Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Kumi-10)
    Hadithi

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Kumi-10)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 6, 2025Updated:May 12, 202529 Comments20 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 09

    Basi nilikata tamaa, chozi lilinibubujika. Nikajikuta nikipandwa na hasira sana, nikasema kwaΒ  mara ya mwisho kwa sauti kubwa ya hasira huku chozi likinibubujikaΒ 

    β€œFungukaaaβ€Ό!” ghafla tu nililiona lile shimo la ajabu likifunguka nyuma yangu, palikua panatoaΒ  mvuke na joto kwa mbali, rangi nyekundu ilikua imelizunguka shimo lile, nilichungulia ndani yaΒ  shimo maana sikuwahi kuingia hivyo nilikua sijui chochote kile hata kunaonekanaje nilikua sijui.Β 

    Nilitumia muda mrefu nikiliangalia tu, kisha niliisikia sauti nzito ikiuliza kutoka ndani ya shimo. Endelea

    SEHEMU YA KUMI

    β€œKwanini umenifungua?” nilishtuka nusura nikimbie, shimo lilikua likiongea. Nilijiuliza nijibuΒ  nini, Nani ananiuliza ni shimo au yule jini. Nilimeza funda zito la mate huku vipele vidogoΒ  vidogo vya hofu vikianza kunitoka.

    β€œMimi….mi-mimi naaa…” nilibabaika sana nikiwa napepesa macho yangu, kila nilochofikiriaΒ  kukisema niliona kama nitakosea, niliendelea kubabaika. Cha ajabu niliulizwa tena kwa kutajwaΒ  kabisa jina languΒ 

    β€œKwanini umenifungua Celin?” hapa nilishindwa hata kujizuia nilionesha ni namna gani mimiΒ  nilikua mwoga, nilishtuka kiasi kwamba hata mate yaligoma kupita kooni, kifua changu kilijaaΒ  upepo huku miguu yangu ikiwa inatetemeka. Nguvu ziliniisha kabisa.Β 

    Nilihema kuliko kawaida, kisha lile shimo lilijifunga likatoweka baada ya Mimi kukaa kimya.Β  Nilishikilia moyo wangu, nilijikuta nikikaa chini taratibu huku nikiendelea kuhema. NilimezaΒ  funda kubwa la mate kisha nikajiulizaΒ 

    β€œNilipaswa kuingia au kujibu?” Nilikohoa mara moja kisha niliutazama ule ukuta ambaoΒ  ulifanya lile pango la ajabu likafunguka. Nilimkumbuka Mama yangu, Baba, Caren na Zena,Β  wote walikua wahanga wa hii nyumba ya ajabu yenye kaburi. Niliingiwa na shahuku yaΒ  kumaliza tatizo kabisa, basi nikasema tena kwa Ujasiri sanaΒ 

    β€œFungukaaa‼” Nilisema kwa nguvu hadi vipele vya msisimko vilinitoka.Β 

    Safari hii sauti yangu moja tu ilifanya lile shimo lifunguke, sikushtuka kama ilivyokua mara yaΒ  kwanza. Niligeuka na kulitazama, nilimwomba Mungu maana nilihitaji kushuka chini ndani yaΒ  lile kaburi la ajabu ili niipate nafsi ya Sabra.Β 

    Nilitembea taribu hatua kama tatu hivi kisha nilifika mbele ya shimo, nikachungulia lakiniΒ  hakuna nilichoambulia ambacho kingenipa uelekeo sahihi. Sikuitaka ile sauti iniulize ninatakaΒ  nini, tayari moyo na akili yangu vilijua nahitaji nini zaidi.Β 

    Niliingiza mguu mmoja kisha nikaingiza mwingine, ndani yake palikua na harufu kali ya udi.Β  Niliuzamisha mwili mzima, ghafla tu nikajikuta ndani ya shimo lenye giza la kutosha, tofauti naΒ  mwanzo nilipoona mwanga ndani ya shimo lakini palikua giza kabisa. Hakuna nilichokionaΒ  mbele wala nyuma yangu, giza nene lilikua limelifunika shimo lote.Β 

    Nilisimama huku nikiangaza kama naweza kuona eneo la kutokea lakini haikua hivyo,Β  nilijiingiza shimoni bila kujua nawezaje kutoka. Palikua kimya sana, udi uliendelea kunukia,Β  nilisimama nisijuwe naelekea wapi. Mara nilisikia sauti ya yule Bibi Kizee, alikua akiimbaΒ  nyimbo zake nisizo zielewa.

