Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tatu-03)
    Hadithi

    Mama Niachie Mume Wangu (Sehemu Ya Tatu-03)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 14, 2025Updated:May 23, 202522 Comments10 Mins Read5K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Mama Niachie Mume Wangu Sehemu Ya Pili 

    Sasa wakati naendelea kumpotezea nilijikuta napeleka macho  yangu nyuma ya gari yaani siti za nyuma kule, gari ilikuwa na siti nne tu, nikawa nimeliona begi lake ambalo halikufungwa  vizuri, ile shuka ya damu ilikuwa kwenye begi lake na kwa  vyovyote alifanya kuwa siri ndio maana nilipomuuliza hakutaka  kunijibu ipasavyo. 

    Nilishtuka sana, lile shuka lilikuwa na damu zilizotoka  kwenye bikra yangu .

    SEHEMU YA TATU

    “Mungu wangu. Hili shuka analipeleka wapi?” nilijiuliza, kiu  ya kutaka kuonana na Mama nimueleze mchezo Mchafu wa Anko  Sanga ilinijaa na vile sikutaka kabisa kumsemesha pale kwenye  gari. 

    Nikajifanya kupotezea kuwa sijaona kitu, safari hii ilikuwa  fupi maana aliendesha kwa spidi huku akiniuliza maswali ya  hapa na pale, aliuliza kama nina Boyfriend, nikampotezea,  aliuliza kuhusu masuala ya nchuo sikumjibu kitu. 

    Ugumu wa safari hii ulikuwa na maumivu ya moyo wangu,  tulipofika nilianza kulia baada ya kumuona Mama aliyekuwa  amesimama mlangoni baada ya kusikia mlio wa gari,  nilikurupuka na kwenda kumkumbatia huku nikilia na chozi  likimiminika kwenye manega yake. 

    Mjomba alikuwamo kwenye gari mpaka kufikia muda ule, Mama  alinikumbatia pia na kuniambia 

    “Ndio ukubwa huo Veronica usilie” alisema, nilishtuka kisha  nilijitoa kidogo na kumtazama huku chozi likiendelea  kunimwagika kwenye mboni za macho yangu 

    “Ndio ukubwa? unamaanisha nini Mama?” nilihoji, nikachukua  kitambaa kutoka kwenye mfuko wa suruali yangu na kujifuta  machozi 

    Mama alikuwa akiniangalia tu bila kunijibu swali langu 

    “Mama! ina maana unajua kinachoniliza?” nilimuuliza swali  lingine, akasema tuingie ndani, wakati tunaingia ndani Mjomba  akawa ameshuka akafunga mlango na kuingia ndani pia. 

    Baada ya kuketi nilijiuliza maswali mengi kuwa Mama anajua  kila kitu ina maana alikuwa akiijua hii safari ya Mlima  Kilimanjaro? na kama alikuwa akijua kulikuwa na jambo gani  hapa nyuma yake? wakati naendelea kutafakari niliisikia sauti  ya Mama 

    “Veronica, hongera na pole kwa kilichotokea” alisema,  aliongea nusu nusu na kunifanya nizidi kuingiwa na wasiwasi

    “Mama umeshiriki kwenye unyama alionifanyia Anko Sanga?”  alikaa kimya akinitazama 

    “Sidhani kama ni kweli umenizaa, sijui kama huyu kweli ni  Kaka yako wa damu! Mama wewe wakupanga hili jambo kweli?”  Nilisema kwa hasira na hisia nzito huku moyo ukizidi kuniuma 

    “Veronica!! Kwasasa bado mdogo huwezi kuelewa hili jambo  lakini ndio uhalisia huo, nilijua hatma ya safari hii na Anko  wako Sanga” 

    “Mama na Kaka yako ni mashetani wakubwa, wakati nikiwa na  tumaini la kupata faraja kutoka kwako kumbe nawe umechangia  kuniumiza?” 

