Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 07
Hatimaye Mama yangu aliungana na Zena na Caren kwenye makazi ya milele. Kilichokua kimebakia kwangu kilikua fumbo kubwa, hakuna aliyejua kuhusu ile nyumba yenye kaburi na jini anayeuwa.
Sikutaka kumwambia yeyote, moyo wangu ulijawa na kisasi. Sikuuona umuhimu wa kuendelea kuishi ikiwa nimepoteza Wapendwa wangu kwa usiri wangu. Baba alifikishwa Mahakamani siku Nne baada ya kumzika Mama, alikiri mbele ya Mahakama kua alitenda Mauwaji hayo kwa mikono yake kwa kile alichokiita wivu wa Mapenzi. Endelea
SEHEMU YA NANE
Baba alivikwa kofia ya Muuwaji, alisemwa na kutukanwa kila kona. Hatimaye alihukumiwa Miaka 13 jela ka kosa hilo, kutokana na Umri wake ilikua rahisi kusema alikua anamalizia Maisha yaliyobakia akiwa gerezani. Siku moja nilimtembelea gerezani, sikuwahi kuzungumza naye tangu tulipoachana siku ile ya kifo cha Mama kule Hospitali.
Japo alikua gerezani lakini Baba alitabasamu mbele yangu na kuniita
“Mwanangu Celin” kisha alinikumbatia kwa hisia ya furaha sana ya kuniona, alinishika mabega yangu akaniambia
“Siku moja utakua Mama, utakua na Watoto ndipo utajuwa nini Maana ya kua Mzazi. Sijali ni shida kiasi gani nitazipata Mwanangu lakini furaha yangu ni kukuona ukitabasamu siku zote, ukiwa huru kama kijana na kutimiza ndoto zako” Nilifumba macho kwa hisia ya maumivu makali ya moyo, maneno ya Baba siyo tu yaliniumiza bali yalinifundisha nini Maana ya kuwa Mzazi.
“Usilie Celin, Mimi Baba yako nitakuombea kila dakika iendayo, kamwe sitakuacha Upotee. Wewe ni Jasiri Celin, unaweza kulimaliza hili, hata kama hautanitoa hapa lakini utapigana hii vita na kulipa kisasi cha Wazazi wako, rudisha ile nyumba mikononi mwako, ni jasho langu nililolipigania Ujana wangu wote” nilishusha pumzi zangu, Baba alikua akizungumza maneno katili sana lakini yalikua yakinipa ujasiri na kunikumbusha kua nimebakia peke yangu nje ya Dunia yake, nje ya Dunia ya Mama yangu.
“Pale chumbani kwangu kuna kabati dogo, nimehifadhi kadi yangu ya Benki. Kuna pesa ya kukusaidia Binti yangu, namba ya siri ni Mwaka wako wa kuzaliwa. Usirudi hapa hadi uwe umelipa kisasi, umerudisha kila kitu. Ikiwa umeshindwa basi nenda mbali na Dunia yangu Celin” alisema Baba kisha alinionesha sura katili sana, akageuka na kuondoka akiongozwa na Askari magereza. Aliniacha nikiwa nimesimama
Baba yangu hakuniaga, aliondoka mbele ya macho yangu mithiri ya Barafu juani, aliniachia kazi nzito sana. Nilimshukuru Mungu kwa baraka ya uzima na uhuru, nilirudi nyumbani kwa mjomba.
Jioni nilimueleza Mjomba wangu kua ninarudi nyumbani, alikua na wasiwasi na maswali mengi lakini nilimueleza jambo moja kua, siwezi kuikimbia nyumba yetu. Huzuni zitanifuata na zitaondoka zenyewe, Mjomba Mgina aliniruhusu nirudi nyumbani japo alijua nitaishi peke yangu.
Kesho yake Asubuhi nilikodi Bajaji ili nirudi nyumbani, moyo wangu ulipasuka, ulikosa Uwoga tena, nilijua naenda kwenye nyumba ya namna gani. Nikiwa ndani ya Bajaji safari ikiwa imeanza, nilianza kuihisi hali ya tofauti sana ambayo mara kadhaa niwapo hatarini huwa naihisi.
