Ilipoishia
Kwanza nilijiuliza ni Nani anayeweza kuja kwetu, kama Mama Amida tayari tulishazungumza. Nilimeza funda zito la mate Kisha nilitembea taratibu kuelekea Mlangoni bila hata kutoa sauti yangu.
Nilisikiliza kusikia sauti lakini palikua kimya sana, sikutoa sauti ya kumkaribisha. Nilisubiria Hadi alipogonga tena ndipo nilipomuuliza yeye ni Nani?
Hakujibu, niliamua kufungua mlango kwa nguvu. Nilikutana na yule Mwanaume mmoja anayefunga macho yake kwa kutumia kitambaa chekundu, kwa namna alivyo ikitokea Watu wamemwona basi wangenitilia shaka, nikamvuta ndani Kisha nikafunga mlango.
Hukusoma SEHEMU ZILIZOPITA? Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI , SEHEMU YA TATU , SEHEMU YA NNE , SEHEMU YA TANO , SEHEMU YA SITA, SEHEMU YA SABA , SEHEMUYA NANE Kisha Endelea
SEHEMU YA TISA
Nikamuuliza aliwezaje kufika ninapoishi? Yeye hakua mzungumzaji sana akanijibu kua ameagizwa na Mkuu anipatie ujumbe, nilishtuka sana huku nikijiuliza haraka haraka kua alikua amepewa ujumbe gani na huyo anayemwita Mkuu?
Akaniambia kua ninaitwa kwa ajili ya kupewa kazi ya kuifanya, moyo ulidunda kwa Kasi sana. Macho yangu yalining’inia kwa Mshangao
“Siwezi kuja huko kwasababu siwaelewi, naomba mniache na Maisha yangu” nilipaza sauti yangu kwa Msistizo, kiukweli sikuhitaji kufanya chochote kile ambacho kilitokana na Ushetani
“Kama ni Pete yenu niwapatie, mtaitoa kwa Mtu mwingine. Nahitaji kuishi Maisha ya kawaida sasa” nilisema, Kisha yule Mtu naye akanijibu kwa haraka kua
“Hauwezi kuvunja Mkataba uliouingia Malkia, wewe ni Mtumishi. Unasubiriwa Kuzimu” alisema Kisha akapotea katika mazingira ya kutatanisha.
Nilianza kulia kwa Uchungu sana, nilijiona nimeingia kwenye kifungo Cha Maisha yangu.
Kilio changu kilikua na maana kubwa sana, nilimuuliza Mungu wangu ni kwanini aliniumba kua Mwanamke anayeitwa Saida? Kama ningelizaliwa
Mwanaume nisingeliingia kwenye hekaheka hizi. Chozi lilibubujika mashavuni mwangu Hadi kwenye nguo niliyoivaa
Japo kulia haikua njia ya kuniokoa lakini angalau niliweza kupunguza maumivu ya Moyo Wangu, niliponyamaza kulia niliukumbuka huo wito wa Kuzimu
Nilifuta chozi langu Kisha nilijisemea kua nataka kwenda Kuzimu, popote nilipohitaji kufika nilifika ndani ya sekunde Moja tu. Kufumba macho na kufumbua nilijikuta ndani ya kile chumba Chenye kiti, yaani kule kwenye Mji wa Kuzimu ambako kwa mara ya kwanza nilipewa nguvu za ajabu
Tena siyo tu kua kwenye kile chumba Bali nilikua nimekalia kiti Cha Kuzimu, mavazi yangu yakiwa yamebadilika kabisa.
“Karibu Saida, umefika sasa” niliisikia ile sauti nzito ikinikaribisha. Sikuiogopa tena kama zamani. Sikusema chochote kile sababu moyo Wangu haukuridhia
“Saida, nimekuita hapa sababu nataka uifanye kazi Moja” ilisema ile sauti, niliweka umakini nikauliza
“Kazi gani?” Ile sauti iliangua Kicheko, Kisha ikaniambia “Nahitaji kafara ya Damu ili kukusimika wewe zaidi” ilisema.
“Unasemaje?” nilimuuliza kwa mshituko mkubwa sana, hakuna kafara bila Mauwaji.
“Ndiyo, mtaji wetu ni Damu. Kwakua wewe ndiye Malkia basi unapaswa kuileta Damu hapa” ilisema sauti hiyo, Kila kilichosemwa kulinifanya nishtuke na kutetemeka.
“Kwahiyo kukutumikia wewe ni Kuuwa Watu?” niliuliza huku nikiruhusu funda zito la mate kupita kooni kwangu.
“Utaelekezwa nini Cha Kufanya kwa kafara Yako ya kwanza” ilisema sauti Kisha ukimya ulitawala, niliishiwa Cha kuuliza wala Cha kusema huku chozi likinibubujika.
