Ilipoishia
“Saida Amka ule chakula, Amka Mwanangu. Amkaaa usilaleee” Mara ghafla nikajikuta nikizinduka kutoka kwenye Yale mawazo. Nilijikuta nipo pale pale kitandani nikiwa Nimekaa, nilikumbuka ni kweli Mama yangu aliniambia nikihisi njaa niende Mezani nikale
Basi nilihema, ndoto za Kutisha zilikua Sehemu ya Maisha yangu. Wakati mwingine niliota ndoto nikiwa nimekaa tena nikiwa macho kabisa, hayo Ndiyo Yalikua Maisha yangu baada ya kuponea chupuchupu kule Rukwa.
Basi, nilinyanyuka taratibu nikaelekea sebuleni, nilikua nikitembea taratibu sana. Nilipofika sebuleni nilikikuta chakula kikiwa hapo, nilifunua Hotipoti. Nilijiandalia chakula Kisha Niliketi, nilianza zoezi la kufungua kichwa changu chenye vidonda vya Ukimya . Hukusoma? Isome Kwa KUGUSA HAPA Kisha Endelea
SEHEMU YA PILI
Nilikua nahisi maumivu makali sana Hadi pale nilipofanikiwa, ngozi ya midomo yangu ilikua imegandana sababu ya Ukimya wangu, hata kula yangu nilikua na uwezo wa kukaa siku tatu bila kula chochote kile Hadi pale nitakapojisikia. Hii Hali ni Bora uendelee kuisoma kutoka kwangu lakini isikukute.
Nilianza kula taratibu, huku macho yangu yakiutazama mlango wa chumba Cha Mama yangu. Mlango ulikua Wazi, siyo kawaida ya Mama yangu kabisa yaani aingie chumbani halafu asiufunge mlango wake? Hapana.
Niliendelea kula huku nikiendelea kuutazama sana ule mlango bila hata kupepesa macho yangu.
Moyo Wangu ulianza kwenda Mbio, sikuelewa ni kwanini. Basi niliacha kula Kisha nilinyanyuka na kuanza kutembea kuelekea Mlangoni kwa Mama yangu.
Taratibu nilikua naendelea kukanyaga sakafu iliyojaa baridi huku nafsi yangu ikiniambia nitarajie kuona kitu kisicho Cha Kawaida. Nilimeza mate Kisha nilisimama mlangoni, halafu niliufungua zaidi ule mlango. Sauti ya Bawaba ilisikika kuashiria kua mlango ulikua ukipitia mateso ya kufunguliwa kwa nguvu.
Nilikosa pumzi kwa nilichokiona, nilihema kwa kukatishia. Macho yalinitoka nikimtazama Mama yangu aliyekua akining’inia kwenye kenchi, mtandio ulikua umeibana shingo yake, Mama yangu alikua amejinyonga
Chozi lilianza kunibubujika, nikajikuta nikipiga goti huku nikifungua mdomo Wangu kwa mara ya kwanza na kumwita
“Mama….Mamaaa…Mamaa” niliita kwa sauti ya chini huku Kila nilivyoendelea kuita ndivyo sauti yangu ilivyotoka vizuri kabisa.
Niliangua kilio kilichowafanya majirani waingie ndani, taratibu za kuutoa mwili wa Mama yangu zilifanyika.
Nililia sana, ilikua ndiyo mara ya kwanza Watu wanaisikia sauti yangu baada ya Miaka mitano kupita, Kila aliyeisikia sauti yangu alishangaa sana kuona nilikua ninaweza kuongea
Mama aliacha Ujumbe juu ya meza uliosomwa na Mjumbe, alisema
“MWANANGU SAIDA, USIHUZUNIKE WALA USILIE KWASABABU NISINGELIWEZA KUENDELEA KUISHI NIKIKUONA WEWE KATIKA HALI HIYO. UMEGUSA MAISHA YANGU, UMEGUSA HISIA YANGU. HATA KAMA SITAKUA KARIBU NA WEWE LAKINI NAFSI YANGU HAITAKUACHA” huo ndio ulikua Ujumbe wa Mama yangu
Kumbe Mama alijinyonga kwasababu yangu, nilizidi kulia na kujilaumu ni kwanini sikufungua kinywa changu na kuzungumza pale alipokuja chumbani kuniita kwa ajili ya chakula, nilijilaumu kwasababu hakusikia tena sauti yangu.
Alianza Baba kufa kwa ajili yangu, Kaka Hamidu, Mjomba Kambona Kisha Mama yangu. Hii iliniumiza sana, sababu ya haya yote ni Salehe na Mzee Mwinyimkuu.
Taratibu za Mazishi ya Mama yangu zilipangwa, ndugu walikuja kutoka Sehemu tofauti tofauti. Kila aliyekuja alishangaa kuniona nilikua nikitoa sauti ya kilio, walishanikatia tamaa na kuamini nilikua Bubu.