    Niliingiwa na hofu lakini niligundua kama vile alikua na pirika zake, kivumbi kilikua ni namnaΒ  ya kuyafanya macho yangu yaone angalau nipate pa kuanzia, nilimsikia tena akitafuna hukuΒ  akitoa miguno ya kufurahia alichokua anakula, vishindo vya kucheza pia nilivisikia.Β 

    Sauti yake haikua karibu sana na Mimi, nilichagua kupapasa kwa kutumia mkono wangu waΒ  kushoto ambao ndio nilikua nautumia sana, niliendelea kupapasa huku nikipiga hatua fulaniΒ  ndogo ndogo za kuvizia. Kadiri nilivyozidi kwenda mbele nilianza kuhisi mwanga kidogo,Β  nikapepesa macho yangu halafu nikaendelea mbele taratibu sana.Β Β 

    Sikutegemea kama kule chini kulikua na nafasi kubwa kiasi kile, niliweza kupiga hatua zaΒ  kutosha kuifuata ile sauti ya yule jini, hapakua pa kawaida kabisa maana kadili nilivyosongaΒ  nilihisi kuna vitu vinaota kwenye mwili wangu mithiri ya manyoya hivi. Nilisisimka sana, hofuΒ  iliendelea kunisumbua lakini sikutaka kukoma nilijiambia kama kufa ni bora nife kulikoΒ  kushuhudia Wazazi wangu wakiwa wameharibikiwa.Β 

    Niliendelea kutembea huku ile hali ya kuota manyoya ikizidi kuendelea hadi nilianza kuhisiΒ  nimekua kiumbe cha ajabu sana, ule mwanga ulizidi kujaa machoni pangu kiasi kwamba nilianzaΒ  sasa kupata nuru ya kuona mbele. Nilichokua nakiona kilizidi kunitia hofu, palikua na mafuvuΒ  mengi chini, panya walikuwa wakiingia kwenye mafuvu na kutoka. Sikutaka hofu iendeleeΒ  kunitawala maana nilijua kama hofu itanitawala basi sitaweza kukamilisha kazi ya kuipata nafsiΒ  ya Sabra.Β 

    Pole pole, nilianza sasa kuisikia ile sauti ya Mwanamke anayeimba. Safari hii niliisikia kwaΒ  ukaribu zaidi, ilionekana ilitoka eneo ambalo niliisikia sauti ya yule jini, niliendelea kusongaΒ  taratibu nikiwa makini sana. Sikutaka hata kujiangalia maana nilijua nikifanya hivyo nitajiogopaΒ  kwa jinsi ambavyo mwili wangu ulikua umeota manyoya madogo madogo.Β Β 

    Nilifika sehemu moja, palikua na mlango ambao ulikua haujafungwa vizuri, upenyo mdogoΒ  uliobakia ndio uliokua ukinipa nuru. Ndani palionekana kua na taa kali sana, sauti ya kuimba naΒ  sauti ya kutafuna vilikua vinaendelea kusikika. Nilisimama kidogo kabla ya kufanya uamuzi waΒ  kuchungulia ndani

    Nilimwona Mwanamke mmoja aliyevalia gauni jekundu, alikua amekaa chini akiimba hukuΒ  chozi likimtoka. Alikua anatoa chozi la damu machoni mwake, kwa haraka haraka nilitafsri kuaΒ  huwenda alikua akimwimbia huyu Jini Bibi Kizee, nilitaka kuona ni nani aliyekua mbele yake.Β Β 

    Niliuingiza mwili wangu nusu ndani ya kile chumba, nikafanikiwa kumwona yule Bibi kizeeΒ  akiwa kwenye umbo la kawaida kabisa kama lile analonitokeaga nalo, alikua akifurahia nyamaΒ  aliyoishikilia mkononi lakini pia alikua akicheza cheza ikionesha namna ambavyo ile nyimboΒ  ilikua ikimburudisha.Β 

    Ndipo nilipo yaaminu maneno ya yule Mwanaume kua ndani ya nyumba yetu palikua na kaburiΒ  ambalo alizikwa yeye pamoja na Dada yake, haitoshi niliamini kua Dada yake Sabra alikuaΒ  akitumikishwa na jini huyo ndiyo maana alikua akiimba huku akiwa analia. Ndani palikua naΒ  mwanga mkali kiasi kwamba hata sisimizi angeweza kuonekana kirahisi sana. Kiumbe chochoteΒ  ambacho kingeingia ndani ya chumba kingeonekana haraka sana.Β 

    Sabra alikua akiimba huku akionesha kama vile alihisi mlangoni palikua na Mtu, shingo naΒ  macho yake vilikua mlangoni mara kwa mara huku akiendelea kuimba na kumburudisha yuleΒ  Bibi kizee.Β Β 

    Mara nyingi alikua akipepesa macho yake yaliyokua yakitiririsha chozi, alikua akiniangalia kishaΒ  akimwangalia Bibi Kizee, sura yake ilionesha mateso makali aliyokua akiyapitia, alikosa nuruΒ  kabisa. Lakini alionesha kunishangaa maana ilikua ndiyo mara ya kwanza Mimi na yeyeΒ  tunaonana halafu isitoshe pale chini palikua ni eneo hatari sana kwa Binadamu wa kawaida kamaΒ  Mimi.Β 

    Nilikua na uhakika kabisa kua ndiye ninayepaswa kuondoka naye ili akakutane na Kaka yakeΒ  waunganishe nguvu zao kwa ajili ya kumwangamiza Bibi Kizee. Wakati naendelea kufikiria niniΒ  cha kufanya nilimsikia Bibi Kizee akisemaΒ 

    β€œInatosha” alisema kwa sauti kavu iliyojaa amri, kisha naye aliacha kula alichokua anakula.Β  Akavuta harufu kwa kutumia pua yake ndefu kama vile alihisi uwepo wa Binadamu.Β 