Midomo yangu ilikua ikitetemeka tu. Mara aliingia yule Mwanaume anayefunga macho yake kwa kitambaa Kisha akaniambia
“Kwa kafara ya kwanza unapaswa kuifanya kwa udogo, taratibu itapanda kadili siku zinavyozidi kwenda mbele.”
“Hata wewe sikuelewi unasema nini, mnataka Damu?”
“Ndiyo Malkia, ni muhimu kwa ajili Yako” alisema, mara zote yeye anasema kwa heshima sana kwangu. Nilishuka kutoka kwenye kiti Kisha nikamwambia
“Kamwe siwezi kushiriki Upumbavu wenu” niliivua ile Pete Kisha nikampatia.
“Nahitaji kua huru na Maisha yangu, siwezi kua muuwaji Mimi” nilisema lakini kabla sijapiga hatua akaniambia
“Malkia, umesha saini Mkataba wa Damu. Unapaswa kuutumikia sababu kama hautafanya hivyo hautaweza kuondoka hapa Kuzimu. Hii Pete ni ufunguo pekee unaouhitaji” alisema. Haraka niliipora ile Pete nikaivaa
Sikutaka kuishia kuzimu. Katikati ya Wasiwasi wangu niliona Kuna njia ngumu ambayo ni lazima niipite ili Nije kuupata uhuru wangu.
“Nifuate nitakusaidia kutimiza kafara Yako ya kwanza” alisema Kisha aligeuka na kuanza kupiga hatua kuelekea nje ya kile chumba. Nikajishauri lakini jibu nililolipata ni kumfuata yule Mtu, nilimfuata tulikatiza korido, Kisha tukaingia chumba kingine
Akaniambia “Ndani ya hiki chumba Kuna mlango kati ya Kuzimu na Ulimwengu wa kawaida. Nitakuonesha Cha kufanya Malkia ili utimize kafara” alisema yule Mtu, chumba kilikua kitupu. Hakikua na dirisha wala mlango ambao yeye alisema
Niliona ilikua ni Hadithi ya Abunuasi, nilipumua vizuri nikameza na mate ya utuo. Akasogea mbele, macho yangu yalikua makini kumtazama
Katikati ya Kuta ukatokea mlango, nilistaajabu sana. Akaufungua, ndipo nilipoona alichokisema, Ulimwengu wa kawaida ulikua tulivu sana tena ukiwa bize bila kujua kua kulikua na Ulimwengu mwingine wa Giza.
“Unayaona Yale Maisha? Sisi tunautawala ule Ulimwengu kupitia huu mlango wa Siri, kupitia huu mlango unaweza kufanya chochote kile.”
“Unamaamisha nini?” nilimuuliza huku ndita zangu zikiwa zimesimama vizuri.
“Kafara Yako ndogo ni Damu za Watoto wachanga wenye siku Moja. Unapaswa Kuuwa Watoto 66” alisema yule Mtu, mwili ulisisimka sana.
“Kuuwa Watoto wachanga?” niliuliza, Mimi Saida nilipewa Mtihani wa kwanza mzito sana.
“Ndiyo, ni idadi ndogo sana kwa kuanzia.”
“Washenzi wakubwa nyiyi, mnaleta majanga na balaa Duniani kwasababu ya hicho mnachokiita nguvu za Kishetani si Ndiyo?” Nilisema kwa ukali sana.
Akanigeukia akaniambia
“Unaweza kukutana tena na Wazazi wako, ukawarudisha wakawa hai endapo utashirikiana nasi Saida”Alisema, maneno yake ni kama yaliuyong’onyeza moyo Wangu.
Kukutana na Wazazi wangu haikua kitu rahisi kufikiria lakini yule Mtu alisema kwa kinywa chake.
Chozi lilianza kunibubujika, nilikua nimeambiwa kitu kilichonipa Hali ya huzuni sana. Yule Mtu aliondoka pale chumbani akiniacha Mimi nikiwa ninalia kwa Uchungu sana. Nilifikiria juu ya nini nataka na ambacho wao wanataka.
Nikikubali nitawaona tena Wazazi wangu lakini nikikataa nitaishi Kuzimu Maisha yangu yote. Nilikua njia panda nisijuwe napaswa kuchagua nini
Maisha ya Watu wengine yalikua muhimu, furaha zao zilikua na maana lakini upande Wangu nilikua nimepoteza Kila kitu, hata kidogo kilichobakia Bado nilipaswa kukilinda kwa kafara ya Damu za Watoto wachanga
***
Nilirudi Duniani, nilipofika nyumbani niliwaza sana. Upande mmoja uliniambia kua kumtumikia shetani ni Maisha yasiyo na maana lakini upande mwingine uliniambia kua napaswa kumwona Mama yangu ili anione nikiwa ninaongea tena.
Roho iliniuma sana, Kila chaguo liliumiza Maisha ya Mtu. Kila hatua ilikua unaenda kuweka kovu kwenye Maisha ya wengine.
