Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (01)

    Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2025

    AFCON

    Ratiba ya kusisimua ya 16 Bora yakamilika AFCON Morocco 2025

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (01)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (01)

    Hamza NgondoBy Hamza NgondoFebruary 2, 2026Updated:February 2, 2026No Comments5 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia SEASON 1 

    Kwasasa nimerudishwa kwetu Dar-es-salaam, niko Magomeni. Maisha yangu yamekuwa ya  Ukimya sana, Sijazungumza tena tokea siku ile nilipozungumza kwa mara ya mwisho Rukwa,  sijaandika chochote na wala sitaki kusema chochote kile ila kupitia mkasa huu nataka ujifunze. 

    Kamwe kwenye Maisha yako usiolewe au kuowa Mtu usiye mfahamu, Dunia ni Kichaka cha  Mateso. Wasichana wengi wanayapitia mateso niliyoyapitia, wengi wanauawa, wengi wanapata  ugonjwa wa akili. Hata wanaume wapo waliopoteza kila kitu, Siku nikifungua kinywa changu  nitawasimulia mengi, kwasasa naishia hapa, naweka kalamu yangu chini.  Endelea na SEHEMU YA KWANZA YA SEASON 2 Hapa  


    SEHEMU YA KWANZA

    MIAKA MITANO BAADAYE 

    Nilikua nimesimama mbele ya Kioo nikijitazama. Nilimeza funda zito la  mate, nilikua nimevalia gauni la harusi lenye kufanana na lile nililolivaa  siku naolewa na Salehe. Sikuwahi kulisahau gauni hili, lilibakia kua  kumbukumbu yangu. Sura ya Salehe ilikua kichwani mwangu, sikuwahi  kumwona wala kumsikia tena tokea wakati ule aliponiaga kua ameagizwa  na Baba yake.  

    Sura ya Mzee Mwinyi Mkuu ilikua ikipita machoni pangu Kila dakika,  mateso niliyoyapata yalitengeneza kovu moyoni mwangu. Niliitazama  miguu yangu, ilikua Haina vidole, yalibakia makovu ya Maisha. 

    Nilidondosha chozi langu taratibu, nilikua katika maumivu ya kihisia  ambayo yalikua yakiendelea kunitesa kwa Miaka mitano. 

    Midomo yangu ilikua imechanika kwasababu tokea wakati ule sikuwahi  kuongea chochote tena, Mama yangu alikua akiendelea kunitunza nikiishi  kama Bubu, hakuwahi kuisikia tena sauti yangu zaidi ya kuliona chozi  langu.  

    Nilijikuta nikilia kwa Uchungu, nilikumbuka namna usichana wangu  ulivyoondolewa na Misukule ya Mzee Mwinyi Mkuu nilipatwa na hasira  sana. Mara Mlango ulisukumwa, aliingia Mama yangu 

    “Saida” aliita Mama, alisogea nilipokua nimesimama. Mama yangu alikua  mwingi wa huzuni, alimpoteza Mume wake kwasababu yangu. Hata moyo  wake ulikua na kovu la maumivu, kama Mama alikua amepoteza Watu  wawili aliowapenda sana, alimpoteza Mume wake lakini alinipoteza Mimi  pia kwasababu nilikua kimya muda wote. 

    “Mwanangu, yaliyotokea yameshatokea. Miaka mitano imepita sasa, huna  sababu ya kuendelea kukumbuka tena” alisema Mama Kisha alinitaka nikae  kitandani, nilikaa taratibu huku chozi likiwa linanidondoka. 

    “Afya Yako sasa imeimarika lakini muda wote upo chumbani tu,  huzungumzi Saida” alisema Mama, chozi lilidondoka machoni pake. 

    Nilizidi kuumia sana Mimi, Mama yangu alikua mpweke sana na mwenye  huzuni, alikonda kwa mawazo. 

    Nilimtazama Mama yangu, nilitamani kusema jambo lakini moyo Wangu  uliniambia napaswa kuendelea kua kimya, sikua Bubu lakini sikutaka  kuongea chochote kile, sauti yangu ilikua chozi langu pekee. 