Kichwa kilianza kua kizito ghafla tu, masikio yalikua yakipiga kelele mithiri ya filimbi ikipulizwa ndani ya sikio langu. Mwili ulikua ukinisisimka sana, nikamuuliza dereva wa Bajaji
“Unaihisi hali ya tofauti?” akacheka kidogo akaniuliza
“Hali ipi hiyo?” swali lake lilikua ni jibu tosha kua alikua katika hali ya kawaida tu wala hakuhisi kama ninavyohisi, nilijiinamia huku nikiwa nimeziba masikio yangu. Bajaji ilikua ikiendelea na safari, mara nilianza kusikia Honi ya Bajaji ikipigwa sana na yule dereva, nilistajaabu.
Wakati nanyanyua kichwa changu niangalie mbele nilisikia sauti moja ya kishindo, nikajigonga mahali na kuumia. Bajaji ilikua imetumbukia mtaroni. Halafu yule dereva akawa wa kwanza kutoka kisha akanitoa na Mimi kwenye bajaji iliyolala mtaroni upande, nilimuliza
“Imekuwaje?” nilikua na maumivu makali kwenye kiwiko cha mkono wa kulia, yule dereva akaniambia
“Nilimwona Bibi mmoja akiwa amesimama barabarani, nilipojaribu kumkwepa ndio tumepata ajali” nilivyosikia tu kuhusu Bibi, nikajua ni yule jini ananiwinda animalize. Sikutaka kuuliza chochote tena, nikamlipa pesa yake ya safari hata kama hatukufika mwisho wa safari, kisha nilichukua begi langu la mgongoni nikaanza kutembea kando ya Barabara.
Kichwa kilikua na mawazo tele, nilijitahidi sana kujiambia kila kitu kitakua sawa lakini nilikua ndani ya vita kali ya Mimi na Mimi, nilijua ninachojiambia kilikua kigumu sana lakini niliendelea kujiaminisha huku nikitembea. Akili yangu ilihama kabisa nikaanza kuwaza mambo mengine ya Kutisha, ghafla nilisikia honi ya pikipiki nyuma yangu.
Ile nageuka tu naiyona Pikipiki ikija kwa kasi ikielekezwa kwangu, macho yalinitoka. Nilikubaliana na akili yangu kuwa siwezi kuikwepa na ilikua hatua chache kunifikia, nilifumba macho yangu nisione namna mwili wangu utakavyovamiwa na ile pikipiki. Ghafla nilihisi kuvutwa nikajikuta pembeni ile pikipiki ikapita kama Mshale wa masafa marefu.
Nilishtuka sana, mkono wa Mtu mwingine ulikua umenishikilia. Niligeuka haraka kumtazama aliyenisaidia nikakutana na yule Mwanaume aliyekufa na kuzikwa ndani ya nyumba yetu. Nilishtuka sana lakini akanipa ishara ya kutulia, kiukweli moyo wangu ulikua unaenda mbio sana. Macho yalinitoka nikiwa ninahema na kumeza mate kupitia koo langu kavu.
“Shiii‼ usiogope Celin” alianza kusema kisha aliniambia nimfuate, nilisimama nikiwa ninamwangalia akitembea. Nilijiuliza maswali mengi ya haraka lakini jibu nililolipata ni kumfwata maana ndiye Mtu pekee anayeweza kunisaidia.
Alinisogeza mahali nikiwa nimebeba begi langu la Mgongoni,alisimama mbele ya gari moja akaniambia
“Ingia kwenye gari nitakupeleka” niliikunbuka ile gari, ni ile ambayo siku ya kwanza tunaonana alinipakia kisha alitoweka nayo. Alinisistiza kwa ishara ya mkono kua niingie ndani ya gari, nilijiuliza mara mbili mbili kabla ya kufungua mlango wa gari na kuingia ndani ya gari, nilipofunga mlango alianza kusema
“Amedhamiria akumalize, ameshaiona hatari kwako” alisema kwa sauti iliyojaa vituo vituo huku akiwa anadadisi nje ya gari kupitia kioo.
“Kama wewe Kaka yangu una nguvu za ajabu kwanini usipambane naye, mimi sina nguvu ya aina yoyote ile” nilisema, alinitazama kisha baada ya sekunde kama kumi na tano hivi
akaniambia “Nimekuchagua sababu una ujasiri ndani yako, unafikiria wamepita wapangaji wangapi kwenye ile nyumba? Wote wamekufa vifo vinavyofanana”
“Nani anaimiliki na kwanini anaipangisha wakati ni nyumba iliyojaa mauzauza?”