Siku zilienda, Kila nilipokua ninalala niliota ndoto za Kutisha sana. Mama yangu alikua akinitokea Kila mara na kunilaumu kutokana na kifo chake, alinitaja Mimi kama sababu.
Nilishindwa kuelewa namna Maisha yangu mapya yalivyobeba maumivu baridi lakini yanayochoma sana.
Siku Moja asubuhi, baada ya kuamka na kujinyoosha. Ilikua kama mishale ya Saa tatu asubuhi, ni wiki mbili baada ya kutoka Kuzimu nikiishi Maisha ya kawaida kabisa peke yangu.
Nilihisi Uchovu Fulani wa kuamka lakini nilianza kusikia sauti nisizozielewa. Sauti zile zilikua zikiongea na kucheka kwa furaha sana. Nilishtuka, nikazisikiliza vizuri na kugundua zilikua zinatokea sebuleni
Mapigo ya Moyo Wangu yalinienda mbio sana. Nilizidi kupagawa baada ya kuzitambua sauti zile, Moja ilikua ya Marehemu Baba yangu na nyingine ilikua ya Marehemu Mama yangu
“Mungu wangu, hawa si Wazazi wangu?” nilijiuliza kwa sauti kuu iliyotoka ndani ya uvungu wa moyo Wangu huku chozi likianza kuchoma macho yangu, Wazazi wangu walikua wamefariki ingewezekana vipi nikawasikia tena?
Basi nilijitoa kitandani taratibu, miguu yangu ikagusa sakafu Kisha safari ya kuelekea Sebuleni ilianza taratibu, kadili nilivyokua natembea ndivyo ambavyo zile sauti zilizidi kua karibu na masikio yangu
Nilitembea kwenye korido pole pole tena kwa hofu sana, nilihisi kama ilikua ndoto lakini haikua hivyo. Nilipoimaliza korido nilikutana na Macho ya Mama yangu yakinitazama, Ndiyo alikua ameniona
Nilisimama kwa Mshangao, Mama alikua ameshikilia chupa ya chai, huku Baba yangu akinywa chai akiwa ameketi kwenye kochi lake pendwa ambalo tulilipa jina la ‘Kochi la Baba’ kwasababu alikua akilipendelea sana kochi Hilo.
“Saida, nilikuacha Upumzike Mwanangu. Njoo” alisema Mama kwa sauti ya furaha iliyosindikizwa na tabasamu. Moyo Wangu ulifanya kama vile unasimama kwa sekunde chache Kisha ukawaka na kuanza kudunda kwa Kasi ya ajabu sana.
Mama alinitazama kisha alianza kuandaa chai Mezani, nilikua nimepigwa na Mshangao wa aina yake. Basi nilisogea taratibu huku nikijiuliza kama nilichokua nakiona na kukisikia kilikua kweli, Baba alinitazama kidogo akapiga chai kidogo halafu akaniambia
“Umeamkaje?” Sikujua hata nijibu nini.
“Saida, mbona umekua kama zuzu vile? Si unasemeshwa na Baba Yako?” Mama alikaza sauti kidogo, hii ilikua ni Tabia halisi ya Mama yangu, anakuchekea kidogo halafu anakua mkali ila Baba yangu huwa mpole wakati wote
Nilimeza funda zito la mate nisijuwe napaswa kujibu nini mbele Yao, Kwa namna nilivyoulizwa na Baba na jinsi Mama alivyokaza sauti ilinipa ishara kua Walikua nyuma ya Muda na pengine walikua wanajua ninazungumza
“Saida una nini?”aliuliza Baba, nikaona sasa ni muda wa kutoa sauti yangu mbele Yao.
“Hakuna Baba, samahani. Shikamoo” nilimsalimia, basi Baba alitabasamu Kisha akanijibu
“Marahaba Binti yangu. Za siku?” hili swali lilinipa wasiwasi ndani yangu, kwanini aniulize za siku Ina maana kati yangu au wao Kuna upande haukuwa nyumbani, itakua ni wao maana Mimi kwa wiki mbili nipo nyumbani
“Salama Baba”
“Kwahiyo Mimi kunisalimia unaona hasara, wewe Mtoto?” alisema Mama, ilibidi nitabasamu katikati ya Giza nene la maswali mazito yasiyo na Majibu
“Samahani Mama, nilikua na wenge la Usingizi” nilijibu huku nikitabasamu kuwaondoa hofu, sikujua walirudi vipi Maishani mwangu
Kabla hata sijamsalimia Mama, Mlango uligongwa. Sote tulitazamana huku Kila mmoja akijiuliza ni Nani ataikikia wito huo hapo mlangoni, kwakua Mimi ndiye Mtoto basi nilielekea mlangoni
Nilipofungua mlango nilikutana na Mtu aliyeushitua Moyo Wangu. Mtu huyo alinifanya nigeuke kuwatazama Wazazi wangu….
Nini kitaendelea kwenye Maisha ya Saida?
USIKOSE SEASON 3.
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

