Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Nane
“Mama! Mama! Umenizaa wewe mwenyewe kweli? Unyama gani huuย unanifanyia Veronica wako? Ulinizaa peke yangu na huna bintiย mwingine” Nilisema nikiwa ninalia, nilikuwa nimejikunyata,ย tatizo kwangu halikuwa Anko Sanga bali ni Mama yangu Mzazi,ย nilijiuliza alikuwa ameingiwa na shetani gani hadi anifanyieย yote yale?ย
“Nisingekuzaa nisingefanya hivi, kwani Wazazi wako wangepigaย sana kelele…leo nimeamua kufanya kwasababu hakuna wa kupigaย kelele” Endelea
SEHEMU YA TISA
“Hayo maisha yana mwisho Mama! Mungu atakuumbua siku moja”ย
“Akijaniumbua nitakuwa nimetajirika vya kutosha, na weweย utakuwa huna kazi bali umeshajifia kama James!” Nililia sanaย Kwanini Mama yangu ageuke kuwa mbaya vile…ย
Nilianza kuishi na ile maiti pale ndani, uzuri ni kuwa simuย ya James ilikuwepo kule kwenye chumba kingine ambachoย nilikuwa nimelala lakini kuipata ndio ulikuwa mtihani kwangu,ย niliwekwa bafuni ambako niliuficha mwili wa James! Nilikataย tamaa ya kutoka na nikasema sitafanya jitihada zozote zile,ย nitafia pale. Nilikuwa mtu wa kulia, nilikaa na maiti yaย James hadi ilipoanza kuharibika, harufu ikawa kali naย ukizingatia chumba cha bafu kilikuwa kidogo mno na mazingiraย ya ile nyumba hayakuwa rafiki hata kidogo.ย
Harufu iliponizidia niligonga mlango ili nifunguliwe,ย niligonga mlango ili nisaidiwe kuokoa Maisha yangu, kilaย nilipomuwaza binti yangu nilijawa na hasira na uchungu,ย sikutaka yamkute yaliyonikuta, nilitamani sana awajue waleย Watu kuwa sio Watu wazuri hata kidogo lakini sikuwa na huoย uwezo hata wa kumuona!ย
“Mnifungulie mnataka nife kwa njaa na harufu kali” nilipigaย kelele nikitaka wanifungulie Mlango nipate hewa safi, nilikaaย mle kwa siku nne bila kula chakula chochote! Ndipo Anko Sangaย alipokuja kunifungulia nikiwa nimechoka njaa pamoja na ileย harufu kunizidi.ย
“Mnataka kuniuwa?” nilimuulizaย
“Utachagua wewe, kufa au kuwa hai kwa ajili ya Mtoto wako?”ย Silaha kubwa kwao ilikuwa ni Mtoto wangu, kila nilichotakaย kukifanya walijificha kwenye mwanvuli wa Mtoto wangu, wakidaiย watamuuwa tuย
Nilirudishwa kwenye kile chumba nilichokuwa ninaishi, chumbaย hiki kilikuwa na ile Simu ya Marehemu James, Nilisubiriaย kwanza Afya yangu iimarike maana nilidhohofu mwili na akiliย kwa kipindi kifupi nilichowekwa na ile maiti ya James.ย
Mama yangu licha ya Unyama wote ule alijifanya Mtu mwema sanaย Kanisani, alisaidia Watoto Yatima na kukarabati kanisa hukuย akitoa ushuhuda kuwa Yesu ndiye aliyemsaidia kupata utajiri,ย ilikuwa ni rahisi kwake kuwajibu nilipo kwani kila Mtuย alikuwa akijua kuwa nilikuwa Mke wa mtu hivyo kilaย waliponiulizia aliwaambia kuwa nipo Dar kwa Mume wangu! kwaย kipindi chote hicho cha miaka mitatu.ย
Ukiachana na unyama aliokuwa akinifanyia bali yeye na Kakaย yake walikuwa wanatoa kafara za Watu ili kuendelea kuwaย matajiri, Mume wangu Jonas akawa ndio Mume wa Mama yangu!ย
Basi Maisha yangu ndani ya lile jumba yaliendelea hukuย nikizidi kuvuta nguvu ya nini nifanye! Siku moja niliiwashaย ile simu ya Marehemu James ili nitafute mawasiliano. Kilaย niliyempigia alikuwa akiuliza sana maswali, mimi ni nani?ย kwanini nina ile simu na James yuko wapi? Sikuona mwangaza,ย nikawa naendelea kutafuta mawasiliano ya Watu wengine iliย kuwataarifu ya kinachoendelea pale ndani lakini haikusaidiaย kabisa.ย
Ule mchezo wa Anko Sanga haukufika kikomo aliendeleaย kunifanya kwa lazima, aliniinamisha na kunifanya atakavyoย huku akipaka yale mafuta, sikupata hisia yoyote zaidi yaย maumivu makali, alikuwa haniandai kabisa na vile nilikuwa naย kisirani sana na yeye.ย
Nilikuwa Mtu wa kulia na kuumia kila saa hadi nilihisi niย Mfu, lile jumba lilikuwa likitumika kwenye makafara yao yaย utajiri na kazi hii waliifanya Mama na Anko Sanga kwa rohoย zao mbaya, kadiri siku zilivyozidi kusonga nilianza kuonaย mambo ya ajabu mno. Sauti za ajabu ajabu zilikuwa zikisikaย usiku, zilikuwa ni sauti za kuomba msaada na nyingine zaย vilio, kila nilipozisikia nilikesha kwenye maombi na sala,ย nilikabidhi Maisha yangu mikononi mwa Yesu ili niwe salama.ย
Nilikuwa nimeporwa kila kitu kwenye Maisha yangu, uremboย wangu ulibadirika na kuwa kitu kisicho na maana kabisaa!ย Nilitafakari sana nini cha kufanya nilipata wazo la kupigaย simu polisi, nikapiga namba ya huduma ya dharura ya polisi,ย ilipokelewa nilitoa maelezo yangu yote kuanzia mahali nilipoย hadi yaliyokuwa yakinisibu.
