Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (08)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua (08)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJanuary 13, 2025Updated:January 14, 202523 Comments18 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Wala hakuongea chochote akaanza kuniandalia chakula nile, nilikua nahema kwa shida sana.ย 

    โ€œKunywa Majiโ€ alisema, alikua haniangalii usoni, nilikua na kiu ya maji lakini kiu kubwa ilikuaย  ni kumuuliza Nauawa lini, nilimuulizaย 

    โ€œMnanimalizia lini nikapumzike?โ€ Kiukweli sikuwa na afya nzuri, ndani ya siku chacheย  nilikonda. Yule Bodaboda akanitazama kisha akaniambiaย 

    โ€œKifo ni siri ya Mungu, hakuna anayeijuwa kesho itakuwajeโ€ alisema kisha akanipa maji, sikuwaย  na nguvu ya kushika kikombe akaninywesha. Jinsi alivyonihudumia alionesha anahitaji niwe hai. Endeleaย 

    SEHEMU YA NANE

    Niliyafakamia yale maji kwanza hadi yalinipalia, halafu nikahema. Akanitolea vidonge vyaย  kunituliza maumivu. Sikusita kumeza kiukweli maana nilikua na maumivu makali sana kishaย  nilimshika mkono nikamuulizaย 

    โ€œNingekuwa mdogo wako ungenifanyia hivi, unajua najisikiaje Kaka?โ€™โ€™ Chozi lilikuaย  linanibubujika bila kuacha, akaniondoa mkono wangu kwa kutumia mkono wake mwingineย  kisha akasimama, akaniambiaย 

    โ€œKula upate nguvuโ€ hakuzungumza tena, alisimama kisha alipiga hatua lakini alipofika mlangoniย  alisimama. Kama kuna kitu alitaka kuniambia lakini alighaili, hakujibu swali langu aliondoka naย  kuufunga mlango kwa funguo, unajua hata kama angeuacha wazi sikuwa na nguvu ya kukimbiaย  kwa namna nilivyokua sina nguvu.ย ย 

    Nilisikia akiondoka, nililia sana Mimi. Hakuna siku inapita bila kudondosha chozi langu,ย  nilimpoteza Kaka Hamidu na nilijiona ni mkosaji, nilijilaumu sababu bila kuolewa na Saleheย  basi Kaka Hamidu angekuwa hai hadi sasa. Kidogo zile dawa zilipunguza maumivu ya mwiliย  lakini siyo maumivu ya Moyo wanguย ย 

    Haikuchukua hata dakika nyingi nilisikia yowe la Mwanaume mmoja, yowe lile lilisikika mojaย  kwa moja kutoka kwenye ile nyumba niliyohifadhiwa Mimi. Moyo ulinilipuka, niliamini ilikuaย  ni nyumba ya Mateso makali zaidi hata nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. Nilisimama hataย  nguvu sikujuwa ilitokea wapiย 

    Nilisogea mlangoni ili kuisikia zaidi ile sauti, ndiyo! Ilitoka ndani ya moja ya vyumba vya ileย  nyumba, nilitamani kupaza sauti ila sikujua alikua akifanywa nini. Nilijiuliza

    โ€œNani yupo ndani ya hii nyumba, anamfanya nini huyu anayepiga yoweโ€ Ilikua ni sawa naย  kujitekenya kisha kucheka mwenyewe, jibu lingetokea wapi ikiwa hata mimi mwenyewe sijuiย  nipo wapiย 

    Yule Mwanaume baada ya kupiga yowe alianza kusemaย 

    โ€œMsaada,Nani yupo ananisikia?โ€ aliendelea kusema hivi, nikapata picha huwenda hata yeyeย  mwenyewe hajui amefikaje na Nani amemleta ndani ya hii nyumba. Kupitia dirishani nilianzaย  kuona jua namna lilivyokuwa likifanya safari ya kwenda kupumzika baada ya kuipiga ardhi kwaย  siku nzima.ย 

    Namna nyumba hii ilivyo ilionekana kujengwa kwa ajili ya kazi ya kuhifadhi Binadamu, hataย  dirisha lake lilikua kama la Mahabusu, lilikua dogo lanye nondo,hapakuwa na taa ndani yaย  chumba kiasi kwamba giza litakapoingia basi patakuwa giza tupu. Nilijikuta nikikaa mwenyeweย  bila hata kuambiwa, kwa namna ilivyo hata ukipiga kelele vipi huwezi kupata Msaada wowote.ย 

    Kwanza sikujuwa Mtu yule alikua ni Nani, sauti yake haikufanana na ya Kaka Hamidu. Wala siย  ya Mtu niliyehisi kuwa niliwahi zungumza naye.ย ย 

    **ย 

    Usiku ulipoingia ndiyo nililiona joto la jiwe, niliandamwa na ndoto za ajabu hadi niliamka, siyoย  Mimi tu hata yule Mwanaume alikua akigugumia nahisi naye alikua kwenye hali kama yangu.ย  Niliamka na kukaa kitako nikaegemea ukutaย 