    Alianza kuimba yeye kwa kuguna guna huku akitikisa kichwa chake, halafu akaweka mikonoΒ  yake mgongoni mwake akaanza mwendo wa kuja mlangoni, Sabra akanipa ishara kwa kutikisaΒ 

    kichwa chake, papo hapo nikajua napaswa kufanya nini. Nikarudi nyuma haraka haraka halafuΒ  nikabana sehemu.Β 

    Ni hatua chache tu kutoka mlangoni, alipofika nje aligeuka alipotoka kisha akasemaΒ Β 

    β€œFungaaa‼” Mara moja ule mlango ukafunga kisha akaondoka zake, sikutaka kutingisha hataΒ  pumzi zangu, nilizibana vizuri sana hadi pale nilipomsikia akisema Fungukaa akiliamlisha lileΒ  shimo nikajua alikua anaondoka.Β 

    Basi haraka nikafika pale mlangoni, japo palikua na giza la kutosha lakini hisia zanguΒ  ziliniongoza vyema hadi nilipofika mlangoni. Mlango ulikua umefungwa, nilipapasa hukuΒ  nikiusukuma kuona labda utaweza kufunguka. Nilijaribu mara kadhaa bila mafanikio hatimayeΒ  niliona ni bora nimwite kwa jina lakeΒ 

    β€œSabra” nilimwita nikiwa nategemea pengine angesogea mlangoni na kunipa msaada waΒ  kuufungua.Β 

    β€œWewe ni Nani?” Niliisikia hii sauti ya kike ya Sabra, ilitoka kwa upole sana. Ilijaa mshangaoΒ  mkubwa wa kuona Binadamu akiwa ndani ya lile kaburi.Β Β 

    β€œMimi ni Celin, Kaka yako amenituma” nilimjibu. Pakawa kimya sana, wastani wa dakika mojaΒ  hivi nikamsikia tenaΒ 

    β€œKaka yangu? Wewe ni Nani hasa na umewezaje kufika huku?” Aliniuliza, nilikua na uhakikaΒ  wa jambo moja, alikua amepoteza tumaini, alishaamini kua nafsi yake ingekua utumwani daima.Β  Hakutegemea kusikia kua kaka yake bado anamhagaikia.Β 

    β€œHaji?” Aliuliza kwa Mshangao zaidi.Β 

    β€œNdiyo, ni yeye. Amenituma kukutoa ndani ya kaburi. Kwa pamoja mtaweza kumuangamizaΒ  huyu jini ambaye amekua akifanya mauwaji kila uchwao tena kwa Watu wasio na hatia,Β  nimepoteza Wazazi wangu kwasababu yake” niligongelea msumari wa mwishoΒ 

    Alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema.

    β€œSijui kama itawezekana, nimedhohofika vya kutosha. Sijioni nikiwa nina nguvu” alisema, sautiΒ  yake ilibadilika kidogo. Aliongea kwa huzuni. Chozi lilikaribia kunitoka, maneno yake yalijaaΒ  hatma isiyo na matumaini.Β 

    β€œHaijalishi Sabra, ni lazima utoke humu ili ukaungane na Kaka yako kwenye Maisha mengine.Β  Hauwezi kua Mtumwa Daima” nilijikuta nikianza kumshawishi niondoke naye japo nilikua sijuiΒ  uhatari mkubwa uliopo mbele yangu.Β Β 

    β€œCelin, upo sehemu iliyojaa hatari kubwa sana. Hiki kiumbe kina nguvu za ajabu sana sijui kamaΒ  unaweza ukatoka ukiwa hai”  

    β€œHaijalishi Sabra,nikifa kwenye mapambano itakua haki yangu kuliko kuishi kwa furahaΒ  iliyokandamizwa na upweke na mateso. Natafuta haki ya kifo cha Mama yangu pamoja na hakiΒ  ya Baba yangu” nilisema kwa Ujasiri, kiukweli nilikua nimefika mwisho wa hofu yangu.Β Β 

    β€œSawa, fungua unitoe” alisema, nilikumbuka namna yule Bibi Kizee alivyoufunga huu mlangoΒ  kwa kusema tu Funga. Nikakumbuka namna hata lile shimo la ajabu linavyofunguka kwaΒ  kuliamrisha, basi nikajiweka sawa ili nisemeΒ 

    β€œFungukaaa‼” Nilisema kwa ujasiri na Mamlaka makubwa sana, mara mlango ulifunguka.Β  Ndani palikua pana nuru ya ajabu inayowaka na kufanya pawe na Mwanga mkali. PalijaaΒ  mafuvu ya vichwa vya Watu, macho yangu yalikutana na macho ya Sabra. Alichokua amekisemaΒ  ndicho nilichokiona kwenye sura yake, alikua amechoka na kukata tamaa.Β 

    β€œTwende Sabra” nilisema kisha nilimpa mkono, aliutazama sana Mkono wangu kwa sekundeΒ  chache za kuhesabu. Hakunipatia mkono wake, sikujali nilichotaka ni kuondoka naye. BasiΒ  tuliongozana akiwa anatembea kwa kuchoka choka hivi.Β 

    Hakutaka nimguse kabisa, hata alipoonekana kua amechoka anaelekea kuanguka, tulisogeaΒ  taratibu na alikua akizijua njia za mule ndani ya lile kaburi kubwa la ajabu, akawa ananiambiaΒ  kila kitu kinachohusiana na njia za mule kwa kila hatua ambayo tuliipiga.Β 

