Ilipoishia Kimya (Nzena-Kijiji Kilicholaaniwa) – 07

“Unajua nini wewe?” Wakati huo Damu nyingi zilikua zikimtoka Mfalme Selasi,  akamwambia Anna 

“Unaenda kutafuta Pete ya Baba Yako, Mimi naijua ilipo. Namjua anayeitumia  huko Duniani, bila Mimi kamwe hutoipata” Anna aligeuka akamtazama Zahoro Kisha Zahoro akamuuliza Mfalme Selasi

“Kama utasema ilipo basi nitakupatia jicho lako. Utajitibia na kupona, ipo kwa  Nani?” Mfalme Selasi akaachia Kicheko Cha maumivu huku Damu ikimtoka  Mdomoni.  Endelea

SEHEMU YA NANE

“Huwezi kuitangaza amani ukiwa umeshika Upanga Kijana, nipatie jicho Kisha  nitawaambia ilipo” Haraka kwa hasira Anna akaelekea chini na kumshika shingoni  Mfalme Selasi Kisha akamwambia 

“Kama unafikiria sitaipata Pete kwa sababu Yako ni Bora ufikirie mara mbili  kwasababu tutakuacha hapa na hutopata msaada. Mji wote wa Patiosa utakua chini  yetu muda siyo mrefu, ni Bora ufanye maamuzi kwasababu hatuna muda tena”  alisema Anna, alimwonesha Mfalme Selasi upande wake wa pili akiwa na hasira. 

“Sitawaambia Hadi mnipatie jicho langu. Hakika hamuijui Dunia, hamtaipata na  kamwe hamtoiongoza Patiosa bila hiyo Pete” Anna akatikisa kichwa chake Kisha  akasimama, akamshika mkono Moana, akasogea naye Hadi mlango wa Kuzimu. 

Akamshika mkono Zahoro Kisha akamwambia Mfalme Selasi 

“Kwa ajili ya Familia yangu basi huo Mji wa Patiosa si Mali kitu. Tunaondoka na  kuifunga Kuzimu, hakuna kitakachoingia wala kutoka. Hadithi ya Maisha Yako  itaishia hapa” alipomaliza kusema wote waliangalia mbele na kuiona jinsi Dunia  ilivyo nzuri, Dunia ilikua ikilishuhudia jua la Mchana wakati huo Kuzimu ilikua ni  Usiku. 

Mara Mfalme Selasi akasema kwa kuweweseka. 

“Sawa nitawaambia lakini mtunze ahadi yenu kwangu…” Anna na Zahoro waligeuka, Kisha Mfalme Selasi akawaambia 

“Pete ipo kwa Mwanasayansi Mkubwa wa Nchi ya Ganza, anayeitwa Steve  Mbasa.”  

“Una hakika ni yeye ndiye aliyeuwa Wazazi Wangu?”  

“Ndiyo Nina hakika, ni yeye ndiye aliyeuwa Wazazi wako hapa. Kisha aliondoka  na Pete, yeye ni Mtu Mashuhuri sana, ni tajiri na ana uwezo mkubwa wa Kisayansi  kwasababu ya hiyo Pete. Sasa nimeshawaambia Ukweli, nipeni Hilo jicho” Zahoro alimtazama Anna ambaye alianza kububujisha chozi lake pole pole Kisha Anna  akamwambia Mfalme Selasi

“Nina hakika na maneno Yako, lakini nikukumbushe Mfalme kua. Ukiuwa kwa  Upanga utauawa kwa Upanga, kwakua ulitutelekeza na sisi tunakutelekeza hapa” 

“Hapana Usifanye hivyo Binti, sikuwauwa wakati ule. Niliwaacha mwende na  Ndiyo maana Hadi Leo mpo hai” 

“Sawa, Nami nakuacha uwe hai” alipomaliza kusema hivi. Waliingia Upande wa  Pili ambao ni Duniani. Kisha waliufunga mlango wa Kuzimu, walijikuta  wametokezea ndani ya godauni Moja lenye kuhifadhi mizigo ya Nafaka. 