    Nikiwa hapo nilianza kuona nuru ya mwanga, ikianza taratibu hadi ikaenea chumba chote, hapaย  nilikua na uhakika kuwa haikuwa ndoto tena bali ni tukio halisi. Nilimuona tena yule Mtotoย  mdogo anayetisha, safari hii alinionesha sura yake, nilikua kwenye Mshangao wa hali ya juuย  sanaย 

    โ€œUmeshindwa kutoka hapa, umeshindwa kujaribu kufanya chochote. Wewe ni Mtu wa aina gani,ย  unataka kila Mtu afe kama Kaka yako Hamiduโ€ Ooh! Jamani nilishtuka, kama ningekua ninaย  presha kwa haya yote ningekuwa tayari nimepotea kwenye uso wa Dunia, namna alivyokuaย  anaongea alionesha alikua na tumaini na Mimi kwenye jambo fulani hasa la kuokoa uhai waย  wengine lakini Mimi mwenyewe nilikua nimeshajikatia tamaa. Japo nilijawa na woga lakiniย  nilimuulizaย 

    โ€œWewe ni Nani, umetokea wapi?โ€ nilipomuuliza alidondosha chozi la damu, alikua Mtoto waย  ajabu sanaย 

    โ€œMimi ni Ashura Mtoto wa Mama Muuza chapati. Nenda kamwambie Mama yangu kuwa badoย  naishi kwenye nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, Mimi sijafaโ€ alisema kwa kupaza sauti kaliย  ambayo ilinifanya nishindwe kuhimili zile kelele, pale pale nilijikuta nikiishiwa nguvu naย  kupoteza fahamu. Kitu pekee kilichobakia kwenye akili yangu ni ,kumbukumbu juu ya yuleย  Mama anayeishi nyumba jirani na Mzee Mwinyimkuu, Mama aliyekuwa akiniuzia Chapati

    Ndiyoโ€ผ yeye ni Mama Ashura, nakumbuka alinitajia jina hili lakini sikuwahi kumuuliza huyoย  Ashura yupo wapi, huyu Mtoto wa ajabu alijitambulisha kwangu kama Ashura na alinitakaย  nimwambie Mama yake kuwa anaishi ndani ya nyumba ya Mzee Mwinyimkuu.ย 

    ***ย 

    Baba yangu aliendelea kuumwa, Mama alikua anamuuguza huku akinitafuta Mimi kwa simuย  lakini aliendelea kutonipata, zilipita wiki mbili bila kupata mawasiliano yoyote yale. Saleheย  hakupatikana, hata Mzee Mwinyimkuu hakupatikana, Kaka Hamidu naye ilikua kama ndiyoย ย 

    kichocheo kipya cha hofu kwa Familia yangu. Mara ya mwisho aliwaeleza anakuja kuonana naย  Mimi lakini baada ya hapo hawakujua kilichomfika na kupelekea kutopatikana kwenye simuย  kwa wiki mbili.ย 

    Vikafanyika vikao vya kututafuta Mimi na Kaka Hamidu maana hawakujua naishi Rukwaย  sehemu gani na pia Kaka Hamidu alikutwa na nini. Ni Mimi pekee ndiye niliyekuwa najua Kuaย  Kaka Hamidu alikua ameuawa.ย 

    Familia ikamtuma Mjomba wetu aliyeitwa Kambona, alikua Mtu mzima na mwenye busaraย  zake.ย ย 

    Akasafiri kutoka Dar-es-salaam hadi Rukwa akiwa na picha yangu, akaanza kunitafuta bilaย  mafanikio kwa zaidi ya siku kumi. Mwishowe akaenda kituo cha Polisi maana sasa hakunaย  aliyekua na amani bila kujua tupo wapi, wote waliamini wakinipata Mimi watajua mahali alipoย  Kaka Hamidu maana mara ya mwisho aliwaambia anakuja kwangu. Polisi wakaanza kunitafutaย  kila kona ya Rukwa lakini hakuna aliyeweza kujua niko wapi, lakini kupitia jina la Mwinyimkuu Ambalo Salehe alilitaja alipokua ananichumbia, ikawawezesha kufika hadi nyumbani kwa huyuย  Mzee.ย 

    Hapa ndipo mahali ambapo nilikuwepo kabla ya kuhamishwa, nyumba hii ndimo alimouawaย  Kaka Hamidu tena kikatili sana na Mzee Mwinyimkuu. Walipofika walimkuta tena walaย  hakuwa na wasiwasi kabisa, najua alitumia akili sana kunihamisha vinginevyo polisiย  wangenikuta mleย 

    โ€œWewe ndiye Mwinyimkuu?โ€ aliuliza polisi baada ya salamu fupiย 

    โ€œMnasemaje?โ€ aliwauliza, alikua haogopi chochote wala Mtu yeyote yule, jeuri na katili mno โ€œSaida anaishi hapa?โ€ akauliza Polisi mmoja.ย 

