Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Nane

“Mama! Mama! Umenizaa wewe mwenyewe kweli? Unyama gani huu  unanifanyia Veronica wako? Ulinizaa peke yangu na huna binti  mwingine” Nilisema nikiwa ninalia, nilikuwa nimejikunyata,  tatizo kwangu halikuwa Anko Sanga bali ni Mama yangu Mzazi,  nilijiuliza alikuwa ameingiwa na shetani gani hadi anifanyie  yote yale? 

“Nisingekuzaa nisingefanya hivi, kwani Wazazi wako wangepiga  sana kelele…leo nimeamua kufanya kwasababu hakuna wa kupiga  kelele” Endelea

SEHEMU YA TISA

“Hayo maisha yana mwisho Mama! Mungu atakuumbua siku moja” 

“Akijaniumbua nitakuwa nimetajirika vya kutosha, na wewe  utakuwa huna kazi bali umeshajifia kama James!” Nililia sana  Kwanini Mama yangu ageuke kuwa mbaya vile… 

Nilianza kuishi na ile maiti pale ndani, uzuri ni kuwa simu  ya James ilikuwepo kule kwenye chumba kingine ambacho  nilikuwa nimelala lakini kuipata ndio ulikuwa mtihani kwangu,  niliwekwa bafuni ambako niliuficha mwili wa James! Nilikata  tamaa ya kutoka na nikasema sitafanya jitihada zozote zile,  nitafia pale. Nilikuwa mtu wa kulia, nilikaa na maiti ya  James hadi ilipoanza kuharibika, harufu ikawa kali na  ukizingatia chumba cha bafu kilikuwa kidogo mno na mazingira  ya ile nyumba hayakuwa rafiki hata kidogo. 

Harufu iliponizidia niligonga mlango ili nifunguliwe,  niligonga mlango ili nisaidiwe kuokoa Maisha yangu, kila  nilipomuwaza binti yangu nilijawa na hasira na uchungu,  sikutaka yamkute yaliyonikuta, nilitamani sana awajue wale  Watu kuwa sio Watu wazuri hata kidogo lakini sikuwa na huo  uwezo hata wa kumuona! 

“Mnifungulie mnataka nife kwa njaa na harufu kali” nilipiga  kelele nikitaka wanifungulie Mlango nipate hewa safi, nilikaa  mle kwa siku nne bila kula chakula chochote! Ndipo Anko Sanga  alipokuja kunifungulia nikiwa nimechoka njaa pamoja na ile  harufu kunizidi. 

“Mnataka kuniuwa?” nilimuuliza 

“Utachagua wewe, kufa au kuwa hai kwa ajili ya Mtoto wako?”  Silaha kubwa kwao ilikuwa ni Mtoto wangu, kila nilichotaka kukifanya walijificha kwenye mwanvuli wa Mtoto wangu, wakidai  watamuuwa tu 

Nilirudishwa kwenye kile chumba nilichokuwa ninaishi, chumba  hiki kilikuwa na ile Simu ya Marehemu James, Nilisubiria  kwanza Afya yangu iimarike maana nilidhohofu mwili na akili  kwa kipindi kifupi nilichowekwa na ile maiti ya James. 

Mama yangu licha ya Unyama wote ule alijifanya Mtu mwema sana  Kanisani, alisaidia Watoto Yatima na kukarabati kanisa huku  akitoa ushuhuda kuwa Yesu ndiye aliyemsaidia kupata utajiri,  ilikuwa ni rahisi kwake kuwajibu nilipo kwani kila Mtu  alikuwa akijua kuwa nilikuwa Mke wa mtu hivyo kila  waliponiulizia aliwaambia kuwa nipo Dar kwa Mume wangu! kwa  kipindi chote hicho cha miaka mitatu. 

Ukiachana na unyama aliokuwa akinifanyia bali yeye na Kaka  yake walikuwa wanatoa kafara za Watu ili kuendelea kuwa  matajiri, Mume wangu Jonas akawa ndio Mume wa Mama yangu! 

Basi Maisha yangu ndani ya lile jumba yaliendelea huku  nikizidi kuvuta nguvu ya nini nifanye! Siku moja niliiwasha  ile simu ya Marehemu James ili nitafute mawasiliano. Kila  niliyempigia alikuwa akiuliza sana maswali, mimi ni nani?  kwanini nina ile simu na James yuko wapi? Sikuona mwangaza,  nikawa naendelea kutafuta mawasiliano ya Watu wengine ili  kuwataarifu ya kinachoendelea pale ndani lakini haikusaidia  kabisa. 

Ule mchezo wa Anko Sanga haukufika kikomo aliendelea  kunifanya kwa lazima, aliniinamisha na kunifanya atakavyo  huku akipaka yale mafuta, sikupata hisia yoyote zaidi ya  maumivu makali, alikuwa haniandai kabisa na vile nilikuwa na  kisirani sana na yeye. 