Mbele Yao walimwona Mzee mmoja ambaye aliwashuhudia Anna, Moana na  Zahoro wakitokea Sehemu ya ajabu sana Kisha Sehemu hiyo kujifuta kama vile  hapakutokea chochote. 

Mzee huyo aliishiwa Cha kusema alibakia akiwatazama wakiondoka hapo Hadi nje  ya godauni. Walijikuta wakiwa wamezungukwa na Maghorofa ya Mji Mkuu wa  Nchi ya Ganza, Moana alitabasamu kwasababu aliyaona magari kwa mara ya  kwanza, Kila kitu kilikua kipya kwake 

Hii pia ilikua ni mara ya kwanza kwa Anna kufika Duniani, naye alijikuta  akishangaa sana. Kila kitu kilikua kipya kwake, kuanzia hewa na Kila kitu. Aliachia tabasamu kama Moana, Zahoro hakushangaa sababu yeye alizaliwa  Duniani hivyo alishawahi kufika ndani ya Jiji Hilo 

“Tunahitaji pesa” alisema Zahoro. Anna aligeuka kumtazama Zahoro, alishangaa  kumwona Zahoro ni Kijana wa Miaka 22 kama alivyopotea na Kijiji Cha Nzena,  alirudi na Umri ule ule wakati Kule Kuzimu alikua na Umri wa kuanzia Miaka 40.  Hata Zahoro alipomtazama Anna alistaajabu kumwona Anna ni Bibi Kikongwe,  aliyejawa na mvi na makunyanzi, asiyejiweza kutembea vizuri. 

Anna alijishangaa pia kutokana na sauti aliyoitoa, alihisi mwili wake kuchoka  sana. Moana yeye alikua mdogo vile vile hakuna kilichobadilika kwake, Anna  akajipapasa Uso wake Kisha akamwambia Zahoro  

“Mimi si wa Duniani, sistahili kua hapa Zahoro” wakati anaongea hivi, Moana  alishangaa kuona mkono wa Mama yake ukiwa na makunyanzi, akainua kichwa  kutazama. Aliona mabadiliko ya Wazazi wake akauliza 

“Mama, Baba….Mmekuaje?” alikua akistaajabu sana, Zahoro akasema 

“Nitakueleza Moana, usijali. Kwasasa tupate mahali pa kufikia kwanza” Anna  alimtazama Moana kwa jicho la huzuni sana huku moyo wake ukimwambia kua  siku Moja ataachana na Moana na hatomwona Milele sababu Moana amefuata asili  ya Baba yake. 

Chozi likamtoka lakini akalifuta, Zahoro akaanza kumsaidia Anna kusonga mbele,  wakavuka barabara. Wakasimama mbele ya Mgahawa, walikua wakihisi njaa pia  hata mavazi Yao yalikua yamechoka sana 

Watu waliwatazama kama Ombaomba wasiojiweza, baadhi waliwasaidia pesa.  Kwa Moana na Anna pesa ilikua ni kitu kigeni kwao, lakini Anna akamwambia  Zahoro kua wanaweza wakapata pesa kama hizo kupitia jicho la Mfalme Selasi 

“Tafuta Sehemu tulivu kisha liambie Hilo jicho la Miujiza linaweza kutupatia  pesa” alisema Anna, basi Zahoro akawasogeza ndani ya Mgahawa ili wapate  chakula Kisha Zahoro akaelekea Chooni 

Akatafuta Sehemu ya kutulia Kisha akaomba pesa kupitia jicho. Maburungutu ya  pesa yakatijitokeza, Zahoro akayaokota na kuyasweka Mfukoni, Kisha akatoka.  

Walikula chakula walichopenda na kulipa pesa Kisha walitafuta Hoteli nzuri  wakachukua chumba. Zahoro aliondoka na kwenda Kununua nguo kwa ajili ya  Moana na Anna Kisha aliporudi walikaa pamoja. 