    โ€œYeye ni Nani?โ€ akawaulizaย 

    โ€œUnajibu kwa dharau kiasi hicho Mzee, Saida ni Mpwa wangu Mimi. Ameolewa na Kijanaย  anaitwa Salehe, upelelezi umeonesha kuwa ni Kijana wako huyo Salehe halafu unauliza niย  Nani?โ€ akaingilia kati mjomba Kambona na kumshika shati Mzee Mwinyimkuu, Polisiย  wakaokoa

    โ€œUnanivunjia heshiam si ndiyo?โ€ akauliza Mzee Mwinyimkuu kwa hasiraย 

    โ€œSiyo heshima tu, ntaivunja hata hii nyumba kama hutonipatia Saida wanguโ€ Mjomba Kambonaย  hakupoa kabisa, alijawa na hasira sana.ย 

    โ€œHuyo Salehe unamfahamu?โ€ Polisi wakamuuliza Mjomba Kambonaย 

    โ€œNdiyo, nimeozesha mwenyewe. Picha si hii hapa ya ndoaโ€ akatoa picha, ile picha akapewaย  Mzee Mwinyimkuu.ย 

    โ€œUmemtambua mtajwa pichani?โ€ akauliza Polisi mmoja, Mzee Mwinyimkuu akaangua kichekoย  kisha akaita kwa sautiย 

    โ€œSalehe, hebu njoo uone maajabu ya Duniaโ€ akaitikia Mtu kutokea ndani na kuwafanya Polisi naย  Mjomba Kambona wakae mkao wa kula kumuona Salehe. Ikachukua kama sekunde kadhaa tuย  Kijana mmoja akatoka ndani, Kijana aliyekuja hakufanana na Salehe wa kwenye picha.ย ย 

    โ€œUnamfahamu Saida?โ€ akauliza Mzee Mwinyimkuu akimuuliza huyo Kijana aliyemtambulishaย  kama Salehe, kiukweli hakuwa yule Salehe aliyeniowa kabisa yaani sura tofauti.ย 

    โ€œHapana, kuna nini?โ€ akauliza huyo Salehe, kiukweli Mjomba Kambona alinywea. Lakini Polisiย  mmoja akasemaย 

    โ€œOngozana na Mimi Kijanaโ€ akamshika mkono Salehe na kwenda naye nje. Lengo la Polisi niย  kutaka utambuzi kwa Majirani maana Upelelezi wao uliwaambia Salehe wa kwemye pichaย  anapatikana kwa Mzee Mwinyimkuu. Wakafika hadi nyumbani kwa Mama Ashura maana ndipoย  palikua na Watu njeย 

    Walipomuona Yule Kijana akiwa na Polisi vijana walikimbia hadi yule Polisi akashangaa, hataย  Mama Ashura naye alikua anataka kukimbia ila Polisi akamzuia Mama Ashura na Kumwambiaย  asikimbie ana maswali kadhaa anataka kumuuliza, ndipo Mama Ashura akabakia lakini kwa hofuย  sanaย 

    โ€œUnamtambua nani pichani?โ€ Yule Polisi akampa picha yule Mama, Mama Ashura akaipokeaย  picha japo kwa wasiwasi lakini alipoiangalia ile picha alishtuka sana, akameza funda la mate.ย ย 

    โ€œHapanaโ€™โ€™akajibu lakini kwa hofu sana kiasi kwamba yule polisi akahisi pengine kuna jamboย  analificha. Kilichomshtua Mama Ashura ni kuniona Mimi kwenye ile picha ya ndoa ambayoย  Mjomba Kambona aliwapatia polisiย 

    โ€œNa huyu Kijana hapa?โ€ akauliza Polisi, Mama Ashura akamtazama yule Kijana. Akaachiaย  tabasamu la hofu kisha akajibuย 

    โ€œNi Salehe, anaishi paleโ€ akaonesha na kidole kabisa. Majibu haya yakamuacha yule polisiย  kinywa wazi, basi akarudi hadi nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. Hakuna ushahidi waย  anachosema Mjomba Kambona. Lakini Mjomba akawaaambia

    โ€œNina namba ya huyu Mzee alikua anawasiliana na Mama yake Saida, hii namba nimepewa naย  Mama Saida. Jina ni hilo la Mwinyimkuuโ€ akasema Mjomba japo kwa sauti ya kupoa, ikabidiย  Polisi waipige ile namba.ย 

    Ikapokelewa na Mtu mwingine kabisa tena Mwanamke akimuuliza yule Polisi Nani wewe?ย  Yalikua kama maigizo ya Filamu lakini lilikua tukio la kweli, nyakati zote hizo Mzeeย  Mwinyimkuu alikua akitabasamu akiwa anamtazama Mjomba Kambona.ย ย 

    โ€œMnaona anavyo nitazama, huyu anajua kila kituโ€ akasema Mjomba lakini hakuwa na ushahidi,ย  maneno yake yalikua ni sawa na kuupaka upepo rangi. Muda wote Mzee katili alikuaย  akitabasamu kwa mpango fulani ulio kichwani pakeย 

