Ilipoishia
“Nani ananiita?” niliuliza kwa Ujasiri sana japo kwa ndani nilikua mwoga lakini sikuruhusu yule Mtu anielewe, nilimkazia macho yangu huku nikichezesha Mguu mmoja.
“Bosi”
“Bosi?”
“Ndiyo”
Nilitazama huku na kule Kisha nikamwambia
“Sawa” Nilisema tu lakini nilikua naogopa sana. Tayari hatma ya Veronica ilitimia, kilichobakia kilikua ni Mimi kulipa Hilo deni ambalo niliambiwa ninadaiwa. Akili yangu iliniambia ni Bora niende hata kama nitateseka na kufia huko.
Hukusoma SEHEMU ZILIZOPITA? Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI , SEHEMU YA TATU , SEHEMU YA NNE , SEHEMU YA TANO Kisha Endelea
SEHEMU YA SITA
Yule Jamaa alitangulia Kisha Mimi nikawa namfuata kwa nyuma. Hakuna hata Mtu mmoja aliyekua akituangalia, tulitembea taratibu sababu kutoka kwa Mama Ashura Hadi nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu siyo mbali, ni mwendo wa hatua kadhaa tu.
Kila hatua niliyoipiga ilikua na maana kwangu, ilinikumbusha wakati ambao nilikua mtumwa ndani ya Nyumba hiyo iliyojaa Siri kubwa, chozi lilikua likinilenga nikizidi kuikumbuka ile siku ambayo niliagizwa vitafunwa kwa Mama Ashura, nilitamani kukimbia ile siku lakini Mzee Mwinyimkuu alinitishia kua angeuwa Wazazi wangu.
Leo ninarudi tena kwa kupiga hatua zile zile lakini hakuna Cha kunitishia tena sababu sina Wazazi wote wawili. Tuliipita ile gari Hadi tukafika getini, akafungua geti kidogo Kisha tukaingia ndani ya Nyumba hiyo.
“Karibu” alisema yule Jamaa alinionesha kwa ishara kua niingie kwenye korido, haikua Sehemu ngeni kwangu. Korido hiyo ilikua na Siri nyingi kuhusu Maisha yangu, mateso na ukatili mkubwa ulioambatana na woga na vitisho. Siwezi kuisahau korido hiyo ambayo Kaka Hamidu aliuawa kikatili sana.
Nilimtazama, sura yake ilionesha tababasamu mbele yangu, nilijiuliza maswali mengi sana lakini sikusita kunyanyua Mguu wangu kuelekea ndani. Nilizifuata hatua za yule jamaa Hadi sebuleni, Kila kitu hakikubadilika kwa Miaka yote mitano
Licha ya kupita muda mrefu sana lakini mazingira yalikua Yale Yale. Nilivuta pumzi zangu niliangaza huku na kule Kisha niliyatupa macho yangu mbele, mwili ulisisimka sana. Nilimwona Salehe akiwa ameketi kwenye kochi, nikamtambua sasa kua ndiye aliyeagiza Mimi niletwe pale maana alivalia vile vile kama yule Mtu aliyekua akitoa maelekezo ya Mimi kufuatwa kule kwa Mama Ashura.
Nilimeza funda zito la mate, hasira iliniingia moyoni mwangu. Chanzo Cha Maisha yangu kuharibika alikua ni yeye Salehe aliyeniowa na kunileta huku Rukwa Kisha kunitelekeza. Chozi lilibakia kidogo kudondoka lakini nililizuia Kisha nikajifanya kama vile sikuumizwa na chochote.
Kando yake alikua amekaa Mzee Mwinyimkuu lakini kwa haraka niligundua alikua Mgonjwa maana miguu yake ilikua imevimba, halafu alikua amepooza mwili wake maana alikaa kama zezeta Fulani hivi.
“Nimefika” nilisema baada ya kitambo Cha kuwatazama, kwa namna nilivyoletwa pale nilikua na uhakika kua hawakuhitaji kunitesa Bali kunifanya nilipe deni, nilitaka kulijua Hilo deni ninalodaiwa ikiwa Mimi ndiye niliyeumizwa na wao Miaka mitano iliyopita.
