Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Tisa-09)
    Hadithi

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Tisa-09)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 5, 2025Updated:May 6, 202515 Comments9 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 08

    Hakika nilikua katika nyakati ngumu zaidi kuwahi kupita kwenye maisha yangu. Hapakua naΒ  yeyote pembeni yangu, nilipoinua macho baada ya kujifuta mchozi nilimwona Mama yanguΒ  Mzazi kitu ambacho kilinishtua sana. Mtu ambaye tulimzika siku chache zilizopita alikuaΒ  amesimama mita kadhaa karibu na Bustani ya Mauwa.Β 

    Alikua amevalia mavazi meupe kama ambavyo inasemekana Malaika huvalia, alikua msafi sanaΒ  kiasi kwamba alikua aking’aa mithiri ya Kioo juani, halafu alikua akitabasamu sana. MachoΒ  yalinitoka nikimtazama Mama yangu, nilijua Mama yangu amerudi kunisaidia kwenye hii vita. Endelea

    SEHEMU YA TISA

    Palikua tulivu ghafla, hapakua na upepo wa aina yoyote ule. Nilitamani kusogea niongee naΒ  Mama yangu pengine alihitaji kuzungumza na Mimi. Mama alinionesha ishara ya kumsogeleaΒ  anikumbatieΒ 

    β€œMamaa‼” niliita kwa sauti ya chini, chozi nalo lilidondoka kwa kasi huku majonzi yakiwaΒ  yametanda. Nilitembea taratibu kumuelekea Mama yangu huku nikimtazama sana, MamaΒ  hakuacha kutabasamu. Nilisogea karibu zaidi, kila hatua ilizidi kunisogeza karibu naye naΒ  kumtazama kwa makini zaidi, alikua ni Mama yangu kabisaΒ 

    Nilibakisha hatua chache kuelekea alipo, niliona nitachelewa pengine ataghaili na kuondoka,Β  nilipiga hatua iliyoambatana na mkimbio. Mazingira yalikua kama yameganda hivi, Dunia kamaΒ  ailikua imesimama hivi.Β 

    Ghafla nililiona shimo kubwa ambalo hatua yangu ilikua ikilielekea shimo lile, hapakua tena naΒ  Mama yangu isipokua Mimi kujiokoa nisitumbukie ndani ya shimo, niligundua ulikua mtego naΒ  bahati nzuri niliweza kufunga breki ya haraka kiasi kwamba niliyumba huku nikijinasua,Β  hatimaye nilifanikiwa kutoingia ndani ya shimo lile.Β 

    Mara nilianza kuisikia sauti ya Mama yangu akicheka kwa kutisha sana. Sauti yake ilikuaΒ  ikiniumiza masikio yangu kiasi kwamba nilihisi kizunguzungu, nilipepesuka kama mlevi.Β  Nikajishikiza ukutani hadi nikafika mlango wa kuingilia ndani.Β 

    Ile sauti ilipotea, ukimya ulianza tena. Yaani palikua na hali tofauti tofauti kila hatua ninayoipiga,Β  mapigo ya moyo yalikua yakizisindikiza hatua zangu. Niliinua macho na kuziangalia ngaziΒ  zinazoelekea juu, kisha nilishusha macho yangu kuelekea kwenye korido ambayo kile chumbaΒ  nilichoambiwa kilikua kinapatikana.Β 

    Hapakua na sauti nyingine isipokua sauti ya kudunda kwa moyo wangu na sauti ya pumzi zanguΒ  zilizokua zikitoka na kuingia bila mpangilio. Nilisimama nikifikiria nielekee wapi, kitu chaΒ  kwanza nilitaka kua na uhakika kua lile jini halipo ndani ya nyumba.Β 

    Mahali pekee ambapo ningeweza kua na uhakika ni kupitia dirisha la Chumbani kwangu,Β  nilipandisha ngazi kuelekea chumbani kwangu. Nilipofika, nilijipa sekunde kadhaa kabla yaΒ 

    kufunua pazia. Nyumba ya yule Mzee jirani ilikua kimya sana, nilikua najua fika kua ilikuaΒ  ikikaliwa na yule jini MzeeΒ 

    Ukimya bado uliendelea kutikisa nyumba nzima na nyumba jirani, niliwaza kwa haraka atakuaΒ  yupo wapi. Niliutazama mkono wangu wenye shanga ya Ulinzi, nilikua na uhakika kuaΒ  asingeliweza kunidhuru kwa mikono yake isipokua kwa akili na kutumia viumbe vingine kamaΒ  alivyofanya wakati ule alivyowatumia Wazazi wangu.Β 