    Alikua anajua kila kitu hata lilipo lile shimo la kutokea ndani ya lile kaburi, kuna namnaΒ  nilijiuliza maswali mengi inawezekanaje Mtu anayejua pa kutokea na asitoroke siku zote hizo?Β 

    Nilipotezea suala hili, nikaweka nguvu zaidi kuhakikisha tunaondoka tukiwa salama kabisa.Β  AkaniambiaΒ 

    β€œNatamani sana kumwona Kaka yangu, ni muda mrefu nimeishi nikiwa mpweke” alisemaΒ  maneno yaliyonigusa moja kwa moja.Β 

    Nilitabasamu kidogo maana aliongea maneno yaliyojaa tumaini na kiu ndani yake, binafsiΒ  sikujua tunawezaje kutoka maana ndani ya kaburi ni udongo, hakuna simenti hivyo hata mahaliΒ  pa kutokea sikupajua.Β 

    Akapaza sauti akasemaΒ 

    β€œFungukaa‼” Haikuchukua hata sekunde nyingi, shimo likajitengeneza. Mwanga wa chumba chaΒ  stoo ukaonekana. Nikageuka kumtazama, nilikua na swali la kumuuliza lakini niliona ni boraΒ  tukitoka nimuulize. Tukafanikiwa kutoka salama ndani ya lile shimo, tukawa tumefika stoo.Β  Kumtoa Sabra ndani ya lile Kaburi ilikua rahisi kuliko hata kaka yake alivyoniambia kituΒ  ambacho kilinipa maswali mengi yasiyo na majibu.Β Β 

    Mara lile shimo likatoweka. Alikua anahema sana kama Mtu aliyechoka, alikua amedhohofuΒ  mno hadi nilimwonea huruma ila nilimuulizaΒ 

    β€œKwanini haukutoka siku zote hizo ikiwa unajua kila kitu?”  

    Nilikua na kiu sana ya kutaka kujua, alinitazama akanijibu harakaΒ 

    β€œKila jambo na wakati wake Celin” lilikua ni jibu fupi jepesi ambalo halikua chakula kizuri chaΒ  fikra zangu. Akanitazama kisha akaniulizaΒ 

    β€œUmevaa nini mkononi?” Swali lake lilinishtua kidogo na kuanza kunipa hofu maana kule chiniΒ  alikataa kabisa kumgusa. Nilijiuliza kwanini alikataa ikiwa yeye ni nafsi salama kama ya KakaΒ  yake ambaye ndiye aliyenipatia ile shanga.Β 

    Nilimeza funda la mate, nikatabasamu kidogo nikampa jibu bila kusema UwongoΒ 

    β€œHuu ni ulinzi amenipatia Kaka yako, ni kinga dhidi ya yule jini” nilimjibu, nilimwonaΒ  akitafakari jambo halafu mdomo wake ukawa mzito kama vile alitaka kusema jambo alafuΒ  akaghaili.

    β€œTwende anaweza kutukuta hapa” akasema kisha nikaongoza mbele maana mimi ndiyeΒ  ninayejua nini cha kufanya. Nilikua tayari nimempata Sabra ila sikujua ni namna gani nitawezaΒ  kumpata Kaka yake ili waunganishe nguvu zao na kupambana na kile kiumbe.Β Β 

    Tulitoka ndani hadi nje kabisa ya nyumba, palikua kimya lakini hali ya kusisimka mwili ilikuaΒ  ikinianza. Hisia hii iliniambia kua lile jini lilikua karibu na Mimi, nilihisi kuchanganikiwa maanaΒ  tayari nilikua nimefanikiwa kumtoa Sabra mle kaburini hivyo kama atatukuta basi ataniuwa.Β Β 

    Barabara ilikua tupu, sikujua nifanye nini lakini kwa haraka haraka nilifikiria niondoke na Sabra kutoka pale kwenda mbali kidogo mahali ambapo yule Kaka yake angeliweza kututokeaΒ  nikamkabidhi mdogo wake.Β 

    Tulitembea taratibu tukiiacha nyumba yetu nyuma, sikutaka tuelekee upande ule wa nyumbaΒ  jirani ya yule Mzee, tulisonga mbele kwa hatua nyingi za kutosha, hadi tulipofika mbali kiasiΒ  chake. Tulisimama, palikua kimya hakuna mazungumzo, niliangaza huku na kule kuonaΒ  huwenda angetokea lakini alikua kimyaΒ 

    β€œYupo wapi Haji?” Aliniuliza, sikua na jibu la moja kwa moja la kumpa maana Haji sikujuaΒ  nawezaje kumwita akatokea maana alikua kama Mzimu fulani hivi wa ajabu ambao ungewezaΒ  kutokea popote pale. Mahali tulipokua tumesimama palikua na miti mikubwa miwili, mmojaΒ  ulikua upande wa pili na mwingine ni upande tuliokua tumesimama Mimi na Sabra.Β 

    Tulisimama kwa dakika kama tano hivi nikiwa sielewi nafanya nini, kwakua Haji ni nafsi basiΒ  atakua ametuona lakini kwanini hatokei kumchukua Dada yake? Nilijiuliza swali hili nikiwa sinaΒ  jibu la moja kwa moja. Niliangaza huku na kule bila mafanikio, nikakata tamaa bila kujuaΒ  nitaenda wapi na Sabra.Β 

    Alikua akiniuliza mara kwa mara mahali alipo Kaka yake, hata pale nilipompa mgongoΒ  nilipogeuka alikua akinitazama sana lakini alikua hataki nimguse kabisa kitu ambacho kilikuaΒ  kinanishangaza kila dakika. Mara nilianza kuhisi kama vile nilikua napigwa na vitu mgongoniΒ  mwangu, sikutaka kugeuka moja kwa moja. Hapo mwili ulikua unazidi kusisimka sana.

    Akili yangu iliwaza mara moja kua pengine yule Bibi Kizee alikua ndiye anayenipiga na vituΒ  mithiri ya vidude vidogo vidogo ambavyo haviumizi lakini baadaye akili yangu ikanambiaΒ  huwenda nilipaswa kugeuka taratibu ili nijuwe ni Nani aliyekua akinishtua kwa nyuma naΒ  kwanini alifanya kua siri.Β 

    Niligeuza shingo kitaalam sana sidhani hata kama Sabra aliweza kung’amua, nilifanya kamaΒ  nageuka hivi. Ndipo nilipomwona Haji Kaka yake Sabra, akanipa ishara ya kunitaka nikaeΒ  kimya.Β 

    Sikujua ni kwanini alitaka nikae kimya, nikawa nazugazuga kama naangalia huku na kuleΒ  kumtafuta Kaka yake Sabra, nikawa naendelea na ule mchezo, nageuka kwa siri siri. BaadayeΒ  akawa ananiambia kwa ishara akimaanisha kua niliyekua nimesimama naye alikua siyo DadaΒ  yake Sabra. Jicho lilinitoka, msisimko ulizidi kuongezeka, mwili ulikosa nguvu ghaflaΒ  nikatamani nipate mahali nikae.Β 

    Sasa nikawa naunganisha mambo kadhaa na moja wapo ni kitendo cha kukataa nisimguse, hapoΒ  nikapata picha halisi sasa kua niliyetoka naye kaburini kwa kufikiria ni Sabra alikua ni yule BibiΒ  Kizee aliyejivika sura ya Sabra. Nilimeza funza zito la mate huku macho yakiwa yamenitoka,Β  japo nilijawa na hofu lakini sikutaka kumpa mwanya wa kugundua kua nimemshtukia.Β 

    β€œHuyo Haji anakuja saa ngapi jamani, siwezi kusubiria kumwona maana niliamini siweziΒ  kumwona tena” alisema Bibi kizee mwenye sura ya sabra, nilimtazama nikaachia katabasamuΒ  nikamwambiaΒ 

    β€œAtakuja muda sio mrefu, mimi sijui namna ya kumwita” 

    β€œOooh‼”  

    Bado alikua akinikwepa, alikua hataki nimguse hata kwa bahati mbaya, alikua anapiga hatua zaΒ  kunikwepa. Nilishajua hawezi kunidhuru kwasababu ya ule ushanga niliopewa na Haji. SikujuaΒ  nini Haji angefanya maana Bi Kizee alikua makini kunitazama kila hatua ninayoipiga, nilielewaΒ  lengo lake lilikua ni kupiga ndege wawili kwa jiwe moja.

    Bado Haji alikua akinipa ishara za siri nigeuke, pengine alikua na mpango fulani ila sasa BibiΒ  Kizee alikua hanipi huo muda, alikua makini zaidi na Mimi. Nilijaribu kugeuza jicho la kuibaΒ  lakini sikufanikiwa kumfikia Haji, ikabidi nimwambie Bibi KizeeΒ 

    β€œNinahisi Mkojo, nahitaji kujisaidia” nilimwambia nikiwa nina mtazama, nilihitaji nafasiΒ  muhimu zaidi kupata wazo la Haji maana aliyekua mbele yangu alikua siyo Sabra bali ni Jini.Β 

    β€œHaina shida, Mimi nitasimama hapa kumsubiria Haji. Usikawie” alinijibu, nilihisi nilikuaΒ  nimeukaribia ushindi. Nyuma yangu palikua na pori dogo lenye mti mkubwa ambao Haji alikuaΒ  amejificha, nikajifanya kuangaza huku na kule kisha nikakimbilia pori dogo ambalo ningekutanaΒ  na Haji.Β 

    Lakini wakati natoka nililiona tabasamu la Bi Kizee, nikajua sasa huwenda amejua kua nilikuaΒ  nimemshtukia. Nilipofika nyuma ya ule Mti nilimkuta Haji, upepo ulikua ukivuma kiasi kwambaΒ  maua yalikua yakituangukia. Haji aliniambia haraka harakaΒ 

    β€œYule Bibi amejua kua umejua, anaweza akaucheza mchezo lakini hawezi kushinda. Chukua hiiΒ  kamba, hakikisha unamfunga popote kwenye mwili wake” alinipa kamba ndogo nyekundu kamaΒ  zile wanazovaa wahindi mkononi.Β 

    Akanipa ishara ya kuondoka, kweli niliondoka pale na kurudi barabarani. Nilipofika nilikutaΒ  peupe. Yule Bibi Kizee hakuwepo pale barabarani, niliangaza huku na kule pengine ningemwona.Β 

    Macho yangu yalikua kodo kila mahali, nilihesabu idadi ya gari zinazopita bila mafanikio.Β  Hatimaye nilipogeuza shingo yangu nilimwona akija akitokea upande wa pili wa barabara.Β  Maswali hayakuniisha sababu nilikua sina uhakika kama alikua amegundua jambo au laa. IlaΒ  moyo wangu ulinieleza mengi juu yake, nilihisi aligundua jambo kama alivyonieleza Haji.Β  Nilipaswa kua muigizaji nguli japo yeye ana nguvu za kutambua mambo kwa haraka kutokanaΒ  na uwezo wake wa Kijini.Β 

    Alipofika nilipo, nilimtazama usoni pake. Alikua na haya fulani iliyoficha jambo. β€œBado hujaonana naye?” 

    β€œNani?” 

    β€œUlisema Haji!” 

    β€œAaah ndiyo, samahani hiki kichwa kinafikiria sana.” Nilisema huku nikifikiria zaidi namna yaΒ  kumfunga kamba yule jini, niliishikilia ile kamba kwa nguvu mkononi nikiwa nimeificha vizuri.Β 

    β€œMimi nafikiria turudi kule ndani, pengine anaweza kuja kule. Kumsubiria hapa ni kamaΒ  tunapoteza muda” alisema, machale yalinicheza kua alikua na lengo la kuniingiza mtegoni.Β 

    β€œAaahβ€Ό Alisema hawezi kuingia mle sababu anamwogopa yule Jini, Mimi naona angalau tuketiΒ  chini ya ule Mti kwa kitambo fulani. Huwenda anaweza kuja” naye aligeuka kuutazama mti huo,Β  ulikua Mti mkubwa uliomea vizuri kijani cha kutosha na matawi makubwa yaliyopeba majaniΒ  mapana. Alinitazama kisha akajibuΒ 

    β€œHakuna shida, kama tunaweza kufanya hivyo. β€œ Nilisubiria atangulie mbele ili nimfunge ileΒ  kamba haraka, kweli aliongoza mbele nami nikawa nyuma ya mgongo wake. Alikua mwingi waΒ  mazungumzo yasiyo isha, ndani yake alionesha alikua akimtaka sana Haji sababu nilishampa siriΒ  pasipo kujua kua yeye ni jini, ile siri ya nafsi mbili kuungana na kummaliza yeye.Β 

    Alikua akiutupa sana mkono wake wa kulia, alikua akitembea kwa kujiachia achia kama siyoΒ  yule aliyedhohofika. Macho yangu yalikuwa hayatulii, mapigo ya moyo yalinienda mbio. KilaΒ  hatua niliyoipiga ilikua ikitoa sauti ya kunikumbusha wajibu wangu wa kumfunga ile kambaΒ  lakini nilijawa na hofu sana.Β 

    Hadi tunafika chini ya Mti sikuweza kumfunga. Tulipokaa chini akaniulizaΒ 

    β€œUmekunja ngumi muda wote huumii?” Aliniuliza huku akiutazama mkono wangu wa kuliaΒ  ambao niliishikilia ile kamba, nilitabasamu kuondoa ngoma juani. Nilikua nawaza mamboΒ  mawiliΒ 

    Pale Mtini ni mahali nilipomwacha Haji, vipi kama atamwona? Swali la pili nilijiuliza nitamjibuΒ  nini?Β 

    β€œAaahβ€Ό Nimezoea siwezi kuumia, wala usihofu” Nilipomjibu hakusema chochote, alipelekaΒ  macho yake barabarani. Kumfunga ile kamba ilikua kazi ngumu sana, aliketi hatua moja kutokaΒ  kwangu pia alikua akigutuka mara kwa mara na kunitazama kama Mtu aliyejiandaa zaidi, hiiΒ  ilinipa hofu sana.

    Hakuruhusu nimsogelee sababu hakutaka kugusana nami akihofia kupata madhara sababu ya uleΒ  Ushanga wa ulinzi niliopewa na Haji. Kimya kilitawala, hisia ilizidi kuniambia kua atanigeukaΒ  endapo nitaonesha dalili zote kua nimegundua siri yake.Β 

    Kuna nyakati alinitazama kama vile alikua anataka kuniambia amegundua kila kitu lakiniΒ  nilimkatisha kwa kuzungumza, sauti za magari zilikua zikisikika kwa kuvuma.Β Β 

    β€œUna hakika Haji atakuja?” Akaniuliza, alijawa na shahuku sana sababu aliona muda ulikuaΒ  ukienda.Β Β 

    β€œNaamini hilo litafanyika, cha msingi ni kuendelea kusubiria”  

    β€œTutasubiria hadi saa ngapi Celin?” 

