Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE

Basi, niliendesha gari kwa mwendo wa kawaida sana maana mvua ilikua  ikinyesha tena haikua mvua ndogo ilikua kubwa sana. Nilipofika maeneo ya  Morocco, taa za upande wa gari zinazotoka Mjini zilikua zimeruhusu, Mimi  nilikua mbele zaidi, wakati tayari nimeshaingia katikati ya Barabara  palitokea gari Moja ndogo nyeusi iliyotokea Kinondoni na kuingia mazima  Barabarani. 

Wakati natahamaki nikajikuta nimegongwa ubavuni, wenge zito  likaniandama. Nilipojiangalia vizuri nilikua nikitokwa na Damu nyingi  kichwani, nilihisi kupoteza uono mara ghafla hata fahamu zangu  ziliniondoka. Endelea

SEHEMU YA NNE

Masaa mawili yalinitosha kurejesha fahamu, nilijikuta nipo Hospitalini.  Kando yangu Upande wa kushoto palikua na Mtoto wa Miaka Mitano, kulia  palikua na Mwanamke mrembo sana 

Nilijiuliza nilifikaje pale, mara ghafla nikakumbuka kilichotokea.  Kumbukumbu zangu zilirudi nyuma na kukumbuka sababu ya kufika hapo,  nikakumbuka kua niligongwa na gari wakati nimetoka kushuhudia Ndoa ya  Zaylisa 

“Zaylisa” ndilo lililokua jina la kwanza kulitamka. Mara yule Mwanamke  mrembo akaniita 

“Jacob”

Nilimtazama, Kisha nilimtazama yule Mtoto nikamwuliza 

“Wewe ni Nani?” yule Mwanamke alinitazama huku akitokwa na machozi,  sikumkumbuka kabisa.  

“Babaaa‼” aliniita yule Mtoto, nilimtazama kwa Mshangao sana. 

“Wewe ni Nani?” nikamuuliza yule Mtoto. Kumbukumbu za Maisha ya  nyuma zilikua zimerejea na kufuta kumbukumbu za Maisha ya sasa.  

“Mdogo Wangu yupo wapi?” nilimuuliza yule Mwanamke nilikumbuka kua  Melisa nilimwacha nyumbani kwa Sudi. Nilimuaga kua naenda  kumwangalia Zaylisa baada ya kumkosa kwenye simu. Nilishangaa  kumwona yule Mwanamke akimchukua Mtoto na kukimbilia nje ya wodi,  yaani kumbukumbu zangu za Maisha ya nyuma zilikua zimerudi lakini za  Maisha ya sasa hazikuwepo. 

Mara aliingia Daktari, akanituliza haraka kwa kunichoma sindano ya  Usingizi. Kisha akaelekea nje kuzungumza na yule Mwanamke Mrembo  ambaye sasa ni Clara. 

Alimkuta Clara akiwa analia sana, Mtoto Wangu Melisa alikua naye akilia.  

“Usilie. Inaonekana amerudia kumbukumbu zake za zamani na kusahau  kumbukumbu za sasa. Usihuzunike kwani taratibu atakaa sawa” 

“Dokta, huyu ni Mtoto wake. Mimi ni Mke wake, kama hakumbuki kuhusu  sisi Maana yake atamkumbuka Zaylisa” 

CHUKUA ZAWADI YAKO KUTOKA KWA ADMIN wa Kijiweni Kwa Kugusa HAPA

“Zaylisa?” 

“Ndiyo” 

“Ni Nani?” 

“Mwanamke aliyempenda sana kabla ya kupata ajali ya kwanza” “Oooh‼ Unapajua alipo huyo Zaylisa?” 

“Hapana, yeye pekee ndiye anayejua. Lakini umepita muda mrefu Dokta,  hakuna namna unaweza kufanya akasahau Maisha ya zamani ili tuishi  vizuri nakuomba Dokta” Clara alikua akilia sana, haikua Siri kwa Melisa  alisikia Kila kitu na kuelewa tatizo lililokua limenipata.  