    Polisi walikosa ushahidi, ikaonekana kuwa Mjomba Kambona aliyakosea maelezo yake. Kibayaย  zaidi hata picha aliyowaonesha Polisi kuwa ndiye aliyeniowa ilikanwa kwa kuoneshwa Saleheย  mwingine na kilichotia nguvu kukosekana ushahidi ni maneno ya Mama Ashura. Angefanyajeย  Mjomba wangu zaidi ya kutoa kitambaa na kujifuta jasho ila moyoni aliamini Mzeeย  Mwinyimkuu alikua anajua wapi nilipo, pia hapakua na ushahidi mwingine sababu Mzeeย  Mwinyimkuu hakuhudhuria ndoa yanguย ย 

    Polisi wakamwambia Mjomba Kambonaย 

    โ€œTutaendelea na Uchunguzi, kwasasa wewe liachie jeshi la Polisi. Tutakupa taarifa ya Uchunguziย  juu ya Saida pia huyo Kaka yakeโ€ haikua kauli yenye matumaini, ilimvunja moyo sana Mjombaย  Kambona. Akamwambia Mzee Mwinyimkuuย 

    โ€œSaida hawezi kutoweka kirahisi, lipo unalolijua. Siondoki Rukwa hadi nihakikishe nampataย  Mpwa wanguโ€ alisema hivyo kisha aliongozana na Polisi kuondoka, Salehe feki na Mzeeย  Mwinyimkuu wakatazamana kisha wakawa wanawatazama namna Polisi na Mjomba Kambonaย  walivyokuwa wanaondoka.ย ย 

    Wala hawakufika mbali, kabla hata hawajapanda kwenye gari ya Polisi. Mjomba Kambonaย  alianguka na kufariki papo hapo akitokwa na Mapovu mdomoni. Licha ya jitihada za jeshi laย  polisi kumkimbiza Hospitali lakini alikua tayari amefarikiย 

    Taarifa ikarudi Dar-es-salaam kuwa Mtu waliyemtuma kuja kututafuta Mimi na Kaka Hamiduย  alikua tayari ameshafariki. Yalikua ni majonzi juu ya Majonzi, taarifa hii ilipomfikia Baba yanguย  alifariki pia kwa presha. Bundi aliizingira familia yangu, misiba miwili ndani ya siku moja,ย  Mzee Mwinyimkuu akashinda tena kwa kishindo kikubwa sana.ย 

    **ย 

    Nilihesabu siku ambazo nilikua ndani ya ile nyumba ya mateso, zilitimia siku saba ngumu.ย  Nilikonda nikawa kama Mtoto mdogo, niliishiwa nguvu. Kilichokuwa kimebakia kwangu ilikuaย  ni kufa tu. Kila nilipoamka nilijikuta nimeshaondolewa kidole kimoja, pumua yangu ikawa yaย 

    shida sana. Nikakosa uwezo wa kuwatambua Watu kirahisi, yule Bodaboda aliendelea kunileteaย  chakula kila siku lakini pia sauti ya Mwanaume mmoja kugumia ilikua ni sauti ya Kila sikuย 

    Lilikua ni jambo la kawaida sana yeye kupaza sauti, sikuwahi kufahamu alikua akipitia matesoย  gani, ila dakika za mwisho niligundua kuwa naye alikua akipelekewa chakula na huyu huyuย  Bodaboda anayeniletea Mimi chakula.ย 

    Sikuweza kusimama tena, vidonda vilianza kutoa funza sababu sikuwa na dawa yoyote isitosheย  joto la mle ndani liliniathiri kwa kiasi kikubwa, Mwenzenu niliwahi kufika Jehannam nikiwaย  Hai.ย 

    Basi siku moja yule Bodaboda alikuja, siku yenyewe palikua na mvua kubwa. Aliingia akiwaย  ameloa sana anatetemeka kwa Baridi, japo nilikua katika nyakati za mwisho kabisa za uhaiย  wangu lakini niliweza kugundua kuwa Baridi lilikua tatizo kubwa kwake. Alikua akiniandaliaย  chakula huku akitetemeka nikagundua anasumbuliwa na tatizo linalo sababishwa na Baridi.ย 

    Akajikaza, akaniwekea chakula. Alipaswa kunilisha sababu Mimi nilikua siwezi tena hataย  kushika kijiko, nilikonda mno hadi mishipa ya Damu ilikua ikionekana. Akajitahidi kuniinua iliย  kunikalisha kitako niweze kuegemea ukuta anilishe vizuri, siku hii nilipanga kuacha kula ili nifeย  mapema maana mateso yalinizidi kabisa, Jamani naposema nilikonda basi ujue nilikonda nikawaย  na kilo chache sana halafu kichwa kikawa kikubwa.ย 

    Nilitamani kumuuliza ana shida gani, huyu Mtu hakuwahi kunitesa wala hakuwahi kunisemeaย  jambo baya isipokua alikua hajibu maswali yangu yote niliyokuwa namuuliza.ย 

