Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya sita

Ghafla, akajikuta ameshika kisu, mikono yake ikiwa imelowa damu. Aliangalia chini— Upendo alikuwa amelala mbele yake, kifua chake kikiwa kimechomwa na kile kisu. 

Macho yake yalikuwa wazi, yakimkodolea kwa masikitiko na hofu. Alitaka kupiga kelele,  lakini sauti haikutoka. 

Sauti nzito, yenye mwangwi, ilianza kuzunguka kichwani mwake, sauti ya Bi. Lugumi.  “Huwezi kuukwepa ukweli, Zahoro… Laana ni yako sasa.”  

SEHEMU YA SABA

Aliangalia mikono yake tena, damu ilizidi kububujika. Upendo alinyanyua mkono wake  dhaifu, akajaribu kumgusa, lakini akayeyuka na kugeuka kuwa moshi mweusi. Kijiji  kizima kiliwaka moto, sauti za vilio zikiwa zinamzingira. Akakimbia, lakini popote  alipogeuka, miili ilikuwa ikimzunguka. 

Kwa mshangao, aliona sura ya baba yake kati ya maiti. Baba yake alifumbua macho,  akamkazia Zahoro kwa majonzi. “Umechelewa, mwanangu.” 

Zahoro alipiga kelele na kuamka kwa nguvu, mwili wake ukiwa umetapakaa jasho.  Alipumua kwa kasi, macho yake yakizunguka chumba kile cha giza. Kibatari bado  kilikuwa kinawaka kwa utulivu. Upendo alikuwa amelala pale pale, pumzi yake ikiwa  tulivu. 

Aliweka mkono wake kifuani, akihisi moyo wake ukidunda kwa nguvu. Ndoto hiyo  ilikuwa halisi mno, na sauti ya Bi. Lugumi bado ilionekana kunong’oneza kichwani  mwake. 

Akiwa bado na woga, alijisogeza karibu na Upendo, kuhakikisha kuwa yupo salama. Hali  ilikuwa shwari… kwa sasa 

Asubuhi ilipofika, nuru dhaifu ya alfajiri ilianza kupenyeza kupitia nyufa za kuta  zilizochakaa. Zahoro alifumbua macho yake kwa tahadhari, bado akiwa na  kumbukumbu ya ndoto ya kutisha aliyoota usiku uliopita. Aligeuza kichwa kumtazama  Upendo, ambaye bado alikuwa amelala, uso wake ukiwa na utulivu wa kinafiki—utulivu  wa mtu aliyekumbwa na machovu ya dunia. 

Alisimama taratibu, akanyosha viungo vyake vilivyokuwa vimechoka. Kibatari kilikuwa  kimezimika, na upepo wa asubuhi ulivuma polepole. Upendo alishtuka kidogo na  kufumbua macho yake, kisha akamtazama Zahoro kwa macho yaliyojaa swali. 

“Ni asubuhi,” Zahoro alisema kwa sauti ya upole. “Tunapaswa kutoka hapa na kutafuta  mahali salama.”

Upendo alikaa sawa, akivuta pumzi ndefu. Hali ya kijiji ilikuwa kimya mno, kimya cha  kutisha kilichoashiria kuwa hakuna kilichoisha. Walijiandaa kwa tahadhari, wakafungua  mlango taratibu na kuchungulia nje. Damu iliyokuwa imekauka ilipamba ardhi, na  upepo mdogo ulisomba majani makavu. Hakukuwa na ishara ya maisha, lakini walijua  kuwa hatari bado ilikuwepo. 

“Twende,” Zahoro alisema, akimshika mkono Upendo kwa upole. Wakatoka nje kwa  umakini, nyayo zao zikipita juu ya ardhi iliyojaa alama za machafuko. Hatua kwa hatua,  walitafuta mahali pa kuelekea, mioyo yao ikiwa mizito kwa hofu isiyosemeka. 

Palikua kimya kama Sehemu iliyopitiwa na vita Kisha Kila Mtu kufa, ardhi ilijaa Damu  na maiti. Upendo alikua mwenye hofu Kila alipokutana na maiti, hapa kua na kiumbe  chochote kilichokua kikitembea, upepo ulikua umetulia sana.  

Walipiga hatua zao taratibu huku wakiangalia Kila upande kwa tahadhari kubwa,  Upendo alikua akitetemeka. Zahoro alikua ameuvaa uanaume kwa kua jasiri anaye  mwongoza Upendo kutafuta msaada zaidi. 

Ghafla, Zahoro alisimama. Upendo aliyekua nyuma ya Zahoro pia alisimama, Upendo  hakujua ni kwanini Zahoro alikua amesimama, alikua akimtazama kwa nyuma bila  kusema chochote kile. 

Zahoro alikua akiangaza macho yake kwa umakini, mara upepo wa ajabu ulianza,  majani kidogo na vumbi vilianza kujiumba taratibu mfano wa kimbunga kidogo. Zahoro  akamgeukia Upendo na kumtaka asiseme chochote kile sababu palikua na dalili ya  uwepo wa Mzimu wa Bibi Lugumi. 

Mara walianza kuisikia sauti ya ajabu ya Bibi Lugumi, sauti hiyo ilikua ikisikika kutokea  mbali lakini taratibu ilianza kufika walipo, Zahoro akamwambia Upendo azibe masikio  yake halafu taratibu wakasogea na kujificha nyuma ya Mti mmoja mahali ambapo  palikua na Migomba. 

