Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Tisa-09)
    Hadithi

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Tisa-09)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 5, 2025Updated:May 6, 202516 Comments9 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 08

    Hakika nilikua katika nyakati ngumu zaidi kuwahi kupita kwenye maisha yangu. Hapakua naย  yeyote pembeni yangu, nilipoinua macho baada ya kujifuta mchozi nilimwona Mama yanguย  Mzazi kitu ambacho kilinishtua sana. Mtu ambaye tulimzika siku chache zilizopita alikuaย  amesimama mita kadhaa karibu na Bustani ya Mauwa.ย 

    Alikua amevalia mavazi meupe kama ambavyo inasemekana Malaika huvalia, alikua msafi sanaย  kiasi kwamba alikua akingโ€™aa mithiri ya Kioo juani, halafu alikua akitabasamu sana. Machoย  yalinitoka nikimtazama Mama yangu, nilijua Mama yangu amerudi kunisaidia kwenye hii vita. Endelea

    SEHEMU YA TISA

    Palikua tulivu ghafla, hapakua na upepo wa aina yoyote ule. Nilitamani kusogea niongee naย  Mama yangu pengine alihitaji kuzungumza na Mimi. Mama alinionesha ishara ya kumsogeleaย  anikumbatieย 

    โ€œMamaaโ€ผโ€ niliita kwa sauti ya chini, chozi nalo lilidondoka kwa kasi huku majonzi yakiwaย  yametanda. Nilitembea taratibu kumuelekea Mama yangu huku nikimtazama sana, Mamaย  hakuacha kutabasamu. Nilisogea karibu zaidi, kila hatua ilizidi kunisogeza karibu naye naย  kumtazama kwa makini zaidi, alikua ni Mama yangu kabisaย 

    Nilibakisha hatua chache kuelekea alipo, niliona nitachelewa pengine ataghaili na kuondoka,ย  nilipiga hatua iliyoambatana na mkimbio. Mazingira yalikua kama yameganda hivi, Dunia kamaย  ailikua imesimama hivi.ย 

    Ghafla nililiona shimo kubwa ambalo hatua yangu ilikua ikilielekea shimo lile, hapakua tena naย  Mama yangu isipokua Mimi kujiokoa nisitumbukie ndani ya shimo, niligundua ulikua mtego naย  bahati nzuri niliweza kufunga breki ya haraka kiasi kwamba niliyumba huku nikijinasua,ย  hatimaye nilifanikiwa kutoingia ndani ya shimo lile.ย 

    Mara nilianza kuisikia sauti ya Mama yangu akicheka kwa kutisha sana. Sauti yake ilikuaย  ikiniumiza masikio yangu kiasi kwamba nilihisi kizunguzungu, nilipepesuka kama mlevi.ย  Nikajishikiza ukutani hadi nikafika mlango wa kuingilia ndani.ย 

    Ile sauti ilipotea, ukimya ulianza tena. Yaani palikua na hali tofauti tofauti kila hatua ninayoipiga,ย  mapigo ya moyo yalikua yakizisindikiza hatua zangu. Niliinua macho na kuziangalia ngaziย  zinazoelekea juu, kisha nilishusha macho yangu kuelekea kwenye korido ambayo kile chumbaย  nilichoambiwa kilikua kinapatikana.ย 

    Hapakua na sauti nyingine isipokua sauti ya kudunda kwa moyo wangu na sauti ya pumzi zanguย  zilizokua zikitoka na kuingia bila mpangilio. Nilisimama nikifikiria nielekee wapi, kitu chaย  kwanza nilitaka kua na uhakika kua lile jini halipo ndani ya nyumba.ย 

    Mahali pekee ambapo ningeweza kua na uhakika ni kupitia dirisha la Chumbani kwangu,ย  nilipandisha ngazi kuelekea chumbani kwangu. Nilipofika, nilijipa sekunde kadhaa kabla yaย 

    kufunua pazia. Nyumba ya yule Mzee jirani ilikua kimya sana, nilikua najua fika kua ilikuaย  ikikaliwa na yule jini Mzeeย 

    Ukimya bado uliendelea kutikisa nyumba nzima na nyumba jirani, niliwaza kwa haraka atakuaย  yupo wapi. Niliutazama mkono wangu wenye shanga ya Ulinzi, nilikua na uhakika kuaย  asingeliweza kunidhuru kwa mikono yake isipokua kwa akili na kutumia viumbe vingine kamaย  alivyofanya wakati ule alivyowatumia Wazazi wangu.ย 

