Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)
    Hadithi

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Hamza NgondoBy Hamza NgondoFebruary 19, 2026Updated:February 19, 2026No Comments9 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia 

    “Saida, wewe ulishakufa baada ya kuokolewa Msituni. Roho Yako iliondoka  Usiku ule ambao ulitoroshwa kule kwenye ile nyumba Msituni. Kuishi  kwako Hadi sasa ni kibali Cha Shetani hivyo unapaswa kumtumikia”  ilisema sauti ile, nilizidi kuchanganyikiwa. 

    Yaani Mimi nilikufa? Chozi lilinibubujika. Sasa kama nilikufa iliwezekanaje  nikawa na akili za Kibinadamu, kwanini Nilikutana tena na Salehe, Salehe  ni Nani Hadi anipatie hiyo Pete inayodaiwa kua na nguvu za Kishetani?  

    Hukusoma SEHEMU  ZILIZOPITA?  Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI  ,  SEHEMU YA TATU , SEHEMU YA NNE , SEHEMU YA TANO , SEHEMU YA SITA, SEHEMU YA SABA Kisha Endelea 

    SEHEMU YA NANE

    Maswali haya yote nilijiuliza bila kupata jibu lolote lile, nilianza kuhisi  kichwa kizito sana, Giza liliingia machoni mwangu Kisha nilijikuta  nikianguka na kupoteza Fahamu zangu. 

    *** 

    Nilianza kuhisi mkono wangu wa kulia ukipata joto kidogo, Kisha mapigo  ya Moyo yakaongezeka halafu macho yangu yakawa na hamu ya kufunguka.

    Nilirudisha fahamu, nilijikuta nikiwa ndani ya chumba kile kile tena nikiwa  nimelala sakafuni, hapakua na yeyote yule isipokua Mimi. Nilihema pole  pole huku nikijiuliza kama baada ya kupoteza Fahamu nilipelekwa wapi au  hakuna Mtu aliyekuja kuniangalia? 

    Nilijinyanyua kidogo Kisha nikakaa kitako, mwili ulikua hauna nguvu  kabisa. Kichwa kilikua kizito, nilijiangalia kidoleni nilikua na ile Pete ya  ajabu.  

    Nilijitahidi Hadi nilisimama, nikajikuta nimekishikilia kile kiti wakati wa  kusimama. Pete ilianza kuwaka tena Kisha ile sauti ikasema tena 

    “Saida, unapaswa kukalia kiti Cha enzi” Safari hii sauti haikua Kali kama ile  ya mwanzo. Aliongea kwa sauti ya utaratibu sana, nilimeza funda la mate  huku nikikiangalia kiti.  

    Moyoni nilijua kua endapo nitakikalia basi nitaanza kuifanya kazi ya  Kishetani. 

    “Mimi sikufa, nilitoroka Usiku ule. Unasema nini wewe?” nilijaribu  kujitetea japo nilikua na uhakika kua isingelikua rahisi kwangu. Chozi  halikuniacha, Kila wakati nilibubujisha chozi langu kwa Uchungu sana 

    “Saida” iliita ile sauti kwa Uzito sana, nilihitaji kuelewa Yale ambayo  sikuyaelewa 

    “Ulikufa, Wewe ni mwili usio na roho halali. Nafsi Yako ipo kwenye hicho  kiti, Unataka kujua ilikuaje?” aliuliza huyo Mtu nisiyemwona. 

    Niliitikia kwa kutumia kichwa changu huku nikifuta chozi. 

