Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (05)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (05)

    Hamza NgondoBy Hamza NgondoFebruary 12, 2026Updated:February 15, 2026No Comments9 Mins Read978 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia 

    “Ina maana Salehe yupo na ananifuatilia?” nilijiuliza. Nilishagundua pale  hapakua salama kwangu, nikageuka ili niondoke lakini ghafla mlango  ulijifunga wenyewe. Pakawa na kigiza Fulani hivi 

    “Nani wewe unanifungia? Fungua mlango..” nilipaza sauti yangu. Niligonga  na kuvuta mlango lakini sikuambulia chochote, hakuna aliyejitokeza lakini  nakumbuka ule Mlango haukufungwa kikawaida, zilitumika nguvu  nisizoziona. Kufungiwa ndani ya kile chumba kulinifanya nirejeshe  kumbukumbu zangu nyumbani kwa Mzee Mwinyi Mkuu. 

     Hukusoma SEHEMU  ZILIZOPITA?  Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI  ,  SEHEMU YA TATU , SEHEMU YA NNE Kisha Endelea 

    SEHEMU YA TANO

    Sikutaka kuyarudia Yale Maisha tena, nilipata nguvu nikawa nausukuma  sana mlango lakini bila mafanikio. 

    Muda ulizidi kwenda hata ile miale ya jua iliyopenya mlangoni ilikua  inaanza kupungua taratibu kuashiria kua jioni ilikua inaingia. Nililia sana  na kumwomba Mungu wangu asiruhusu nikarudi kwenye Maisha ya Miaka  mitano iliyopita. 

    Palikua kimya sana tofauti na mwanzo nilipokua nasikia sauti za Magari,  palikua kimya sana kama vile Watu walikua wameondoka Duniani. Nilikaa  chini nikiwa nimejikunyata nikisubiria Hatma yangu.  

    “Eeh Mungu basi simama na Mimi wakati huu. Usiruhusu nikarudi kwenye  ile Dunia” nilijisemea taratibu huku nikiwa ninalia. Nilijiinamia baada ya  kuona nimekosea tumaini 

    Zilipita dakika kadhaa, Kisha niliusikia mlango ukifunguka, nasema  niliusikia sababu nilijiinamia hivyo nilichokisikia na kunifanya niamini  ulikua ukifunguka ni sauti za Bawaba. 

    Nilinyanyua kichwa haraka sana, kweli mlango ulikua umefunguka  wenyewe, hapakua na Mtu yoyote yule kusema ndiye aliyeufungua. Moyo  ulinidunda sana.  

    Nilinyanyuka taratibu kutoka pale nilipokua nimekaa, akili yangu  iliniambia kua ninapaswa kukimbia eneo Hilo haraka sana maana halikua  salama kwangu.  

    Nilikua ninahema sana huku nikihisi mwili Wangu ukikosa nguvu kutokana na ule uwoga wa ghafla ulionijaa, ni kweli jioni ilikua imeshaingia. Jua  lilikua limepoa kabisa huko nje, huwezi amini kwa muda wote niliokua  ndani ya kile chumba sikupata hata wazo la kupiga simu popote pale. 

    Basi niliangaza huku na kule Kisha niliutosa Mguu wangu nje, ghafla  nikajikuta nimekamatwa na Wanaume wawili ambao sijui walitokea wapi,  nilipiga kelele waniachilie lakini walikua na nguvu sana. Walinisomba Hadi  nje, hapo nikaikuta ile gari nyeusi ambayo ilikua ikinifwatilia sana. 

    Ilikua imesimama kwenye uchochoro wa kuelekea Barabara kuua ya lami,  hawakunipa nafasi ya kufanya chochote kile. Watu wale hawakua na woga  wowote maana Watu Bado walikua wakipita lakini walinichukua kwa nguvu  sana na kunitia kwenye gari. 

    Nilijaribu kufanya purukushani lakini sikuweza kupata hata nafasi ndogo  ya kuwakimbia.  