    Nilijiambia moyoni kua sipaswi kuamini chochote kile sababu unaweza kua mtego kamaย  alivyotaka kuninasa dakika chache zilizopita kupitia taswira ya Mama yangu.ย 

    Kuishi ndani ya ile nyumba lilikua ni wazo lililogoma kukubaliwa na moyo wangu, nilipaswaย  kuifanya kazi niliyoambiwa siku ya leo, kwakua sikumwona yule jini na palikua kimya sana,ย  niliona ni muda muafaka wa kwenda chumba cha chini kuitoa nafsi ya Sabra.ย 

    Niliuelekea mlango taratibu, kwakua nilikua nimeufunga nililazimika kuufungua ndipo nitokeย  chumbani kwangu, palikua tulivu sana kiasi kwamba kila hatua yangu niliisikia vyema. Sauti yaย  Bawaba za mlango zilipiga kelele wakati naufungua mlango, nilishupaza shingo yangu naย  kuminya macho yangu huku nikiendelea kuufungua mlango kwa adabu sana.ย 

    Nilipomaliza kuufungua Mlango, zoezi la kutoka chumbani lilianza taratibu, nilishusha ngaziย  baada ya kuimaliza korido fupi kutoka chumbani kwangu. Nilitembea taratibu na kwa tahadhariย  kubwa, nilipofika ngazi ya mwisho nilianza kuisikia ile sauti ya Mwanamke anayeimba.ย 

    Alikua akiimba kwa masikitiko sana japo sikuitambua lugha yake ila sauti yake ilinifanya nihisiย  masikitiko yake, nilisimama nikiendelea kuisikia huku nikifikiria nini cha kufanya, nilisimamaย  kwa dakika kama mbili hivi nikiendelea kutafakari, mwisho niliamua kuifuata ile sauti. Hapoย  moyo wangu ulikua umekufa kwa woga, mwili wangu ulikua hauna nguvu, nilikua natetemekaย  sana.ย 

    Kila mara niligeuza macho yangu huku na kule nikiwa kwenye korido naelekea chumba chaย  mwisho ambacho ndimo lile shimo la kuelekea kaburini lilikuwamo. Nilipofika niliuwonaย  Mlango ukiwa umefungwa, sauti ya kuimba wala haikukoma isipokua ilikua ikihama kadiriย  nilivyokua najaribu kusogea hadi nilipofika Mlangoni.ย 

    Kitasa cha mlango kilikua kinaniangalia Mimi, nami nilikitazama huku mkono wangu ukiwa naย  shahuku ya kukitekenya kitasa hicho chenye rangi ya dhahabu, kitasa cha kizamani chenyeย  urembo wa maua. Niliutoa mkono wangu, ukasogea hadi kukikamata kitasa kisha nikakitekenyaย  kikatoa sauti ya kufunguka.ย 

    Upenyo mdogo ulionekana baada ya mlango kufunguka kidogo, nilihitaji ujasiri wa ziada iliย  kupeleka macho yangu ndani. Mwili ulianza kusisimka, nywele zilinisimama kichwani mwanguย 

    Haikua hali ya kawaida, ilikua ni hali ya hatari. Mara nilianza kusikia sauti ya kitu kikitembea,ย  kwa namna nilivyokua nakisikia kitu hicho wala hakikua Binadamu wala Mdudu isipokua ni kituย 

    cha ajabu sana, kishindo kilikua kinasikika kwa uzito sana halafu paliongezeka sauti nyingineย  kama ya kiatu kirefu cha kike hivi. Sauti hiyo ilikua ikisikika nyuma yangu, niligeuka harakaย  kuangalia, niliambulia kuona kivuli cha kutisha sana.ย 

    Kiumbe hicho kilikua bado hakijafika kwenye ile korido ya kuelekea chumbani, nilifikiria niniย  cha Kufanya. Haraka Ubongo wangu ukaniambia niingie ndani ya chumba hicho maana nyumaย  palikua haparudiki. Niliingia halafu kwa taratibu sana niliufunga mlango, nikawa nimejifungia,ย  sauti ya yule Mwanamke kuimba ilikoma.ย 

    Pakawa kimya sana, ndani ya kile chumba cha stoo kilikua vile vile, vitu vingi tulivyoviwekaย  vilikaa kwa mpangilio ule wa Mwanzo, nilitafuta lile shimo la ajabu lakini halikuwemo. Sasaย  nikaona ni bora nijifiche huwenda kile kiumbe cha ajabu kingeweza kuingia ndani ya kileย  chumba.ย 