    Nilijiambia moyoni kua sipaswi kuamini chochote kile sababu unaweza kua mtego kamaΒ  alivyotaka kuninasa dakika chache zilizopita kupitia taswira ya Mama yangu.Β 

    Kuishi ndani ya ile nyumba lilikua ni wazo lililogoma kukubaliwa na moyo wangu, nilipaswaΒ  kuifanya kazi niliyoambiwa siku ya leo, kwakua sikumwona yule jini na palikua kimya sana,Β  niliona ni muda muafaka wa kwenda chumba cha chini kuitoa nafsi ya Sabra.Β 

    Niliuelekea mlango taratibu, kwakua nilikua nimeufunga nililazimika kuufungua ndipo nitokeΒ  chumbani kwangu, palikua tulivu sana kiasi kwamba kila hatua yangu niliisikia vyema. Sauti yaΒ  Bawaba za mlango zilipiga kelele wakati naufungua mlango, nilishupaza shingo yangu naΒ  kuminya macho yangu huku nikiendelea kuufungua mlango kwa adabu sana.Β 

    Nilipomaliza kuufungua Mlango, zoezi la kutoka chumbani lilianza taratibu, nilishusha ngaziΒ  baada ya kuimaliza korido fupi kutoka chumbani kwangu. Nilitembea taratibu na kwa tahadhariΒ  kubwa, nilipofika ngazi ya mwisho nilianza kuisikia ile sauti ya Mwanamke anayeimba.Β 

    Alikua akiimba kwa masikitiko sana japo sikuitambua lugha yake ila sauti yake ilinifanya nihisiΒ  masikitiko yake, nilisimama nikiendelea kuisikia huku nikifikiria nini cha kufanya, nilisimamaΒ  kwa dakika kama mbili hivi nikiendelea kutafakari, mwisho niliamua kuifuata ile sauti. HapoΒ  moyo wangu ulikua umekufa kwa woga, mwili wangu ulikua hauna nguvu, nilikua natetemekaΒ  sana.Β 

    Kila mara niligeuza macho yangu huku na kule nikiwa kwenye korido naelekea chumba chaΒ  mwisho ambacho ndimo lile shimo la kuelekea kaburini lilikuwamo. Nilipofika niliuwonaΒ  Mlango ukiwa umefungwa, sauti ya kuimba wala haikukoma isipokua ilikua ikihama kadiriΒ  nilivyokua najaribu kusogea hadi nilipofika Mlangoni.Β 

    Kitasa cha mlango kilikua kinaniangalia Mimi, nami nilikitazama huku mkono wangu ukiwa naΒ  shahuku ya kukitekenya kitasa hicho chenye rangi ya dhahabu, kitasa cha kizamani chenyeΒ  urembo wa maua. Niliutoa mkono wangu, ukasogea hadi kukikamata kitasa kisha nikakitekenyaΒ  kikatoa sauti ya kufunguka.Β 

    Upenyo mdogo ulionekana baada ya mlango kufunguka kidogo, nilihitaji ujasiri wa ziada iliΒ  kupeleka macho yangu ndani. Mwili ulianza kusisimka, nywele zilinisimama kichwani mwanguΒ 

    Haikua hali ya kawaida, ilikua ni hali ya hatari. Mara nilianza kusikia sauti ya kitu kikitembea,Β  kwa namna nilivyokua nakisikia kitu hicho wala hakikua Binadamu wala Mdudu isipokua ni kituΒ 

    cha ajabu sana, kishindo kilikua kinasikika kwa uzito sana halafu paliongezeka sauti nyingineΒ  kama ya kiatu kirefu cha kike hivi. Sauti hiyo ilikua ikisikika nyuma yangu, niligeuka harakaΒ  kuangalia, niliambulia kuona kivuli cha kutisha sana.Β 

    Kiumbe hicho kilikua bado hakijafika kwenye ile korido ya kuelekea chumbani, nilifikiria niniΒ  cha Kufanya. Haraka Ubongo wangu ukaniambia niingie ndani ya chumba hicho maana nyumaΒ  palikua haparudiki. Niliingia halafu kwa taratibu sana niliufunga mlango, nikawa nimejifungia,Β  sauti ya yule Mwanamke kuimba ilikoma.Β 

    Pakawa kimya sana, ndani ya kile chumba cha stoo kilikua vile vile, vitu vingi tulivyoviwekaΒ  vilikaa kwa mpangilio ule wa Mwanzo, nilitafuta lile shimo la ajabu lakini halikuwemo. SasaΒ  nikaona ni bora nijifiche huwenda kile kiumbe cha ajabu kingeweza kuingia ndani ya kileΒ  chumba.Β 