    Nilichoka kwa kuhangaika bila msaada nikawauliza 

    “Niachilieni, mnanipeleka wapi?” hakuna aliyenijibu, waliniweka Siti ya  nyuma ambako mmoja aliketi upande Wangu wa kulia na mwingine  upande Wangu wa kushoto. Wanaume wale waliovalia mawani myeusi  walikua kimya

    “Mbona hamnijibu nyiyi ni akina Nani na kwanini mmenikamata” nilisema  tena kwa nguvu sana lakini sauti yangu iliishia ndani ya gari, Watu  waliopita nje walikua wakiendekea na Pilika zao, hakuna aliyenisikia tena.  Kwanza hata kama wangelinisikia wasingeliweza kufanya chochote sababu  hata wa mwanzo hawakutoa msaada wowote kwangu. 

    Mara aliingia Mtu mmoja kwenye gari Kisha akaliondoa gari. Sikutaka  kuchukuliwa kilaini, nilileta vurugu sana, nikadhibitiwa Kisha  nikapotezewa fahamu zangu, sijui hata walifanya nini. Baada ya hapo  sikujua chochote kilichokua kinaendelea, sikujua nilikua napelekwa wapi na kufanya nini lakini kitu kimoja kilichokua akili mwangu ni kua Watu hao  ndio wale walioniambia kua Nina deni. 

    Maneno ya yule Kichaa yalitimia kua watakuja kunichukua ila sikujua Watu  hao ni akina Nani, lakini niligundua hawakua Watu wa kawaida na pengine  walikua Wachawi wenye nguvu sana.  

    ** 

    Nilianza kuhisi Uhai ndani yangu, pumzi zangu zilikua zinapita puani kwa  shida kidogo. Nilianza kuhisi mapafu yangu yalikua yakiamka, hata macho  yangu yalifunguka. Nilijikuta ndani ya chumba kimoja kitupu, chumba  hicho kilikua kina harufu fulani za ajabu hasa Udi 

    Niliamka haraka nikaanza kuangaza huku na kule. Kila nilivyokua  nakikiangalia vizuri chumba kile nilianza kukikumbuka. Masikini Mimi  Saida nilikua nimerudishwa Rukwa kwa mara nyingine, nilianza kutokwa  na Machozi hasa nilipozikumbuka zile Kuta zenye Siri za mateso kwangu,  mateso ya Miaka mitano iliyopita. 

    Nilikumbuka namna nilivyopona kutoka Kifo, sikutaka kuyaamini macho  yangu, niliyafumba ili niyafumbue tena pengine lilikua wenge langu.  Nilipofumbua tena hakuna kilichobadilika, nilikua ndani ya chumba kile  kile ambacho nilibakwa na wale Misukule wa Mzee Mwinyi Mkuu.  

    Kabla hata sijatulia vizuri nilisikia sauti ya Mtoto Mchanga akilia,  mauzauza Yale Yale yalikua yakianza kujitokeza kwangu. Nilitembea  taratibu kuelekea Mlangoni, niliutekenya. Kitasa kilikubali ombi langu,  mlango ukafunguka 

    Kuta zile zile zilikua mbele yangu, sakafu ile ile aliyoburuzwa Kaka Hamidu  ilikua mbele ya Macho yangu. Nilimeza mate nikiwa ninachungulia Korido,  nilipeleka macho yangu huku na kule. Hakuna kilichokua kimebadilika,  mazingira yalikua Yale Yale

    Ile sauti ya Mtoto kulia ilipotea Kisha nilisikia sauti ya kusukumwa kwa  vyombo, sauti ilitokea kwenye chumba Cha Jiko. Basi niliutosa Mguu  wangu kukanyaga Korido, sikua mgeni na nyumba hiyo niliijua vizuri kua  kutoka ni jambo gumu sana. 

    Nilipiga hatua ndogo ndogo huku nikijishikiza ukutani, nilipofika mlango  wa kuelekea Jikoni nilimkuta Msichana mmoja akichambua Mchicha.  Aliponiona alinitazama bila kusema chochote lakini alikua na bandeji  mguuni 

    Alikua akipitia Yale niliyoyapitia Mimi, nilipepesa macho yangu huku hofu  ikiwa kubwa sana kwangu. Nilimsogelea yule Msichana Kisha nikamsalia 

    “Mambo” hakujibu, aliendelea kuchambua Mchicha, Bandeji yake ilikua  imetapakaa Damu.  

