Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป MSALA Sehemu Ya Ishirini Na Moja-21
    Hadithi

    MSALA Sehemu Ya Ishirini Na Moja-21

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaSeptember 2, 2024Updated:September 7, 202411 Comments8 Mins Read4K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    MSALA
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    “Ilipoishia” Roho ya Elizabeth ilifukuta kwa maumivu Makali sana, hapo alipaswa kufanya kazi mbili, moja ni kumwokoa MUHONZI Kutoka mikononi mwa mwenyekiti wa chama cha Upinzani na pili alipaswa kutoisalimisha ile flash Muhimu aliyoificha kwenye chupi yake.

    Dakika Moja walizungukwa kila upande โ€œMikono juuโ€ ilisema sauti komavu iliyojaa hasira, ilikua ni sauti ya Brigedia Antony, kila upande walizungukwa na kikosi kazi, Hatimaye Elizabeth aliamini ameshafikia mwisho baada ya siku Tatu za Hekaheka nzito.ย  Endelea MSALA SEASON 3ย 

    SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

    Chozi liliendelea kumbubujika Elizabeth, alishakiona kifo mbele yake, mwili wa Msichanaย  huyu ulitweta ghafla. Alikosa nguvu, Moyoni alimwona Mzee Kimaro kama Msaliti, alionaย  Mzee huyo hakupaswa kujisalimisha kirahisi vile, Uamuzi ule ndiyo ukapelekeaย  Makomandoo kuzidi kuwazunguka kila kona.ย ย 

    Brigedia Antony alikua wa kwanza kusogea hapo akiwa na Bunduki yake mkononi,ย  alishachoka dharau na kebehi za Bi. Sandra, alijawa na hasira. Alilizunguka Jiwe naย  kuwakuta Mzee Kimaro pamoja na Elizabeth wakiwa wameketi. Macho ya Brigedia Antonyย  hayakutulia, kwanza alistaajabu kumwona Msichana mwenyewe, alikua Mdogo siyo waย  kuwasunbua kwa Muda wote huo, pili ni Mtu aliyekua akimsaidia Msichana huyo,ย  alimtazama kama Mzee Goigoi asiyeweza lolote.ย 

    Akachuchumaa akimkodolea macho Elizabeth, mara akaja Komandoo mmoja kabla hataย  Brigedia Antony Kesi hajasema chochote.ย 

    โ€œTuna maagizo ya kumchukua sasa hiviโ€ alisema Komandoo huyo aliyemsimamia Brigediaย  Antony kwa nyuma, Brigedia alipogeuka alikutana naye uso kwa uso, mazungumzo yalikuaย  yakifanyika kwa sauti kubwa kwasababu ya kelele ya panga boi za Helkopta zilizotanda juu.ย 

    Brigedia Antony hakua na sauti, akasimama ili Elizabeth achukuliwe japo aliona kamaย  amedharaulika mbele ya wanajeshi wengine lakini alijua maelekezo hayo yalitoka Ikulu kwaย  Rais, hakuna aliyekua na taarifa kua tayari Rais aliuawa.ย 

    Makomandoo waliwaswamba Mzee Kimaro na Elizabeth ili wawaingize kwenye Helkopta,ย  Elizabeth akaweka ngumu baada ya kusimama mbele ya Brigedia kisha akamwambiaย 

    โ€œUnafanya kosa kubwa sana, utalijutia siku mojaโ€ baada ya kusema hivyo alisukumwa kwaย  nguvu kuelekea kwenye Helkopta, Hatimaye Elizabeth na Mzee Kimaro walinaswa. Taarifaย  ya kunaswa kwao ilifika Ikulu kwa Waziri Mkuu Haji Babi mwenye tamaa na Madaraka,ย  nyuso za Tabasamu ziliwajaa.ย 