    Nilijibanza mahali nikisikiliza nini kitakachotokea, ile sauti ya kishindo ilianza kuja karibu nami.Β  Nilizidi kuogopa, jasho la hofu lilikua likinimwagikaΒ 

    Kile kishindo kiliishia mlangoni kisha palikua kimya sana. Kimya kiliendelea kwa kitamboΒ  kirefu kama cha dakika kumi na tano hivi hadi nilianza kujiuliza maswali mengi yasiyo naΒ  majibu. Kwanza nilijiulza kishindo kile kilikua cha kiumbe gani, pili nilijiuliza kiumbe hichoΒ  kilikua kimeondoka pale mlangoni au nini kilimfanya awe kimya.Β 

    Nikataka kujua, nikasimama ili nielekee mlangoni, mara ghafla mlango ulifunguliwa harakaΒ  sana, pale pale nilijibanza tena kwa uhakika kabisa kua sijaonekana, ule mlango niliupa begaΒ  huku shingo yangu nikiwa nimeikata upande mwingine. Sikutaka kuangalia ni Nani aliyeufunguaΒ  ule mlangoΒ 

    β€œCelin upo hapa?” nilisikia sauti ya yule Bibi jini, nilizidi kutetemeka. Nikauziba mdomo wangu.Β  Aliendelea kuniita kwa sauti ya kunong’ona, sauti yake ilikua na nguvu sana kiasi kwambaΒ  nilijizuia sana nisiitikieΒ 

    Sikujua kama alikua amegundua nipo ndani ya kile chumba au la. Niliendelea kupumua kwa shida, nilisali sala zote. Basi, naona hakuwa na uhakika kuwa nipo ndani ya kile chumbaΒ 

    Taratibu nami nilitaka kumwona, nilikua na uhakika kwa asilimia zote kua hajagundua chochote.Β  Niligeuza shingo yangu taratibu huku macho yangu yakiwa makali niweze kumwona,Β  nilipofanikiwa kugeuza shingo ndipo nilipokiona kiumbe cha kutisha sana.Β 

    Kwa uhakika alikua na umbo la Binadamu, alivalia gauni chakavu lenye rangi nyeupe, nyweleΒ  zake zilikua chafu pia halafu ni ndefu sana kiasi kwamba zilikua zinakaribia kiunoni mwake.Β  Alikua na kucha ndefu sana kama ndege tai, alikua amenipa mgongo na laiti kamaΒ  angelinionesha sura yake basi ingelikua mbaya zaidi.Β 

    Miguuni alikua na kwato kama za ng’ombe, kiukweli kilikua kiumbe cha ajabu kuwahi kukionaΒ  maishani mwangu. Mwili ulikua unaendelea kusisimka tu, cha ajabu baada ya dakika kama mojaΒ 

    na ushee hivi alibadilika kutoka kwenye lile umbo na kua yule Bibi Kizee ambaye ni jiniΒ  MuuwajiΒ 

    Moyo wangu ulizidi kwenda mbioo nikikumbuka namna alivyosababisha nikamuuwa MamaΒ  yangu, kifo cha Zena na Caren chanzo ni yeye. Aligeuka huku na kule kama vile alikuaΒ  akihakikisha kua hakuna anayemwona. Kisha alisogea mbele kidogo karibu na pembe ya ukutaΒ  akasemaΒ 

    β€œFungukaa‼” sauti yake ilikua kali ya kutisha, mara lile shimo la ajabu lilifunguka. Huu sasaΒ  ndio mlango wa kuelekea kaburini kwenye nafsi ya Sabra, shimo namna lilivyofungukaΒ  lilinishtua sana nikakumbuka ile siku nilimwona Baba na Mama wakitoka kwenye shimo lileΒ  wakiwa uchi wa mnyama.Β 

    Nilimwona yule jini akiingia ndani ya shimo hilo lenye rangi jekundu, lilikua mfano wa mlangoΒ  wa Andaki hivi lenye kuwaka rangi nyekundu na moshi mithiri ya mvuke wa maji ya moto.Β  Baada ya yeye kuingia ndani ya shimo palijifunga kama vile hapajatokea kitu chochoteΒ 

    Nilistaajabu sana, nilisogea taratibu kwa tahadhari kubwa. Hapakua na shimo lolote wala daliliΒ  kwamba pana mlango, nililitafuta lakini ilikua ni sawa na kujiuliza maswali yasiyo na majibu.Β  Nilibaki nikiwa nimesimama sijui naanzia wapi ili nami niingie humo kwenye shimo labdaΒ  ningeweza kuipata mafsi ya Sabra.Β 