Ule upepo ulikua unaongezeka taratibu. Walikua macho kutazama ni kitu gani  kingetokea, Upepo ulizidi kuvuma huku sauti ya Bibi Lugumi ikiwa inapaa, Upendo  alikua akitetemeka kwa hofu na Mashaka, wasiwasi ulikua ukimwendesha kwa kiasi  kikubwa 

Hakuna aliyejua nini kingetokea hapo, taratibu ule upepo ulipungua. Vumbi lilikua  limetapakaa kutokana na ule upepo wa ajabu Kisha Hali ya hewa ilibadilika na kua  shwari kabisa, kivuli kirefu kilionekana. 

Hata Zahoro alianza kuingiwa na hofu mno, alimshikilia vizuri Upendo huku akimpa  ishara ya kumtaka asipige kelele yoyote ile sababu alionekana kutetemeka hivyo  angeweza kumpiga kelele za hofu. 

Kivuli hicho lilikua Cha Kiumbe Cha ajabu sana ambacho lilikua na taswra ya Binadamu  wa kutisha, aliyechongoka pua mithiri ya Mzimu wa ajabu. Alikua na macho makali  yenye kuwaka kama taa nyekundu yenye mionzi mikali sana.

Hali ya kutetemeka iliendelea kwa Upendo na Zahoro, hawakuwahi kushuhudia kiumbe  Cha kutisha kiasi hiki, pumzi za Upendo zilikua zinaingia na kutoka kwa Kasi sana huku  mapigo ya moyo wake yakidunda kwa Kasi kama Ngoma.  

Zahoro akageuka na kumtazama Upendo Kisha akamwambia kwa sauti ya kunong’ona  iliyojaa hofu. 

“Usipige kelele, tuondoke taratibu” Upendo akaitikia kwa kutumia kichwa, midomo  yake ikiwa inatetemeka huku chozi likiwa linamtoka mwili mzima. 

Pole pole kwa tahadhari kubwa Zahoro alikua wa Kwanza kusimama, Kisha Upendo  akafuatia huku ule Mti ukiwa umewakinga na kile kiumbe Cha ajabu kilichokua  kimesimama kwa hisia ya kuhisi uwepo wa Binadamu hapo.  

Zahoro akamwongoza Upendo kuondoka hapo huku wakikwepa sauti yoyote ya  Mkanyago eneo Hilo lenye majani mengi makavu. Taratibu waliendelea kupiga hatua,  lakini ghafla simu ya Zahoro ilianza kuita. Ile sauti ikakishtua kile kiumbe Cha ajabu  Kisha kikageuka na kutazama uelekeo wa sauti ya simu. 

Zahoro aligeuka taratibu nyuma, akakiona kiumbe kikiwa kinamtazama. 

“Tukimbie” akasema Zahoro, wakaanza kukimbia ili kujiokoa kutoka kwa kiumbe kile  Cha ajabu. Kadili walivyokua wakikimbia kwa nguvu ndivyo kile kiumbe kilicho  ambatana na upepo mkali kilivyokua kinawakimbiza. Zahoro alihisi miguu yake ilikua  imefungwa mota, alikua anakimbia kuliko uwezo wake wa kawaida lakini kikwazo Cha  yeye kufika mbali zaidi lilikua ni Upendo ambaye alikua akikimbia kwa hofu bila  mpangilio mzuri. 

Zahoro alijitahidi kukimbia pamoja na Upendo lakini kiumbe lilikua kinawafikia kwa  haraka zaidi. Hatimaye Upepo mkali ulikua hatua Moja kuwafikia na kuwasomba. 

** 

Nje ya Kijiji Cha Nzena. 

Mtu mmoja aliyesimama mbele ya Waziri alitikisa kichwa chake huku akiwa ameshikilia  simu mkononi. Waziri wa Maliasili akakuna shingo yake huku akibana Taya zake kwa  jaziba. 

Jioni ilikua tayari imeingia, mpango kazi wa kugundua chochote kuhusu Kijiji Cha  Nzena ulikua umekwama kwa siku hiyo. Simu iliyokua ikipigwa kwa mmoja wa Watu  walio ndani ya Kijiji ilikua haipokelewi. Haikua rahisi kukiacha Kijiji hicho kiende na  utajiri mkubwa wa Madini, walikua tayari wameshajenga Mahema kwa ajili ya makazi  eneo Hilo la pori. 

Giza lilipoingia liliwakuta wakiwa wanakunywa kahawa inayofuka mvuke, redio ilikua  ikitoa baadhi ya taarifa ambazo masikioni mwa Waziri zilikua zinaitesa akili yake  akaamua kuizima. Maafisa waliomzunguka walijua ni kiasi gani alikua ametingwa. 

Siku iliyofuata, Serikali iliongeza Watu zaidi ili kumsaidia Waziri kazi ya utafiti eneo la  tukio, sio TU wataalam kutokea Ganza bali Afrika nzima pamoja na Mataifa kadhaa ya 

Ulaya. Sayansi ilikataa kutoweka kwa Kijiji hicho lakini shahidi za kimazingira ikiwemo  ramani pamoja na Wakazi wa vijiji jirani zilichagiza uzito wa jambo lenyewe. 

Pamoja na uwepo wa Sayansi lakini nyuma ya pazia Waziri Majula Majula alikua  akishirikiana na Mganga aliyemwamini huku akiwa amepoteza Imani na Sayansi ya  Mazingira ambayo ilikua ikiendelea Kuchunguza kupotea kwa Kijiji Cha Nzena. 

Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA NANE Hapa Hapa Kijiweni

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

6 Comments

Leave A Reply

Exit mobile version