“Kila kitu katika fikra zake hufanya kazi kwa mpangilio maalum. Ni suala la  kusubiria Clara, siwezi kukuthibitishia chochote ila naweza kukushauri,  mtafute Zaylisa. Mweleze Hali halisi, mueleze wewe ni Nani kwa Jacob”  

“Nikisha Mueleza”

“Itasaidia kumweka naye mbali, muda mrefu umepita huwenda ana Maisha  yake, hii itasaidia kuleta amani pande zote mbili” alisema, maneno ya  Daktari yalimwingia Clara.  

*** 

Baada ya Muda mrefu wa kua kitandani, hatimaye niliamka na maumivu  makali sana ya Kichwa. Zaylisa alikua amejaa kichwani, ndiye Mtu pekee  ambaye mara ya mwisho kabla sijagongwa na gari nilionana naye  ukiachana na Mdogo wangu Melisa. 

Nilijitajidi kufungua macho yangu, Bado Clara alikua mbele yangu akiwa  amempakata Mtoto Melisa. Nilijiweka sawa kidogo Kisha nilimuuliza  

“Wewe ni Nani, kwanini Kila wakati upo hapa?” alitabasamu akaniambia “Mimi ni rafiki tu, niliposikia umepata ajali nilikuja kukuangalia”  “Rafiki?” 

“Ndiyo, Jacob” alisema Bila wasiwasi, sikutaka kumuuliza tena kuhusu  yeye. Nikamuuliza swali lingine 

“Melisa alikuja hapa?” akaniangalia sana, Kisha akanijibu 

“Ndiyo, ameenda kukuandalia Chakula” nilihisi amani na furaha sana,  Mdogo wangu alikua Ndiyo Kila kitu kwangu.  

CHUKUA ZAWADI YAKO KUTOKA KWA ADMIN wa Kijiweni Kwa Kugusa HAPA

“Na huyo Binti ni Mwanao?” 

“Ndiyo, anaitwa Melisa” niliachia tabasamu sababu alikua na jina la Mdogo  wangu, sikua na kumbukumbu kua alikua ni Binti yangu.  

“Mmefanana sana. Hata hivyo Mimi siwezi kuendelea kua hapa, nahitaji  kuonana na Zaylisa.” Nilijikuta nikianza kukosa Raha, kichwani kwangu  nilijua kabisa Zaylisa alikua ameshaolewa, niliishuhudia ile ndoa kwa  macho yangu lakini mapenzi yangu kwake yalikua makubwa sana na  nilikua na uhakika kua alikua akinipenda sana. 

“Kwani Zaylisa ni Nani?” aliniuliza Clara. 

“Mwanamke ninayempenda sana, nataka kujua ni kwanini ameolewa  wakati alisema hawezi kumpenda Mwanaume mwingine zaidi yangu”  Nilisema, nilipotaka kunyanyuka Clara alinituliza. Akaniuliza 

“Anaishi wapi, nipo tayari kumleta Hapa. Huwezi kutoka kwasababu Hali  Yako Bado haijakaa sawa Jacob”  

“Una uhakika utamleta Zaylisa mbele ya Macho yangu?” 

“Ndiyo, nakuahidi Jacob” Alisema Clara alionesha Hali ya maumivu sana  ndani yake. Nikamuuliza 

“Kwanini unalia sasa?” haraka akajifuta machozi akaniambia “Kwasababu umeamka Jacob, ulikua katika Hali mbaya sana”  

“Usijali, nenda kamchukue Zaylisa kwa ajili yangu, nakuomba sana Mama  Melisa, Anaishi Msasani, nyumba namba 324” 

“Sawa” Basi Clara alinyanyuka huku akinitazama, jicho lake lilikua  likibubujisha chozi. Aliondoka wodini akiwa analia, aliniacha nikiwa  nimejawa na tumaini la kumwona tena Zaylisa. Kilichokua mbele yangu  kilishapita Miaka mitano lakini kumbukumbu zangu zilinianbia ilikua ni  siku Moja tu. 

