Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 05
Taratibu nilitembea kuelekea mbele ya gari kumsikiliza yule Mwanaume, alikua mnene kiasi na pia alikua na ndevu nyingi mfupi wa wastani, alikua ananukia manukato makali sana. Nilitembea taratibu huku nikijikwaa jiwe dogo lililonipa mwendo zaidi hadi nilisogea kabisa karibu yake, akanipa pole huku akigeuka na kunitazama nikitembea taratibu hadi nilipofika mbele yake.
“Usiwe na wasiwasi Celin, usiogope sababu nusura ya Maisha yenu yapo mikononi mwako” niliyafinya macho yangu kwa mshangao mkubwa sana, moyo ulilipuka ghafla na kuanza kwenda mbio
“Unamaanisha nini?” nilimuuliza nikiwa na mhemko wa alichoniambia, tayari nilikua nimepoteza marafiki zangu wawili. Endelea
SEHEMU YA SITA
“Ninachomaanisha ni hiki, Sisi tulizaliwa wawili tu. Mimi pamoja na Dada yangu Sabra, Baba yetu alikua tajiri sana. Mama yetu alifariki muda mrefu, Baba yetu hakutaka kuowa kabisa. Alitulea kwa mikono yake hadi tulipokua wakubwa” alisema huku nikimwona kama Mtu anayekaribia kulia. Nilimeza mate huku nikiwa na shahuku kubwa ya kusikia alichokusudia kukisema. Kisha aliendelea
“Pesa hugeuza Dunia juu chini, Usiku mmoja. Kaka yake Baba yetu alimuuwa Baba yetu akimtuhumu kujilimbikizia mali ambazo alirithi kutoka kwa Baba yao. Usiku ule bado unaishi ndani yangu, Mimi na Dada yangu Sabra tulishuhudia ukatili ule. Baba mkubwa akaagiza tusakwe mle ndani tuuawe, tulikimbilia chumba cha chini ambacho mara zote Baba alisema kua
kama itatokea shida basi tukimbilie humo kujificha, wakati huo Mimi nilikua na Miaka 11 na Sabra alikua na Miaka 15.” Alipofika hapa alijiinamia, alikua akilia. Nilitamani kumshika na kumtuliza lakini alikua Mtu mgeni kwangu istoshe nilikua nikimwogopa. Niliishia kumtazama tu hata neno la kuongea sikuwa nalo.
Aliinua kichwa chake kunitazama, nusura nikimbie. Alikua na macho meupe yasiyo na kiini.
“Usikimbie, huu ndiyo ukweli pekee unaoweza kunusuru Maisha yenu Celin” alisema, niliitikia kwa kutumia kichwa lakini moyoni nilikua nimejawa na hofu sana, miguu yangu ilitamani kukimbia kuliko kusimama mbele ya yule Mwanaume.
“Jitihada zetu hazifukua dafu, walitukamata. Walituambia tupige magoti, tulifanya hivyo kisha Baba yetu Mkubwa alifika kule chini kisha alituambia hakukusudia kutudhuru sisi isipokua tulishuhudia kifo cha Baba yetu. Aliamuru wale watu watuuwe, walichinja shingo zetu na kumaliza Uhai wetu kule chini” niliachama, hewa ya ghafla iliingia kwa mshangao mkubwa, ina maana nilikua nazungumza na Mfu? Nilijiuliza ndani yangu lakini cha ajabu alinijibu kama vile nilizungumza kwa sauti
“Ndiyo, Mimi ni mfu. Msaada wangu ni wewe Celin. Walituzika kule kule chini kisha waliuziba mlango wa kuelekea kule chini, sijui kuhusu Baba yetu alienda kutupwa wapi. Lakini kule chini tulizikwa Mimi na Dada yangu Sabra. Nasfi zetu zimeishi kwenye ile nyumba kwa miaka mingi,
kila aliyeamia kwenye ile nyumba alikutana na mikasa ya ajabu kila uchwao, wengi walikimbia.”