“Baba, kwanini mmebadilika?” aliuliza Moana. Zahoro alionesha tabasamu kidogo  Kisha akamwambia Moana. 

“Kwasababu tupo Duniani sasa, tupo mahali ambapo Mimi nilizaliwa na kukua.  Mama Yako yeye si Mtu wa huku Ndiyo maana baada ya kuingia hapa  amebadilika.” 

“Mbona na wewe pia umebadilika?”  

“Sijui Moana, lakini wakati nimepotea nilipotea nikiwa na Umri huu. Pengine  Maisha yangu Duniani yalisimama, niliporudi Ndiyo yameendelea. Wewe  umefuata asili yangu, wewe ni Mali ya huku” 

“Kwahiyo Mama ataondoka si Ndiyo?” 

“Ndiyo, wakati ukifika. Mengine utayajua Taratibu sawa?”

“Sawa” alisema Moana Kisha alimtazama Mama yake kwa huzuni sana, alikua  amelala kitandani akionekana ni Mzee aliye dhahifu sana.  

“Anna, tunahitaji kumpata Steve Mbasa haraka sana. Sijui itawezekana vipi lakini  ni lazima iwe hivyo, tuipate Pete ya Baba Yako Kisha tutaieleza Dunia juu ya Kijiji  Cha Nzena”  

“Sawa Zahoro, nahisi baridi naomba nilale” alisema Anna, Zahoro akamfunika  Anna shuka gubigubi Kisha yeye akaketi kochini. Moana naye akapitiwa na  Usingizi Mzito. 

** 

Waliitumia siku yote kupumzika, kuzoea mazingira. Siku iliyofuata asubuhi,  Zahoro aliwasha televisheni. Alikutana na taarifa ya Mwanasayansi Steve Mbasa  aliyekua akifanya mahojiano na kituo Cha Runinga Cha Taifa kua anatarajia  kuzindua kifaa kipya Cha kuelekea angani. 

Ndipo Zahoro alipoiona sura ya Steve Mbasa aliyetajwa na Mfalme Selasi wa  Kuzimu. Akatamani kuiona hiyo Pete inayosemwa, kweli aliiyona Pete nyekundu  kidoleni. Pete hiyo haikuonekana kua ya Kisasa, pia ilikua ya kifalme. 

Zahoro akamwambia Anna kua alichokisema Mfalme Selasi kilikua sahihi, jinsi ya  kuipata Pete hiyo ilibaki kua ndoto ya Mchana.  

Watawezaje kumfikia na kuichukua Pete? Zahoro alijiona ni Mtu pekee aliye na  nguvu lakini hakua na mamlaka. Akamwuliza Anna 

“Nifanye nini angali upo Kitandani?” 

“Ili ufike kwake unapaswa kua tajiri, au Mtu mkubwa Zahoro. Msaada pekee ni  Pete ya Miujiza. Inaweza kukufanya ukawa hivyo, ukiipata Pete Ndiyo nafuu  yangu Mimi.” Alisema Anna. Basi Zahoro alianza kuliomba jicho limpatie pesa  nyingi zitakazompa jina kubwa Mjini. 

Lakini jicho hilo halikutoa pesa, halikufanya chochote. Zahoro alichukia sana akatamani kulipasua lakini jicho hilo likamwambia 

“Hata ukiwa na pesa kiasi gani, hauwezi kuipata ile Pete. Anayepaswa kuichukua  Pete ni Anna” wote walishangaa, Anna angewezaje kuipata Pete wakati yeye ni  Bibi Mzee aliye kitandani.