    Hali yake ilianza kuwa mbaya, akashindwa hata kunishikilia akaanguka chini na kuanza kugalaย  gala kwa maumivu Makali sana, mlango ulikuwa wazi hakuufunga sababu alipoingia alikuaย  tayari ana hiyo hali ya Maumivu, niliona ni nafasi ya kutoroka lakini sikuwa na akiba yoyote yaย  nguvu iliyobakiaย 

    Nikatamani kuendelea kuishi ghafla tu, namna pekee ya kuendelea kuwa hai ni kutoroka. Hukoย  nje mvua ilikua ikinyesha na kusababisha kelele kubwa sana kwenye Bati. Sikuwa na nguvu yaย  kusimama, nikaona ni bora nijiburuze nione kama naweza kufika njeย 

    Yule Bodaboda alipoona naanza kujiburuza akajua nataka kumtoroka, akili yake ikatamaniย  anizuie lakini mwili ulimsaliti, nguvu zilimwisha akiwa sakafuni anapumua kwa shida sana.ย  Nikaendelea kujivuta taratibu huku nikiwa ninasali Mungu niliyemkatia tamaa azidi kunipaย  nguvu, unajua kwanini niliamini naweza kuondoka pale?ย 

    Kwasababu hapakua na mtu mwingine aliyekuwa anakuja isipokua yeye, hivyo hakuna tena waย  kunizuia, halafu niliwaza kufika chumba ambacho yule Mwanaume anagumia ili kama yeye anaย  nguvu tusaidiane kutoroka.ย 

    Nilijiburuza kama nyoka hadi nilipotoka nje ya chumba kile, palikua na funguo kwenye kitasa.ย  Nikapata akili ya dharura kuwa huwenda funguo ile inaweza nisaidia kufungua milango mingineย 

    maana ilikua na funguo tatu zilizowekwa sehemu moja, naipataje Funguo ni lazima nisimameย  niichomoeย 

    Kivumbi kilianzia hapo, nilikonda Mimi kiasi kwamba upepo unaweza nipeperusha, Malaikaย  Mtoa roho alikua amenisimamia akiniuliza nasimama au achukue roho yangu, sijui nguvuย  zilitoka wapi nikasimama kwa kuyumba huku nikitetemeka. Nikachomoa funguo, ile natakaย  kupiga hatua nikaangukaย 

    Basi nikagugumia kwa maumivu, nilihitaji kufanya haraka maana kama yule Bodaboda atapataย  nguvu basi sitaweza tena kuondoka, nikamkumbuka Mama na Baba yangu, nikamkumbuka Kakaย  Hamidu. Ghafla nguvu zikaamkaย 

    Nikajikaza na kuanza kujiburuza sakafuni kama nyoka vile, kwa mwendo huo huo nilijikutaย  nikikiacha chumba kwa mbali kidogo, sikuufunga ule mlango wa chumba nilichomuachaย  Bodaboda.ย ย 

    Basi nilipofika kama chumba cha tano hivi nikasikia Mtu akiugonga mlango kwa nguvu hukuย  akisemaย 

    โ€œNjoo unitoe humu Mshenzi wewe, mtauwa wangapi. Siku ikifika mtakufa kama Kukuโ€ alisemaย  kwa hisia sana lakini hakujuwa kuwa Mimi nilikua tayari nipo mlangoni. Mlango ulikuaย  umefungwa, korido lilikuwa refu halafu vyumba vilikua mbali mbali. Nilijitahidi sana kusimamaย  nifungue mlango lakini nilikua nakosa nguvu, nilijaribu kama mara tatu lakini niliishia kuangukaย 

    Wakati nikiwa nimeanguka nikageuka nyuma, ndipo nilipomuona yule Bodaboda akijikongojaย  kwa maumivu kuja nilipo, alikua amelishikilia tumbo lake. Hapo sasa yule Malaika mtoa rohoย  nikamuona kama anachukua koleo kwa ajili ya kuichukua roho yangu.ย 

    Sauti ya yule Mwanaume ilizidi kusema, kibaya zaidi Mimi ndiye mwenye funguo halafu sautiย  yangu ilikua haitoki. Nikasema kama sisimami basi siondoki. Yule Bodaboda akawa anazidi kujaย  upande wangu kwa kasi akionekana kuanza kupiga hatua za nguvu. Nikamtaja Mungu nikasemaย 

    โ€œMungu nipe nguvu niishinde hii vitaโ€ nikajivuta haraka nikasimama nikiwa ninayumba,ย  nikaanza kusaka tundu la kuweka funguo maana nguvu yenye ilikua sifuri, nikawa najitahidiย  huku nikiwa natetemeka. Mara naingiza mara nakosea, huku yule Bodaboda akizidi kunisogelea,ย  hata nilipopaatia nilikua nimeingiza funguo isiyo yake.ย 