    “Samahani nakusalimia” Nilisema tena, yule Msichana hata hakuhangaika  kusema chochote, alikaa kimya akiendelea kuchambua Mchicha kama vile  alikua hajanisikia. Niliemeza funda zito la mate, nilishusha na pumzi zangu 

    Nilitoka pale jikoni baada ya kukosa majibu. Hakuna Sehemu ya nyumba  ile ya Mzee Mwinyi Mkuu ambayo nilikua siijui, nilizifahamu Kuta zote na  kumbukumbu zake. Kila nilipokua ninapiga hatua nilikumbuka mateso  makali niliyoyapitia 

    Nilitoka nyumba kubwa nikawa naelekea mlango wa kutoka ndani ya  Nyumba. Kila kitu kilikua vile vile, kilichobadilika ni kwamba ilikua ni  mara yangu ya pili naingia ndani ya Nyumba hii. Nilitembea taratibu Hadi  nilipofika mlangoni, nikajaribu kuufungua Mlango, ulifunguka bila shida  yoyote. 

    Nikayatupa macho yangu mbele, mazingira Yale Yale niliyoyaacha Miaka  mitano iliyopita yalikua vile vile. Watoto walikua wakicheza eneo la Wazi  kama zamani, kando Yao alikuwepo Mama anayetengeneza vitumbua na  chapati, alikua kwenye foleni kubwa sana. 

    Nilimkumbuka yule Mama ambaye dakika za mwisho nilibadilishiwa na  kuwekewa Mama mwingine kabisa.  

    “Mama Ashura” nililikumbuka jina lake, niligeuka nyuma Kisha nilipiga  hatua zangu kuelekea kwa Mama Ashura, nilitembea taratibu sana huku  nikiwaza mambo mengi kichwani kwangu. Kwanza nilijiuliza ni kwanini  nilirudishwa Rukwa, kwanini nimeachwa huru? Sikupata majibu ya  

    maswali yangu

    Nilipofika kwa Mama Ashura, nilimsalimia kwa adabu sana. Niliamini  angenikumbuka lakini aliipokea salamu yangu kama Mtu asiyenifahamu.  Nilitabasamu nikamuuliza kama ananikumbuka 

    “Hapana, Ndiyo kwanza nakuona Leo” alisema Mama Ashura huku  akiendelea kutengeneza chapati.  

    “Mimi Saida, tuliwahi kuzungumza Miaka mitano iliyopita” Nilisema. Yule  Mama aliniangalia Kisha akaniambia hanikumbuki, niliangalia Yale  mazingira nikaona Watu walikua wakituangalia hivyo sikutaka  kumkumbusha chochote. Niliketi pembeni nikisubiria foleni ya chapati  iishe huku macho yangu yakiitazama sana nyumba ya Mzee Mwinyi Mkuu. 

    Macho yangu yalikua kama ya Digidigi hivi, sikutaka kuacha kumwangalia  Mama Ashura lakini wakati huo huo nikiwa makini kule nyumbani kwa  Mzee Mwinyi Mkuu. Zikapita kama dakika saba hivi ndipo nilipoliona gari  Moja likifika pale kwa Mzee Mwinyimkuu. Umakini ukahama kutoka kwa  Mama Ashura nikawa naliangalia sana lile gari lililolisimama mbele ya  nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. 

    Niliona Watu wa ajabu sana ambao sikutarajia, Watu hao walikua  wamevalia mashuka meupe pia Usoni walikua wamejipaka Unga mweupe.  Namna walivyo walifanana sana na Misukule, gari ile aina ya Noah nyeusi  ilishusha Hao Watu kama Nane hivi 

    Nilishtuka sana Kisha nikamwangalia Mtu mmoja aliye kando yangu, naye  alikua akiangalia kule kule, nikajua sikua peke yangu ambaye nilikua  nikiwaona wale Watu.  

    Sikujua kama naye alikua akiona kama nionavyo Mimi au ilikua kwangu tu,  mapigo yangu ya Moyo yalikua yakienda mbio sana.  