Siku iliyofuata, Mama yangu kipenzi alizikwa. Baada ya mazishi, ndugu walijadili kuhusu Mimi. Kutokana na Hali yangu walinitaka nikaishi Kibaha kwa Shangazi yangu lakini nilikataa. Walinisihi sana kua isingelikua busara kuishi mwenyewe, niliwaambia kua ningependa niishi peke yangu
Ushawishi wao haukufua dafu kwangu kwani nilikua tayari nimedhamiria, sikutaka kusikia habari za kwenda Kibaha au kunipa Mtu wa kuishi naye,
nilisimamia msimamo wangu Hadi dakika za mwisho Kila mmoja alikubaliana na Mimi japo kwa shingo Upande.
Msiba ulipoisha walianza kuondoka mmoja mmoja Hadi wote walipomalizika na kuniacha Mimi na nyumba yangu. Nyumba ilikua kimya sana, niliachiwa pesa na ndugu zangu sababu nilikua Sina kazi.
Nilipata Matibabu ya Mdomo Wangu, nilipona kabisa. Nilianza kuishi kwa kujipenda, nikanawiri vizuri sana. Nilivaa vizuri, niliacha Tabia ya kukaa mwenyewe, mara nyingi nilikua nazungumza na Watu.
Kila aliyeniona mwanzo alishangaa sana kuniona nimekua Saida yule waliyemjua, Saida aliyewavutia wengi kwa kujisitiri na kujifunza. Nilikubaliana na Hali halisi kua Maisha yaliyopita yalikua mabaya lakini yalishapita
Kitu kimoja ambacho kilibakia kwangu ni chuki dhidi ya Wanaume, sikuhitaji mahusiano na Wanaume, Alichonifanya Salehe hakikutoka kabisa akilini Mwangu.
Nilianza Maisha mapya yaliyojaa amani ndani yangu, hata zile ndoto za Kutisha zilipotea. Nilikula na kulala vizuri bila wasiwasi, Miezi ilipita, kifo Cha Mama yangu kilibadili kabisa Maisha yangu
Bahati nzuri nilipata kazi kwenye sheli Moja pale pale Magomeni. Nilijipatia pesa ya kukidhi mahitaji yangu, Sikuhangaika kuhusu pesa ya kula, wala matumizi yangu Binafsi.
**
Siku Moja ilikua mishale kama ya Saa Moja hivi Usiku, nilikua kazini nahudumia Wateja. Mara ilikuja gari Moja nyeusi, siikumbuki ilikua gari gani. Ilipofika, nilijua ni mteja wa mafuta
Lakini Cha ajabu, kilishushwa kioo tu Kisha ukatoka mkono. Sikumwona aliyekua ndani sababu alizima taa za ndani halafu hata kioo chenyewe hakukishusha chote, kingine nilikua na hekaheka na haraka.
Nilipewa karatasi Moja. Kisha gari iliondoka, nilistaajabu sana lakini kabla hata sijaisoma ile karatasi walikuja Wateja wengine hivyo nikaanza kuwahudumia. Nilipomalizana na wale Wateja, niliitoa ile karatasi Mfukoni
Niliketi kwenye kiti ili niangalie kilikua kimeandikwa nini, nilipoiangalia nilikutana na maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa yakisema
“SAIDA BADO UNA DENI NA SISI”
“MH!” Niliguna, nikalikumbuka ile gari, ilikua gari ya kifahari. Nikajiuliza Nina deni kwao kwa kipi, sikuwahi kumkopa Mtu pesa pia sikua na ukaribu na Watu wenye pesa.
Nikanyanyuka na kumfuata Mdada mmoja ambaye naye alikua akifanya kazi pale kwenye kituo Cha kuuza mafuta, nikampatia ile karatasi. Alipoisoma akaniangalia Kisha akaniuliza
“Eeh shoga yangu, deni Hilo ilikuaje?”
“Hata Mimi nashangaa kuambiwa nadaiwa halafu sikumbuki ni deni gani” “Mh! Kua makini tu Saida, wasije kua watoa Figo hao. Mjini hapa Ohooo‼”
“Weee Mimi mwenyewe Mtoto wa Mjini” nilisema Kisha nilirudi kwenye pampu yangu nikawa nahudumia Wateja.
Japo nilimwonesha yule Mdada kua Sina hofu ila moyoni mwangu nilikua Nina wasiwasi sana, Kila nilipofikiria sikupata jibu la swali langu Hadi nilipoondoka na kurudi nyumbani, nilikumbuka Kauli ya yule Dada kua huwenda ni Watoto Figo.
Basi nikahakikisha nafunga milango vizuri, nikaoga Kisha nikala chips nilizonunua Barabarani. Nilijikuta nimekua mwoga ghafla tu. Nilipomaliza kula nilienda Moja kwa moja chumbani kulala, nilikua nimehama chumbani kwangu nikawa nalala chumbani kwa Marehemu Mama yangu.
