Ilipoishia “Madam tumeshafikaโ ilikua ni sauti iliyomzindua Elizabeth ฤทutoka katika fikra nzito ya namna alivyokutana na Mke wa Rais hadi kupanga njama za wizi ndani ya Ikulu. Mbele yake aliona Hoteli maalum ambayo Rais Mbelwa alihitaji Elizabeth akae hapo kisiri kwa siku mbili kabla ya kuondoka kuelekea mafichoni Uskochi kukwepa jicho la Usalama wa Taifa ambao walipanga kummaliza.ย
Endeleaย
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Aliingizwa hadi ndani ya chumba ambacho alipaswa kuishi, bado dereva alimsimamia โUnahitaji nini zaidi ya kuniacha mwenyewe hapaโ alizungumza Elizabeth akiwa amemkodolea macho yule dereva, hakupewa jibu lolote, Dereva aliondoka Hotelini.
Haraka Elizabeth alimpigia simu Muhonzi aende hapo Hotelini ili wazungumze kuhusu Brifkesi
ambalo liliondolewa Ikulu na kupelekwa PIZA HUNT. Dakika chini ya arobaini Muhonzi aliwasili hapo akiwa na Pikipiki yake iliyopanda hewani, akaiegesha maegesho kisha akaishika korido itakayompeleka hadi chumbani kwa Elizabeth, akausukuma mlango na kujikuta akiwa ndani ya chumba hicho
โRais amepanga kuniondoa Nchini ndani ya siku nbili zijazo, kama tutashindwa kupata nyaraka itakula kwetuโ alisema Elizabeth Mlacha, haraka Muhonzi alisogea na kuketi kwenye kiti huku akiiachia mikono yake kama Mtu anayeogelea โBrifkesi iko PIZA HUNT, Hapana shaka zipo siri nyingi za Rais pale, chini ya jengo ndimo lilimo pelekwaโ alisema Muhonzi huku akiivua mawani yake, akasimama na kumsogelea
Elizabeth
โNi lazima tuzinase kabla ya huo wakati kufika, nafikiria jambo lakini sina hakikaโ alisema Muhonzi huku akiuma midomo yake aliyoisogeza upande mmoja kama Mtu aliyepooza
โYes!! Ni lazima kutakua na njia ya kufika kutokea ndani ya jengo la Piza Hunt bila kufika eneo la maegesho, lakini nafikiria kuhusu ulinzi wa pale. Hatuwezi kuikosa hiyo pesa kirahisiโ alisema Muhonzi
โKazi hiyo inabidi uifanye Muhonzi tena kwa haraka sana, ukishajua ulinzi uko vipi itakua rahisi kuingia pale, kama samaki ameliwa umebakia mkia tu. Vipi tushindwe mwisho?โ alisema Elizabeth huku akiachia tabasamu nono la matumaini.
Muhonzi akalifungua begi lake jeusi alilolipachika mgongoni, akaitoa Kompyuta Mpakato aina ya TOSHIBA kisha akaiwasha, haraka akatafuta picha za jengo la Piza Hunt namna lilivyo kwa nje na ndani
โUnafikira kma Rais ameamua kulifanya eneo lile kua maficho yake itakua rahisi kupata ramani iliyo sawa?โ akahoji Elizabeth akiwa anatazama namna Muhonzi alivyokua akihangaika
โOooh yes, napaswa kuingia hakuna njia nyingineโ alisema Muhonzi akiwa anahema kama mwenye Baridi yabisi, akapikicha mikono yake akiwa amekodoa macho, kabla hajasema neno lingine ikasikika sauti ya kugongwa mlango wa Chumba cha Elizabeth, wote walishtuka
Haraka Elizabeth akagundua kua Mgongaji alikua Mtu makini, namna alivyogonga aligonga kiustadi sana, kitendo bila kuchelewa Muhonzi akaikusanya Kompyuta yake na kuirejesha begini
Kisha akajificha nyuma ya Kabati, Elizabeth akaweka mazingira yake sawa kisha akaelekea kufungua Mlango uliogongwa mfululizo, alikutana na sura ngumu iliyokua imemkodolea macho, jitu jeusi lililopanda hewani lilikua limesimama
โMimi ni Mlinzi wako kutoka Ikuluโ alisema Mwanaume huyo asiyeonesha tabasamu, Rais alimpenda Elizabeth bila kujua kua ni Mtu hatari.
โOoh sawa!!โ alisema Elizabeth kisha aliufunga mlango, akaganda kwa sekunde tatu kusikiliza hatua za Mwanaume huyo lakini hakuzisikia, ndipo alipogundua kua alikua amesimama Mlangoni, akaelekea nyuma ya Kabati mahali alipo Muhonzi
โUnatakiwa kwenda, Mlinzi amefika kunilinda. Haitakua rahisi Mimi kutoka hapa kwasasaโ alisema Elizabeth akiwa anasogea dirishani, akalifungua. Uzuri dirisha hilo halikua na nondo isipokua kioo pekee, ikawa rahisi kwa Muhonzi kuchumpa hadi chini, akadandia Pikipiki yake kisha akaondoka eneo la Hoteli hiyo huku akiwa na kazi ya kuelekea PIZA HUNT kuangalia Ulinzi ili wajuwe ni namna gani wataiba nyaraka zitakazo wapa pesa nyingi, nyaraka hizo zilikua na siri nyingi za Rais, mikataba feki, wizi na mipango Mingi ya hatari.
Msitu wa Magoroto, Saa Nne baadaye.
Helkopta za Kijeshi zaidi ya saba zilikua zinauzunguka Msitu hatari wa Magoroto kumsaka Rubani Benjamin, hapakua na dalili yoyote kua Benjamin alikua hai ndani ya Msitu huo ambao Watu walikua wakipotea kimaajabu.
Haikutosha, Rais akaagiza kikosi kizame ndani ya Msitu huo hatari, akazuia vyombo vya Habari kueneza taarifa yoyote ile ya operesheni hiyo ya Kijeshi, akafunga mtandao wa Intaneti baada ya kuanza kusambaa kwa taarifa kua waliokisambaratisha Kijiji cha Mwambisi walikua ni Wanajeshi wa Tanzania.
Kikosi maalum chenye askari jeshi Mia moja na hamsini kilishushwa kwa kamba maalum kutoka juu ya Helkopta ili kumasa Benjamin, Msitu mzima ulikua unawaka taa tupu, hapakua na giza sababu Chopa zilizo juu zilikua zikimulika chini ya Msitu huo.
Askari walipofika kwenye lile Bwawa ambalo Benjamin alitumbukia alipojirusha kutoka juu ya Helkopta, walikuta Hatua zenye ufanano na Binadamu, lakini zilikua kubwa mno, haikua rahisi kufikiria zingeweza kua za Binadamu wa kawaida. Askari hao walianza kuzifuata hatua hizo taratibu kwa umakini wa hali ya juu sana.
Ndani ya vichwa vyao walijua msitu wa Magoroto ni Msitu hatari wa maajabu na hapajawahi kutokea Mtu anayeweza kuzama huko akarejea kusimulia alichokutana nacho, kama siyo amri ya Rais basi askari hao wasingeliweza kuingia ndani ya Msitu huo.
Walizifwata nyayo kwa tahadhari, upepo wa wastani ulikua ukipeperusha majani makavu na baadhi ya matawi dhaifu, kila mmoja alizisikia pumzi zake zilivyokua zinaenda mrama, wakafika mahali kiongozi wao wa ndani ya Msitu akawapa ishara wasimame, kisha akapeleka tochi chini kutazama jambo
Walikuta Buti moja la Kijeshi lililooza, haraka akawataka kukaa tayari, askari walioingia ndani ya Msitu wa Magoroto walikua na kamera maalum ambazo ziliungamishwa kambi ya Kijeshi ili kufwatilia operesheni hiyo, wote waliliona Buti hilo, waliposogea mbele kidogo waliona kofia ya kijeshi ya chuma yenye kutu ikiwa chini.
โTawanyikaโ alisema kiongozi wa wale wanajeshi, akawapa na ishara ya Kijeshi huku akiyakaza macho yake kutazama mbele, yakatengenezwa makundi matatu yenye idadi sawa ya Askari.
Kila kundi likawa na kiongozi wao, msako ukaendelea ndani ya msitu wa Magoroto, hatua kadhaa baada ya Askari kutawanyika kundi moja likapewa ishara ya kusimama, ishara hiyo ilitoka kwenye redio call kutoka Makao makuu ya Jeshi, kamera walizozivaa ziliwasaidia walio Makao Makuu kuona dalili ya uwepo wa mtego, kisha haraka Mkuu wa Majeshi kupitia redio call akawaambia warudi nyuma.
Kabla hata hawajapiga hatua za kurudi nyuma, eneo walilokua wamesimama lilibomokea kwa ndani, ulikua mtego wa shimo, askari wote wakafukiwa ndani ya mtego huo, hapakusikika sauti yoyote hata ya kuomba Msaada.