“Hakuna aliyepata ujasiri wa kufwatilia chochote kile. Nafsi zetu ziliwasumbua sana, ndipo Baba Mkubwa alipotafuta Mganga kwa ajili ya kuizindika ile nyumba lakini hata zindiko lake halifukufanya kazi isipokua lilitengeneza jini ambalo wewe umekutana nalo mara kadhaa. Jini mzee aliyeishi kwenye ile nyumba na kuzidi kuuwa Watu, hata Baba Mkubwa aliuawa na lile jini, ni jini hatari sana ambalo linaondoa Kila anayeishi ndani ya ile nyumba. Awali Baba mkubwa aliishi mule lakini aliikimbia nyumba mwenyewe kutokana na mauza uza, aliiacha nyumba yenyewe”
“Katika harakati za kupambana na lile jini nilijikuta nikiondoka kwenye kaburi na sijui naweza vipi kurudi tena ndani ya ile nyumba. Ujasiri wako, udadisi wako ulinivutia sana Celin, naomba unisaidie jambo” alisema, hadi kufikia hapo nilikua na simulizi halisi ya ile nyumba ambayo niliitilia sana shaka tokea mwanzo.
“Nitasaidia nini, siwezi kupambana na vitu kama hivyo. Sina hiyo nguvu Mimi” nilisema, alinitazama kisha akaniuliza
“Unajua wazazi wako wanapitia nini ndani ya ile nyumba? Usije ukawapoteza kirahisi hivyo Celin, Baba na Mama yako wanahitaji msaada na msaada pekee ni wewe kuitoa nafsi ya Dada yangu, ikiwa huru tunaweza kupambana na jini linalouwa kila anayeifahamu siri ya ile nyumba. Jini hilo ni Bibi Mzee, ameuwa kila Mtu anayehoji kuhusu nyumba ile, nimekuokoa padogo sana
lakini bado atakuwinda akumalize” chozi lilianza kunibubujika, sikuwaamini Wazazi wangu lakini niligundua walikua hawana hatia, pengine hilo jini ndilo linalowatumikisha.
“Usilie Celin, nitakupa njia ya nini ufanye unapofika ndani ya chumba ambacho huwa unamsikia Mwanamke akiimba au kulia, huyo ni Dada yangu Sabra. Amekuwa Mtumwa wa huyo jini katili aliyepandikizwa na Baba Mkubwa” Alisema, nilijaza hewa kifua changu maana niliyoyasikia yalikua ni mambo ya kutisha sana.
Ilikua ni kama nasoma kitabu cha Riwaya ya kutisha kilichoandikwa kwa mtiririko wa ajabu sana, mishipa ya kichwa ilinisimama. Nguvu zilikua zikiniondoka taratibu huku nikihema juu juu, alichokisema ndicho nilichokua nikikitafuta kukisikia lakini baada ya kukisikia nilitamani nisingelisikia kabisa.
Hadithi ya kuogofya iliyoondoa wapendwa wangu pamoja na Dalali aliyetutafutia nyumba. Haikua rahisi kuelewa, sikuacha kumtazama yule Mwanaume ambaye kwa mujibu wa hadithi yake ni Mtu aliyekufa muda mrefu, ni nafsi inayohangaika kumtafuta Dada yake aliyezikwa chini ya nyumba yetu tuliyoinunua. Sikutaka kujua nyumba ipo chini ya nani
Kila nilichokisikia kuhusu nyumba yetu kilinipa uhakika wa kile alichoongea, kuhusu Mwanamke anayeimba na kulia hilo ni jambo dhahiri sana. Nilipata kujua kuhusu jini Mzee anayeishi ndani ya nyumba yetu na kufanya Mauwaji.
“Kuna Mzee nyumba jirani, unamfahamu?” nilimuuliza.
“Ndiyo‼ Unachokiona ni fikra zako na jinsi ambavyo jini yule mbaya anataka uone. Hakuna uhalisia kwani Mzee yule alifariki Miaka mingi, nyumba yake iko tupu, inakaliwa na huyu jini ambaye ndiye aliyemuuwa huyo Mzee” nilipepesa macho yangu, kila kitu kilikuwa kipya masikioni mwangu.
Chozi lilinitoka, alinipa nafasi ya kumuuliza nisichokijua. Alikua akinitazama huku akisubiria swali langu.
“Kuhusu wazazi wangu?” japo sikutaka kusikia sana kuhusu Wazazi wangu, nilihisi ingeniumiza sana. Yule Mwanaume alinitazama akaniambia
“Ni watumwa, unapaswa kuwakomboa kabla hawajatoweka. Kwakua ameshajua wewe unajua kuhusu siri ya ile nyumba unaweza ukawa na muda mchache sana wa kuwasaidia.” Alisema, nilizidi kuumia ndani ya nafsi yangu. Baba yangu aliniumiza zaidi sababu alitumia pesa zake za kustaafu kununua nyumba ya ndoto zake lakini nyumba hiyo ndiyo chanzo cha Matatizo yote.
