Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 07
Hatimaye Mama yangu aliungana na Zena na Caren kwenye makazi ya milele. KilichokuaΒ kimebakia kwangu kilikua fumbo kubwa, hakuna aliyejua kuhusu ile nyumba yenye kaburi naΒ jini anayeuwa.Β
Sikutaka kumwambia yeyote, moyo wangu ulijawa na kisasi. Sikuuona umuhimu wa kuendeleaΒ kuishi ikiwa nimepoteza Wapendwa wangu kwa usiri wangu. Baba alifikishwa Mahakamani sikuΒ Nne baada ya kumzika Mama, alikiri mbele ya Mahakama kua alitenda Mauwaji hayo kwaΒ mikono yake kwa kile alichokiita wivu wa Mapenzi. Endelea
SEHEMU YA NANE
Baba alivikwa kofia ya Muuwaji, alisemwa na kutukanwa kila kona. Hatimaye alihukumiwaΒ Miaka 13 jela ka kosa hilo, kutokana na Umri wake ilikua rahisi kusema alikua anamaliziaΒ Maisha yaliyobakia akiwa gerezani. Siku moja nilimtembelea gerezani, sikuwahi kuzungumzaΒ naye tangu tulipoachana siku ile ya kifo cha Mama kule Hospitali.Β
Japo alikua gerezani lakini Baba alitabasamu mbele yangu na kuniita
βMwanangu Celinβ kisha alinikumbatia kwa hisia ya furaha sana ya kuniona, alinishika mabegaΒ yangu akaniambiaΒ
βSiku moja utakua Mama, utakua na Watoto ndipo utajuwa nini Maana ya kua Mzazi. Sijali niΒ shida kiasi gani nitazipata Mwanangu lakini furaha yangu ni kukuona ukitabasamu siku zote,Β ukiwa huru kama kijana na kutimiza ndoto zakoβ Nilifumba macho kwa hisia ya maumivuΒ makali ya moyo, maneno ya Baba siyo tu yaliniumiza bali yalinifundisha nini Maana ya kuwa Mzazi.Β
βUsilie Celin, Mimi Baba yako nitakuombea kila dakika iendayo, kamwe sitakuacha Upotee.Β Wewe ni Jasiri Celin, unaweza kulimaliza hili, hata kama hautanitoa hapa lakini utapigana hiiΒ vita na kulipa kisasi cha Wazazi wako, rudisha ile nyumba mikononi mwako, ni jasho languΒ nililolipigania Ujana wangu woteβ nilishusha pumzi zangu, Baba alikua akizungumza manenoΒ katili sana lakini yalikua yakinipa ujasiri na kunikumbusha kua nimebakia peke yangu nje yaΒ Dunia yake, nje ya Dunia ya Mama yangu.Β
βPale chumbani kwangu kuna kabati dogo, nimehifadhi kadi yangu ya Benki. Kuna pesa yaΒ kukusaidia Binti yangu, namba ya siri ni Mwaka wako wa kuzaliwa. Usirudi hapa hadi uweΒ umelipa kisasi, umerudisha kila kitu. Ikiwa umeshindwa basi nenda mbali na Dunia yanguΒ Celinβ alisema Baba kisha alinionesha sura katili sana, akageuka na kuondoka akiongozwa naΒ Askari magereza. Aliniacha nikiwa nimesimamaΒ
Baba yangu hakuniaga, aliondoka mbele ya macho yangu mithiri ya Barafu juani, aliniachia kaziΒ nzito sana. Nilimshukuru Mungu kwa baraka ya uzima na uhuru, nilirudi nyumbani kwaΒ mjomba.Β
Jioni nilimueleza Mjomba wangu kua ninarudi nyumbani, alikua na wasiwasi na maswali mengiΒ lakini nilimueleza jambo moja kua, siwezi kuikimbia nyumba yetu. Huzuni zitanifuata naΒ zitaondoka zenyewe, Mjomba Mgina aliniruhusu nirudi nyumbani japo alijua nitaishi pekeΒ yangu.Β Β
Kesho yake Asubuhi nilikodi Bajaji ili nirudi nyumbani, moyo wangu ulipasuka, ulikosa UwogaΒ tena, nilijua naenda kwenye nyumba ya namna gani. Nikiwa ndani ya Bajaji safari ikiwaΒ imeanza, nilianza kuihisi hali ya tofauti sana ambayo mara kadhaa niwapo hatarini huwa naihisi.Β
Kichwa kilianza kua kizito ghafla tu, masikio yalikua yakipiga kelele mithiri ya filimbiΒ ikipulizwa ndani ya sikio langu. Mwili ulikua ukinisisimka sana, nikamuuliza dereva wa BajajiΒ
βUnaihisi hali ya tofauti?β akacheka kidogo akaniulizaΒ
βHali ipi hiyo?β swali lake lilikua ni jibu tosha kua alikua katika hali ya kawaida tu walaΒ hakuhisi kama ninavyohisi, nilijiinamia huku nikiwa nimeziba masikio yangu. Bajaji ilikuaΒ ikiendelea na safari, mara nilianza kusikia Honi ya Bajaji ikipigwa sana na yule dereva,Β nilistajaabu.