“Saida, hebu kaa” alisema Salehe, hakulisahau jina langu. Nilimeza tena funda zito la mate, alikua akiniangalia kwa kuvizia vizia sana. Basi nikasogea nikaketi kochi jingine kando Yao, sura yangu ilikua kavu sana.
Palikua kimya, Mzee Mwinyimkuu alikua akitokwa na udenda, kwa namna alivyo asingeliweza tena kua Mtu katili kwangu, nilimtazama Salehe, nilikua na maswali mengi sana ya kumuuliza lakini nilichagua kukaa kimya.
“Saida” aliita Salehe, alinitazama Usoni. Sikukwepesha macho yangu, nilimkazia macho pia.
“Unaweza ukajiuliza maswali mengi kuhusu Mimi, kuhusu Mzee Mwinyimkuu.” Alisema kwa sauti ya taratibu sana kitu ambacho kiliniudhi, sikuweza kuvumilia kusubiria atasema nini
“Yote siyo muhimu kuyafahamu, nataka kujua kwanini nipo hapa Salehe” nilisema kwa hasira huku nikishindwa kuzuia hisia ya kulia, uwepo wa Salehe mbele yangu ilikua ni kama nimetoneshwa kidonda kilichokua kimeanza kupona. Kama siyo Salehe pengine ningelikua nimeolewa na Mwanaume mwingine sahihi kwangu, hata Wazazi wangu wangelikua hai Hadi Leo, nisingepoteza niwapendao, nisingepoteza vidole vyangu ya Miguuni.
Midomo yangu ilikua ikitetemeka sana, chozi lilinidondoka nikiendelea kumtazama Salehe kwa hasira, nilitamani nimvamie nimpige lakini sikuweza.
“Najua unavyojisikia Saida, hata kama ningelikua Mimi ningelijisikia kama wewe. Nina uhakika uliupata Ujumbe wangu ambao ulikuja juu chini kwako” alisema, nilijiuliza ni Ujumbe gani aliokua akiuzungumzia. Nilimeza funda zito la mate, hasira ilinizuia kuongea chochote kile.
“Nilikutumia Ujumbe kua sijamalizana na wewe, ninakudai. Lakini ujumbe huu ulikua unasomeka kua wewe Ndiyo hujamalizana na sisi, unatudai.” Alisema Salehe. Nilishtuka, badala ya wao kunidai Mimi kumbe Mimi ndiye niliyekua nawadai, nilijiuliza kwa Mshangao nilikua nawadai kitu gani? Kama ni Mimi nawadai nilipaswa Mimi kuwakosesha wao amani na siyo wao kunikosesha Mimi amani.
“Unasemaje wewe Mshenzi?” nilimuuliza Salehe kwa hasira, Hali ya woga iliondoka kabisa Maishani Mwangu hasa wakati huu ambao niliona Sina Cha kupoteza tena maana yote niliyo yahofia yalitokea Maishani mwangu.
Salehe akamgeukia Mzee Mwinyimkuu aliyekua akitokwa na udenda, Kisha Mzee huyo akanyanyua shingo yake kama zombi akanitazama usoni, Kisha akatikisa kichwa chake. Kumbe mkono wake mmoja ulikua na nguvu, akauingiza Mfukoni Kisha akatoa Pete akampatia Salehe.
Salehe baada ya kuipokea Pete akaichezea kidogo mkononi halafu akaniambia.
“Hii Pete ni thamani ya deni unalotudai, tuliharibu Maisha Yako Saida” alisema Salehe Kisha akanyoosha mkono wake ili kunipatia ile Pete yenye rangi ya bluu bahari. Sikutaka kuipokea, nikasimama Kisha nikamwambia
“Kumbe mnajua kua mliharibu Maisha yangu, kama mliweza kujutia ni kwanini mnaharibu Maisha ya yule Msichana kule jikoni? Hamjatubu kiukweli, basi Laana iwe nanyi” nilisema kwa hasira Kisha niliondoka ndani ya ile nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Nilipofika nje nilijiuliza nitawezaje kupata pesa ya Nauli ya kurudi Dar, nilitembea haraka haraka nikaondoka kabisa pale Kisha nikasogea Hadi Mjini kabisa.