    Akawa karibu zaidi kiasi kwamba akipiga hatua tatu anakuwa amenifikia na kunizuia kuufunguaย  mlango, nikapapasia kwa bahati nzuri nikapatia funguo nikavuta nguvu za mwisho nikatekenyaย  kitasa lakini tayari Bodaboda alikua ameshanivaa na kuniangusha chini, Bahati nzuri ule mlangoย  ulikua tayari umeshafungukaย 

    Akatoka mwanaume mmoja na kuanza kumkita mateke yule Bodaboda hadi akamtupilia mbaliย  huko akiwa hoi sana anatokwa na damu mdomoni, eneo la Korido lilikua linawaka taa isipokuaย 

    vyumbani tu. Sikuamini macho yangu Mtu ambaye nilikuja kumuona na kumtambua japoย  nilimuona mara moja tuย ย 

    Alikua ni yule Mwanaume niliyemuazimaga simu kule Buchani, Ndio! Ni Abuu, masikini nayeย  alikua mateka wa Mzee Mwinyimkuu baada ya kujulikana ananifuatilia Mimi, kwa muda mfupiย  naye alikua amepungua sana japo alikua na nguvu.ย 

    Hakuniuliza chochote zaidi ya kuninyanyua na kuweka mkono wangu kwapani kwake tukawaย  tunaelekea nje, mvua bado ilikua inanyesha. Tulipokua tunakaribia kutoka kabisa tukamuonaย  Mtu anakuja Mbio, tena akikimbia kwenye mvua, ikatubidi tujifiche nyuma ya Mlango waย  kutokeaย 

    Yule Mtu alipofika, breki ya kwanza ilikua vyumbani kisha akamrudia yule Bodaboda aliyekuwaย  anagala gala. Akamuuliza kwa hasiraย 

    โ€œUmefanya nini Mpuuzi wewe?โ€ aliuliza kwa sauti ambayo niliitambua, ilikua ni sauti ya Mzeeย  Mwinyimkuu. Nilishtuka na kupata nguvu, nilipokumbuka kuwa yeye ndiye mtesi wangu basiย  mkojo ulinibana. Ghafla tu nikajiona ni Binadamu ninayehitaji kujiteteaย 

    โ€œNenda, hatuwezi kuondoka wote. Kaiambie Dunia kuhusu huyu Mzee, kama nitarudi tutakutanaย  na kama nitafia hapa basi Roho yangu itakua salamaโ€ alisema Abuu, roho iliniuma. Sikua naย  uwezo wa kuzungumza. Mdomo wangu wa juu na chini nilihisi kama vimeungana sababu nilikuaย  na vidonda mdomoni hivyo kukaa kimya ndiyo yalikua maisha yangu.ย 

    Nikaitikia kwa kutumia kichwa kisha nikasimama kama Mzimu, Mungu akaamua kunikumbuka.ย  Akanipa nguvu na ujasiri, alichotaka Abuu ni kumzuia Mzee Mwinyimkuu. Wakati naanza safariย  Mzee Mwinyimkuu akaja mbio nahisi alikua anaanza kutusaka, sijui alijuaje kuwa tunatoroka.ย  Huyu Mzee alikua Mchawi haswa, aliponikaribia tayari Abuu alimdaka Mzee Mwinyimkuuย  wakaanza kupalangana, muda huo nami nikaanza kujivuta kuondoka pale taratibu hadi nikaingiaย  kwenye mvua.ย 

    Ulikua mchana lakini anga lilikua na wingu la kutosha kiasi kwamba palikua na giza fulaniย  isitoshe palikua Porini. Nilipopigwa na mvua nikapata nguvu ya kuanza kuchanganya Miguuย  yangu vizuri. Nikaanza kukimbia huku nikiyumba kama mleviย 

    Sijui nilikimbia umbali gani lakini nilikimbia bila kuangalia nyuma, nilikimbia sana hadiย  nilichoka kabisa nikaanguka na kupoteza fahamu zangu.ย 

    Nilirudisha fahamu na kuanza kujitambua nikiwa naburuzwa kwa kasi sana, watu walikua kamaย  vile wamenizunguka. Walikua na mavazi ya kufanana, nilikua kwenye kitanda kiendacho kwaย  kasi mno, nikawasikia wakisemaย 

    โ€œApelekwe ICU Haraka sana, kazi ianze mara mojaโ€ niligundua nilikua Hospitalini, waleย  wauguzi walionekana kunikatia tamaa sababu nilikua na hali mbaya sana. Lakini mimiย 

    mwenyewe nilijiona ni mzima wa Afya zote, mahali nilipokuwepo palikua ni hatari zaidi yaย  Kuzimu.ย ย 

    Chozi lilinibubujika nikafumba macho yangu huku nikimshukuru Mungu. Madaktari walifanyaย  kazi yao kwa wiki tatu kuhakikisha najitambua zaidi, wakaniweka kwenye uangalizi maalumย  kwa kipindi chote hicho hadi nilipokumbuka yaliyonisibu.ย 