“Sawa Tulia hapo hapo tunakuja” Ilisikika sauti kupitia simuย na palepale ile simu ilizima chaji, nilihangaika kutafutaย chaja ili niweze kuijaza lakini sikupata nilijitahidi kupekuaย pangine ningepata lakini ilishindikana. Baada ya saa mojaย nilisikia king’ora cha gari ya polisi kikiwa kinalia, kadiriย gari ilivyokuwa ikisogea ndivyo Sauti iliyokuwa ikija kwaย karibu. Sasa kile chumba kilikuwa upande wa nyuma ya nyumbaย tofauti na chumba cha Anko Sanga ambacho kilikuwa upande waย mbele hivyo nilishindwa hata kuiona hiyo gari.ย
Nilipiga kelele ili wale Askari wanisikie lakini kupigaย kelele kungekuwa kunasaidia kwenye ile nyumba ningelikuwaย nimepiga muda mrefu sana ili nipate msaada, nikajaribuย kuwasha ile simu pengine ingeita kidogo ili niwasiliane nao,ย ilikuwa haina chaji kabisa iliwaka na kuzimaย
“Mungu wangu! shit” Nilizunguka pale chumbani kamaย mwendawazimu, bado king’ora kilikuwa kikisikika kutokeaย kwenye geti.ย
Baada ya dakika 10 nilisikia kikiondoka ni wazi kuwa Polisiย walikuwa wakiondoka, nikajiuliza wanawezaje kuondoka wakatiย nilishawapa ramani kamili ya mahali nilipo?ย
“Msaada! nisaidieni nipo huku” Nilipaza sauti, Mlango waย chumba ulifunguliwa aliingia Anko Sanga, mkononi nilikuwa naย ile simu, alinitia kofi kisha akaninyang’aya ile simu naย kuivunja vunjaย
“Unajua unachokifanya mjinga wewe?”ย
“Nautaka uhuru wangu mliouchukuwa Anko Sanga, nipeni bintiย yangu tafadhari”ย
“Sasa endelea na huo ujinga utaona nitakacho kufanyia”ย Alifunga mlango na kuondoka zake!ย
Usiku wa siku hiyo walikuja kunihamisha wakiwa na wanaumeย wawili, walinipeleka sehemu nyingine kabisa, walinipatiaย video ya Mtoto wangu na kuniambia niendelee kuwa mpole kamaย nikifanya vurugu sitamuona tena, nilipomtazama Moyoย nilijikuta nikilia, alikuwa akitabasamu kwenye video kamaย vile alikuwa akijua nilikuwa namtazamaย
“Pole moyo wangu! Ipo siku utapata mapenzi ya Mama yako”ย Nilisema ndani ya Moyo wangu, walinifungia kwenye nyumbaย nyingine.