Wakati nanyanyua kichwa changu niangalie mbele nilisikia sauti moja ya kishindo, nikajigongaΒ mahali na kuumia. Bajaji ilikua imetumbukia mtaroni. Halafu yule dereva akawa wa kwanzaΒ kutoka kisha akanitoa na Mimi kwenye bajaji iliyolala mtaroni upande, nilimulizaΒ
βImekuwaje?β nilikua na maumivu makali kwenye kiwiko cha mkono wa kulia, yule derevaΒ akaniambiaΒ
βNilimwona Bibi mmoja akiwa amesimama barabarani, nilipojaribu kumkwepa ndio tumepataΒ ajaliβ nilivyosikia tu kuhusu Bibi, nikajua ni yule jini ananiwinda animalize. Sikutaka kuulizaΒ chochote tena, nikamlipa pesa yake ya safari hata kama hatukufika mwisho wa safari, kishaΒ nilichukua begi langu la mgongoni nikaanza kutembea kando ya Barabara.Β
Kichwa kilikua na mawazo tele, nilijitahidi sana kujiambia kila kitu kitakua sawa lakini nilikuaΒ ndani ya vita kali ya Mimi na Mimi, nilijua ninachojiambia kilikua kigumu sana lakiniΒ niliendelea kujiaminisha huku nikitembea. Akili yangu ilihama kabisa nikaanza kuwaza mamboΒ mengine ya Kutisha, ghafla nilisikia honi ya pikipiki nyuma yangu.Β
Ile nageuka tu naiyona Pikipiki ikija kwa kasi ikielekezwa kwangu, macho yalinitoka.Β Nilikubaliana na akili yangu kuwa siwezi kuikwepa na ilikua hatua chache kunifikia, nilifumbaΒ macho yangu nisione namna mwili wangu utakavyovamiwa na ile pikipiki. Ghafla nilihisiΒ kuvutwa nikajikuta pembeni ile pikipiki ikapita kama Mshale wa masafa marefu.Β
Nilishtuka sana, mkono wa Mtu mwingine ulikua umenishikilia. Niligeuka haraka kumtazamaΒ aliyenisaidia nikakutana na yule Mwanaume aliyekufa na kuzikwa ndani ya nyumba yetu.Β Nilishtuka sana lakini akanipa ishara ya kutulia, kiukweli moyo wangu ulikua unaenda mbioΒ sana. Macho yalinitoka nikiwa ninahema na kumeza mate kupitia koo langu kavu.Β Β
βShiiiβΌ usiogope Celinβ alianza kusema kisha aliniambia nimfuate, nilisimama nikiwaΒ ninamwangalia akitembea. Nilijiuliza maswali mengi ya haraka lakini jibu nililolipata niΒ kumfwata maana ndiye Mtu pekee anayeweza kunisaidia.Β
Alinisogeza mahali nikiwa nimebeba begi langu la Mgongoni,alisimama mbele ya gari mojaΒ akaniambiaΒ
βIngia kwenye gari nitakupelekaβ niliikunbuka ile gari, ni ile ambayo siku ya kwanza tunaonanaΒ alinipakia kisha alitoweka nayo. Alinisistiza kwa ishara ya mkono kua niingie ndani ya gari,Β nilijiuliza mara mbili mbili kabla ya kufungua mlango wa gari na kuingia ndani ya gari,Β nilipofunga mlango alianza kusemaΒ
βAmedhamiria akumalize, ameshaiona hatari kwakoβ alisema kwa sauti iliyojaa vituo vituo hukuΒ akiwa anadadisi nje ya gari kupitia kioo.Β
βKama wewe Kaka yangu una nguvu za ajabu kwanini usipambane naye, mimi sina nguvu yaΒ aina yoyote ileβ nilisema, alinitazama kisha baada ya sekunde kama kumi na tano hiviΒ
akaniambia βNimekuchagua sababu una ujasiri ndani yako, unafikiria wamepita wapangajiΒ wangapi kwenye ile nyumba? Wote wamekufa vifo vinavyofananaβΒ
βNani anaimiliki na kwanini anaipangisha wakati ni nyumba iliyojaa mauzauza?βΒ
βYule jini ndiye anayeimiliki baada ya kumuuwa Baba yetu. Kila anayepangishwa pale anaishiaΒ kufa kifo kibaya sana, hakuna aliyewahi hata kupata muda wa kuchunguza chochote kile,Β walikufa kikatili sana. Sijui wewe ni Binadamu wa aina gani ambaye uliweza kuichunguza ileΒ nyumba. Yule jini amekua akijigeuza kwenye sura ya Baba na kutafuta dalali kwa ajili ya kuiuzaΒ au kuipangisha lakini wote walifia mleβ alisema huku akitumia mikono yake kumaanishaΒ alichokua anakisemaΒ