    “Veronica….msikilize Mama yako” Anko Sanga akadakia, kama  vile aliupuliza moto uliokuwa ukiwaka 

    “Wewe ndio mshenzi kabisa, hufai kuitwa Anko, fedhuli mkubwa  wewe” nilisema na kuangusha kilio, waliponisemesha  nilikimbilia chumbani kwangu na kujifungia. 

    Mama alirudi Sebleni baada ya kuja kunigongea mlango bila  mafanikio, Anko Sanga akatoa ile shuka na kumuonyesha Mama,  kisha Mama akamwambia aipeleke Kwa Mganga wao! 

    “Jambo hili lapaswa kuendelea kuwa siri hivyo zungumza na  Mwanao vizuri” Alisema Anko Sanga akiwa anairudisha ile Shuka  kwenye begi 

    “Hilo ni jambo langu, nenda sasa” Aliongea Mama, Anko Sanga  akaondoka Mchana uleule. 

    Majira ya Usiku nikiwa nimejifungia mle chumbani, hasira  zikiwa zinapoa taratibu maana hakukuwa tena na Mtu wa  kuzipandisha, nilichukua simu na kuwasha tochi kisha  nikaziangalia sehemu zangu za siri maana ile damu na maumivu  sikupata nafasi ya kujiangalia vizuri. 

    Niliona pakiwa pamekaa vizuri tuu, hata yale maumivu yalikuwa  yamepoa kabisa nikawa najisikia vizuri, japo Mama yangu  alifanya kitendo cha Kinyama vile nilijikuta nikiingiwa na  huruma hasa yale Maneno makali niliyoyazungumza mbele yake. 

    Nikawa natafakari jinsi ya kumuomba msamaha wakati huo nikiwa  nasikiliza nyimbo ya Kayumba inayoitwa Mama, ikanifanya  nifikirie jinsi Mama alivyonilea nikiwa mdogo kabisa, Baba  alitukimbia akanilea kwa shida hakukata tamaa.

    Jinsi alivyonipigania hadi nikafika chuo ilikuwa ni namna ya  kipekee sana, nilijikuta nikijilaumu kwa kumtolea lugha za  matusi, Punde nikasikia sauti ya Mtu akiwa analia kwa nje,  nilipoitafakari nikagundua kuwa inatokea sebleni na ilikuwa  ni sauti ya Mama! 

    “Mama analia? itakuwa nimemkosea sana Mama yangu” nilisema na  moyo wangu. Nilijikuta nikizidi kuumia kwenye nafsi yangu,  ikanipasa nifungue mlango na kuelekea sebleni. 

    Mama alikuwa akilia huku akiwa amejiinamia, alilia sana na  kunifanya nikubali makosa yangu. 

    “Mama naomba unisamehe” Nilimwambia Mama baada ya kumsogelea “Veronica umenisemea maneno mabaya sana, nimeumia mno” 

    “Ndio maana naomba msamaha Mama, nimetambua makosa yangu na  sina budi kuomba radhi kwa maneno yangu makali niliyoyasema  mchana” Baada ya kumuomba radhi, alinisamehe na Maisha  yakaendelea nikiwa nimeshatolewa usichana wangu na Ako Sanga  ambae ni Kaka wa Mama yangu Mzazi. 

    Sikutaka tena kumuuliza kuhusu lile shuka ambalo lilikuwa na  damu yangu ya Bikra, nilionelea nikae kimya kwa kuhofia  kumkwaza tena Mama, sikumuona wala kumsikia tena Anko Sanga. 

    Baada ya mwezi mmoja likizo ilikuwa imeisha nilitakiwa kurudi  chuo kuendelea na Masomo, Mama aliniita usiku wa kuamkia  safari. 

    “Veronica nenda kasome, Nakupigania sawa?” 

    “Mh! Mama unanipigia kila siku hilo nalijua” 

    “Ni kweli lakini nitahakikisha maisha yanabadirika,  namshukuru Mungu kunijalia Mtoto kama wewe” Alisema Mama,  nikakumbuka alikua akinipigia simu mara nyingi nikiwa chuo  akinitaka sana nijitunze, nijiepushe na masuala ya Wanaume. 