Haraka Mkuu wa Majeshi akampa taarifa Mkuu wa Msafara wa Askari kua askari 50 walikua
Wameshatoweka Umakini ukaongezeka, Msitu wa Magoroto wilayani Muheza ulikua ni zaidi ya kaburi la
giza, mitego ya kutosha ilikua imetegwa ndani ya Msitu huo wenye miti mirefu na mito kadhaa iliyo katiza ndani ya Msitu huo, Helkopta zilijitahidi kumulika taa lakini hapakuonekana dalili ya uhai kwa wale askari Hamsini waliotumbukia shimoni.
Ghafla popo weusi wakubwa walianza kuwashambulia askari, walitokea ghafla na kuanza vita na Askari, risasi zikarindima Msituni, popo walikua wakiwararua askari usoni na kutoboa macho yao huku wengine wakikimbia, Popo walikuwa wengi sana.
Wengine walikua wametanda angani na kuziba eneo lote walilokua wale askari, kundi linguine kikawa linazifuata zile Helkopta ambazo haraka ziligeuza na kuukimbia Msitu wa Magoroto ambao ulikua giza tupu baada ya Helkopta kukimbia.
Hapakusikika tena risasi, zaidi ya Sauti ya POPO hao hapakua na sauti nyingine, Mkuu wa Majeshi alihema na kuagiza Maji ya Baridi kisha akagida bila kupumzika, aliposhusha chupa chini simu yake ilianza kuita.
Alikua ni Rais Lucas Mbelwa ndiye aliyekua akimpigia, akasogea pembeni ili asije akadhalilishwa mbele ya Wanajeshi aliowazidi cheo โNdiyo Mkuuโ aliitika huku akijua fika Rais atamfokea. Cha ajabu Rais alisema kwa upole โNimeona kilichotokea, hakua Mwanadamu anayeweza kutoka ndani ya ule Msitu, nina Uhakika yule rubani amefia hukoโ ilikua ni sauti laini lakini iliyo na wasiwasi na kupooza.
โUle Msitu ni hatari sana Mkuu, kama yale yanafanywa na Binadamu basi huyo siyo Binadamu wa kawaida, ni Mzimuโ alikazia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, alikua huru sababu Rais hakua katika hasira
โIGP anakagua Miili kuona kama kuna mwili wa Elizabeth, ndiyo tumaini pekee lililobakiaโ alisema Rais kisha alikata simu, Mkuu wa Majeshi akiwa amejishika kiuno chake akitafakari kilichotokea Msitu wa Magoroto, aliona wazi kua kilikua kisanga kizito sana.
**
โTupumzike hapaโ alisema Elizabeth Mlacha, saa Nane usiku iliwakuta Elizabeth na Mzee Kimaro wakiwa wanainyatia Picha ya ndege, walibakiza kilomita sita pekee kufika, haikua rahisi kwasababu Askari walizingira maeneo yote yaliyozunguka Kijiji cha Mwambisi.
Mzee Kimaro aliweka Bunduki yake kwa kuiegemeza kwenye Mti, akapenga Makamasi yake kisha akashushia na Muhayo mzito, huku akijitupa chini kama Mzigo. Elizabeth alikua akizitazama nyota angani jinsi zilivyokua zikiwaka
โPole kwa ajili ya familia yakoโ alisema Elizabeth kwa sauti iliyojaa kujali.
โHata haikua familia yangu, nilienda kujificha kwenye Kijiji kile kwasababu nilikua na kesi ya kuuwa Wamangโatiโ alisema Mzee Kimaro, Elizabeth akakaa kitako huku akili yake ikimwambia kuwa Mzee huyo alikua Mtata sana
โ,Uliuwa Wamangโati?โ
โNdiyo, miaka miwili iliyopita. Nimeishi Mwambisi kwa Miaka miwili ndipo nilipokutana na yule Mwanamke nikaishi kwakeโ alisema Mzee Kimaro.
โKwanini wanaitafuta hiyo Flashi?โ aliuliza Mzee Kimaro, alikua Mdadisi haswa.
โKuna siri nyeti za Rais, natakiwa kuzifikisha Mahali, nikifanikiwa kufika basi nitapata ujira mkubwa sana. Sitokusahau Mzee Kimaro, umeniokoa sana kutoka mikononi mwa wale Shwainiโ alisema Elizabeth, akajilaza tena na kutazama nyota.
โLakini yupo aliyenifanya nikawa hai hadi sasa, lakini ni ujinga wake akajikamatisha kwa Askari, Benjamin Ahsante, nina Uhakika unateseka kwasasaโ alisema Elizabeth akiwa anabadilisha Mkao wake.