βBahati nzuri ni kwamba pana uvumi mkubwa wa watu kupotea ndani ya ile nyumba, lakini kwaΒ yeyote anayefwatilia hukuiona cha Mtema kuni.β Alisema kisha aliwasha gari, safari ilianza. Aliniacha na maswali mengi sana kichwani kwangu, sikujua niseme nini na nini NnyamazeΒ
βNimepoteza kila kitu maishani, sina thamani. Mimi ni chanzo cha maafa yote, laiti kamaΒ nisingeliikubali ile nyumba pasingelitokea maafa yoyote yaleβ nilisema huku nikitokwa naΒ machozi. Yule Mwanaume aliyeniambia kua ni Mfu alikua akiendesha lile gari kwa mwendo waΒ kawaida.Β
βUsijali Celin, giza totoro ni ishara ya mapambazuko. Kila kitu kitakuwa sawaβ aliniambiaΒ
βHata kama kila kitu kitakaa sawa sitaweza kumrejesha Mama yangu, sitaweza kumtoa BabaΒ yangu jela, pia siwezi kuwarudisha Zena na Caren. Nimepoteza furaha, nimebakia kopo tupuβΒ nilizidi kutokwa na Machozi huku nikiitumia mikono yangu kufuta chozi langu.Β
βKila jambo hutokea kwa sababu Celin, Mungu alikuleta hapa ili umalize kila kituβ aliendeleaΒ kusema, maneno yake yalijaa faraja lakini nafsi yangu ilitawaliwa na kutu ya kutosha kiasiΒ kwamba nilihitaji tumaini zaidi ya maneno matupu.Β Β
βSijui naanzia wapi namalizia wapi, napambana vipi?β nilimuuliza, akanijibuΒ Β
βNitakueleza namna ya kufumbua hili fumbo Celin, kwasababu una hiyo shanga mkononi,Β hawezi kukudhuru kwa chochote labda amtumie Binadamu kama alivyofanya kuwatumia wazaziΒ wako kukudhuru wewe. Unatakiwa kwenda kwenye chumba ambacho sauti ya Dada yangu huwaΒ inasikika, hakikisha unakaa humo hadi mlango ufunguke, ukiweza kuingia ndani ya shimoΒ ndimo lilimo kaburi la Dada yangu. Mwambie Haji amekutuma umsaidie kutoka ndani ya lileΒ kaburi, ukiweza kumtoa ndio mwarobaini wa hili tatizo Celin, tutaunganisha nguvu zetu naΒ kummaliza yule jini, tutakuachia nyumba kwa amani na utaishi kwa amani zaidi bila tatizoΒ loloteβ alisema.Β
Haikua rahisi kuingia ndani ya nyumba ile, niliyoyaona kwa yule jini yalinifanya niingiwe naΒ hofu kubwa, alikua akiniwinda sana aniuwe lakini nilikua nanusurika.Β
βNajua una hofu lakini gharama ya kumtoa Dada yangu ni ndogo zaidi ya utakachofanyiwa naΒ yule Jini, atakuandama Maisha yako yote wewe na kizazi chako. Hamtaishi kwa amani hadiΒ atakapo hakikisha amekumaliza Celin, vaa ujasiri. Mimi siwezi kurudi ndani ya ile nyumba,Β nguvu kubwa inanizuia Mimi kukanyaga ile ardhi na siwezi kupambana nayo, wewe unawezaΒ kuingia ndani ya ile nyumba sababu ni Binadamuβ alizidi kunipa moyo na ujasiri niwezeΒ kiifanya kazi ngumu iliyo mbele yangu.Β
Alipokaribia karibu na nyumbani alisimamisha gari mita kadhaa akaniambiaΒ
βHapa ndiyo mwisho wangu, siwezi kusogea zaidi na kama nitakua mbishi basi nafsi yanguΒ itaangamia na huu mpango hautafanya kazi tena. Nenda Celin, unawezaβ alisema kwa ujasiri naΒ hamasa ya hali ya juu sana. Nilihema kwa nguvu ili nijiandae kuteremka ndani ya gariΒ
Nilifungua kioo, palikua kimya. Nilisadiki maneno ya huyu Mfu kua yule jini alikua anauwaΒ Watu wa nyumba jirani. Upepo wa taratibu ulikua unasomba majani makavu yaliyoangukaΒ barabarani, alinitazama tena akanipa ishara ya kichwa kua niende. Niliteremka kutoka ndani yaΒ gari nikiwa nina hofu sana, nilimaliza miguu yote. Mwili wangu ilikua nje ya lile gari la maajabuΒ ambalo baada ya Mimi kushuka lilipotea tena katika mazingira tatanishi.Β