Nilijifunika shuka gubi-gubi, nilijilazimisha sana Usingizi. Hali ya hofu ilinitawala sana, kilichonipa wasiwasi zaidi ni kutajwa kwa jina langu kwenye ile karatasi, niliulazimisha Usingizi Hadi uliponiteka.
Nilishtuka asubuhi mapema, nikajiandaa Kisha nikaelekea kazini. Nikamsimulia yule Mdada aliyekua akiitwa Veronica
“Basi nenda polisi ukatoe taarifa Saida” alinishauri, lakini nilifikiria nikaona anachokisema kipo sahihi.
“Nitaenda mchana Wacha kwanza nifanye kazi za Watu hizi.” Nilimwambia Veronica Kisha nikaendelea kufanya kazi huku nikisubiria Mchana niende kituo Cha polisi kutoa taarifa.
Ilipofika saa Nne asubuhi, alikuja Kichaa mmoja wakati huo Wateja walikua wamekata. Alinitazama sana yule Kichaa Hadi niliogopa, nikampatia Shilingi mia Tano ili aondoke lakini hakuondoka alikua akinitazama sana
Nikamwita Veronica, alipokuja akajaribu kumfukuza yule Kichaa ambaye alikua na nywele ndefu zilizotawaliwa na Uchafu, alikua amebeba Begi
chakavu, alivalia suruali chakavu. Alikua akitutazama kwa hasira halafu akasema
“Wewe utakufa kwasababu unaingilia Maisha ya Watu” alimnyooshea kidole Veronica.
“Wewe fala nini, atakufa Mama Yako. Wewe jifanye chizi Mimi ni chizi zaidi Yako” akasema Veronica kwa hasira, sote tulimchukulia kama chizi wa kawaida tu. Halafu akaniangalia Mimi akaniambia
“Watakuja kukuchukua kwasababu hawajamalizana na wewe Saida” nilishtuka sana, sikuwahi kumwona kabla yule Kichaa lakini alilitaja jina langu kuonesha kua alichokisema alikua anakimaanisha. Kisha alimtazama Veronica akamwambia
“Kimbelembele kimekuponza” Kisha aliondoka zake, namna alivyokua akizungumza alionekana siyo Kichaa kama alivyoonekana. Veronica alinitazama huku nikiuwona uso wa Uwoga ukimtawala.
“Saida, twende Polisi. Wanaanzaga hivi hivi hawa halafu waje kufanya matukio” Hata Mimi nilikua naogopa sana, tukamwita Meneja tukamsimulia. Akaturuhusu twende Polisi kutoa taarifa ya vitisho tulivyopewa na Watu tusio wafahamu.
Tulibadilisha zile Sare za kazi, tukavalia nguo za kawaida Kisha tukaondoka ili twende Polisi. Kutoka kazini kuelekea Kituo Cha Polisi siyo mbali sana, tuliamua tutembee kwa Miguu, Njiani tulikua Tukizungumza kwa mkazo kua Watu wale huwenda ni Majambazi walikua wakisoma ramani au ni Watoa Figo
Tulipokaribia kituo Cha Polisi, tulimwona yule Kichaa akitoka kituoni. Alikua akishusha ngazi, Mimi nilikua wa kwanza kumwona Kisha nikamwambia Veronica
Tulisimama tukimtazama namna alivyokua alishusha ngazi, Kisha tulitazamana kwa Mshangao mkubwa. Mtu tuliyekua tunaenda kumshitaki alikua akitoka kituoni tena akiwa amevalia nguo zile zile za kuchakaa. Mioyo yetu ilianza kwenda Mbio
“Sasa tufanyaje Veronica?” nilimwuliza huku kijasho Cha hofu kikianza kunitoka. Nilikua ninahema sana.
“Saida, si unaona? Yule siyo Kichaa na ukitaka kuamini jiulize kwanini alienda kituo Cha Polisi?” aliniuliza Veronica akiwa amenishika bega, mara alisimama yule Kichaa Kisha aligeuza shingo kutazama tulipokua
tumesimama. Nikamvuta Veronica tukajificha nyuma ya gari Moja lililokua limepaki nje ya kituo Cha Polisi
Tukawa tunamchungulia, alitazama sana pale tulipokua tumesimama, Kisha aliondoka zake akipitia upande mwingine ambao ulikua na geti la kutokea, sisi tulikua upande wa geti la kuingilia pale kituo Cha Polisi.
“Mama yangu!” Nilisema huku nikishika Sehemu ulipo moyo Wangu, nilikua nimeishiwa nguvu sababu ya Mshituko. Veronica akanyanyua kichwa kumtazama akamwona akiondoka
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU Sasa ( Comments ziwe nyingi)
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx


