Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Whittaker Aibuka Mshindi Baada ya Presha Kali ya Wallace

    Matola Aondoka Kambi Ya Simba Afrika Kusini

    Simba Queens Mbabe Kwa Yanga Princess Ngao Ya Jamii

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Naamini Kuwa Medeama Ndio Msaada Mkubwa Kwa Yanga
    Africa | CAF

    Naamini Kuwa Medeama Ndio Msaada Mkubwa Kwa Yanga

    MhaririBy MhaririFebruary 23, 20243 Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Wachezaji wa Medeama Sc
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Wengi mmejikuta mnaangalia hatma ya Yanga kwa kuangalia tu mechi mbili za Yanga dhidi ya CR Belouizdad na ile ya mwisho dhidi ya Al Ahly. Hakuna ambaye amewaza ni jinsi gani Medeama anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Yanga.

    Ukweli ni kuwa Yanga ni ngumu sana kuvuka kwa kucheza mechi zake pekee maana kama ambavyo tumejadili sana inahitaji amfunge CRB kwa tofauti ya goli 4 jambo ambalo ni gumu sana ingawa kwenye mpira lolote linaweza kutokea. Ikipata ushindi tofauti na huo Yanga inahitaji kupata angalau sare dhidi ya Al Ahly jambo ambalo nalo lina ugumu fulani.

    Njia iliyo rahisi zaidi kwa Yanga ni kwa Yanga kumfunga CRB kwa ushindi wowote ule huku wakiombea Medeama ipate ushindi leo dhidi ya Al Ahly. Medeama ana nafasi kubwa ya kushinda leo kwa sababu Al Ahly bado hawako vizuri na wataendelea kuwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu kutokana na majeraha. Vilevile changamoto za hitilafu za ndege yao na uchovu wa safari unaweza ukawaathiri kwa kiasi fulani Al Ahly.

    Matokeo ya mechi hizo mbili yakienda kama nilivyosema, kitakachobaki ni katika mechi za mwisho kwa Yanga kuiombea Medeama itoe sare dhidi ya CRB huku yenyewe haihitaji kupata sare wala ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Al Ahly.

    Kwenye mechi walizokutana wenyewe kwa wenyewe ni wazi kabisa kuwa Yanga ina faida mbele ya Medeama kwa hiyo ikitokea wamelingana alama basi Yanga anafuzu.Siioni Al Ahly ikiendelea kuwa na makali hasa nikitazama ile mechi yao dhidi ya CRB, walicheza mpira wa kawaida sana.

    Yanga ana uwezo wa kukomaa kule Misri na akato sare, kikubwa kesho apate ushindi mzuri kama unavyosema, sare Yanga ana uwezo wa kuipata kule Cairo kama akienda kwa nidhamu uwepo wa viungo kama Aucho, Mudathir, Pacome, Maxi ni viungo ila wanajua haswa kukaba pia.

    SOMA ZAIDI: Asec vs Simba Sio Mechi Ya Kawaida , Ni Vita Ngumu Sana

    Al Ahly Medeama sc yanga sc
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Stori Mpya October 5, 2026

    Whittaker Aibuka Mshindi Baada ya Presha Kali ya Wallace

    Bondia wa Uingereza katika uzito wa light-heavyweight, Ben Whittaker, amenusurika mashambulizi makali ya dakika za…

    Matola Aondoka Kambi Ya Simba Afrika Kusini

    Simba Queens Mbabe Kwa Yanga Princess Ngao Ya Jamii

    Ni Taifa Stars Dhidi Ya Madagascar Leo

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.