Safari hii sikushtuka tena sababu nilishaambiwa mengi, nilitembea taratibu kama Mtu mwenyeΒ vidonda mapajani, akili yangu ilitaka kwenda lakini moyo wangu ulikua ukidunda kwa hofuΒ huku ukiniambia nirudi naelekea kwenye hatari.Β
Nilitembea hivyo hivyo huku picha halisi ya namna nilivyomuuwa Mama yangu ikiendeleaΒ kupita akilini, ilinipa uchungu, nilimkumbuka Baba yangu pia. Yupo Magereza kwasababuΒ yangu Mimi, kauli zake za mwisho zilijirudia. Nilijipa moyo na ujasiri uliendelea kunivaa kadiliΒ nilivyokua napiga hatua kuielekea nyumba yetu.Β
Sauti ya ajabu ya kunongβona ilikua ikiniita jina langu, nilihisi sauti hii ikitokea kila kona. SautiΒ ilikua ya yule Bibi Kizee jini, aliniita huku akicheka kwa sauti kubwa sana.Β Β
Sikujali vitisho vyake, nilitaka kumaliza mchezo wote ili Mama yangu apumzike kwa amani, iliΒ nitimize alichoniambia Baba, pia niipate nyumba ya ndoto ya Baba yangu japo alikua gerezani.Β Hivyo vitu vitatu vilinisukuma hadi nililifikia getiΒ
Sauti ilizidi kusambaa kila kona, haikua sauti moja pekee bali zilikua sauti nyingi, niliisikia sautiΒ ya Caren na Zena, nilikua nawasikia wakiniita. Niliogopa lakini sikua na sababu ya kurudiΒ nyuma, sikutaka hata kutazama nilipotoka ili nisije kupata woga zaidi.Β
Nilijua ilikua ni hatua muhimu sana maishani mwangu, ilikua ni hatua ya jasho na damu.Β Nilipaswa kuwa askari ndani ya Uwanja wa vita, nilizidi kutetemeka, nilipolifungua geti nilihisiΒ hali ya utofauti kabisaΒ
Palikua na ubaridi wa ajabu halafu sauti za maongezi yangu ya mwisho na Caren zilikuaΒ zikisikika, Caren alivyokua akiniambia kua anaondoka Usiku ule. Chozi lilinivuja, nilifuta choziΒ
langu, palikua na nguvu kubwa sana iliyokua ikinivuta kuelekea ndani ya nyumba yetu. NyweleΒ zilikua zinahesabika kama vile zinanyonyoka.Β
Hakika nilikua katika nyakati ngumu zaidi kuwahi kupita kwenye maisha yangu. Hapakua naΒ yeyote pembeni yangu, nilipoinua macho baada ya kujifuta mchozi nilimwona Mama yanguΒ Mzazi kitu ambacho kilinishtua sana. Mtu ambaye tulimzika siku chache zilizopita alikuaΒ amesimama mita kadhaa karibu na Bustani ya Mauwa.Β
Alikua amevalia mavazi meupe kama ambavyo inasemekana Malaika huvalia, alikua msafi sanaΒ kiasi kwamba alikua akingβaa mithiri ya Kioo juani, halafu alikua akitabasamu sana. MachoΒ yalinitoka nikimtazama Mama yangu, nilijua Mama yangu amerudi kunisaidia kwenye hii vita.
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TISA
COMMENTS ZIWE NYINGI SASAΒ
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
32 Comments
Maskin weeeππ
Mmmhhhh?!!
Sehem ya tisa inatok lin asee simuliz ni nzur saan
Jmn admin iweke next
Ohhh its hurtsπ₯²π₯²
Hatar sanah hii
Malizia admin tamu sana
Aiseeeee ni maumivu sanaaa
Adimini kuna buku la soda toa cha tisa
Ooh mbn huzunii leta ya 9 admin
Dahπ€
Mwaga ya tisa mkuu
Oooooh my. Godπ₯Ίπ₯Ίπ₯Ί
Mola ampe ujasiri aumalize mtihani salama salminiππ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½
Sehemu ya tisa jaman
Kaka mkubwa eeeee ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½ππ½
Tupe ya9 chaaaaaΓ aaaaaaaaaaapππ½ππ½
1sre4a
Next plzπ
Noma Sana
Vita inazidi kua nzitoo, story inazid kunoga aiseee
Uchawi upo jmn tusimame na Munguπ
Next pleaseππΎ
Tuletee sehemu ya tisa
owyijz
gp0gsa
a8nu1n
evpym9
z6rpeh
cs0m9n
m7pu0d
pzhtkz
h2aq45
76yu24