    “Sawa Mama siwezi kukuangusha kwenye kila jambo” 

    Niliondoka Alfajiri na kurudi Dar kwa ajili ya kuendelea na  Masomo yangu huku kichwani nikifikiria jinsi nilivyomsaliti  Jonas, Konzo alikuwa wa kwanza kunipa taarifa kuwa Jonas  alianzisha mahusiano mengine na Mwanafunzi mwingine aliyeitwa  Agatha.

    “Siamini kama Jonas anaweza kutembea na Agatha kwa jinsi  anavyokupenda lakini nimethibitisha kwa macho yangu mawili”  alisema na kuniaminisha kwa kauli yake, sasa nilipofikiria  kumfuata Jonas moyo ulisita kwani nami nilikuwa msaliti kwake  japo nilikuwa nimebakwa na Anko Sanga. 

    “Naanzaje kumlaumu Jonas?” nilijiuliza nikiwa peke yangu  baada ya kuachana na Konzo, ilikuwa ni siku ya pili baada ya  kurejea Dar. 

    “Mimi mwenyewe nimemsaliti na kutolewa bikira yangu”  Niliachana na wazo la kumuuliza Jonas japo hata mimi niliona  amebadirika huku kisingizio kikiwa ni kutompa penzi. 

    “Jonas nipo tayari kukupa penzi” nilimwambia nilipokutana  nae, alishangaa kwasababu sikuwahi kumwambia vile 

    “Uko serious?” 

    “Ndio, Jonas sitaki nikupoteze” nilisema tukiwa tumekaa  chumbani kwetu, ilikuwa ni kawaida kwa Wanaume kuingia vyumba  vya Wanawake na wanawake kuingia kwa Wanaume. Konzo na  marafiki wengine walitupisha kwakuwa nilishawaambia kuwa nina  hamu na Jonas 

    “Nafurahi kusikia hivyo Kipenzi, jinsi nilivyokuwa  nakuhangaikia kila siku” alisema akiwa ananiingia maungoni,  hisia zilipanda lakini wazo la kuwa Nilikuwa nimekeketwa  likaja ghafla, nikaogopa kuumbuka pale. 

    “Jonas subiria kidogo” nilisema kwa tabu alikuwa tayari  ameanza kunyonya chuchu zangu! Mhemko ulikuwa umepanda sana 

    “Nisubirie nini mpenzi jamani” Jonas alionekana kuzidiwa na  kunihitaji sana wakati ule, alikuwa ameshavua shati lake na  kulitupa chini. Maziwa yangu yakiwa yametolewa kwenye sidiria 

    “Subiria kwanza una Condom?” nilimuuliza kimtego ili tu  kuahirisha zoezi, nilikuwa nikimpenda sana Jonas na  nilihitaji aje kuwa Mume wangu siku za usoni. 

    “Aaah! unaona unavyoboa Veronica? ulivyonipigia nilikwambia  nakuja na Condom, hatuwezi kufanya sex bila kinga” akasema  huku akiendelea kuninyonya na kunifanya nipandwe na mzuka wa  ajabu! 

    “Subiria kidogo, Jonas hapa hatuwezi kuwa huru. Kachukue  Chumba Lodge tulale wote” 

    “Veronica bhana, nilijua tu utanizungusha zungusha”

    “Siwezi kukuzungusha My love, napenda tuwe huru zaidi” “Lini twende Lodge?” 

    “Tutaongea kwenye simu” Nilisema, Jonas hakukaa aliondoka  zake na nilijua tu nimemkwaza. 