“Yule jini ndiye anayeimiliki baada ya kumuuwa Baba yetu. Kila anayepangishwa pale anaishia kufa kifo kibaya sana, hakuna aliyewahi hata kupata muda wa kuchunguza chochote kile, walikufa kikatili sana. Sijui wewe ni Binadamu wa aina gani ambaye uliweza kuichunguza ile nyumba. Yule jini amekua akijigeuza kwenye sura ya Baba na kutafuta dalali kwa ajili ya kuiuza au kuipangisha lakini wote walifia mle” alisema huku akitumia mikono yake kumaanisha alichokua anakisema
“Bahati nzuri ni kwamba pana uvumi mkubwa wa watu kupotea ndani ya ile nyumba, lakini kwa yeyote anayefwatilia hukuiona cha Mtema kuni.” Alisema kisha aliwasha gari, safari ilianza. Aliniacha na maswali mengi sana kichwani kwangu, sikujua niseme nini na nini Nnyamaze
“Nimepoteza kila kitu maishani, sina thamani. Mimi ni chanzo cha maafa yote, laiti kama nisingeliikubali ile nyumba pasingelitokea maafa yoyote yale” nilisema huku nikitokwa na machozi. Yule Mwanaume aliyeniambia kua ni Mfu alikua akiendesha lile gari kwa mwendo wa kawaida.
“Usijali Celin, giza totoro ni ishara ya mapambazuko. Kila kitu kitakuwa sawa” aliniambia
“Hata kama kila kitu kitakaa sawa sitaweza kumrejesha Mama yangu, sitaweza kumtoa Baba yangu jela, pia siwezi kuwarudisha Zena na Caren. Nimepoteza furaha, nimebakia kopo tupu” nilizidi kutokwa na Machozi huku nikiitumia mikono yangu kufuta chozi langu.
“Kila jambo hutokea kwa sababu Celin, Mungu alikuleta hapa ili umalize kila kitu” aliendelea kusema, maneno yake yalijaa faraja lakini nafsi yangu ilitawaliwa na kutu ya kutosha kiasi kwamba nilihitaji tumaini zaidi ya maneno matupu.
“Sijui naanzia wapi namalizia wapi, napambana vipi?” nilimuuliza, akanijibu
“Nitakueleza namna ya kufumbua hili fumbo Celin, kwasababu una hiyo shanga mkononi, hawezi kukudhuru kwa chochote labda amtumie Binadamu kama alivyofanya kuwatumia wazazi wako kukudhuru wewe. Unatakiwa kwenda kwenye chumba ambacho sauti ya Dada yangu huwa inasikika, hakikisha unakaa humo hadi mlango ufunguke, ukiweza kuingia ndani ya shimo ndimo lilimo kaburi la Dada yangu. Mwambie Haji amekutuma umsaidie kutoka ndani ya lile kaburi, ukiweza kumtoa ndio mwarobaini wa hili tatizo Celin, tutaunganisha nguvu zetu na kummaliza yule jini, tutakuachia nyumba kwa amani na utaishi kwa amani zaidi bila tatizo lolote” alisema.
Haikua rahisi kuingia ndani ya nyumba ile, niliyoyaona kwa yule jini yalinifanya niingiwe na hofu kubwa, alikua akiniwinda sana aniuwe lakini nilikua nanusurika.
“Najua una hofu lakini gharama ya kumtoa Dada yangu ni ndogo zaidi ya utakachofanyiwa na yule Jini, atakuandama Maisha yako yote wewe na kizazi chako. Hamtaishi kwa amani hadi atakapo hakikisha amekumaliza Celin, vaa ujasiri. Mimi siwezi kurudi ndani ya ile nyumba, nguvu kubwa inanizuia Mimi kukanyaga ile ardhi na siwezi kupambana nayo, wewe unaweza kuingia ndani ya ile nyumba sababu ni Binadamu” alizidi kunipa moyo na ujasiri niweze kiifanya kazi ngumu iliyo mbele yangu.