    β€œSijui lakini hakuna kitakacho haribika, cha muhimu ni kwamba nimekutoa kwenye mateso yaΒ  yule jini mshenzi” nilisema kwa kujikaza ili angalau kumwaminisha kua hakuna kilichojulikanaΒ  kuhusu yeye. Alitoa tabasamu tu wala hakusema neno lingineΒ 

    Muda ulivyozidi kwenda nilianza kuingiwa na hofu sana, maana alinionesha dalili kuaΒ  angenidhuru. Kuna muda akawa anazungusha sana macho yake kisha akasimama nikamuulizaΒ 

    β€œKuna nini?” Nilimuuliza nikiwa nimesimama pia, alinitazama tu kisha aliketi bila kusemaΒ  chochote kile. Aliufanya moyo wangu udunde sana, hofu ilizidi kuongezeka. Mwili ulikuaΒ  ukisisimka sana.Β 

    Alikua kama mbwa, alikua akinusa harufu sana. Akapiga hatua kama mbili hivi, akawaΒ  amesimama mbele yangu akiwa amenipa mgongo. Harufu ya kifo ilianza kukita pua zangu,Β  damu yangu ilizunguka haraka, mapigo ya moyo yalizidi kuongezeka.Β 

    Silaha pekee niliyonayo ilikua ni ile kamba nyekundu niliyopewa na Haji, sikujua baada yaΒ  kumfunga kingetokea nini lakini nilipaswa kuamini kua ilikua ni silaha muhimu sana, nilionaΒ  wazi kua alikua akihangaika kunusa jambo, nikaukunjua mkono wangu. Kiganjani nilikua na ileΒ  kamba, safari hii nilijiambiaΒ 

    β€œLiwalo na liwe, ni kheri nife kuliko kuuishi Uwoga” 

    Nilivuta pumzi zangu katika hali ya kujiandaa, nilijiapiza kisha nilifanya uamuzi wa kumfuataΒ  kwa kasi kisha nikaushika mkono wake, kitendo cha kumshika alibadilika na kua KiumbeΒ  chenye sura mbaya iliyoungua. Macho yalimtoka kisha alipiga ukunga kama tembo anayemtafuta Mtoto wake. Sikujali sababu hakuna nisichokiona kutoka kwake, nilimfunga ileΒ  kamba halafu nikasogea pembeniΒ 

    Akabadilika kabisa kutoka kwenye sura ya Sabra hadi kua Bibi Kizee mwenye sura mbaya sana.Β  Kitendo cha kumwacha kilimfanya aache kupiga ukunga, aliuinua mkono wake kisha akaiangalieΒ  ile kamba halafu akaniambiaΒ 

    β€œHii vita haitakuja kufika mwisho Celin, kama unafikiria utashinda basi ndiyo kwanza vita hiiΒ  imeanza” alikua akisema huku akinifuata, nilikua ninarudi nyuma nyuma lakini kadili alivyokuaΒ  akinifuata niliona alikua akibadilika viungo vyake na kua sanamu kavu la kufinyangwa.Β 

    Akawa ameganda akiwa anapiga hatua kuja nilipo kisha akaniambiaΒ 

    β€œSiku nikiwa huru Dunia yako itapiga yowe Celin, hakuna Mtu atakusaidia” kisha alipomalizaΒ  aliganda kila kiungo chake na kua sanamu. Nilichoka kwa hofu nikajikuta nikianguka na kukaaΒ  chini. Chozi lilikua likitoka, sanamu lake lilikua hapo mbele yanguΒ 

    Mara alikuja Haji, alinitazama huku chozi likiwa linambubujika. Akaniambia β€œNi muda wa kumkomboa Sabra, twende kwenu”  

    β€œVipi kuhusu hilo sanamu?” 

    β€œUtalivunja kisha utatenganisha udongo wake, udongo mwingine uchome moto kisha mwingineΒ  utupe Baharini, hawezi kamwe kurudi Duniani” alisema Haji, sikutaka kumwambia alichokisemaΒ  Bibi KizeeΒ 

    Basi, kwa uwezo wake wa kimiujiza tulitoweka pale pamoja na lile sanamu. Tukajikuta ndani yaΒ  nyumba yetu. Kila kitu kilibadilika kuanzia hewa na hata mimea ilionekana kua na nuruΒ  kuashiria ukombozi. Tulipofika kwenye korido tuliiacha sanamu kisha tuliingia stoo pamoja,Β  kitendo cha kuingia tu shimo lilijitengeneza kisha lilituulizaΒ 

    β€œMnataka niwafayie nini?” Tulitazamana halafu Haji akasema

    β€œTunamtaka Sabra kutoka kwako” pakawa kimya kisha ikaja harufu kali ya marashi, Sabra akatoka ndani ya lile shimo, alipomwona Kaka yake alimfuata na kumkumbatia kwa nguvu.Β  Ilinifanya nitabasamuΒ 

    β€œCelin, asante kwa msaada na ujasiri ulionao. Nimempata Sabr, tunakutakia Maisha MemaΒ  rafiki” alisema Haji kisha walitoweka sikujua hata walielekea wapi, lile shimo liliniulizaΒ 

    β€œUnataka nifanye nini tena?” Nikalitazama kisha nikasemaΒ 

    β€œFunga na usifunguke Daima Milele, usiwe njia ya kufika chini” baada ya kusema lile shimoΒ  lilitoweka kabisa, nikatoka stoo kisha nikaenda kwenye korido, nikalichukua sanamu kishaΒ  nikaenda nalo njeΒ 

    Nikalivunja vunja, nikatemganisha udongo kisha nikauchoma moto. Mwingine nikaenda kuutupaΒ  Baharini, nikawa nimemaliza kazi nzito ya kuliangamiza lile jini, nikaenda Gerezani kumuelezaΒ  Baba yangu. Alifurahi kisha akaniambiaΒ 