Basi, Clara aliondoka Hospitalini akiwa na gari yake ndogo. Akapitia kwa  Dada yake wa Hiari akamwachia Mtoto, Kisha yeye akaelekea mahali  nilipomwelekeza, sikujua kichwani kwake alikua na mpango gani lakini  niliamini alikua ananiletea Zaylisa pale Wodini. 

Nilisubiria kwa muda mrefu sana, mara alikuja Daktari aliyekua  akinihudumia pale Hospitalini, aliketi kando ya Kitanda. Akaniuliza kwa  sauti ya taratibu 

“Unajisikiaje Bwana Jacob?” nilijitingisha kidogo, Kitanda kikapiga kelele.  Nikamjibu 

“Namshukuru Mungu Daktari, afya yangu inaelekea vizuri. Umemwona  Mdogo wangu Melisa?” Daktari alionekana kushtuka kidogo halafu ghafla  akatabasamu na kuonesha kukumbuka 

“Aaah! Nilimwona wakati Fulani, nikaambiwa ametoka kuandaa chakula  Jacob. Hata yeye ana hofu sana na wewe, tafadhali tulia tu, Kila kitu  kitakua sawa”  

“Dokta, siwezi kua sawa ikiwa Mwanamke ninaye mpenda hayupo hapa na  Mimi” 

“Yeye ametoka hapa muda sio mrefu” 

“Hapana, yule anaitwa Mama Melisa. Ni rafiki tu” nilimwambia, alionekana  kunichunguza lakini sikua na shaka sababu yeye ni Daktari. 

“Oooh nilifikiria ni Mke wako Bwana Jacob, basi kama ni hivyo atakua na  roho nzuri sana maana ameshinda na wewe hapa kwa muda mrefu”  nilitabasamu

Mara Mlango ulifunguliwa, nilianza kuhisi harufu ya Zaylisa, harufu ya  pafyumu yake. Nilijua alikua ameshafika, Mama Melisa alifanikiwa, kweli  macho yangu nilipoyatupa mlangoni nilimwona Zaylisa akiwa amesimama  akiniangalia 

CHUKUA ZAWADI YAKO KUTOKA KWA ADMIN wa Kijiweni Kwa Kugusa HAPA

Moyo Wangu ulilipuka kwa furaha niliamini ulikua ni wakati mwingine wa  kua na Zaylisa. Alinitazama kwa tabasamu, nyuma yake alikuwepo Clara. 

Taratibu kwa mwendo wake alisogea Hadi karibu na kitanda, Daktari  alinyanyuka Kisha alimsomba Clara pale mlangoni wakaondoka.  

Zaylisa alisogea na Kuketi taratibu kwenye kiti, alinitazama kwa sura  iliyonipa maswali mengi sana. 

Dokta aliongozana na Mama Melisa ambaye ni Clara Hadi ofisini. Kisha  akamuuliza kwa sauti ya kumlaumu. 

“Ndiyo umefanya nini sasa Clara, kwanini umemleta Zaylisa hapa? Nilikwambia unapaswa kumweka mbali na Jacob ili kumfanya amsahau  taratibu”  

“Dokta” aliita Clara akiwa na sura ya Huzuni sana. 

“Kwa jinsi ninavyo mpenda Jacob, sikutaka aumie. Nimemleta Zaylisa kwa  ajili ya jambo Moja tu, kumfanya Jacob apone, akikumbuka Kila kitu  hawezi kuiacha familia yake” 

“Akili Yako haipo sawa, wakati unafikiria kua unamsaidia basi ndivyo  unavyo chimba Kaburi lako. Wale Watu hawakupaswa kuonana tena”  

“Najua lakini nafanya hivi ili Melisa awe karibu na Baba yake, kumbuka  Bado Jacob hajajua kua Mdogo wake Melisa alishafariki kwa kuuawa na  rafiki yake Sudi. Nimeongea na Zaylisa pamoja na Mume wake wamekubali  Zaylisa amsaidie Jacob kurejesha kumbukumbu zake” 

“Atarejeshaje?” 