Alipokaribia karibu na nyumbani alisimamisha gari mita kadhaa akaniambia
“Hapa ndiyo mwisho wangu, siwezi kusogea zaidi na kama nitakua mbishi basi nafsi yangu itaangamia na huu mpango hautafanya kazi tena. Nenda Celin, unaweza” alisema kwa ujasiri na hamasa ya hali ya juu sana. Nilihema kwa nguvu ili nijiandae kuteremka ndani ya gari
Nilifungua kioo, palikua kimya. Nilisadiki maneno ya huyu Mfu kua yule jini alikua anauwa Watu wa nyumba jirani. Upepo wa taratibu ulikua unasomba majani makavu yaliyoanguka barabarani, alinitazama tena akanipa ishara ya kichwa kua niende. Niliteremka kutoka ndani ya gari nikiwa nina hofu sana, nilimaliza miguu yote. Mwili wangu ilikua nje ya lile gari la maajabu ambalo baada ya Mimi kushuka lilipotea tena katika mazingira tatanishi.
Safari hii sikushtuka tena sababu nilishaambiwa mengi, nilitembea taratibu kama Mtu mwenye vidonda mapajani, akili yangu ilitaka kwenda lakini moyo wangu ulikua ukidunda kwa hofu huku ukiniambia nirudi naelekea kwenye hatari.
Nilitembea hivyo hivyo huku picha halisi ya namna nilivyomuuwa Mama yangu ikiendelea kupita akilini, ilinipa uchungu, nilimkumbuka Baba yangu pia. Yupo Magereza kwasababu yangu Mimi, kauli zake za mwisho zilijirudia. Nilijipa moyo na ujasiri uliendelea kunivaa kadili nilivyokua napiga hatua kuielekea nyumba yetu.
Sauti ya ajabu ya kunong’ona ilikua ikiniita jina langu, nilihisi sauti hii ikitokea kila kona. Sauti ilikua ya yule Bibi Kizee jini, aliniita huku akicheka kwa sauti kubwa sana.
Sikujali vitisho vyake, nilitaka kumaliza mchezo wote ili Mama yangu apumzike kwa amani, ili nitimize alichoniambia Baba, pia niipate nyumba ya ndoto ya Baba yangu japo alikua gerezani. Hivyo vitu vitatu vilinisukuma hadi nililifikia geti
Sauti ilizidi kusambaa kila kona, haikua sauti moja pekee bali zilikua sauti nyingi, niliisikia sauti ya Caren na Zena, nilikua nawasikia wakiniita. Niliogopa lakini sikua na sababu ya kurudi nyuma, sikutaka hata kutazama nilipotoka ili nisije kupata woga zaidi.
Nilijua ilikua ni hatua muhimu sana maishani mwangu, ilikua ni hatua ya jasho na damu. Nilipaswa kuwa askari ndani ya Uwanja wa vita, nilizidi kutetemeka, nilipolifungua geti nilihisi hali ya utofauti kabisa
Palikua na ubaridi wa ajabu halafu sauti za maongezi yangu ya mwisho na Caren zilikua zikisikika, Caren alivyokua akiniambia kua anaondoka Usiku ule. Chozi lilinivuja, nilifuta chozi
langu, palikua na nguvu kubwa sana iliyokua ikinivuta kuelekea ndani ya nyumba yetu. Nywele zilikua zinahesabika kama vile zinanyonyoka.
Hakika nilikua katika nyakati ngumu zaidi kuwahi kupita kwenye maisha yangu. Hapakua na yeyote pembeni yangu, nilipoinua macho baada ya kujifuta mchozi nilimwona Mama yangu Mzazi kitu ambacho kilinishtua sana. Mtu ambaye tulimzika siku chache zilizopita alikua amesimama mita kadhaa karibu na Bustani ya Mauwa.
Alikua amevalia mavazi meupe kama ambavyo inasemekana Malaika huvalia, alikua msafi sana kiasi kwamba alikua aking’aa mithiri ya Kioo juani, halafu alikua akitabasamu sana. Macho yalinitoka nikimtazama Mama yangu, nilijua Mama yangu amerudi kunisaidia kwenye hii vita.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TISA
COMMENTS ZIWE NYINGI SASA
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
13 Comments
Maskin weee😎😎
Mmmhhhh?!!
Jmn admin iweke next
Ohhh its hurts🥲🥲
Hatar sanah hii
Malizia admin tamu sana
Aiseeeee ni maumivu sanaaa
Adimini kuna buku la soda toa cha tisa
Ooh mbn huzunii leta ya 9 admin
Dah🤔
Mwaga ya tisa mkuu
Oooooh my. God🥺🥺🥺
Mola ampe ujasiri aumalize mtihani salama salmini🙏🏽🙏🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽
Kaka mkubwa eeeee 🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽
Tupe ya9 chaaaaaàaaaaaaaaaaap🙌🏽🙌🏽