“Anna yupo kitandani hajiwezi, atawezaje kuipata Pete?” Zahoro akauliza, lile  jicho likasema 

“Udhaifu wa Steve Mbasa ni kusikia habari za Kuzimu. Mara nyingi husisimka  sana na kuhitaji kujua kuhusu Kuzimu kwasababu hufanya safari za mara kwa  mara kuelekea Kuzimu kuonana na Mfalme Selasi” Zahoro alimtazama Anna,  Kisha Zahoro akapata wazo akasema 

“Tutampigia simu na kumdokeza machache kuhusu Kuzimu, kuhusu Mfalme  Selasi na Mji wa Patiosa. Nina uhakika akisikia atahitaji kutufahamu. Hapo ndipo  tutakapoweka mtego na kuipata Pete” akaachia tabasamu. Zahoro aliondoka  Hotelini na kuanza kuuulizia namna ya kupata mawasiliano ya Mwanasayansi  Steve Mbasa 

Akafika Hadi kwenye makao Makuu ya Mwanasayansi huyo maarufu Duniani,  mahali hapo palikua na Ulinzi wa kutosha lakini hakuogopa sababu alijua nguvu  aliyonayo  

Taratibu alipandisha ngazi na kufika lango kuu, hapo alikutana na eneo la  mapokezi.  

“Habari‼” alisalimia Zahoro kwa utulivu sana huku akiachia tabasamu. “Nzuri, Karibu sana.” Mdada aliyepo mapokezi alimjibu. Kisha Zahoro akasema 

“Ninahitaji kuonana na Bwana Steve Mbasa” akaachia tabasamu kidogo, yule  Mdada akamwuliza 

“Una miadi naye?” 

“Hapana, Mimi ni Mtu maalum kwake. Sihitaji Miadi” Yule Mdada akacheka  kidogo akamwambia Zahoro  

“Huwezi kuonana naye bila Miadi, hauonekani kama Mtu maalum. Istoshe yupo  Nje ya Bara la Afrika” alisema. 

“Ooh! Pengine Mimi ninaweza kumfanya arejee haraka sana kwa ajili yangu,  unaonaje?” akasema Zahoro kwa kujiamini sana. 

“Sidhani, Kuna jambo unahitaji msaada?” 

“Hapana, yeye ndiye anayehitaji Msaada kwangu. Mpigie Umwambie Kua Mfalme  wa Patiosa amefika” alisema Zahoro, yule Mdada akashangaa. 

“Mfalme? Dunia ya Sasa Ina Mfalme mweusi? Hata hivyo siwezi kupoteza muda,  unaweza ukaondoka au niite walinzi wakuondoe hapa?” 

“Kama utampigia na kumwambia kua Mfalme wa Patiosa nimefika Kisha  akakwambia hanifahamu unaweza ukawaambia Walinzi wanikamate na kunitupa  nje” alisema tena kwa kujiamini. Yule Mdada akamtazama sana Zahoro, Ujasiri  alionao ukamsukuma akashika simu akampigia Steve Mbasa. 

“Samahani Bosi, Kuna Mtu amekuja hapa amejitambulisha kama Mfalme wa  Patiosa. Anasema anahitaji kukuona” Yule Mdada alibakiwa na simu sikioni huku  akimtazama Zahoro  

Kisha simu ikaondolewa sikioni, akamwambia Zahoro  

“Kwanini ameshtuka kusikia upo hapa?” 

“Nilikwambia” 

“Nenda chumba namba 555, floo ya saba” alisema, Zahoro akatabasamu Kisha  akaongoza kuelekea Alipoelekezwa. 

Alipofika floo ya saba akazuiliwa na walinzi, akasachiwa Kisha akaruhusiwa  kuingia ofisini kwa Steve Mbasa. Hofu ikaanza kumwingia Zahoro huku akijiuliza  kama ataweza kukabiliana na Steve Mbasa. 

Alikutana na macho ya Steve Mbasa yakimwangalia kwa shahuku kubwa,  akayafinya macho yake akimtazama Zahoro. Alikua na tafakari kubwa baada ya  kumwona Zahoro, huku akijiuliza maswali mengi sana. 