    “Baada ya mateso kwenye nyumba ya Mwisho, Hali Yako ilikua mbaya  sana. Ndipo alipokuja Mtu Kisha akaanza kuumwa, ulipata nafasi ukatoka  ukijiburuza na kwenda kufungua chumba kingine, hapo ndipo ulipopata  msaada ukakimbia, lakini ulianguka na hukujua kilichoendelea, Sasa Usiku  ule ulipiga kichwa chako kwenye jiwe. Roho Yako iliondoka na kukuacha  mtupu, Mimi nilikurudishia Uhai Saida kwasababu niliamini ulikua na  nafasi ya kuishi tena, lakini baada ya kurudi kua hai haukua Saida yule wa  mwanzo. Uliingia Kuzimu ukiwa macho, ulifanya matukio ya Mauwaji kwa  uwapendao” alisema huyo Mtu, ni kweli nilikua na kovu kwenye paji la Uso  wangu, ilibidi nilishike.  

    “Uliuwa Mama Yako kwa nguvu zako, uliuwa Veronica kwa nguvu zako.  Unauwezo wa kufanya Mauwaji ukiwa mbali na eneo husika, sasa kama  unahitaji kurudi kua hai tena basi Kalia hicho kiti ukutane na nafasi Yako  kwa sharti la kunitumikia” ilisema hiyo sauti, mengi aliyoyasema yalikuwa 

    dhahiri kabisa, Kuna wakati nilikua napotea kifikra na kujihisi nipo  Sehemu nyingine lakini la Kumuuwa Mama yangu ndilo lililo niumiza zaidi,  nilizidi kulia. 

    Kumbe nilimuuwa Mama yangu, pia nilimuuwa Veronica kwa Mikono  yangu?  

    “Ndiyo, sasa utakua na nguvu zaidi ya Mzee Mwinyimkuu. Yeye alikua  mtumishi wangu lakini alienda kinyume ndio maana ameporwa Pete,  kuanzia sasa Pete hiyo ni Mali Yako. Karibu kwenye ufalme wangu Saida,  utakua Mtumishi wangu, utakua tajiri kuliko Mtu yeyote yule Duniani.”  Ilisema hiyo sauti ambayo ilijitambulisha kwangu kua ndiye shetani,  niliiangalia mikono yangu, sikuamini kama nilikatisha Uhai wa Mama  yangu.  

    Nilililaumu lile chozi nililomwaga kwa makosa niliyoyafanya, nilitamani  kukutana na Nafsi yangu, nilipiga hatua kwa hasira Kisha nilikaa juu ya kile  kiti. 

    Kitendo Cha kukalia kile kiti nilihisi Hali ya tofauti sana, kwanza nilikua  kama nimevaa kitu kisichoonekana, halafu nilijikuta nikijitambua zaidi  tofauti na mwanzo, nikavishwa taji la Malkia Kisha mavazi yangu  yalibadilika na kua Meupe yanayo ng’aa sana  

    Nywele zangu zilikua kidogo na kufika mgongoni. Miguuni nilivalia viatu  vya rangi ya dhahabu vilivyo ng’aa sana. Halafu nilikua Nina ngozi ya  kung’aa kuliko kawaida, kingine nilikua na uwezo wa kuiangalia Dunia kwa  namna ya ajabu sana, nilisikia sauti nyingi za Watu wakizungumza 

    Kingine Cha ajabu nilihisi kutimiliwa na vidole vya Miguuni ambavyo  vilikua vimekatwa na Mzee Mwinyimkuu. Nilihisi ufahari wa ajabu sana,  Kisha ile sauti ikasema 

    “Hatimaye Umekua Malkia Saida, nakupa Ulimwengu wote ni Mali Yako”  ilisema ile sauti, pale pale waliingia wale Watu wawili wanaofunika macho  Yao kwa vitambaa vyekundu, wakapiga magoti mbele yangu na kuniambia 

    “Tutakutumikia Malkia” walisema kwa sauti za pamoja kama Watumwa  mbele yangu, sikujua hata nitaweza vipi kuwaamrisha au nitazungumza nao  nini, nilikua nawatazama tu. 

    Kisha waliinuka na kuondoka zao, nilishusha pumzi zangu. Sikua na Hali ya  woga ila nilifikiria ni jinsi gani nitamtumikia huyo shetani, kitu kimoja  nilichokikumbuka ni wale Watu niliowaacha kwenye Basi wakati tunatoka  Rukwa tunaelekea Dar. 