    Roho iliniuma kuona nimefeli zoezi muhimu sana ambalo lilikua ni hatua kubwa kwangu kufikiaΒ  hitimisho ya matatizo yanayoikumba familia yangu. Nilifikiria nami nifanye kama alivyofanyaΒ  ili lile shimo lifunguke. Nilisogea pale karibu na pembe ya ukuta kisha nikasemaΒ 

    β€œFunguka‼” mara ya kwanza hapakua na chochote kilichotokea, nikarudia tena na tena. Zaidi yaΒ  mara tano lakini shimo halikutokea. Nilitamani nilie maana sikua na uwezo wa ziada waΒ  kutambua mambo mengi isipokua machache ambayo yule Mwanaume aliyejitambulisha kamaΒ  Haji aliniambiaΒ 

    Basi nilikata tamaa, chozi lilinibubujika. Nikajikuta nikipandwa na hasira sana, nikasema kwaΒ  mara ya mwisho kwa sauti kubwa ya hasira huku chozi likinibubujikaΒ 

    β€œFungukaaaβ€Ό!” ghafla tu nililiona lile shimo la ajabu likifunguka nyuma yangu, palikua panatoaΒ  mvuke na joto kwa mbali, rangi nyekundu ilikua imelizunguka shimo lile, nilichungulia ndani yaΒ  shimo maana sikuwahi kuingia hivyo nilikua sijui chochote kile hata kunaonekanaje nilikua sijui.Β 

    Nilitumia muda mrefu nikiliangalia tu, kisha niliisikia sauti nzito ikiuliza kutoka ndani ya shimo.

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI

    COMMENTS ZIWE NYINGI SASAΒ 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

     

     

    riwaya mpya riwaya za kuvutia soma riwaya bure

    15 Comments

    1. Nailaty on May 5, 2025 7:59 pm

      Asanteee mambo yanazid kunoga

      Reply
    2. David ben on May 5, 2025 8:25 pm

      Nzuri

      Reply
    3. Aura on May 5, 2025 8:28 pm

      Ooh to be continued………………πŸ₯€

      Reply
    4. Rio on May 5, 2025 9:26 pm

      Sehemu ya 9 iwe mapema daah kali sana

      Reply
    5. Said on May 5, 2025 9:28 pm

      πŸ™πŸ™πŸ™πŸ€πŸ€πŸ€

      Reply
    6. Piana on May 5, 2025 9:28 pm

      Admin tuletee sehemu ya 10
      Ni nzuri sana πŸ‘Œ

      Reply
      • Erick Elisha on May 6, 2025 8:01 am

        Ongeza utamu wa mziki DJ wapi sehemu ya kumi

        Reply
    7. Salma on May 5, 2025 9:29 pm

      Tamuu

      Reply
    8. Shedrack on May 5, 2025 10:19 pm

      Next⏩ episode

      Reply
    9. nyamwirila manumbu on May 5, 2025 10:28 pm

      Nzuri sana ila inatisha sisi tulio masingle kusoma usiku nijau

      Reply
    10. Yahaya on May 6, 2025 12:53 am

      Daaah hii kituu kadrii unavyo zidiii som nd utamu unazidii kukoleaa aiseeh!!! Inasisimuaa snaa snaa BRAVO βœ…..

      Reply
    11. KingzJeelay on May 6, 2025 6:43 am

      Sauti kutoka ndani ilikuw unauliza nini πŸ€·πŸ½β€β™‚οΈπŸ€·πŸ½β€β™‚οΈπŸ€·πŸ½β€β™‚οΈπŸ€·πŸ½β€β™‚οΈ
      Tunakungoja Kaka mkubwa tumalzie mission impossible yetuπŸ™„πŸ™„πŸ€£πŸ™„πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½

      Reply
      • Karimu on May 7, 2025 3:02 pm

        Kazi mzuri

        Reply
    12. [email protected] on May 6, 2025 3:45 pm

      Mbona sehemu ya 7 na 8 sijaona majama

      Reply
    13. πŸ“ + 1.13200 BTC.NEXT - https://graph.org/Ticket--58146-05-02?hs=3f9505a64f17ee5b35ce0a78993c6557& πŸ“ on May 11, 2025 1:57 am

      lwwiy0

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 12, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya kwanzaΒ  β€œBaba” aliita Zahoro, Mzee Miroshi alimtazama Zahoro bila…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.