alikuwa na nusu saa tuu iliyobakia, muda huu alikuwaย  ameshazunguka hadi Msimbazi polisi, alikuwa sasa eneo laย  Msikiti wa Shekh Idrisa, alikuwa makini kuliko wakati wowoteย  katika Maisha yake, alijuwa hiyo ndiyo nafasi pekee naย  pengine ingelikuwa kazi yake ya mwisho kutokana na umri wakeย  na pia kuondolewa kwake kwenye kitengo na Rais.ย 

    Kwa mbali asikia sauti ya Helkopta ambayo ilikuwa ikielekeaย  China plaza kwa ajili ya kumchukua Mzee Shomari, muda huoย  Faudhia alikuwa ameshafika upanga kwenye msikiti wa Maamurย  ili kuingia kwenye hiyo chemba itakayotumika kutorosha pesaย  kutoka Benki kuu. Alipofika hapo aliona Watu watatu wenyeย  asili ya kiarabu wakiwa wamekaa kwa nje, aliwatazama kwaย  jicho la kijasusi aligundua Watu hao ambao ni wanaumeย  walikuwa na silaha walizozificha kwenye viuno vyao, Faudhiaย  alifikiria atumie njia gani kufika pale, alifikiria kwa zaidiย  ya dakika mbili huku ile presha kuwa muda unaisha ilizidiย  kumjaa aliona ni bora aamuwe kufanya kitu kimoja.ย 

    Alisogea hadi kwenye ukuta kimya kimya pasipo wale Wanaumeย  kushtuka huku wanaume hao wakionekana kusoma vitabu ya dini,ย  alijuwa ulikuwa mtego ili watu wasishtuke chochote, alionaย  pia baadhi ya Watu wakitoka na kuingia Msikitini hapo,ย  ilikuwa ngumu kwake kujuwa kuwa Watu hao walikuwa wema auย  maadui. Pembezoni aliona nguo zilizokuwa zinetundikwa naย  zilikuwa ni za kiume, haraka Faudhia alizichukua na kuzivaa.

    Alihakikisha anaonekana kama Mwanaume, na kweli alifanikiwaย  kwenye hilo, alivuta pumzi zake ili kujiondoa wasiwasi kishaย  aliitoa bastola aliyoichukua baada ya kumuuwa Diana,ย  aliangalia Bastola hiyo yenye risasi tatu pekee alionaย  isingeliweza kumfaa ila ingelimsaidia kwa kiasi fulani,ย  aliiweka sawa Bastola yake kisha aliingia barabara ya lamiย  akawa anasogea, Wale Wanaume walipomuona Faudhia walionekanaย  kumkagua kwa kutumia macho yao yaliyojaa wizi hukuย  wakijifanya wengine kusoma na mwingine kuchezea tasbihi.ย  Walipeana isharaka kisha mmoja akaingia ndani wawiliย  wakabakia pale, Faudhia alisogea hadi lango la Msikiti.ย  Mwanaume mmoja aliyekaa alimsalia Faudhia kwa Salam yaย  Kiislamย 

    “Asalaam Alaykum?” Alisalimia huku akimtazama Faudhia ambayeย  alikuwa amevalia kiremba na kuificha sura yake kwa kuangaliaย  pembeni, yule Mwanaume alimsalimia tena Faudhiaย 

    “Asalam Alaykum Shekh” Alisalimia bila wasiwasi, Faudhiaย  alihema sana akijuwa kuwa jamaa huyu alikuwa ameshamshtukia,ย  kisha Mwanaume huyo aliinuka na kumsogelea Faudhia ambayeย  hakutaka kuonesha sura yake.ย 

    Sura ya Mwanaume huyo ilianza kubadilika na kuwa ya hasira,ย  alikuwa tayari ameshamtilia Mashaka Faudhia. Alizidi kusogeaย  kisha alimuuliza Faudhiaย 

    “Wewe ni nani?” Aliuliza kwa rafudhi ambayo ilionesha waziย  kuwa Mwanaume huyo alijifunza kiswahili siku si nyingi,ย  mapigo ya moyo ya Faudhia yalizidi kwenda mbio. Yule Mwanaumeย  akawa anasogea kuitazama sura ya Faudhia, endapo atagunduaย  kuwa Faudhia si Mwanaume itakuwa shida kwa Faudhiaย 