“Celin” aliniita na kuniondoa kwenye fikra za kuogofya. Nilimtazama, nilimwona kama Mkombozi wangu ambaye anaweza kuyarudisha Maisha yangu ya furaha ya huko nyuma.
“Abee!” niliitika kwa utuo, chozi lilikua likinibubujika tu.
“Kulia hakuwezi kuokoa Wazazi wako na wapendwa wengine. Vaa Ujasiri, ukiweza kumaliza hili nitakupa shukurani” alisema, niliyatafakari maneno yake. Ni kweli nilihitaji kuuvaa Ujasiri wa hali ya juu sana lakini haiwezi kuondoa huzuni iliyojaa ndani yangu. Niliitikia kwa kutumia kichwa kisha akaniambia
“Nitakua nawe bega kwa bega hadi mwisho, ikiwa utashindwa nitashindwa pia, ukishinda nitashinda na wewe” kisha aliingiza mkono mfukoni na kunipatia ushanga mwembamba uliotungwa vizuri.
“Nipe mkono wa kulia” kisha alimalizia na ishara ya Kichwa huku akinyoosha Mkono kuuomba mkono wangu, alionesha kuhitaji kunivisha ule Ushanga wenye rangi nyeupe. Japo bado nilikua namwogopa lakini nilimpatia mkono wangu. Halafu akanifunga ule Ushanga mkononi kama kembe hivi.
“Huo ndiyo Ulinzi wako Celin. Rudi nyumbani ishi kama kawaida lakini nitakua nawasiliana nawe mara kwa mara kukwambia nini cha kufanya” alisema huku nikiwa nautazama ule ushanga, nilipoinua kichwa changu sikumwona tena yule Mwanaume hata lile gari halikuwepo tena. Nilijikuta mwenyewe msituni
Nilianza kuhangaika kutafuta pa kutokea, niliongoza ile barabara tuliyokuja nayo, nilikua ninahema huku nikiwa nina hofu sana. Nilianza kukimbia, nilipojikwaa nilinyanyuka hadi nilipofika Barabara kuu iliyokua ikielekea Mjini.
Nilipunga Mkono wangu kuomba msaada, hatimaye nilipata msaada wa ‘lifti’. Gari moja ndogo iliyobeba wanafamilia ilinisaidia hadi nikafika Mjini. Niliwashukuru kwa msaada wao, nilitazama juu palikua na jua kali, saa yangu iliniambia kua ni saa sita Mchana. Niliufungua mkoba wangu, nikaitoa simu na kumpigia Mama yangu. Niliposikia sauti yake nilishusha pumzi zangu maana aliniambia wapo salama, nami nilimwambia kua ndiyo nimetoka chuoni narudi nyumbani.
Nilielekea kituo cha treni, kisha nilipanda treni hadi mitaa ya nyumbani, nikatembea kidogo hadi nilipofika nyumbani, nilisimama getini nikiiangalia nyumba yetu. Chanzo cha yote ni hiyo nyumba. Ilikua ni nyumba nzuri iliyojaa utulivu kwa nje lakini ndani ilikua na vibweka vya kutisha, masikio yangu yalianza kupiga kelele mithiri ya filimbi za sungusungu.
Sikujua ilikua ni ishara gani, sijui ni kitu gani kilinifanya niangalia pembeni ule upande wa nyumba ya yule Mzee, nilimwona yule Mzee akiwa amesimama akinitazama bila hata kupepesa macho. Sasa nilikua na siri ya huyu Mzee kua si Mtu halisi bali ni mzimu wa Mzee aliyeuawa na yule Jini Mzee.
Alikua kimya sana, akinitazama bila kupepesa macho yake. Ghafla akatoweka katika mazingira tata, nilishtuka sana nusura nizimie. Hayakua mambo ya kawaida, nilizoea kuyatazama kwenye filamu na tamthilia za kizungu. Kisha nilisikia geti likitoa sauti ya maumivu ya Bawaba kama
vile lilikua likisukumwa na Upepo hivi. Ile sauti ilikua ndiyo sauti pekee iliyotawala masikio yangu.
Niliingiwa na shahuku na kusogea, bado masikio yalikua yakipiga kelele sana. Nilianza kupiga hatua za taratibu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee ili nione geti hilo lilikua likipiga kelele kwasababu ya upepo gani wakati palikua tulivu sana, nikakumbuka siku ile niliona geti hilo likiwa limejaa kutu, inawezekana vipi likapiga kelele hivyo?