    Walikua wafu lakini niliamini walistahili kuendelea na safari. Nikauliza 

    “Nipo wapi hapa?” Nilijibiwa na ukimya, mara wakaja wale waliofunga  macho Yao na kunijibu kwa pamoja kua nipo Mji wa Kuzimu.  

    “Nahitaji kwenda lilipo lile basi haraka” nilisema, ilikua ni amri yangu ya  kwanza. 

    “Kama Usemavyo Malkia, unaweza kwenda popote utakapo kwa kuamrisha  tu” walinijibu, nikapata jibu kua naweza kwenda kule. Basi nikasema kua  nahitaji kufika lilipo lile basi. 

    Huwezi amini ilikua ni kitendo Cha sekunde Moja nilijikuta nipo nje ya lile  basi kule Msituni, niliamuru wale Watu warudishiwe Uhai wao Kisha wawe  safarini. Mara Moja lile basi lilitoweka pale 

    Nilianza kuhisi Raha sababu niliamuru mambo na yalikua yakitokea, lakini  nilikua na Mkataba na shetani. Mkataba wenyewe ulikua ni kumtumikia.  Niliamua kurudi Dar haraka, mara Moja nilijikuta nipo nje ya nyumba yetu  lakini nikiwa na mavazi yangu Yale ya kawaida 

    Nilichukua funguo chini ya UA dogo ambalo tulikua tukificha funguo,  nikaingia ndani ya Nyumba yetu, Bado palikua Giza sababu ulikua Usiku. 

    Nilipofika chumbani kwa Mama yangu nilianza kuhisi huzuni sana,  niliangalia pale ambapo Mama yangu alikua amejitundika, kidogo chozi  lilitaka kunitoka lakini nililizuia, Kisha nilihitaji kukumbuka namna  nilivyomuuwa Mama yangu kikatili. 

    Nilianza kuiona taswira kama vile nilikua naangalia filamu, ile siku wakati  ambao Mama alikuja chumbani kwangu na kuzungumza maneno yenye  hisia Kali Kisha aliondoka. Nilijiinamia, hapo ndipo nilipofanya tukio la  kutisha sana 

    Akili yangu ilikua kama imevamiwa nikaota ndoto ya ajabu sana, lakini  wakati naipata ile ndoto nilikua natembea huku nikielekea Chumbani kwa  Mama yangu, Mama aliponiona alijua nimekuja kwa ajili ya kuzungumza  naye kutokana na Maneno ya hisia aliyonianbia, lakini haikua hivyo 

    Mama aligundua kua nilikua nimebadilika na kua Mtu wa ajabu sana,  macho yangu yalikua mekundu. Nilikua nimechanganyikiwa, ndipo Mama  alipojaribu kukimbia lakini nilimzuia 

    Nilimbana Mama yangu kwa kutumia mikono yangu eneo la shingo Hadi  nilipohakikisha amekufa Kisha nilimfunga kamba Shingoni na kumtundika  juu kama Mtu aliyejinyonga.

    Baada ya pale nilirudi chumbani kwangu na kukaa pale pale, ndipo ndoto  yangu ya kutisha ilipoisha na kuikumbuka Kauli ya Mama kua nikihisi njaa  niende sebleni kupata chakula, ndipo nilipoelekea sebleni nikiwa  ninajitambua. 

    Niliuwona Mlango wa Mama ukiwa Wazi, nilijua haikua kawaida yake  Kisha nilinyanyuka kutoka kwenye kiti ili niangalie ni kwanini mlango wa  chumba Cha Mama ulikua Wazi, ndipo nilipomkuta Mama akiwa amekufa  huku akili yangu ikiniambia kua Mama yangu alijinyonga mwenyewe baada  ya Kuona Mimi sizungumzi chochote kile.  