    β€œMama yako atakua amepumzika salama, hata Mimi sina wasiwasi na adhabu yangu sasa. NendaΒ  ukatimize ndoto zako za kua Msanifu Celin” alisema Baba, tokea siku hii nilianza Maisha mapyaΒ  ndani ya nyumba yetu, palijaa tumaini, amani ya kutosha. Sikusikia mauzauza wala Mazonge yaΒ  aina yoyote ile, kilichobakia ni kutimiza ndoto ya kua Msanifu.Β 

    Nataka kuwashuri mnaonunua Nyumba au viwanja kua makini sana sababu nyumba zingine zinaΒ  maagano mabaya ya kichawi, viwanja vingine ni makaburi ya zamani. Nyumba nyingi zipo juu yaΒ  Makaburi.Β 

    MWISHOΒ 

    MNATAKA SIMULIZI IJAYO IWE YA NAMNA GANI? MAPENZI AU UJASUSI? COMMENTS ZIWE NYINGI SASA NIIACHIE MAPEMA MAANA KAKA MKUBWA AMEREJEA NA SIMULIZI ZA KUTOSHA

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

     

    riwaya mpya riwaya za kijasusi riwaya za kusisimua soma riwaya bure

    29 Comments

    1. Watende on May 6, 2025 3:32 pm

      Mapenzi

      Reply
      • Aura on May 6, 2025 8:40 pm

        Kabisa

        Reply
    2. Mama eddy on May 6, 2025 3:42 pm

      Nzuri ila inatisha nmejifunza na nimependa asanteh adimin

      Reply
      • Mama eddy on May 6, 2025 3:43 pm

        Tuletee story nyingn adimin

        Reply
        • Ally Simba on May 6, 2025 5:18 pm

          Ujasui

          Reply
        • Noreen on May 9, 2025 9:51 pm

          Asantee β€οΈπŸ™πŸ™

          Reply
      • Yahaya on May 6, 2025 4:21 pm

        Dah inafunzaa snaa sna hiii Dram aiseh Pongeziii Adminii πŸ™πŸ™.. story ijayo iwe ya KIJASUSI

        Reply
        • Ally Simba on May 6, 2025 5:18 pm

          Ujasusi

          Reply
        • Neema Tesha on May 6, 2025 8:55 pm

          Aisee funzo kubwa nmepata katk hii story,,honger sana Kaka Mkubwaa

          Now
          Tuletee ya Mapenzi

          Reply
      • Aura on May 6, 2025 8:41 pm

        Admin ajengewe sanam manzese anajua sana

        Reply
    3. G shirima on May 6, 2025 3:45 pm

      Ujasusi kama hile ya msala

      Reply
    4. Zajuko on May 6, 2025 4:10 pm

      Iwe ya mapenzi

      Reply
      • Aura on May 6, 2025 8:43 pm

        Kabisa admin azingatie

        Reply
    5. Mary on May 6, 2025 4:50 pm

      nzurii sanaa duh inatisha lakini inamafundishooo mazuri

      Reply
    6. Geofrey on May 6, 2025 5:01 pm

      Iwe ya mapenzi

      Reply
    7. Dotho sanga on May 6, 2025 5:26 pm

      Iwe ya kijasus jinsi gan unaweza kutoka katika hali Fulani ya maisha na kuingia kwenye matumaini mfano kutoka kwenye umaskin kwenda utajiri asante admin

      Reply
    8. Slavius on May 6, 2025 5:54 pm

      Iweya majini

      Reply
    9. Aziza Juma on May 6, 2025 6:22 pm

      Mapenzi

      Reply
    10. Aura on May 6, 2025 8:40 pm

      Iwe ya mapenzi kaka mkubwa

      Reply
    11. Yuster on May 6, 2025 9:41 pm

      Ya mapenzi tuliosalitiwa tupate mbinu mpyaπŸ˜‚πŸ˜‚

      Reply
    12. Bern on May 7, 2025 12:02 am

      Mapenzi

      Reply
    13. KingzJeelay on May 7, 2025 6:06 am

      IT’S TIME FOR UJASUSI KAKA MKUBWAAAπŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½

      Reply
    14. KingzJeelay on May 7, 2025 6:07 am

      IT’S TIME FOR UJASUSI KAKA MKUBWAAAπŸ™ŒπŸ½πŸ™πŸ½

      Reply
    15. KingzJeelay on May 7, 2025 6:08 am

      Emu tuanze na UJASUSI kwnz..halaf. ndo yafate mapenzi pliz πŸ™ŒπŸ½πŸ™πŸ½

      Reply
    16. Samwel mkangi on May 7, 2025 3:46 pm

      Daaah ni nooooumaaaaa

      Reply
    17. Josephat on May 7, 2025 4:24 pm

      Ujasusi

      Reply
    18. Dalire on May 7, 2025 8:48 pm

      Ujasusi

      Reply
    19. Shedrack jr on May 9, 2025 1:27 pm

      Dah noma sana admin we noma sana kwakweli imetoa funzo kubwa. UJASUSI⏭️

      Reply
    20. [email protected] on May 10, 2025 5:38 pm

      Shukran mtunzi, nimejifunza mengiπŸ€πŸ™

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE β€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.