Nilijiuliza nikiwa ninazidi kupiga hatua za kuhesabu, moja mbili, moja mbili nikiwa nazidi kutembea mwili nao ulikua ukisisimka sana kuashiria nilikua naikaribia hatari. Katika hali isiyo ya kawaida kabla hata sijafika getini, nilikua ubavuni naelekea nikaona kitambaa kikipepea pale getini, hakikua kitambaa kidogo kilikua kikubwa na jinsi macho yangu yalivyoniambia niliona gauni jeupe, ilikua ni ishara kua palikua na Mtu aliyejibanza getini ili anishambulie.
Nilisimama, ghafla nilianza kusikia sauti ya ajabu iliyojaa ushawishi sana. Sauti hiyo ilikua ni sauti ya kizee ikiniambia
“Celin, njooooo‼ njoo Binti, unakaribia” ni sauti ya taratibu sana iliyotoka kwa kunong’oneza, sauti hiyo ilikua ikisikika kila sehemu, ilikua inazidi kunivuta katika hali ya ajabu sana nizidi kuelekea getini. Vitu viwili vilitokea, mwili wangu ulikua unakataa lakini akili ilikua inataka kwenda, niliharibiwa kisaikolojia nikajikuta nikijivuta kusogea.
Namna nilivyoyaona mazingira ilikua kama vile nipo Dunia ya peke yangu, isiyo na Mtu mwingine. Niliona giza la ajabu na mwanga hafifu, kipande cha gauni kiliendelea kupepea. Sauti ya yule Bibi Kizee jini iliendelea kuniangamiza kisaikolojia, jasho lilikua likinitoka. Nilikua naendelea kupiga hatua za mvutano, kumbe wakati yote yanaendelea Mama yangu alikua ghorofani akinitazama kwa Mshangao.
Nilikua namsikia akiniita lakini nguvu ya ile sauti ya yule Bibi ilinizidia kiasi kwamba nilitamani kupaza sauti kumwambia Mama kua anisaidie lakini nilishindwa, hata kugeuka kumtazama Mama kilikua kipengeleze kizito sana. Shingo yangu ilikaza ikitazama mbele, udenda ulikua ukinitoka.
Hakika huyu Jini alikua na nguvu za ajabu sana. Alikua akiniita huku akicheka kanakwamba alikua na uhakika kua ameniweza, nilijitahidi sana kupambana na nafsi yangu lakini sauti yake ilikua na nguvu ya ajabu sana.
Nilisogea karibu kabisa na geti, hatua moja ndiyo iliyobakia kufika alipo yule jini, gauni lake lilikua likipepea huku sauti yake ikizidi kuwa karibu zaidi. Niliweka mikono yangu masikioni, nilijua nateswa na ile sauti lakini sikua na nguvu ya kupambana nayo.
Nilikua natetemeka, nilijaribu kujizuia kwa nguvu lakini nilikua sina hiyo nguvu zaidi ya kunyanyua mguu ili nifike alipo yule Jini. Ghafla nilishikwa na kuvutwa nyuma, fahamu zilinirudia, hali ya hewa ilitulia, sauti ilikatika sikuisikia tena.
Mbele yangu alikua amesimama Mama pamoja na Baba yangu, macho yalinitoka pima kama fundi cherahani anayetungisha uzi kwenye zindano, udenda ulikua ukinitoka nikawahi haraka kuufuta lakini tayari Baba na Mama walikua wameshaniona katika hali ile ya uzezeta.
Walikua kimya wakiniangalia nilivyokua najihangaisha kujiweka sawa kanakwamba kila kitu kilikua vizuri. Mama aliniambia
“Tumeona kila kitu, unajaribu kuficha nini?” sauti ya Mama yangu ilinisuta, alizungumza kama Mama aliyegundua Uwongo wa Binti yake, macho ya Baba yangu yalikua kwangu pia akiniangalia kwa mshangao pia.
Niliinamia chini, aibu ilikua imenishika vibaya sana. Baba akaniuliza
“Mkononi umevaa nini Celin?” macho yangu nikayapeleka mkononi, nikagundua alikua akiuongelea ule Ushanga niliopewa kama Ulinzi na yule Mwanaume nisiyemjua jina.