    Namna walivyo wale Watu walifanana sana na Misukule kutokana na  mionekano Yao. Baada ya wote kushuka na kuelekea ndani, Mtu mmoja  ambaye kwa mbali sikumwona vizuri akasogea pale Kisha akawa anaongea  na Mwanaume mmoja aliyekua amesimama 

    Nilihisi kama alikua akimwonesha mahali nilipo, moyo ulinienda mbio.  Hakika alikua akinionesha kidole Mimi japo sikujua alikua akimwambia  nini yule Mtu. 

    Nilitamani kukimbia lakini nilikumbuka kua baada ya kutekwa kule  Mburahati nililetwa huku Rukwa ndani ya Nyumba ya Mzee Mwinyimkuu.  Watu walioniteka hawakunidhuru kwa chochote kile, tena waliacha mlango 

    Wazi hivyo kwa haraka niliamini kama hawakunifungia mle maana yake  walikua na jambo la tofauti dhidi yangu 

    Nilijiambia kwa Ujasiri sana “Saida umekimbia sana, sasa kua jasiri” sauti  kutoka ndani ya nafsi yangu iliniambia kwa Ujasiri sana, niliendelea kukaa  pale pale huku wengine wakiwa wanaendelea na shughuli zao bila hata  kujali kuhusu Mimi. Hata yule Mtu aliyekua akiangalia nyumbani kwa  Mzee Mwinyimkuu alikua naye anaendelea na mambo yake. 

    Nilivuta pumzi zangu nikajiambia kua hata kama Dunia itakua imefika  mwisho kwa Upande Wangu ni Bora iwe hivyo lakini siwezi kuendelea  kukimbia tena, halafu Hali ya hasira iliniingia kutokana na mateso makali  niliyoyakumbuka niliyokua nikiyapata nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. 

    Nilimkumbuka sana Mama yangu, kidogo chozi lilianza kunitoka lakini  nililizuia. Nilipofuta chozi nilirudisha macho yangu kule kwa Mzee  Mwinyimkuu, nikamwona yule Mtu aliyekua akioneshwa nilipo alikua akija  upande huu nilipo, nilijua alikua akinifuata Mimi hivyo sikuogopa wala  nini.  

    Yule Mtu alitembea haraka haraka Hadi alipofika nilipo, nilimtazama kwa  macho makavu bila kumwonesha wasiwasi. Alisimama hatua kadhaa Kisha  alinionesha ishara ya kuniita. Niliangalia huku na kule, hapakua na yeyote  yule aliyekua akiniangalia wala hata kumwangalia yule jamaa.  

    Nilisimama, halafu nikaelekea alipo. Akaniambia kwa sauti ya chini 

    “Samahani, unaitwa” alisema huku akionesha kidole kule kwa Mzee  Mwinyimkuu, hapakua na yeyote tena kule isipokua lile gari lililoleta  Misukule. Nami nilikifuata kidole chake nikaangalia kule halafu  nikarudisha macho yangu kwa yule Jamaa 

    “Nani ananiita?” niliuliza kwa Ujasiri sana japo kwa ndani nilikua mwoga  lakini sikuruhusu yule Mtu anielewe, nilimkazia macho yangu huku  nikichezesha Mguu mmoja. 

    “Bosi” 

    “Bosi?” 

    “Ndiyo” 

    Nilitazama huku na kule Kisha nikamwambia 

    “Sawa” Nilisema tu lakini nilikua naogopa sana. Tayari hatma ya Veronica  ilitimia, kilichobakia kilikua ni Mimi kulipa Hilo deni ambalo niliambiwa ninadaiwa. Akili yangu iliniambia ni Bora niende hata kama nitateseka na  kufia huko.  Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya SITA

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx  Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

    riwaya mpya Riwaya ya Goryanah Riwaya Ya Kisasi Changu riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Hadithi February 23, 2026

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Ilipoishia  Kwanza nilijiuliza ni Nani anayeweza kuja kwetu, kama Mama Amida tayari  tulishazungumza. Nilimeza funda…

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.