Nilikuwa Mtu wa kulia na kuumia kila saa hadi nilihisi ni  Mfu, lile jumba lilikuwa likitumika kwenye makafara yao ya  utajiri na kazi hii waliifanya Mama na Anko Sanga kwa roho  zao mbaya, kadiri siku zilivyozidi kusonga nilianza kuona  mambo ya ajabu mno. Sauti za ajabu ajabu zilikuwa zikisika  usiku, zilikuwa ni sauti za kuomba msaada na nyingine za  vilio, kila nilipozisikia nilikesha kwenye maombi na sala,  nilikabidhi Maisha yangu mikononi mwa Yesu ili niwe salama. 

Nilikuwa nimeporwa kila kitu kwenye Maisha yangu, urembo  wangu ulibadirika na kuwa kitu kisicho na maana kabisaa!  Nilitafakari sana nini cha kufanya nilipata wazo la kupiga  simu polisi, nikapiga namba ya huduma ya dharura ya polisi,  ilipokelewa nilitoa maelezo yangu yote kuanzia mahali nilipo  hadi yaliyokuwa yakinisibu.

“Sawa Tulia hapo hapo tunakuja” Ilisikika sauti kupitia simu  na palepale ile simu ilizima chaji, nilihangaika kutafuta  chaja ili niweze kuijaza lakini sikupata nilijitahidi kupekua  pangine ningepata lakini ilishindikana. Baada ya saa moja  nilisikia king’ora cha gari ya polisi kikiwa kinalia, kadiri  gari ilivyokuwa ikisogea ndivyo Sauti iliyokuwa ikija kwa  karibu. Sasa kile chumba kilikuwa upande wa nyuma ya nyumba  tofauti na chumba cha Anko Sanga ambacho kilikuwa upande wa  mbele hivyo nilishindwa hata kuiona hiyo gari. 

Nilipiga kelele ili wale Askari wanisikie lakini kupiga  kelele kungekuwa kunasaidia kwenye ile nyumba ningelikuwa  nimepiga muda mrefu sana ili nipate msaada, nikajaribu  kuwasha ile simu pengine ingeita kidogo ili niwasiliane nao,  ilikuwa haina chaji kabisa iliwaka na kuzima 

“Mungu wangu! shit” Nilizunguka pale chumbani kama  mwendawazimu, bado king’ora kilikuwa kikisikika kutokea  kwenye geti. 

Baada ya dakika 10 nilisikia kikiondoka ni wazi kuwa Polisi  walikuwa wakiondoka, nikajiuliza wanawezaje kuondoka wakati  nilishawapa ramani kamili ya mahali nilipo? 

“Msaada! nisaidieni nipo huku” Nilipaza sauti, Mlango wa  chumba ulifunguliwa aliingia Anko Sanga, mkononi nilikuwa na  ile simu, alinitia kofi kisha akaninyang’aya ile simu na  kuivunja vunja 

“Unajua unachokifanya mjinga wewe?” 

“Nautaka uhuru wangu mliouchukuwa Anko Sanga, nipeni binti  yangu tafadhari” 

“Sasa endelea na huo ujinga utaona nitakacho kufanyia”  Alifunga mlango na kuondoka zake! 

Usiku wa siku hiyo walikuja kunihamisha wakiwa na wanaume  wawili, walinipeleka sehemu nyingine kabisa, walinipatia  video ya Mtoto wangu na kuniambia niendelee kuwa mpole kama  nikifanya vurugu sitamuona tena, nilipomtazama Moyo  nilijikuta nikilia, alikuwa akitabasamu kwenye video kama  vile alikuwa akijua nilikuwa namtazama 

“Pole moyo wangu! Ipo siku utapata mapenzi ya Mama yako”  Nilisema ndani ya Moyo wangu, walinifungia kwenye nyumba  nyingine.

“Niko tayari kuwa Mtumwa wenu kwa maisha yangu yote, sitodai  uhuru wangu tena bali nahitaji tu Mtoto wangu aishi na mimi  hapa” Lilikuwa ni ombi langu kabla hawajaondoka, Anko Sanga  alitabasamu kisha aliondoka zake bila kunipatia jibu lolote  lile. 

Niliuchukua Mto wa kochi na kuanza kuubembeleza  nikimfananisha na binti yangu, nilikuwa karibu kuwa chizi  sababu ya yale mateso makali niliyokuwa nayapitia. 

MAHAKAMANI: Nilikuwa bado nimesimama pale kizimbani naelezea  jinsi ilivyokuwa hadi nikamuuwa Mama yangu Mzazi, kila Mtu  alikuwa akitokwa na machozi, Hakimu alikuwa amejiinamia akiwa  analia, hata askari waliokuwa pale walikuwa wakitokwa na  Machozi. Miguu yangu ilikuwa ikitetemeka kwa kusimama kwa  takribani masaa mawili bila kupumzika. 