    Dakika moja, Helkopta zilianza kuondoka eneo hilo la mpaka wa Kiluvya, Uelekeo ukawa niย  Black Site kupitia Msitu wa Magoroto Mkoani Tanga, mahali ilipo Black Site ni siri nzitoย  sana. Mara moja wakapigwa na kupoteza fahamu ili wasijuwe wanapopelekwa.ย 

    **ย 

    Gari nyeusi isiyo na namba ya Usajili iliyokua ikitumiwa na Zagamba ilifika eneo laย  Godauni, mshale wa saa yake ulikua ukisoma saa 11:15 Alfajiri, Dakika kadhaa baada yaย 

    tukio la kunaswa kwa Elizabeth. Uso wake ulijawa na Hasira sana, akaelekea kwenyeย  chumba alichohifadhiwa Muhonzi.ย 

    โ€œUnasikia wewe Mshenzi, Elizabeth amenaswa Muda mchache uliopitaโ€ alisema Zagambaย  akiongea kwa hasira kisha akamwonesha video ya kunaswa kwa Elizabeth, moja ya Askariย  walio eneo la tukio walimtumia video hiyo kwa siri sana. Muhonzi alishtuka sana,ย  alichokiona kilimduwaza, akajikuta akipepesa macho yake kama fundi saa aliyepoteza nati.ย 

    Hakujua aseme nini, mikono yake ilifungwa kwa nyuma hivyo hakuweza hata kunyanyuaย  chochote. Alijitingisha lakini hakuweza hata kusogea, mara akavutwa kwa nguvuย 

    โ€œSema ni wapi ilipo M21!โ€ Alingโ€™aka Zagamba akilihitaji faili la siri la Rais Lucas Mbelwa,ย  Mara simu ya Zagamba iliita, alimkata jicho kali Muhonzi wakati anaitoa simu yakeย  mfukoni. Kisha aliondoka eneo hilo kwa ajili ya kuzungumza na Simuย 

    **ย ย 

    Jua lilikua tayari limeshatua, palionekana kua na hali ya kawaida sana siku hiyo lakiniย  palikua na siri nzito juu ya kifo cha Rais Mbelwa, Waziri Mkuu Haji Babi na washirika wakeย  walifanya kikao cha siri ndani ya Ikulu, kikao hicho kilikua na ajenda kuu moja, ni jinsi ganiย  watafanya mapinduzi baada ya kifo cha Rais Mbelwa, kitu cha kwanza walichokipaย  kipaumbele ni nyaraka M21 ambayo ilikua na siri nyingi za Rais Mbelwa na baadhi yaย  viongozi wengine wa ngazi za juu akiwemo Bi. Sandra ambaye alikua Mshirika mkubwa waย  Rais Mbelwa, hata yeye Waziri Mkuu kuna siri zilikuwamo ndani ya Nyaraka hiyo kumhusu.ย 

    Jukumu la kupatikana kwa nyaraka akakabidhiwa Bi. Sandra ambaye aliaminika kua ni Mtuย  hatari sana, akaondoka Ikulu asubuhi hiyo kwa Helkopta tayari kuelekea Kitengo nyeti chaย  Black Site.ย 

    **ย 

    Jua lilikua linawaka kwa wastani, asubuhi tulivu ilimkuta Benjamin Kingai akiwa ameketiย  juu ya jiwe moja ndani ya Msitu wa Magoroto, mazingira hayo yalimfanya Benjamin ajisikieย  vizuri, mbele yake palikua na bwawa dogo ambalo alikua akilitupia vijiwe vidogo vidogoย  ambavyo vilikua vinatoa sauti nzuri vinapoingia ndani ya Maji.ย 

    Mara alikuja Malkia Zandawe na kuketi kando ya Benjamin, hakua na hofu tena na Bintiย  huyo baada ya kuona mambo makubwa ambayo Binti huyo aliyafanya.ย ย 

    โ€œUnajisikiaje?โ€ aliuliza Zandawe akiwa ni mwenye kutabasamu, Benjamin naye aliachiaย  tabasamu lisilo na uhakika wa kipi anachokifurahia, akamjibu Malkia Zandaweย 

    โ€œVizuri, nipo ndani ya Msitu wakoโ€ kisha alisindikiza kauli yake na kicheko kidogo, akatupaย  tena vijiwe ndani ya bwawa.ย 

    โ€œUsiwe na wasiwasi Benjamin, utaondoka ndani ya Msitu muda siyo mrefu, kwasasa angaliaย  zaidi kuhusu hatma ya Maisha yako baada ya kutoka hapaโ€ akasema Malkia Zandawe hukuย  naye akitupa vijiwe, wakaufanya huo kua ni mchezo kwao.

    โ€œAsante kwa kusaidia Maisha yangu, sijui bila kunisaidia ningekua wapi sasa hivi, pengineย  ningekua nimeshauawa.โ€ Akasema Benjamin akiwa analengwa na choziย 

    โ€œUnafikiri ni kwanini huyo Msichana alikua na hizo nyaraka? Na hizo nyaraka zinahusu niniย  hasa?โ€ akahoji Malikia Zandawe akiwa anamtolea macho zaidi Benjaminย 

    โ€œInaonekana kuna taarifa za siri sana kumhusu Rais, lakini sijui kwa hakika zaidi ni kwaniniย  aliziibaโ€ย ย 

    โ€œBasi huyo Msichana kama atakua hai basi atakua sehemu ya hatari zaidi, kwa Msako uleย  sidhani kama atapata mahali pa Kujifichaโ€ akasema Malkia Zandaweย 

    โ€œLakini yule Msichana anaonekana kua zaidi ya Msichana, si Mtu wa kawaida. Ana mamboย  mengi ya siri anayoyaficha, kingine ni mjuzi wa mbinu za kivitaโ€ alisema, pakawa na ukimyaย  wa kutosha kisha Zandawe akatupa swali lingineย 

    โ€œUmewaza kuhusu Hatma ya Mtoto wako na mpenzi wako, nyuma yako kuna niniย  kitawakuta?โ€ swali hili lilimpa nyakati ngumu Benjamin, akashindwa kulizuia choziย  likamtoka likashuka hadi kwenye mashavu yake Madogo.ย 

    โ€œKuwaza hatma yao ni sawa na kusema hakuna kifo, nachelea kusema pengineย  wameshauawa huko waliko, roho yangu inanisuta ni kwanini niliwakimbia, nilikua mbinafsiย  nikasalimisha Maisha yangu bila kuangalia ni Jambo gani litawafikaโ€ Alipoimaliza hii kauliย  aliangusha kilio Benjamin, Malkia Zandawe akajawa na huzuni sana akamwambia Benjaminย 

    โ€œHata ukilia kwasasa haitokua na Msaada, kikubwa ni kujua ni wapi walipo, na je wapo hai?โ€ย ย 

    โ€œKujua walipo ni jambo gumu sana, ile sehemu ni hatari, ni sehemu ya siri sana. Ni ngumuย  kujua nini kimewafika, naweza kusema wameshakufaโ€ akasema Benjamin kisha akajiinamia.ย 

    โ€œNitalichunguza hilo Benjamin, subiriaโ€ akasema Malkia Zandawe kisha akatoka spidiย  kuzama Msituni, Benjamin hakuelewa ni kitu gani kilimfanya Zandawe azame Msitumi kwaย  kasi namna ile.ย 

    Msichana Zandawe, alizidi kukimbia hadi alipofika eneo la Bwawa, hapo aliangaza huku naย  kule, eneo hilo ndilo ambalo Benjamin alikua amejitupa Siku ile kwa lengo la kuokoa Maishaย  yake kutoka juu ya Helkopta ya Kijeshi.ย 

    Akasogea hadi chini ya Mti mmoja, hapo chini aliziona kamba ambazo alifungwa nazoย  Benjamin, kisha akazichukua kamba hizo akakimbia kurudi alipomwacha Benjamin, alikuaย  msichana wa Msituni anayeutawala Msitu huo hatari unaowasumbua wengiย 