Niliulizia ilipo Stendi ya Mabasi nikaelekezwa, nilipofika niliona Mabasi mengi. Nikaulizia kama naweza pata basi la Usiku la kuelekea Dar, bahati nzuri nilipata. Sasa kilichokua kimebakia ni Nauli, nikakumbuka kua Nina simu yangu
Nikazunguka pale Stendi kutafuta mteja, bahati nzuri nilipata mteja, nikaiuza nikapata pesa ya kunitosha. Nikarudi ofisi ya basi nikakata tiketi ya kurudi Dar, nilishusha pumzi zangu nikapata nafasi ya kutafuta chakula. Jioni ilikua inaingia, walau yalibakia masaa machache kuianza safari.
Nilisubiria Hadi muda wa kuingia kwenye basi ulipofika, niliingia kwenye basi kama abiria wengine Kisha Niliketi kwenye siti yangu. Nilijitupa Kama mzigo, Maisha yangu yalizongwa na mambo mengi yenye utata. Angalau nilikua ninaweza kuhema kidogo.
Giza lilianza kuingia kwa Kasi, Basi lilijaa Kisha safari ya kutoka Rukwa kuelekea Dar-es-salaam ilianza. Sikuyaamini macho yangu kua nilikua nimepona kwenye mkasa mpya tena bila kuumia popote pale, lakini sikuacha kufikiria kuhusu ile Pete ambayo Salehe alitaka kunipatia.
“Ile Pete Ina maana gani? Lakini siyo muhimu kwangu” nilisema huku nikijitanua vizuri maana siti niliyoketi kando palikua patupu hapakua na abiria wa jirani.
Basi lilitembea kwa muda mrefu kiasi kwamba nilianza kuhisi Usingizi ulikua ukinitongoza taratibu, sikuweza kabisa kupingana nao nikajikuta nikilegeza macho yangu. Hatimaye Usingizi ulichukua nafasi kubwa
Safari ilikua ikiendelea, baadaye nilianza kupata ndoto Moja. Ndoto hiyo ilianza pole pole kama picha isiyoonekana vizuri lakini baadaye niliiyona taswira ya Mtu akiketi kando yangu pale pale kwenye basi, Bado ilikua ndoto kwa Upande Wangu nikiwa Usingizini.
Mtu yule alikua Bibi kizee mmoja anayetembea kwa Usaidizi wa fimbo. Nilimtazama kwa sekunde chache Hadi alipoketi Kisha nilimsalimia, hakuitikia kwa haraka ila akaniuliza baadaye
“Kwanini unakimbia Binti?” Nilishtuka kidogo, nikamuuliza
“Mimi?” Niliuliza huku nikiweka mkono kifuani kwangu. Akatabasamu Kisha akasema
“Ndiyo”
“Nakimbia nini?” nilimuuliza nikiwa Bado kwenye Mshangao. Yule Bibi akacheka kidogo Kisha akasema
“Unakijua unachokikimbia lakini hutaweza kukikwepa. Hata hii safari hautafika Hadi pale utakapokubali kuchukua Mikoba” alisema yule Bibi, nilizidi kushangaa. Nikaangalia Watu wengine pale ndani ya Basi nikaona walikua bize na Mambo Yao, wengine walikua wamelala.
“Mbona sikuelewi na sijui hata unaongelea nini, inawezekanaje ukaongea mambo ya ajabu ikiwa haunifahamu?” nilisema kwa sauti kavu. Yule Bibi akacheka kidogo Kisha akasema
“Nakujua vizuri sana Saida, nawezaje kukusahau?” nilizidi kushtuka, nikarudi pembeni kidogo Hadi nikagusa kioo Cha gari, kutaja jina langu ni ishara kua hakukosea.
“Wewe ni Nani?” nilimuuliza huku mapigo ya Moyo Wangu yakinienda mbio sana.
“Hakuna haja ya kunifahamu, ni lazima uichukue ile Pete” alisema yule Bibi, safari hii aliongea kwa sauti ya hasira Kisha alimeza funda zito la mate. Macho yalinitoka nikiwa ninamtazama yule Bibi. Hadi kufikia hapo niligundua kua alichokua anakisema kwangu wala hakukikosea.