    Nikawaandikia jina Langu, mahali nilipotoka maana nilikua siwezi kuzungumza tena, Hospitaliย  ikasambaza jina na taarifa zangu ndipo Mama yangu alipokuja Mbeya akiongozana na Nduguย  wengine kunitambua. Mama alilia sana, sikuwahi kumuona Mama yangu akilia namna ile, yaleย  Maisha yaliniathiri sana kisaikolojia. Nikapoteza uwezo wa kuzungumza kabisa. Taarifa ya Kifoย  cha Baba ilinihuzunisha mno, ikanitoa chozi.ย 

    Polisi walipokuja niliandika maelezo yangu, ilikua baada ya wiki sita. Mwezi mmoja na sikuย  kadhaa, afya yangu ilianza kukaa sawa lakini sikuwa na Uwezo wa kuzungumza chochoteย  isipokua kuandika. Polisi walinichukua ili nikawapeleke mahali nilipoteswa yaani nyumbani kwaย  Mzee Mwinyimkuuย ย 

    Mimi na Mama tulienda, palikua ni pale pale kwa Mzee Mwinyimkuu. Namba ya nyumba ilikuaย  ni ile ile, mazingira yale yale, chozi lilinibubujika sana hadi Mama akashindwa kujizuia.ย ย 

    Nilikua natembezwa kwenye kiti cha Walemavu maana bado miguu ilikua haipo sawa pia sikuaย  na vidole nilikua najiuguza. Nikampa ishara Mama yangu kuwa anipeleke kwanza nyumbaย  jirani, pale kwa muuza chapati, nilimkuta Mwanamke mwingine kabisa akitengeneza chapati,ย  nikaandika kwenye karatasiย 

    โ€œMama Ashura yupo wapi?โ€ nilikua na ujumbe wa Mtoto wake Ashura nilitaka kwanza nimpeย  ujumbe, wakati huo polisi walikua wameizingira nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Mamaย  akamsomea yule Mwanamke, lakini cha ajabu eti akadai yeye ndiye Mama Ashura, nilishtukaย  alafu kingine kilichonipa mshituko ni kumuona Ashura mwenyewe, alikua ni Ashura yule yuleย  niliyemuona Nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuuย 

    Haya mambo yalinifanya nianze kuonekana akili yangu bado haiko sawa, nikajitahidiย  kuwaambia kwa maandishi lakini niliishia kupewa pole tu, kisha nikapelekwa kwa Mzeeย  Mwinyimkuu. Nako nikakutana na stori mpya kabisaย 

    Kwanza ile nyumba si ya Mzee Mwinyimkuu, hawamfahamu. Wao wanaishi hapo Kwa Miakaย  mingi, nilitokwa na Mchozi, nyumba ile ile mazingira yale yale lakini stori tofauti. Nikaombaย  niingizwe ndani, nikapelekwa kwenye chumba nilichokuwa nalalaย 

    Nikakuta magunia ya vyakula, tena kilikua chumba chenye makorokoro mengi sana naย  hakikuonekana kua chumba cha kulala Mtu. Mama akaniambiaย 

    โ€œSaida, najua umeteseka sana huku lakini hukumbuki chochote tena. Siku ukikumbuka nakuahidiย  tutarudi, yule Kijana na Baba yake watalipaโ€ Kauli ya Mama yangu ilinimaliza akili yangu,ย 

    nilifikia hatua nikakubali kuwa akili yangu haipo sawa, inawezekanaje kila kitu kibadilike kwaย  haraka vile. Hakuna aliyeniaminiย 

    Lakini sasa wakati natoka nikajikuta nikipeleka macho yangu jikoni, nikaiona ile sufuria kubwaย  ambayo kwa mara ya kwanza nilipika mchicha mwingi, nikashtuka alafu nikauona Mchichaย  mwingi ukiwa kwenye Beseni. Kilichonishtua ni kwamba nilimuona Msichana wa umri wanguย  akiutengeneza.ย 

    Nilijikuta nikipiga yowe kali sana. Hali ya afya yangu ikawa sio nzuri nikarudishwa tenaย  Hospitali. Tokea siku ile nilikua Msichana ninayekaa kimya hadi leo hii nawasimulia hiki kisa,ย  sikumpata Mzee MwinyiMkuu wala Salehe, lakini sitakubali. Siku moja nitarudi Rukwa iliย  walipe kwa maumivu na mateso makali ninayoyapitia hadi sasa.ย 

    Kwasasa nimerudishwa kwetu Dar-es-salaam, niko Magomeni. Maisha yangu yamekuwa yaย  Ukimya sana, Sijazungumza tena tokea siku ile nilipozungumza kwa mara ya mwisho Rukwa,ย  sijaandika chochote na wala sitaki kusema chochote kile ila kupitia mkasa huu nataka ujifunze.ย 