Nilimtazama Baba kisha Mama, halafu nikasema “Ni urembo tu huu Baba” sauti yangu na matendo yangu yaliwaambia uhalisia wangu kua kuna jambo nalificha. Haikuishia hapo, Mama alienda mbali zaidi akasema
“Hii siyo mara ya kwanza nakuona unanyata kuelekea kwenye nyumba jirani, Celin unaficha nini ambacho huwezi kuzungumza na Sisi? Umepoteza marafiki wawili kwa mpigo, kuna nini kinachoendelea?” Maswali ya Mama yangu yalikua kama Mshale ulionichoma kooni, nilikaukwa mate na maneno ya kujibu.
Niliishia kuwatazama, mara radi zilisikika. Wingu zito hata lilikotokea hakuna aliyejua, papo hapo mvua ilianza kunyesha, hakuna aliyetaka kuikimbia mvua. Sote tulisimama tukitazamana, Wazazi wangu walihitaji majibu kutoka kwangu.
“Mama, tutaongea ndani mvua inazidi kua kubwa” nilisema kisha nilikimbilia ndani nikiwaacha wazazi wangu wakiwa wamesimama. Nilipanda ghorofani hadi chumbani kwangu, niliwatazama Wazazi wangu pale nilipowaacha lakini sikuwaona, nikahisi huwenda nao wamekimbilia ndani.
Niliiangalia nyumba jirani, kichwani nilikua na majibu kua nyumba ile ilikua ikikaliwa na yule jini Muuwaji. Cha kushangaza niliwaona wazazi wangu wakiwa wamesimama getini, ni kama vile walihitaji kujua nilikua nafuatilia kitu gani, moyo ulinilipuka mithiri ya Volkano kali ya moto.
Mvua ilikua ikiwapiga, kibaya zaidi mbele yao alikua amesimama Yule Bibi Kizee akiwa amevalia gauni jeupe akiwaita Wazazi wangu kwa kutumia mkono wa kushoto huku akirudi nyuma nyuma. Kilichowakuta Wazazi wangu ndicho kilichokua kinanivuta na Mimi, niliwashuhudia Wazazi wangu wakiwa kama mazombi.
Hawajitambui, walikua wakilifungua lile geti huku macho yao yakiwa kwa yule Bibi Kizee, tena walikua na haraka sana wamfikie. Walikua wakiielekea hatari ile ile ambayo wao waliniokoa
nayo, sasa ulikua ni wajibu wangu kuwasaidia. Haraka nilifungua mlango na kuanza kushusha ngazi niwawahi wazazi wangu wasiingie mikononi mwa yule Bibi kizee
Niliteremka ngazi haraka haraka hadi nikafika chini, moja kwa moja nikakimbilia getini, nikalifungua geti haraka Halafu nikakimbilia getini kwa yule Mzee. Nilipofika niliwaona Wazazi wangu wakiwa wamesimama nyuma ya yule Bibi Kizee Muuwaji. Walikua wameinamisha shingo zao, mvua bado ilikua ikinyesha, geti lilikua wazi.
Walikua wakitazama chini, yule Bibi alikua akinitazama halafu aliangusha kicheko kikubwa. Alikua na sauti mbaya mithiri ya radi, ghafla alianza kutokwa na kucha ndefu, sura yake ilikua ndefu, nywele ndefu zilizo dhohofika, macho yake yalikua mekundu, meno yalichomoka.
Alikua na sura mbaya ambayo ilitosha kuniambia kua ni kweli ndiye Jini Muuwaji. Alikua kama amewateka Wazazi wangu kifikra. Nilianza kuogopa, alikua akinisogelea taratibu
Nilikua nikihema, Wazazi wangu walikua wamesimama vile vile kama Watu wasiojitambua. Yule Bibi aliendelea kunisogelea huku mguu wake mmoja akiwa anauburuza. Ulikua kama una dosari ya ukilema hivi, nilikua kwenye butwaa ambayo ilihitaji Mtu anitingishe ndiyo nitoke katika ile hali tata.
Fumba na kufumbua Macho yule Bibi Kizee alikua amejaa machoni pangu akinimulika na macho yake makali, nilishtuka na kutoka katika ile hali ya Butwaa. Nilipohitaji kukimbia alinishika mkono na kunivuta kwake lakini alipigwa na shoti kali, niliona moto mkali uliomsukuma na kumtupa chini.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SABA
COMMENTS ZIWE NYINGI SASA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
7 Comments
Admin wa kwanza apa ntagi mm sehemu inayofuata 😍nzur sana nmeipenda
Awesome https://is.gd/N1ikS2
Familia ya Celin ina kumbwa na majanga
Very good https://is.gd/N1ikS2
Good https://is.gd/N1ikS2
Awesome https://is.gd/N1ikS2
👌👌👌