“Zaylisa atakua karibu na Jacob watakua karibu kama wapenzi lakini  wakati huo Zaylisa anampa kumbukumbu Jacob. Nipo tayari kuishi kama  rafiki wa Jacob, lakini najua na Nina amini ipo siku atanikumbuka” 

“Haupo sawa, unataka Zaylisa na Jacob waendelee kua wapenzi? Unafanya  Kosa kubwa sana Clara na utakuja kulijutia” alisema Daktari, Clara alikua  njia panda asijuwe ni jambo gani analopaswa kulifanya. 

“Clara hebu rejesha fahamu zako, wewe ni rafiki yangu tokea tupo shule.  Sikushauri kabisa, Zaylisa na Jacob ni Watu waliokua wapenzi, una hakika  gani kua Zaylisa Hana hisia za Mapenzi kwa Jacob?” 

“Zaylisa ni Mke wa Mtu, nimefanya jitihada kubwa sana kumshawishi yeye  pamoja na Mume wake. Nimekubali kuwalipa pesa” Dokta akashusha  pumzi zake, shingo upande akamkubalia Clara lakini akiwa na wasiwasi  sana. 

Basi, upande wa pili pale wodini. Zaylisa aliketi na kunitazama kwa jicho la  huruma sana lakini lenye Fumbo ndani yake.  

“Jacob” aliniita. Mwili Wangu ulisisimka, sauti yake ilikua tulizo kubwa  sana kwangu. Kisha akaniambia 

“Samahani, niliolewa lakini sikua na chaguo. Nilisubiria sana unichumbie  lakini hukua na uwezo” alisema kwa suati ya pole pole sana, iliyokua  imetulia sana. 

“Hujui nimeumia kiasi gani Zaylisa, moyo Wangu hauwezi kukusahau wewe  kamwe. Hata Melisa akikuona hapa atathibisha maneno yangu, sijawahi  kutulia hata mara Moja” nilisema kwa hisia sana, hisia za Mapenzi ya dhati,  hisia zilizotoka ndani ya Uvungu wa Moyo Wangu. 

“Najua lakini sijui Cha kufanya. Mimi ni Mke wa Mtu Jacob…..halafu  samahani sana Jacob kwa nitakachokwambia, nakuomba utulie sawa? Tulia  kwa ajili Yako pia kwa ajili yangu…” niliweka umakini ili nisikilize kile  alichokusudia kuniambia 

“Pole, Melisa amefariki kwa mshituko wa Moyo” Maneno haya yalinifanya  nihisi mwili ukizizima kwa maumivu makali ya moyo, chozi lilianza  kunidondoka. Zaylisa alikua akinituliza lakini sikuacha kulia, sikukumbuka  kama niliwahi kuisikia hii taarifa lakini ukweli ni kwamba ilikua ni mara ya  Pili naambiwa kuhusu kifo Cha Melisa, sikukumbuka Maisha ya sasa.  Nilikumbuka Maisha ya zamani, Maisha ya Miaka mitano iliyopita bila  kujua kua Miaka mitano ilikua imeshapita. 

CHUKUA ZAWADI YAKO KUTOKA KWA ADMIN wa Kijiweni Kwa Kugusa HAPA

“Jacob, usilie…..najua umeumizwa lakini Mimi nimeumia pia na nipo na  wewe bega kwa bega kuhakikisha kua unakua sawa” niliona chozi la Zaylisa  machoni pake. 