    Kamwe kwenye Maisha yako usiolewe au kuowa Mtu usiye mfahamu, Dunia ni Kichaka chaย  Mateso. Wasichana wengi wanayapitia mateso niliyoyapitia, wengi wanauawa, wengi wanapataย  ugonjwa wa akili. Hata wanaume wapo waliopoteza kila kitu, Siku nikifungua kinywa changuย  nitawasimulia mengi, kwasasa naishia hapa, naweka kalamu yangu chini.ย 

    AHSANTE……….MWISHO

    Comments zikiwa nyingi TUNAANZA MPYA Chaap

    USISAHAU PIA Kununua Kitabu Cha KOTI JEUSI Kwa Kutuma Message WhatsApp Namba+255760871896 Ufikishiwe Mpaka Ulipo

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapaย 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xxย  Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    23 Comments

    1. Mwaija Seleman on January 13, 2025 5:00 pm

      Hadi mwili umenisisimka ๐Ÿ™Œ

      Reply
    2. Halinga1 on January 13, 2025 5:03 pm

      Kaka umetisha

      Reply
    3. Mama Edward on January 13, 2025 5:05 pm

      Wowoooh fupi na inafundisha sana nmepata somo apa nmejifunza mengi poleee saida wetu.

      Reply
      • Amasa tz on January 14, 2025 7:36 am

        Hatar sana,, mungu amekpgania pakubwa,, mm kama kijana ambae sjaoa hakka nmepata kitu kwa riwaya hii,, mungu akupe maisha mazur

        Reply
    4. Egibeth on January 13, 2025 5:05 pm

      Dag

      Reply
      • jas on January 15, 2025 10:57 pm

        pole sana

        Reply
    5. Eva Mpume on January 13, 2025 5:22 pm

      Jamani hatujajua mwisho wa kijana aliyemukoa Saida,,, mwandishi ungesogeza kidogo

      Reply
    6. G shirima on January 13, 2025 5:31 pm

      Lini utafungua kiywa Chako tuendelee maan bado nataka kujua zaid

      Reply
    7. Ahmed Ruta on January 13, 2025 5:46 pm

      Hahahahaha๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜… umepigaje apooooooooooooooโœ๏ธ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

      Reply
    8. Ahmed Ruta on January 13, 2025 5:48 pm

      Navuta picha mwandishi mwili wako ulikua kama wa Ile muv BABU SISU

      Reply
    9. Msangazi Rams on January 13, 2025 6:50 pm

      Hii ya leo machozi yamenibubujika sijui nisemeje lakin naamin Allah anajua zaid yaliyopo mioyon mwetu wanadamu

      Reply
    10. Fawziya Hassan on January 13, 2025 7:30 pm

      Maskini Saida jamani ๐Ÿ˜ฅ
      Simulizi ya Maajabu Nzuri yenye mazingatio makubwa jamani
      Uchawi upo
      Ila uchawi wa MwinyiMkuu ni zaidi ya Uchawi
      Mungu atunusuru maisha yetu na Wachawi
      Mungu AWAANGAMIZE WASHIRIKINA WOTE MOTONI.
      Ameen.

      Reply
    11. Fatbaloz on January 13, 2025 11:32 pm

      Safi sana mtunzi tumejifunza sana mim pamoja nawasomaji wenzangu Big up

      Reply
    12. Dorcus semu on January 14, 2025 12:07 am

      Inauzunisha sana pole saida ๐Ÿ˜ข

      Reply
    13. Cathbert on January 14, 2025 7:16 am

      Kazi mzuri na pole sana

      Reply
    14. Abuu bura on January 14, 2025 7:20 am

      ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญnimelia kama mtoto

      Reply
    15. Steven on January 14, 2025 10:35 am

      Daah atali

      Reply
    16. Juma on January 14, 2025 6:51 pm

      Ni hatar

      Reply
    17. Gyakiee on January 15, 2025 6:16 am

      Munguu hamtupii mja wake hakika Munguu ni mwemaa

      Reply
    18. Given Gihsy on January 16, 2025 2:56 pm

      ๐Ÿฅนnianze kwa kuhiluzunika ,ila mtu kuna sehem nmecheka dadeq, KWAMBA NYIE WASHENZ NIFUNGUENI MTAKUF KAMA KUKU , YAN MUUNI YUPO KWENY MATATZO ILA BADO AJAL, KWEL MAN IS STRONG NATURAL

      Reply
    19. Perfect on January 18, 2025 11:23 pm

      Kwani story ni yakwel

      Reply
    20. Sharo love malkx ๐Ÿ’– on January 24, 2025 8:25 am

      Dah sijui niseme nini
      Mhhh ila pole

      Reply
    21. ๐Ÿ—’ ๐Ÿ”” Alert - 0.3 BTC waiting for withdrawal. Confirm >> https://graph.org/Get-your-BTC-09-04?hs=245ecef015fd586244ce32903a04bac6& ๐Ÿ—’ on October 17, 2025 1:46 am

      gx3yc0

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Hadithi February 23, 2026

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Ilipoishiaย  Kwanza nilijiuliza ni Nani anayeweza kuja kwetu, kama Mama Amida tayariย  tulishazungumza. Nilimeza funda…

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.