Baadaye Hakimu aligonga nyundo yake sote tulikaa kimya,  alizungumza kwa sauti iliyoambatana na majonzi makubwa  akasema 

“Kwa miaka yangu zaidi ya 30 ya kufanya kazi za mahakama  sijawahi kukutana na kisa kilichoniliza kama hiki, kesi hii  itasikilizwa baada ya Veronica kuwaeleza Mawakili wa Serikali  na binafsi kuwa nini kiliendelea. Inasikitisha kukaa hapa  kumsikiliza hivyo itawasilishwa kwa kifupi na hao Mawakili  baada ya siku tano za kumsikiliza Veronica, hakuna kifungu  cha sheria kinachosema haya niliyoyasema bali nimetumia  nafasi na cheo changu kutamka haya, Hali ya Veronica  imedhohofu hivyo asingeliweza kumudu kusimulia kwa muda  mrefu”. Alisema yule Hakimu, pale pale Askari walinichukua na  kunirudisha kwenye chumba maalum. 

Taarifa yangu iligonga vichwa vya walio wengi kila Mtu  alitaka kujua kilichoendelea na jinsi nilivyomuuwa Mama  yangu, nilihitaji utulivu wa akili kwa masaa mengi ili niweze  kusimulia jopo la Mawakili. 

Mama Sofia hakuacha kunipa moyo, alikuja kuniona jioni akiwa  na Mwanangu, Askari walimzuia asinipatie Mtoto lakini yule  Askari aliyepewa jukumu la kunilinda aliwaambia wamuache  afanye hivyo, alinipatia binti yangu Moyo, aliponiona  alinishika sura yangu, nilimuona akitabasamu! Nilimbusu Binti  yangu 

“Naweza nisiwe karibu na wewe Mwanangu lakini siwezi kuwa  mbali na upendo wako! hata iweje sitaacha kukuombea Mwanangu”

“Mamaaa!” Moyo aliita na kunifanya nitokwe na machozi, Mama  Sofia alimchukua Moyo akaondoka naye. 

Siku iliyofuata Mchungaji wa kanisa letu la Arusha alikuja  kuniona baada ya kusikia masahibu yangu, 

“Pole Veronica, kondoo mweupe uliyepakwa rangi nyekundu ili  kuuficha uhalisia wake, siku zote umekuwa kondoo mwema sana” 

“Amin Baba Mchungaji, nashukuru kwa kuwa upande wangu.  Unanipa moyo na tumaini la kuwa haki itatendeka kwenye ufalme  wa Mungu kwani haki ya Mwanadamu haiwezi kufanana na haki  atoayo Mungu” 

“Najivunia moyo wako wa Ujasiri, unazidi kunifanya niendelee  kukuweka kwenye maombi yangu ya kila siku Veronica, Hakika  Mama na Mjomba yako walikuwa watumwa wa Ushetani” 

Niliishia kulia tu, ukweli japo nilimuuwa Mama yangu lakini  haikuondoa uhalisia kuwa alikuwa ni Mama pekee aliyenizaa,  alikuwa ni Mama pekee aliyenilea na kunisomesha kwa tabu sana  baada ya Baba kukimbia. 

“Usilie! katika ufalme wa Mungu dhambi hujitenga na walio  wema, Huruma ya Mungu ikuangaze katika hukumu yako” Alikuwa  akimaliza kunipa maneno ya kiimani yaliyonipa moyo sana 

“Baba Mchungaji! kama nitafungwa Naomba Muelekezeni Mtoto  wangu katika kufanya yaliyo mema! Mwambieni hasara za tamaa,  Mwambieni Mama yake nilimeyatia doa Maisha yangu ili awe hai”  Nilisema nikiwa nimemshika mkono Baba Mchungaji, alikuwa  akidondosha chozi pia 

“Ubaki salama Veronica” Mchungaji aliondoka na kuniacha  nikiwa kwenye ulinzi mkali wa Askari wenye silaha. 

Siku iliyofuata nilitakiwa kuelezea kilichoendelea baada ya  kuhamishwa kwenye ile nyumba na kupelekwa nyumba nyingine,  niliketi kwenye kiti nikiwa nimezungukwa na wale Mawakili  akiwemo yule aliyeajiliwa na Mama Sofia ambaye alikuwa  akimlea Mtoto wangu kwa sasa. 

“Hujazungumzia Maisha ya Jonas akiwa kwenye mahusiano na Mama  yako?” 

“Vipi kuhusu Anko wako! Alikufa au alikimbia?” 

“Je, uliwezaje kutoka?”

Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA KUMI

JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

8 Comments

Leave A Reply

Exit mobile version