Zahoro akaketi pole pole kitini huku akikikagua chumba Cha ofisi, ilikua ni ofisi  kubwa yenye picha nyingi ukutani, Steve Mbasa alikua ameketi kitini akimtazama. 

“Wewe ni Nani?” akauliza. 

“Mimi ni Mtu ninayekufahamu Steve Mbasa” alisema. Steve Mbasa akaachia  Kicheko kidogo Kisha akamuuliza

“Umetumwa na GGB si Ndiyo? Nafikiria nahitaji kukufundisha somo ili  ukamwambie aliyekutuma kua Steve Mbasa si Mtu wa kuchezea” alisema Steve  Mbasa Kisha akachomoa Bastola na kujiweka vyema tayari kumuuwa Zahoro. 

Macho yakamtoka pima Zahoro, akajua fika kua hapaswi kufanya Mchezo kwani  Steve Mbasa ni Mtu katili asiyejali utu. Akamwambia 

“Kabla hujanimaliza, natamani kukwambia kua kwasasa hutaweza tena kuelekea  Kuzimu kwasababu funguo ya huko ninayo Mimi. Mfalme Selasi Hana tena  madaraka, najua unaelewa kua ili Pete uliyonayo iendelee kufanya kazi unapaswa  kuelekea Kuzimu Kila baada ya Muda Fulani.” Maneno ya Zahoro yalizidi  kumfanya Steve Mbasa azidi kupagawa, akajikuta akichanganikiwa. 

Aliyoambiwa na Zahoro yote yalikua ni kweli, si mambo ambayo hata GGB alikua  akiyafahamu hivyo Zahoro alikua Mtu wa kipekee aliyeijua Siri ya Steve Mbasa. 

“Wewe ni Nani?” akauliza. 

“Mimi ni Mtu kutoka kuzimu. Nitaonana na wewe, nitakueleza ni wapi tukutane.  Usisahau kua Nina funguo ya jicho la Mfalme Selasi” alisema Zahoro Kisha  alisimama na kumwambia 

“Ni lazima uniache nikiwa hai ili uilinde hii Siri ambayo hutaki Watu waijue,  tutaonana Nje ya Mji, Jioni ya Leo. Uje peke Yako nitakupa jicho la Kuzimu”  alisema Zahoro Kisha akaongeza 

“Makutano ya Mji. Karibu na mnala wa Mashujaa, nitakua hapo kuanzia sasa 12  jioni nikikusubiria” alisema Kisha Zahoro aliondoka ofisini hapo akimwacha Steve  Mbasa akiwa amepagawa.  

Alijiuliza maswali mengi sana, mgeni huyo aliwezaje kuyajua yote Yale wakati  ilikua ni Siri kubwa kati yake na Mfalme Selasi?  

“Ni kweli hua naenda Kuzimu Kila baada ya Miezi kadhaa. Aliwezaje kuyajua  yote haya, Ina maana ni kweli ametokea Kuzimu, kama ni hivyo napaswa kuipata  hiyo funguo iwe yangu Milele. Nitaweza kwenda Kuzimu na kurudi Duniani  nitakavyo Mimi” alijisemea Steve Mbasa 

**

Jioni ilipofika, gari ndogo ya kifahari iliongoza kuelekea Makutano nje kabisa ya  Mji, Kisha gari Hilo likaegesha karibu na Mnara wa Mashujaa, palikua tulivu,  kimya. Ni eneo la kihistoria ya Mashujaa wa zamani waliopigana vita.  

“Nitakuuwa Kisha nitakuchukua jicho bila sharti lolote lile” alisema Steve Mbasa  huku akiweka sawa Bastola yake Kisha aliisweka kiunoni. Akashuka kwenye gari  na kuiruhusu miguu yake kusogea taratibu Hadi eneo la Makaburi ya Mashujaa. 