Upande wa pili, tayari jua lilikua limeshatua, asubuhi nyingine iliyojaa Hekaheka. Barabara ya Morogoro ilikua imeshafungwa, hakuna Mtu aliyekua akiitumia Barabara hiyo. Muhonzi alijiandaa kwa ajili ya kwenda Picha ya ndege kumsaidia Elizabeth, dakika chache mbele alikua tayari kwa ajili ya kutoka.
Alijiangalia kwenye kioo, moyoni alijua hiyo haikua kazi rahisi kuifanikisha, aliiweka sawa Bastola yake, akachukua kofia ngumu ya kuendeshea Pikipiki, ukutani palikua na picha ya Elizabeth aliyekua akitabasamu, naye akatabasamu kisha akatoka ndani kwa ajili ya kuondoka.
Alipofika nje, aliangaza huku na kule, pikipiki yake ilikua mita chache kutoka mlangoni, purukushani za magari zilikua zikiendelea Barabarani, aliona hali ilikua shwari, akaidandia Pikipiki lakini kabla hajawasha aliwaona Wanaume wawili wenye suti nyeusi wakiwa nyuma yake, kabla hajazungumza chochote aliwekewa Bastola kwa nyuma.
โUsijaribu kufanya chochote, shuka kwenye Pikipikiโ alisema Mwanaume mmoja aliyekua amemwekea Bastola mgongoni tena kwa namna ambayo hakuna aliyeshtukia tukio hilo zaidi yao.
โMnataka nini?โ aliuliza Muhonzi akiwa ameshavua kofia ngumu kichwani
โOngoza ndaniโ alishusha pumzi zake, akashuka kwenye Pikipiki kisha akaongoza kuelekea ndani
โMnataka nini?โ akahoji Muhonzi tena kwa kungโaka. Akapigwa ngumi ya pua โOoooh!!!โ akagugumia, kikavutwa kiti haraka kisha akasukumizwa aketi, akatema damu nzito
โMnataka nini?โ akauliza tena Muhonzi akiwa anaifuta damu eneo la pua, Mwanaume mmoja akauweka mguu wake juu ya Kiti kisha akamwuliza
โM21 iko wapi?โ Muhonzi akapepesa macho yake huku akili ikiwa imefunguka, akatambua Watu hao walikua wametokea Ikulu kwa Rais
โM21?โ akauliza Muhonzi kama vile alikua hajui kuhusu M21, ngumi nyingine nzito ya pua ikatua palepale palipo pigwa mwanzo, akazidi kuugulia maumivu, Mmoja akaanza kupekua pale ndani akivuruga kila kitu ili kupata wanachokitafuta.
Aliyekua akipekua akamfwata tena Muhonzi tena kwa Jazba na hasira
โM21 iko wapi?โ akauliza akiwa amehamanika vya kutosha, Muhonzi akawa anababaika baada ya kugundua Watu hao walikua na uhakika kua anahusika na upotevu wa Nyaraka za siri za Rais Mbelwa, akapigwa ngumi nzito eneo la kichwa akapoteza fahamu, kisha wakamchukua na kundoka naye.
Gari ndogo iliyombeba Muhonzi iliwasili ndani ya godauni moja, akashuhswa na kuburuzwa hadi ndani ya Chumba kimoja kilicho kitupu, akamwagiwa Maji ili azinduke. Maji yalimzindua Muhonzi akajikuta ndani ya kiza kizito, akawakumbuka wale wanaume akataka kuleta vurugu lakini aligundua kua Mikono yake ilikua imepigwa kudu ya nguvu sana.ย Akiwa hajatuliza akili vyema ilisikika sauti ya kiatu ikija walipo, wote waligeuka nyuma.
Nini kitaendelea? Usikose sehemu ya 15 ya MSALA ndani ya SEASON 2ย
Hatma ya Mzee Kimaro na Elizabeth itakuaje? vipi kuhusu Muhonzi?
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
15 Comments
Oyah hili Ngoma n balaaaa
Dizaini flan kama movie aseeee ambayo ni ya kijasusi hivi
Daaah hiyo M21 jmn๐๐
hongera sana story haichoshi na wala haiboi
Haya masuala ya ujasusi ni hatari. Ila mwandishi noma, kama amewahi vile kuwa jasusi
Kama kweli vule
hHa
Ya moto sanaa hii
Stori nzuri sana
Iko njema saaaana admin
Yeo ndefu adi raha
Well done
Benjamin hajulikani alipo, Muhonzi kashatiwa nguvuni, Elizabeth nae anasubiri msaada duh hii ngoma bado mbichi sn….
HONGERA SANA KAKA MKUBWA
Admin niruhusu kucheza hii filamuu please