    Alifika alipomwacha Benjamin akiwa anahema sana, kisha akamwonesha Benjamin zileย  kamba, haraka Benjamin akazikumbuka, akashuka kutoka juu ya jiwe hadi aliposimamaย  Zandawe.ย 

    โ€œUnataka kufanya nini?โ€

    โ€œSubiria uoneโ€ akasema Zandawe kisha akapiga mluzi mkali, ghafla ikasikika sauti ya ndegeย  mmoja akija walipo, ndege huyo alikua mweupe anayefanana na njiwa mzuri wa kufugwa,ย  alipofika hapo alitua juu ya jiwe ambao Benjamin alilikalia muda mchache ulio pitaย 

    โ€œHuyu ni rafiki yangu anaitwa Gola, ni mpelelezi mzuri anayenipa taarifa nyingi kuhusu haliย  ya Msitu, nataka kumtumaโ€ alisema Malkia Zandawe, kila alichokisema kilikua kama ndotoย  kwa Benjamin, alijikuta akitabasamu.ย 

    Mambo kama hayo aliyasoma kwenye kitabu, ni Mfalme Suleiman pekee ndiye aliyekua anaย  uwezo wa kuzungumza na ndege lakini Msichana Zandawe alikua na uwezo kama ule waย  kuzungumza na ndege.ย 

    โ€œUmtume wapi?โ€ย ย 

    โ€œHuko mahala pa siri, nataka kupajua. Nataka kujua hatma ya Familia yako Benjaminโ€ย  alisema Malkia Zandawe kisha alimsogelea ndege Gola, akazungumza naye kwa lugha zaย  ndege kisha akampatia ile kamba kama alama ya wapi ilipo Black Site. Kisha ndege huyoย  akaruka kwa spidi, akiwa ameishikilia ile kamba mguuni.ย 

    โ€œGola ataleta majibu ni wapi ilipo Black Siteโ€ akasema Malkia Zandawe kisha akampaย  tabasamu zito Benjamin ambaye alijawa na Bumbuwazi zito, midomo yake ikawa mizitoย  kiasi kwamba hakuweza kusema chochote.ย  Nini Kitaendelea?

    Usikose sehemu ya ishirini na mbili ya MSALA SEASON 3 Kujua kama Elizabeth alipona kwenye Msala huu

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

    MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

    Msala Msala Kijiweni Riwaya Ya Msala

    11 Comments

    1. Guyton on September 2, 2024 4:52 pm

      Kubabeki๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ.
      Mwandishi upewe maua yako..๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
      • SWAHABABA on September 2, 2024 6:44 pm

        Hii story unaisoma huku unaiona movie. Mungu azidishe kipaji chako.

        Reply
    2. Ahyen on September 2, 2024 5:00 pm

      wa kwanza kuisoma

      Reply
    3. Hendry on September 2, 2024 6:40 pm

      Watu kusoma

      Reply
    4. Deo on September 2, 2024 7:47 pm

      Mambo hayo moto ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    5. Xalvan on September 2, 2024 8:28 pm

      ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    6. Calvin paul on September 2, 2024 8:42 pm

      ๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹

      Reply
    7. Tyson on September 2, 2024 9:18 pm

      bonge moja la story ningekuwa muigizaji ningeandaa movie

      Reply
    8. Sadick on September 2, 2024 10:30 pm

      Hakika mwandishi unatuleteaga story kali lakini hii ni zaidi ya story kali hongera sana admin mungu akupe maisha marefu

      Reply
    9. Godwin Clemence on September 3, 2024 12:08 pm

      Story inanikumbusha vitu vingi na venye nasoma Kwa picha

      Reply
    10. EMMANUEL STEVEN MUSSA on September 3, 2024 2:32 pm

      Ni ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ•บ kongole adimini mkeka ukitiki hii msala ni kali mno..utakula 3k

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 14, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-03

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya pili Alipiga magoti na kujiinamia huku chozi likimtoka Zahoro,…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.