Alipofika hapo aliangaza huku na kule, kwa mbali akamwona Mtu akiwa ameketi.  Alisogea taratibu Hadi alipomfikia, Mtu huyo alikua ameketi kwenye kiti Cha  walemavu. Alipofika karibu alimwona Anna, hakumfahamu sababu hakuwahi  kumwona popote lakini alishangaa kumwona Mzee eneo Hilo badala ya Zahoro. 

Akaangaza huku na kule Kisha akamuuliza Anna  

“Nilipaswa kuonana na wewe hapa?” Anna akamtazama Steve Mbasa kwa sekunde  kadhaa Kisha akamwambia 

“Ndiyo, nimekusubiria hapa kwa kitambo kidogo” alisema kwa sauti ya Uzee  iliyojaa mikwaruzo.  

“Iko wapi hiyo funguo?” aliuliza.  

“Kabla sijakupa, nataka makubaliano.” 

“Enhee‼ makubaliano gani?” 

“Naitaka Pete” alisema Anna. Steve Mbasa akaangua Kicheko Kisha akasema 

“Oooh kwahiyo unahitaji Pete ili unipe funguo ya Kuzimu. Nisipokupa utafanya  nini?” 

“Nitaichukua kama ulivyoichukua mikononi mwa Baba yangu Kisha ukamwua”  alisema Anna, Steve Mbasa akajua sasa alikua akiongea na Mtoto wa Mfalme wa  zamani wa Patiosa ambaye ndiye mmiliki wa Pete hiyo, akahamaki akachomoa  Bastola yake 

“Huwezi kuichukua Pete kutoka kwangu kamwe, hii Pete Ndiyo maana halisi ya  Maisha yangu. Pete hii ni Uzima Wangu, ni utajiri Wangu hivyo siwezi kukupatia.  Kwanza siwezi kukuacha ukiwa hai, ninakuuwa”

“Kama unaona ni rahisi kufanya hivyo basi niuwe Steve Mbasa, nimeishi Maisha  yangu nikiwa na kisasi juu yako. Niliusubiria huu wakati kwa muda mrefu sana”  alisema Anna, pale pale Steve Mbasa akafyatua risasi ya ghafla kuelekea kwa  Anna. 

Risasi ikapenya na kumrarua eneo la kifua, Damu nzito ikaruka. Anna akatoa  Mchozi Kisha akamwambia 

“Nimekuja kulipa Kisasi Steve Mbasa” Akapigwa risasi nyingine, Kisha akapigwa  nyingine, akapigwa Risasi nyingi Hadi Bastola ya Steve Mbasa ikaishiwa na risasi.  Jasho lilikua likimtoka Steve Mbasa huku akimtazama Anna aliyekua ameinamisha  kichwa chake. 

Baada ya kuona alikua amemwua Anna, aligeuka ili aondoke lakini ghafla  alikutana na Sura ya Zahoro. Akapigwa na nyundo kichwani, akaangukia pembeni.  Damu nzito ikawa inamtoka, Zahoro akamfuata na kuanza kumpiga na nyundo  kichwani Hadi akahakikisha amemmaliza. 

Akauvuta mwili wa Steve Mbasa kuelekea kwa Anna, Kisha akaukamata mkono  wa Anna na kuutumia kuivua Pete, Kisha Pete hiyo akamvisha Anna. Ghafla polisi  wakafika hapo kutokana na zile risasi zilizo sikika. 

Wakamweka chini ya Ulinzi Zahoro. Mtu pekee aliye hai hapo alikua ni Zahoro,  akakamatwa na Polisi kwa Kosa la Kumwua Mwanasayansi Steve Mbasa. Lakini  Zahoro akawaambia  

“Ni kweli Mimi ni Muuwaji lakini nimeuwa ili kuiokoa Dunia yetu dhidi ya Watu  kama Steve Mbasa” Polisi walistaajabu Kauli ya Zahoro, wakatamani kumwuliza  zaidi 