    “Saida, Mama Yako nakulilia na kukuombea Kila dakika ili urudi kua sawa  kama zamani. Wewe ni Mtu pekee uliyebakia kwenye Maisha yangu, Mimi  Mama Yako Sina mwingine zaidi Yako wewe.” Alisema Mama, niliondoa  macho yangu kwake, sikutaka kabisa kumtazama Mama yangu sababu  ningeendelea kuumia  

    Mama alifuta chozi lake Kisha akaniambia 

    “Ukihisi njaa, chakula kipo Mezani. Naenda chumbani” alisema Mama  Kisha alinyanyuka taratibu akifuta chozi lake. Alipofika mlangoni aligeuka  na kunitazama, Kisha aliondoka na kuufunga mlango. 

    Nililia sana Mimi Saida, moyo uliniuma sana sababu kama nitatoa japo  sauti yangu basi nitaweza kumpa tabasamu Mama yangu lakini nilijiapiza  kua sitazungumza tena katika Maisha yangu yote. Saikolojia yangu ilijaa  mateso makali, nilishuhudia mengi yaliyonifanya nipoteze uwezo wa  kujiamini na kujithamini kama Binadamu. 

    Sikujipenda tena, niliishi kwasababu Mungu hakutaka kuichukua pumzi  yake, lakini Dunia ilinifundisha kuchoka, sikutamani kuendelea kuishi.  Nilikua naishi nikisubiria siku Moja kifo kinichukue nikapumzike mbele ya  safari. 

    ** 

    Masaa yalienda sana, Mchana uliondoka Bado nilikua nimekaa pale pale  kitandani nikilitazama dirisha namna lilivyokua likibadilisha mwanga  wake. Jioni iliingia kwa Kasi sana, jua halikuwepo tena dirishani pangu,  chozi lilikua likiendelea kunibubujika bila kupumzika. 

    Ghafla nikajikuta nikihisi moyo Wangu ukidunda kwa Kasi kama vile  nilikua nazinduka kutoka kwenye Usingizi. Nilikua nasikia sauti ya Mtoto  akilia kando yangu, nilianza kuhema kwa Kasi sana 

    Nilikua nimezungukwa na Watu wengi waliovalia nguo nyeupe tena  wakionekana kua walikua wenye haraka sana kama vile walikua  wakinishughulikia.

    “Niacheee, Washenzi nyie. Wachawi haooo” nilijikuta nikipiga yowe Kali  sana. Mara nilichomwa sindano, nikapoteza uwezo wa kufikiria pia nguvu  ziliniisha nikajikuta nikiona Giza zito halafu Usingizi ukaiteka akili yangu. 

    Nikiwa Usingizini, nilianza kuhisi nilikua ninaitwa. Sauti ya Mama yangu  ilikua ikipita masikioni mwangu kwa mtindo wa kunong’ona. Mama alikua  akiniambia 

    “Saida Amka ule chakula, Amka Mwanangu. Amkaaa usilaleee” Mara ghafla  nikajikuta nikizinduka kutoka kwenye Yale mawazo. Nilijikuta nipo pale  pale kitandani nikiwa Nimekaa, nilikumbuka ni kweli Mama yangu  aliniambia nikihisi njaa niende Mezani nikale 

    Basi nilihema, ndoto za Kutisha zilikua Sehemu ya Maisha yangu. Wakati  mwingine niliota ndoto nikiwa nimekaa tena nikiwa macho kabisa, hayo  Ndiyo Yalikua Maisha yangu baada ya kuponea chupuchupu kule Rukwa. 

    Basi, nilinyanyuka taratibu nikaelekea sebuleni, nilikua nikitembea taratibu  sana. Nilipofika sebuleni nilikikuta chakula kikiwa hapo, nilifunua Hotipoti.  Nilijiandalia chakula Kisha Niliketi, nilianza zoezi la kufungua kichwa  changu chenye vidonda vya Ukimya 

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA PILI Sasa

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx  Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

    Msala Kijiweni Riwaya ya Goryanah riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Hadithi February 2, 2026

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (01)

    Ilipoishia SEASON 1  Kwasasa nimerudishwa kwetu Dar-es-salaam, niko Magomeni. Maisha yangu yamekuwa ya  Ukimya sana,…

    Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2025

    AFCON

    Ratiba ya kusisimua ya 16 Bora yakamilika AFCON Morocco 2025

    Hapa MSUVA Pale MPENJA Ofa Kibao Kutoka LEONBET

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.