    Yule Mwanaume alisogeza mkono ili amshike Faudhia amgeuze,ย  Faudhia alifumba macho yake kuwa asingeliweza kufurukutaย  hapo, ghafla kabla hata hajamgusa Faudhia liliingia gari laย  kubebea maiti lililoleta maiti kwa ajili ya kuswaliwa.ย  Purukushani za watu zikawa nyingi na kwakuwa walisimamaย  katikati ya lango iliwapasa kulipisha gari hilo, Faudhiaย  alibakia upande wa kulia na yule Mwanaume alirudi upande waย  kushoto kisha gari ikapita katikati yao. Fumba na kufumbuaย  Macho yule Mwanaume aligundua kuwa Faudhia ameshatoweka pale,ย  haraka alipiga simu kwa wenzake kuwa eneo hilo si salamaย  tena, aliwavuka Watu na kuelekea kwenye mlango wa kuzidiย  kuzama ndani ya Msikiti huo.ย 

    Naam!! Sasa, Mzee Shayo alikuwa ameshafika chini ya Jengo laย  China plaza, jengo hilo lilikuwa refu lenye vioo, Mzee Shayoย  alipochungulia kwa mbele aliona kuna Watu waliokuwaย 

    wamesimama pembezoni, alijuwa tu Watu hao siyo watu salamaย  kwake, muda huo Helkopta ilikuwa hewani juu ya Ghorofa hilo,ย  alijuwa ndiyo wakati sahihi wa kuanza kukiwasha ili kuzuiaย  Mzee huyo asitoweke eneo la tukio. Haraka alisogea mbele yaย  jengo, alimvizia mlinzi wakwanza kisha alimnyonga kwa kutumiaย  kamba ya kiatu chake, alimvuta hadi mahali ambako kulikuwa naย  jenereta kubwa la kuzalisha umeme, huyu wa pili alikuwaย  amempa mgongo Mzee Shayo hivyo ilikuwa ni rahisi kumalizanaย  naye, alimpiga kiwiko eneo la shingo, alifanya kimya kimyaย  kisha alimvuta na kumsogeza pembeni, alihakikisha anawasachiย  na kuchukua silaha zao. Alikuwa ni Mtu makini sana ambayeย  aliijuwa thamani ya kazi aliyokuwa akiifanya, alisogea hadiย  mlango wa kuingilia, jengo lilikuwa kimya sana na hakukuwa naย  dalili kuwa Kulikuwa na mitembeo ya Mtu zaidi ya sauti yaย  Helkopta iliyokuwa juu ya Jengo, humo ndani Mzee Shomariย  alidhamiria kuhakikisha kuwa anachukua kila kitu kabla yaย  kutimka, alichotaka ni kuhakikisha Chogo anatoroka na pesaย  hizo ndani ya benki kwanza kabla yeye hajaondoka sababuย  alishajuwa ni wapi watakutana kwa ajili ya kugawana kiasiย  hichoย 

    Alimpigia Chogo na kumwambia kuwa ni muda wa kuondoka, upandeย  huo wa Benki tayari Chogo alikuwa na kiasi hicho cha pesaย  ndani ya mabegi kilichobakia kilikuwa ni kuondoka tuu,ย  aliwaambia vijana wake kuwaย 

    “Tunaenda kuwa Mamilionea leo” Alisema Chogo kwa tabasamu,ย  aliamuru waifuate Chemba kwa ajili ya kuondoka, tayariย  alikuwa ameshawaweka vijana huko wakawa wanachimba naย  kuunganisha chemba hiyo ambayo hadi kufikia muda huo ilikuwaย  tayari kilichobakia kilikuwa wao kuondoka tuu. Alipofikaย  kwenye Korido alikumbuka kuna kitu amesahau kisha aliwaambiaย  vijana wake kuwa wamsumbirie kwenye chemba, Chogo aliendaย  kwenye Chumba ambacho alimuacha Selina. Huwezi amini Chogoย  alikuwa ameshampenda Selina, alipofika alimtazama Selinaย  ambaye alikuwa analia akiwa amekaa juu ya meza, chogo alijawaย  na huruma huku simu yake ikiwa inazidi kuita, alikuwa ni Mzeeย  Shomari ndiye aliyekuwa akimpigia simu.ย 