“Ndiyo, Steve Mbasa amekufa akiwadanganya kuhusu Sayansi yake lakini ukweli  ni kwamba yeye ni Mtu mbaya aliyejificha gizani, amefanya Mauwaji mengi ili  kuificha Siri yake. Hakuna anayenijua Mimi lakini naweza kuwaeleza ukweli kua  niliishi Kuzimu kwa muda mrefu, Mimi ni miongoni mwa Wakazi wa Kijiji Cha  Nzena kilichopotea Duniani, mnakijua hiki kisa si Ndiyo?” Polisi wakatazamana,  Kila mmoja akapata shahuku ya kusikia kuhusu kisa Cha Kijiji Cha Nzena  kilichoibua maswali mengi yasiyo na Majibu.

“Mimi ni Mhanga wa kile Kijiji ambacho Hadi Leo kipo Kuzimu, Kijiji kile  kilikumbwa na laana. Ndiyo sababu ya Kupotea kwake na hakiwezi kurudi tena  Duniani, siyo Kijiji kile tu Bali Kuna Miji Mingi ipo kule, Nani anajua kuhusu  Pete ya Steve Mbasa?” aliuliza, kuhusu swali hili wala hapakua na Siri sababu  GGB aliwahi kuwaambia Watu kuhusu Sayansi feki ya Steve Mbasa akiitumia Pete  ya Kuzimu. 

“Nipo tayari kupokea adhabu lakini naomba mniruhusu nimrudishe Kuzimu huyu  aliye kitini” wote waligeuka kumtazama Anna, walipigwa na Butwaa wakajikuta  wakimwachia Zahoro Kisha Zahoro kwa kutumia Jicho akafanikiwa kuifungua njia  ya Kuzimu pale pale, akamsukuma Anna kuelekea huko. Baada tu ya Anna  kukanyaga ardhi ya Kuzimu akaonekana akibadilika na kua Mwanamke mrembo  kama zamani, tena akiwa hai kabisa. Wote walistaajabu Kisha Anna akanyanyuka  kutoka kitini na kuwaambia Polisi 

“Hii Ndiyo Dunia iliyojificha, Dunia iliyobeba Siri na Miujiza Mingi. Kuanzia sasa  naifunga hii njia na hakuna atakayeweza kufika huku. Zahoro naomba umtunze  Moana” alisema Anna huku taratibu ile njia ikijifunga. 

Chozi la Anna lilimfanya Zahoro aangue Kilio, alikua anaachana na Anna Milele.  Hadi mlango unajifunga polisi wote walikua wanashangaa, Waandishi wa Habari  walikua hapo wakionesha tukio Hilo Moja kwa moja. Rais wa Nchi ya Ganza  akahitaji kuzungumza na Zahoro, akachukuliwa na kupelekwa Ikulu, akaeleza  kuhusu Kijiji Cha Nzena. 

Akawa ni shuhuda pekeee aliyepotea na kurejea Duniani. Serikali ikamwachilia  huru Zahoro, vikaaandikwa vitabu vingi juu ya mapenzi ya Anna na Zahoro, juu ya  Mwanasayansi Steve Mbasa. Miongoni mwa waliotajwa kuwa Mashujaa basi GGB  naye alikua miongoni mwao sababu alisema huu ukweli Miaka Mingi lakini  hakusikilizwa. 

Zahoro aliendelea kumlea Moana kama Binadamu wa kawaida, Kisha Mji wa  Patiosa ukawa chini ya Anna na Alice ambaye alishinda vita na kuurudisha Mji  chini ya Himaya Yao, Mji wa Patiosa ulipata Nuru tena baada ya utawala wa Damu  kukoma. Anna na Alice wakaanza kutafuta Watu waliokwama kwenye Miji  mingine na kuwaingiza Patiosa ili waishi. 

MWISHO.

Unatamani Riwaya Inayofuata Iwe Na Maudhui Gani? Mapenzi au Ujasusi au Maisha?

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx Nzena xx 

3 Comments

Leave A Reply

Exit mobile version