    Nilijibanza mahali nikisikiliza nini kitakachotokea, ile sauti ya kishindo ilianza kuja karibu nami.ย  Nilizidi kuogopa, jasho la hofu lilikua likinimwagikaย 

    Kile kishindo kiliishia mlangoni kisha palikua kimya sana. Kimya kiliendelea kwa kitamboย  kirefu kama cha dakika kumi na tano hivi hadi nilianza kujiuliza maswali mengi yasiyo naย  majibu. Kwanza nilijiulza kishindo kile kilikua cha kiumbe gani, pili nilijiuliza kiumbe hichoย  kilikua kimeondoka pale mlangoni au nini kilimfanya awe kimya.ย 

    Nikataka kujua, nikasimama ili nielekee mlangoni, mara ghafla mlango ulifunguliwa harakaย  sana, pale pale nilijibanza tena kwa uhakika kabisa kua sijaonekana, ule mlango niliupa begaย  huku shingo yangu nikiwa nimeikata upande mwingine. Sikutaka kuangalia ni Nani aliyeufunguaย  ule mlangoย 

    โ€œCelin upo hapa?โ€ nilisikia sauti ya yule Bibi jini, nilizidi kutetemeka. Nikauziba mdomo wangu.ย  Aliendelea kuniita kwa sauti ya kunongโ€™ona, sauti yake ilikua na nguvu sana kiasi kwambaย  nilijizuia sana nisiitikieย 

    Sikujua kama alikua amegundua nipo ndani ya kile chumba au la. Niliendelea kupumua kwa shida, nilisali sala zote. Basi, naona hakuwa na uhakika kuwa nipo ndani ya kile chumbaย 

    Taratibu nami nilitaka kumwona, nilikua na uhakika kwa asilimia zote kua hajagundua chochote.ย  Niligeuza shingo yangu taratibu huku macho yangu yakiwa makali niweze kumwona,ย  nilipofanikiwa kugeuza shingo ndipo nilipokiona kiumbe cha kutisha sana.ย 

    Kwa uhakika alikua na umbo la Binadamu, alivalia gauni chakavu lenye rangi nyeupe, nyweleย  zake zilikua chafu pia halafu ni ndefu sana kiasi kwamba zilikua zinakaribia kiunoni mwake.ย  Alikua na kucha ndefu sana kama ndege tai, alikua amenipa mgongo na laiti kamaย  angelinionesha sura yake basi ingelikua mbaya zaidi.ย 

    Miguuni alikua na kwato kama za ngโ€™ombe, kiukweli kilikua kiumbe cha ajabu kuwahi kukionaย  maishani mwangu. Mwili ulikua unaendelea kusisimka tu, cha ajabu baada ya dakika kama mojaย 

    na ushee hivi alibadilika kutoka kwenye lile umbo na kua yule Bibi Kizee ambaye ni jiniย  Muuwajiย 

    Moyo wangu ulizidi kwenda mbioo nikikumbuka namna alivyosababisha nikamuuwa Mamaย  yangu, kifo cha Zena na Caren chanzo ni yeye. Aligeuka huku na kule kama vile alikuaย  akihakikisha kua hakuna anayemwona. Kisha alisogea mbele kidogo karibu na pembe ya ukutaย  akasemaย 

    โ€œFungukaaโ€ผโ€ sauti yake ilikua kali ya kutisha, mara lile shimo la ajabu lilifunguka. Huu sasaย  ndio mlango wa kuelekea kaburini kwenye nafsi ya Sabra, shimo namna lilivyofungukaย  lilinishtua sana nikakumbuka ile siku nilimwona Baba na Mama wakitoka kwenye shimo lileย  wakiwa uchi wa mnyama.ย 

    Nilimwona yule jini akiingia ndani ya shimo hilo lenye rangi jekundu, lilikua mfano wa mlangoย  wa Andaki hivi lenye kuwaka rangi nyekundu na moshi mithiri ya mvuke wa maji ya moto.ย  Baada ya yeye kuingia ndani ya shimo palijifunga kama vile hapajatokea kitu chochoteย 

    Nilistaajabu sana, nilisogea taratibu kwa tahadhari kubwa. Hapakua na shimo lolote wala daliliย  kwamba pana mlango, nililitafuta lakini ilikua ni sawa na kujiuliza maswali yasiyo na majibu.ย  Nilibaki nikiwa nimesimama sijui naanzia wapi ili nami niingie humo kwenye shimo labdaย  ningeweza kuipata mafsi ya Sabra.ย 