    Pamoja na yote ila Kuna kitu kimoja sikukikumbuka, Mama aliacha  Ujumbe kua anafanya uamuzi wa kuondoa Maisha yake baada ya  kushindwa kuendelea kuniona nikiteseka, sasa nilijiuliza kama ni kweli  nilimuuwa Mama yangu ni kwanini aliandika ule ujumbe, kwanini  sikumbuki kama Niliwahi kuuandika ule ujumbe? 

    Nilijikuta nikikaa chini huku roho ikiniuma sana, jina la Salehe niliendelea  kulilaani kwasababu alikua chanzo Cha yote yaliyotokea. Nilikaa hapo Hadi  Usingizi uliponichukua 

    Asubuhi ilinikuta nikiwa nimelala hapo, nilishtuka baada ya kupigwa na  Mwanga wa jua. Nilijinyoosha kwa Uchovu halafu nilinyanyuka, nilielekea  bafuni nikaoga Kisha nikatulia sebleni 

    Nilikua nawasikia majirani wakiongea majumbani mwao sababu nilikua na  huo uwezo wa kusikia sauti za mbali hata bila kufika eneo la tukio,  nilipotezea. Kisha nilitoka na kuelekea nje, nikasimama kwenye varanda 

    Moyo Wangu ulikua na Siri niliyoificha, Mama Amida aliponiona alikuja  kunisalimia. Alikua akinijali na kunipenda sana, siyo tu kwasababu Mama  yangu amefariki Bali hata alipokua hai 

    “Eeeh Saida, ulienda wapi mwenzetu bila hata kuaga?” alisema Mama  Amida, nilitabasamu tu Kisha nilisogea karibu naye nikamsalimia, alipoitia  ndipo nikamwambia kua nilikua kwa rafiki yangu. 

    “Basi siku nyingine uwe unaaga Mwanangu sawa? Maana ulinitia wasiwasi  sana” alisema kwa sauti yake ya Upole akiwa ameshikilia ufagio mkononi  mwake, alikua ametoka kwa ajili ya usafi wa nje 

    “Sawa Mama” nilisema Kisha aliniambia anataka kufanya usafi hivyo  tutazungumza wakati mwingine. Aliondoka pale akaelekea nyumbani  kwake na kuanza kufanya usafi kwa nje

    Nilimtazama kidogo akiwa anafanya usafi, Kisha nilielekea ndani kwa ajili  ya kuandaa chai. Sikuona ule utajiri aliousema yule Shetani kua nitakua  nao, nilifikiria kuelekea kazini baada ya chai 

    Basi nilianza kuandaa chai ili ninywe maana njaa ilikua ikinikwangua sana,  nikiwa jikoni nilisikia Mtu akibisha hodi 

    Kwanza nilijiuliza ni Nani anayeweza kuja kwetu, kama Mama Amida tayari  tulishazungumza. Nilimeza funda zito la mate Kisha nilitembea taratibu  kuelekea Mlangoni bila hata kutoa sauti yangu. 

    Nilisikiliza kusikia sauti lakini palikua kimya sana, sikutoa sauti ya  kumkaribisha. Nilisubiria Hadi alipogonga tena ndipo nilipomuuliza yeye  ni Nani? 

    Hakujibu, niliamua kufungua mlango kwa nguvu. Nilikutana na yule  Mwanaume mmoja anayefunga macho yake kwa kutumia kitambaa  chekundu, kwa namna alivyo ikitokea Watu wamemwona basi wangenitilia  shaka, nikamvuta ndani Kisha nikafunga mlango. 

    Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya TISA

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

    SOMA KISASI CHANGU HAPA  

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx  Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

    Msala Kijiweni riwaya mpya Riwaya ya Goryanah Riwaya Ya Kisasi Changu riwaya za kijasusi riwaya za kusoma mtandaoni
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua
    Hadithi February 23, 2026

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Ilipoishia  Kwanza nilijiuliza ni Nani anayeweza kuja kwetu, kama Mama Amida tayari  tulishazungumza. Nilimeza funda…

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (07)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.