“Niko tayari kuwa Mtumwa wenu kwa maisha yangu yote, sitodaiย uhuru wangu tena bali nahitaji tu Mtoto wangu aishi na mimiย hapa” Lilikuwa ni ombi langu kabla hawajaondoka, Anko Sangaย alitabasamu kisha aliondoka zake bila kunipatia jibu loloteย lile.ย
Niliuchukua Mto wa kochi na kuanza kuubembelezaย nikimfananisha na binti yangu, nilikuwa karibu kuwa chiziย sababu ya yale mateso makali niliyokuwa nayapitia.ย
MAHAKAMANI: Nilikuwa bado nimesimama pale kizimbani naelezeaย jinsi ilivyokuwa hadi nikamuuwa Mama yangu Mzazi, kila Mtuย alikuwa akitokwa na machozi, Hakimu alikuwa amejiinamia akiwaย analia, hata askari waliokuwa pale walikuwa wakitokwa naย Machozi. Miguu yangu ilikuwa ikitetemeka kwa kusimama kwaย takribani masaa mawili bila kupumzika.ย
Baadaye Hakimu aligonga nyundo yake sote tulikaa kimya,ย alizungumza kwa sauti iliyoambatana na majonzi makubwaย akasemaย
“Kwa miaka yangu zaidi ya 30 ya kufanya kazi za mahakamaย sijawahi kukutana na kisa kilichoniliza kama hiki, kesi hiiย itasikilizwa baada ya Veronica kuwaeleza Mawakili wa Serikaliย na binafsi kuwa nini kiliendelea. Inasikitisha kukaa hapaย kumsikiliza hivyo itawasilishwa kwa kifupi na hao Mawakiliย baada ya siku tano za kumsikiliza Veronica, hakuna kifunguย cha sheria kinachosema haya niliyoyasema bali nimetumiaย nafasi na cheo changu kutamka haya, Hali ya Veronicaย imedhohofu hivyo asingeliweza kumudu kusimulia kwa mudaย mrefu”. Alisema yule Hakimu, pale pale Askari walinichukua naย kunirudisha kwenye chumba maalum.ย
Taarifa yangu iligonga vichwa vya walio wengi kila Mtuย alitaka kujua kilichoendelea na jinsi nilivyomuuwa Mamaย yangu, nilihitaji utulivu wa akili kwa masaa mengi ili niwezeย kusimulia jopo la Mawakili.ย
Mama Sofia hakuacha kunipa moyo, alikuja kuniona jioni akiwaย na Mwanangu, Askari walimzuia asinipatie Mtoto lakini yuleย Askari aliyepewa jukumu la kunilinda aliwaambia wamuacheย afanye hivyo, alinipatia binti yangu Moyo, aliponionaย alinishika sura yangu, nilimuona akitabasamu! Nilimbusu Bintiย yanguย
“Naweza nisiwe karibu na wewe Mwanangu lakini siwezi kuwaย mbali na upendo wako! hata iweje sitaacha kukuombea Mwanangu”
“Mamaaa!” Moyo aliita na kunifanya nitokwe na machozi, Mamaย Sofia alimchukua Moyo akaondoka naye.ย
Siku iliyofuata Mchungaji wa kanisa letu la Arusha alikujaย kuniona baada ya kusikia masahibu yangu,ย
“Pole Veronica, kondoo mweupe uliyepakwa rangi nyekundu iliย kuuficha uhalisia wake, siku zote umekuwa kondoo mwema sana”ย
“Amin Baba Mchungaji, nashukuru kwa kuwa upande wangu.ย Unanipa moyo na tumaini la kuwa haki itatendeka kwenye ufalmeย wa Mungu kwani haki ya Mwanadamu haiwezi kufanana na hakiย atoayo Mungu”ย
“Najivunia moyo wako wa Ujasiri, unazidi kunifanya niendeleeย kukuweka kwenye maombi yangu ya kila siku Veronica, Hakikaย Mama na Mjomba yako walikuwa watumwa wa Ushetani”ย
Niliishia kulia tu, ukweli japo nilimuuwa Mama yangu lakiniย haikuondoa uhalisia kuwa alikuwa ni Mama pekee aliyenizaa,ย alikuwa ni Mama pekee aliyenilea na kunisomesha kwa tabu sanaย baada ya Baba kukimbia.ย
“Usilie! katika ufalme wa Mungu dhambi hujitenga na walioย wema, Huruma ya Mungu ikuangaze katika hukumu yako” Alikuwaย akimaliza kunipa maneno ya kiimani yaliyonipa moyo sanaย
“Baba Mchungaji! kama nitafungwa Naomba Muelekezeni Mtotoย wangu katika kufanya yaliyo mema! Mwambieni hasara za tamaa,ย Mwambieni Mama yake nilimeyatia doa Maisha yangu ili awe hai”ย Nilisema nikiwa nimemshika mkono Baba Mchungaji, alikuwaย akidondosha chozi piaย
“Ubaki salama Veronica” Mchungaji aliondoka na kuniachaย nikiwa kwenye ulinzi mkali wa Askari wenye silaha.ย
Siku iliyofuata nilitakiwa kuelezea kilichoendelea baada yaย kuhamishwa kwenye ile nyumba na kupelekwa nyumba nyingine,ย niliketi kwenye kiti nikiwa nimezungukwa na wale Mawakiliย akiwemo yule aliyeajiliwa na Mama Sofia ambaye alikuwaย akimlea Mtoto wangu kwa sasa.ย
“Hujazungumzia Maisha ya Jonas akiwa kwenye mahusiano na Mamaย yako?”ย
“Vipi kuhusu Anko wako! Alikufa au alikimbia?”ย
“Je, uliwezaje kutoka?”
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA KUMI
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
8 Comments
Fupi Tamu ndefu inanoga admin toa tena.
What a story..๐๐๐
Daaaah Ahsante kwa Story Tamu Sema Imekuja kwa Kuchelewa leo Naomba Admn Iwe Ndefu Ndefu Kidogo
Daaahhh!! Admn unajua kesho itoke mapema
Asee Dunia ni mapito,, kabla hujafa hujaumbika,, admin tunaomba mwendelezo kwa wakati ๐
Asantee ๐ฅฐ
Kazi mzuri
Du kweli huu mkasa unatia huruma mtu unasoma mpaka machozi yanatoka