    Roho iliniuma kuona nimefeli zoezi muhimu sana ambalo lilikua ni hatua kubwa kwangu kufikiaย  hitimisho ya matatizo yanayoikumba familia yangu. Nilifikiria nami nifanye kama alivyofanyaย  ili lile shimo lifunguke. Nilisogea pale karibu na pembe ya ukuta kisha nikasemaย 

    โ€œFungukaโ€ผโ€ mara ya kwanza hapakua na chochote kilichotokea, nikarudia tena na tena. Zaidi yaย  mara tano lakini shimo halikutokea. Nilitamani nilie maana sikua na uwezo wa ziada waย  kutambua mambo mengi isipokua machache ambayo yule Mwanaume aliyejitambulisha kamaย  Haji aliniambiaย 

    Basi nilikata tamaa, chozi lilinibubujika. Nikajikuta nikipandwa na hasira sana, nikasema kwaย  mara ya mwisho kwa sauti kubwa ya hasira huku chozi likinibubujikaย 

    โ€œFungukaaaโ€ผ!โ€ ghafla tu nililiona lile shimo la ajabu likifunguka nyuma yangu, palikua panatoaย  mvuke na joto kwa mbali, rangi nyekundu ilikua imelizunguka shimo lile, nilichungulia ndani yaย  shimo maana sikuwahi kuingia hivyo nilikua sijui chochote kile hata kunaonekanaje nilikua sijui.ย 

    Nilitumia muda mrefu nikiliangalia tu, kisha niliisikia sauti nzito ikiuliza kutoka ndani ya shimo.

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya KUMI

    COMMENTS ZIWE NYINGI SASAย 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

     

     

    riwaya mpya riwaya za kuvutia soma riwaya bure

    16 Comments

    1. Nailaty on May 5, 2025 7:59 pm

      Asanteee mambo yanazid kunoga

      Reply
    2. David ben on May 5, 2025 8:25 pm

      Nzuri

      Reply
    3. Aura on May 5, 2025 8:28 pm

      Ooh to be continued………………๐Ÿฅ€

      Reply
    4. Rio on May 5, 2025 9:26 pm

      Sehemu ya 9 iwe mapema daah kali sana

      Reply
    5. Said on May 5, 2025 9:28 pm

      ๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿค๐Ÿค๐Ÿค

      Reply
    6. Piana on May 5, 2025 9:28 pm

      Admin tuletee sehemu ya 10
      Ni nzuri sana ๐Ÿ‘Œ

      Reply
      • Erick Elisha on May 6, 2025 8:01 am

        Ongeza utamu wa mziki DJ wapi sehemu ya kumi

        Reply
    7. Salma on May 5, 2025 9:29 pm

      Tamuu

      Reply
    8. Shedrack on May 5, 2025 10:19 pm

      Nextโฉ episode

      Reply
    9. nyamwirila manumbu on May 5, 2025 10:28 pm

      Nzuri sana ila inatisha sisi tulio masingle kusoma usiku nijau

      Reply
    10. Yahaya on May 6, 2025 12:53 am

      Daaah hii kituu kadrii unavyo zidiii som nd utamu unazidii kukoleaa aiseeh!!! Inasisimuaa snaa snaa BRAVO โœ…..

      Reply
    11. KingzJeelay on May 6, 2025 6:43 am

      Sauti kutoka ndani ilikuw unauliza nini ๐Ÿคท๐Ÿฝโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคท๐Ÿฝโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคท๐Ÿฝโ€โ™‚๏ธ๐Ÿคท๐Ÿฝโ€โ™‚๏ธ
      Tunakungoja Kaka mkubwa tumalzie mission impossible yetu๐Ÿ™„๐Ÿ™„๐Ÿคฃ๐Ÿ™„๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ๐Ÿ™Œ๐Ÿฝ

      Reply
      • Karimu on May 7, 2025 3:02 pm

        Kazi mzuri

        Reply
    12. [email protected] on May 6, 2025 3:45 pm

      Mbona sehemu ya 7 na 8 sijaona majama

      Reply
    13. ๐Ÿ“ + 1.13200 BTC.NEXT - https://graph.org/Ticket--58146-05-02?hs=3f9505a64f17ee5b35ce0a78993c6557& ๐Ÿ“ on May 11, 2025 1:57 am

      lwwiy0

      Reply
    14. ๐Ÿ“˜ โš ๏ธ ATTENTION: You received 0.75 BTC! Click to claim >> https://graph.org/RECEIVE-BTC-07-23?hs=3f9505a64f17ee5b35ce0a78993c6557& ๐Ÿ“˜ on August 6, 2025 6:06 am

      osca4r

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE โ€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.