    Upande mwingine ndani ya Msikitini, Mtafutano ulikuwa mkubwaย  mno, Faudhia aliijuwa ramani ya ilipo chemba hiyo yaย  utoroshwaji wa pesa ndani ya Benki, alijificha mahali ambapoย  aliamini ingelikuwa rahisi kuwaona Wanaume hao, wanaumeย  walipofika ndani waliufunga mlango huo ili kisisikikeย  chochote kutokea humo na kwenda kule Msikitini ambakoย  kulikuwa na harakati za kuanza ibada ya kuisalia Maiti.ย 

    Walifunga viwanbo vya kuzuia sauti kwenye Bastola zao iliย  kuhakikisha hakuna kitakachosikika ili wasije haribu mpangoย wao. Faudhia alikuwa kwenye moja ya vyumba ambavyo vilikuwaย  ndani ya Eneo hilo, wale wanaume waligawana Majukumu yaย  kumsaka Faudhia.ย 

    Chumba alichojificha Faudhia kilikuwa kina dirisha la Kiooย  hivyo ilimpa urahisi wa kuona na kuonwa pia endapo adui yakeย  atatazama kwenye kioo, mlango ulitekenywa huku Faudhia akiwaย  amjibanza ukutani, bastola yake ilikuwa kiunoni sababuย  aliamini matumizi ya Bastola yangelimfanya agundulike. Waleย  magaidi waliambiana kuwa wanapaswa kuingia kwa pamoja kwenyeย  vyumba na kutoka pamoja hivyo endapo mmoja hatotoka basiย  chumba hicho ndicho ambacho adui yao atakuwa yumo.ย 

    Wakati kitasa kinatekenywa, Faudhia aliona Upanga kwenye konaย  ya Chumba hicho, aliuchukua taratibu bila kupiga kelele yaย  aina yoyote ile, alijiweka sana huku kioo kikiwa ndio msaadaย  pekee kwake, yule Mwanaume alivyotokeza kichwa alikutana naย  upanga ambao ulizama kichwani, haraka Faudhia alimvutaย  Mwanaume huyo ndani kisha alichukua Bastola ya Mwanaume huyoย  alafu akasikia sauti ya kwanza ikisemaย 

    “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba kingineย  ikisemaย 

    “Safi” wakimaanisha kuwa vyumba vyao vipo salama hapo ndipoย  Faudhia aliposhtuka kuwa anapaswa kuwa nje ya chumba harakaย  sana ili awawahi Wanaume hao, alifanya hivyo upesi sana hukuย  akiwa ameelekeza Bastola yake mbele mahali ambako sauti hizoย  zilitoka, wale wanaume hawakuisikia sauti ya tatu ya mwenzaoย  ndipo walipotoka nje haraka ila walikuwa wamechelewa,ย  walikutana na mishale ya risasi kutoka kwa Faudhia, Msichanaย  kutoka Mbeya, aliwamaliza kimya kimya bila kusikika popoteย  sababu bastola ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti .ย 

    Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA TISA

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย 

    riwaya mpya Riwaya ya Goryanah riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni soma riwaya bure

    7 Comments

    1. Joyx Son on June 6, 2025 3:53 pm

      Thanks alot kijiwen
      But mnafanya niunge megabyte zangu always ili tyu kupata hii zaid ya story
      Kubali Sanaa faudhia people ya green city

      Reply
    2. bayser on June 6, 2025 4:25 pm

      hatarii
      hizi ndio tunataka sio za kichawi usiku hatulali

      Reply
    3. Bad hunter on June 6, 2025 6:38 pm

      Hatar sqna kiongozi

      Reply
    4. Alex on June 6, 2025 7:48 pm

      Iko pw ila inachelewa sana kupostiwa tupia inayofuata

      Reply
    5. Adam on June 6, 2025 8:24 pm

      Story Nzuri Saana Ila Tunaomba Jaman Mnazichelewesha Saana Ni Inasisimua Saana Hiii

      Reply
    6. Yamungu.E.Dawson on June 6, 2025 11:05 pm

      Daaah!! nzuri saaana, sehemu ya 9 tafadhari naisubiria kwa hamu.

      Reply
    7. ๐Ÿ“ˆ Notification- TRANSFER 1,664974 BTC. Withdraw >>> https://yandex.com/poll/5JjqQt7R61CTYdYVd17t6p?hs=bac62aedd0772e8da1c8374dc3ec040f& ๐Ÿ“ˆ on June 7, 2025 5:13 am

      f8qmc5

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 6, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya sabaย  “Naomba niongee na Shayo haraka” Alisema Rais, mara…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.