“Melisa alikua ndiye Kila kitu Maishani mwangu, sikua na ndugu mwingine  Mimi. Ni Bora Mungu angenichukua Mimi akamwacha Melisa, amekufa  akiwa Bado Mdogo Jamani” nilizidi kulia 

“Jacob, unajua umekua hapa kwa wiki mbili. Tayari Melisa ameshazikwa,  nilikuwepo wakati Melisa anazikwa bila uwepo wako” alisema Zaylisa na  kunifanya nizidi kuumia, sikujua kama nilikua Hospitalini kwa wiki mbili  

lakini niliamini Hilo kwani kwa Upendo wa Zaylisa kwangu ilitosha  kuamini Kila kitu. 

Mara akaingia Clara, alinikuta nikilia. Nikamuuliza 

“Ulisema Melisa alikua hapa kumbe alikua ameshafariki, kwanini  hukuniambia ukweli?” nilihisi kudanganywa na Clara, masikini sikujua kua  yeye ndiye aliyepambana na Mimi katika nyakati ngumu lakini sasa kwangu  alikua mgeni kabisa, kumbukumbu zangu hazikutaka kumkumbuka Clara  wala Mtoto Wangu Melisa. 

“Samahani Jacob, sikutaka uumie zaidi Ndiyo maana nilijaribu kuficha  Hadi atakapokuja Zaylisa” nililia sana kumpoteza Melisa. 

Baada ya Siku Moja niliruhusiwa kutoka Hospitalini. Clara na Zaylisa  walinichukua Hadi Makaburi ya Kinondoni ili kunionesha Kaburi la Melisa  Wangu. 

Ilikua ni mara ya Pili nafika hapo lakini kumbukumbu zangu zilinianbia  kua ilikua ni mara ya kwanza, kushoto Clara, kulia Zaylisa. Mioyo yao  iliongea zaidi. 

Basi, baada ya kuliona Kaburi na kumaliza tulirudi kwenye gari la Clara.  

“Jacob, nimeona ni Bora nikuchukue ukaishi nyumbani kwangu. Kwasasa  Hali Yako haijatengemaa, Zaylisa atakua anakuja kukuona” alisema Clara. 

“Clara, Sina shida ya Sehemu ya kuishi, ikiwa Zaylisa yupo karibu yangu  Kila kitu kwangu naona ni sawa tu” nilisema nikimtazama Zaylisa, Clara  akaonekana kunywea, moyoni alikua akiumia sana lakini alijikaza tu. 

“Clara, nipo tayari kuachana na Mume wangu ili niishi na Jacob. Sijawahi  kumpenda Mwanaume mwingine tofauti na Jacob” 

“Unasemaje wewe? Hivi…” alisema Clara kwa sauti ya ukali halafu  akajishtukia na kuanza kuzungumza kwa sauti ya kawaida. 

“Hupaswi kufanya hivyo Zaylisa, ndoa siyo jambo la Mchezo ujue.” 

“Ulitaka kusema nini Clara, hatukukubaliana hivi si Ndiyo?” aliuliza  Zaylisa, Kauli zao zilionesha walikua na mazungumzo ya Siri ambayo  hawakutaka niyajue, waliniweka njia panda. 

Clara alinitazama kidogo na kasura ka Upole Kisha akatabasamu kidogo 

“Basi hakuna shida Zaylisa, mnaweza kuishi wote ikiwa jambo lako la  talaka litakamilika” maneno ya Clara yalinipa tabasamu kubwa, basi  Tuliachana na Zaylisa ambaye aliaga kua anarudi kwake. 

Mimi na Clara tuliondoka Kisha tulimpitia Mtoto wake ambaye ni Melisa,  Kisha tulielekea nyumbani kwa Clara. Kila kitu kilikua kipya kwangu,  niliyaona mazingira yakiwa mageni kabisa, sikukumbuka kuhusu Mtoto  Melisa kua ni Mwanangu wa Damu kabisa na Clara ni Mke halali wa ndoa.  

Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya TANO

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love xx Love 

 

Leave A Reply

Exit mobile version