Mara nilishtuka kutoka Usingizini, Bado safari ilikua ikiendelea. Lakini Cha ajabu ambacho kilinishangaza ni kwamba nilimwona tena yule Bibi Siti ya pembeni, yaani tulikua tumekaa Sehemu Moja. Haikua ndoto tena, alikua vile vile, nywele fupi zilizojaa mvi.
Wala hakua na nguo za gharama, alijifunga khanga eneo la kifua, Mabega yalikua wazi. Namna alivyo ni kama alikua Hana muda na Mimi maana hakugeuka kunitazama isipokua Mimi nilikua mwenye hofu sana. Sikutegemea ile ndoto ingekua kweli
Wakati naendelea kumshangaa akageuka kunitazama Kisha akaniambia
“Chukua” alisema huku akinyoosha mkono kuja kwangu, alikua akinipatia ile Pete niliyoikataa kutoka Kwa Salehe. Moyo ulikua unadunda kwa mapigo makubwa sana ambayo nilihisi ulikua unataka kutoka.
Hakutikisika, aliukaza mkono kwangu bila kusema neno lolote lile. Halafu ile Pete ilikua kama inatoa mwanga Fulani hafifu lakini wenye rangi ya Kijani.
Nilikua ninahema sana maana hofu niliyokua nayo haikunipa hata nafasi ya kumeza mate, Koo lilikauka huku macho yakiwa yamenitoka nikimtazama yule Bibi pamoja na ile Pete
“Usipoichukua hii Pete na kuivaa Watu wote ndani ya hili Basi watakufa kwa ajali mbaya sana isipokua wewe, kama upo tayari hutaichukua hii Pete lakini kama upo tayari naiacha hii Pete hapa” alisema yule Bibi Kisha alisimama, akaiweka ile Pete juu ya Siti yake halafu akaondoka kama vile alikua anatoka chumba kimoja kwenda kingine.
Nilisimama ili nimtazame alipokua anaelekea lakini ni kama alipotelea hewani nisijuwe alienda wapi, nilizidi kushtuka. Mwili ulikua baridi sana, nilisisimkwa Kila kiungo Cha Mwili Wangu, niliitazama tena ile Pete iliyokua juu ya Siti.
Nilijiuliza mara mbili mbili kama kile alichokisema kitakua kweli itakuaje, Watu walikua wamelala, wengine walikua wakizungumza mambo Yao, pia nilimwona Mama Mmoja akimbembeleza Mtoto Mchanga.
Roho ya huruma iliniingia japo sikua na uhakika kama alichokisema kingetokea. Nikiwa nimesimama nilihisi kama Kuna Mtu amesimama nje ya gari, niligeuka haraka. Nikamwona yule Bibi akinipungia Mkono Kisha akapotea kama upepo vile.
Nilishtuka nikaketi kwenye siti. Nilizidi kuhema kwa nguvu bila kupumzika, mara nilihisi mtikisiko wa gari, nikasimama haraka nikaona
gari ilikua ikilikwepa gari nyingine, kwa namna nilivyoona ilibakia kidogo itokee ajali. Moyo Wangu ulianza kuuma
Niliitazama tena ile Pete huku chozi lilikaribia kunitoka, sikujua ni kwanini nilipaswa kuivaa ile Pete, ni Mikoba gani ambayo nilipaswa kukabidhiwa? Nilijiuliza yote huku nafsi yangu ikiniambia niichukue Pete ili kuokoa Maisha ya Watu wengine ndani ya basi.
Wala haikuchukua hata dakika Moja ukatokea mtikisiko mwingine mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo, hata abiria wengine walianza kupiga kelele, lakini dereva aliliweka tena gari Barabarani, nilijua lilikua onyo kwangu na pengine sasa pasingelikua na onyo jingine
Niliiokota ile Pete Kisha niliivaa bila kusita, Pete ilizima. Hali ya utulivu ilipatikana ndani ya Basi, pakawa kimya safari ikiwa inaendelea kuelekea Dar-es-salaam. Sikuhisi chochote kile mwilini mwangu, ilikua kama vile nilikua nimevaa Pete ya kawaida tu.
Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya SABA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