    “Nimeshindwa kufanya nae” 

    “Veronica una shida gani kwani? si ulisema una hamu naye sana  sasa kilichokufanya usikate kiu leo ni nini?” Alisema Konzo  kwa kunilaumu sana, alijua tayari nimetolewa usichana wangu  na Jonas 

    “Sio hivyo tatizo naona aibu Konzo, unajua mimi ni Bikra” 

    “Sasa utaona aibu hadi lini Veronica? Jonas akikosa kwako  ataenda kusex na mwingine” 

    “Najua. Unanishauri nifanye nini?” 

    “Sex nae” 

    “Naogopa, naona aibu” 

    “Nina wazo, hiyo siku tumia kilevi ili kuikata aibu” “Unamaanisha Pombe?” 

    “Ndio, hiyo ndio njia pekee. Unatakiwa ujifunze pombe”  Alinipa wazo la kutumia kilevi ili nisex na Jonas, wakati  nalifikiria hilo nikapata wazo lingine. 

    “Utanifundisha basi Konzo maana sijawahi kuitumia”  nilimueleza kwakuwa alikuwa akitumia Pombe hivyo anifundishe,  Sasa wazo lililonijia ni kwamba nikishaijua vizuri hiyo pombe  nimshawishi na Jonas tulewe kwanza ndipo tusex kwa kuamini  Mtu akilewa anakuwa hana muda na kuangalia au kuchunguza  vitu. Nikajisemea kuwa hawezi kugundua kuwa nimekeketwa 

    Basi, Konzo alianza kunifunisha pombe. Alinipeleka kwenye  kumbi za starehe nyakati za usiku na kuanza kunifundisha  taratibu, alianza na bia zenye kilevi asilimia ndogo kisha  aliniingiza kwenye pombe kali kama Konyagi ili nilewe haraka. 

    “Sitaitumia kwa Maisha yangu yote nitaiacha baada tu ya kusex  na Jonas”

    “Hayo ni maamuzi yako Mwaya, ukiipenda endelea nayo maana  mwenzio naipiga kama sina akili nzuri na wala haiingilii  maisha yangu ya Chuo” 

    Nilipanga iwe hivyo yaani nikishasex na Jonas niiache, basi  nilianza kuizoea nikawa napiga mpaka chupa tatu, kichwa  kikawa kigumu kuelewa nikaanza kupiga Konyagi hapo ndipo  nilianza kujihisi nimelewa. 

    Nilipoona nipo sawa kukutana na Jonas kimwili nilimtafuta  maana mawasiliano yetu hayakuwa mazuri. Alinishutumu  simpendi, nina mwanaume mwingine kwasababu tu sikumpa  alichotaka. 

    “Ukinizingua leo ndio umejiharibia mwenyewe nitakaa mbali na  wewe” Alisema, nilimpa uhakika kuwa siku hiyo ni lazima nimpe  penzi 

    “Kumbe unakunywa pombe Veronica?” alishangaa nikiwa nakata  maji kama kambale kwenye tope 

    “Ndio nakunywa!” 

    “Humtaki tena Yesu? ulisema huwezi kunywa kwakuwa una imani  kubwa sana…nakushangaa leo” alisema huku nae akipigilia  unywaji, ni kweli niliwahi kumkatalia kuwa situmii Pombe  kwani yeye alikuwa akitumia. 

    Alishawahi kuniwekea mtego wa pombe ili nisex nae  niliposhtuka niliondoka zangu! 

    “Jonas mimi nakunywa pombe vizuri tu, Nimetokea Arusha watu  wengi kule wanatumia Pombe” 

    “Mh! Haya” Tuligida unywaji siku hiyo tukiwa Baa, tulikula  nyama choma na chips mayai. Kama unavyojua Jonas alitokea  kwenye familia bora yenye uwezo kifedha. 

    Tulipiga mtungi hadi nilihisi nazima, tuliondoka pale Usiku  tukiwa tumelewa hadi Lodge, ile akili ya kuwa nilikuwa  nimekeketwa iliondoka kabisa maana pombe niliyokunywa  ilikimbilia huku Chini, Jonas nae alikuwa na Mzuka wa ajabu  sana wala hakuchelewesha. 

    Mapenzi ya pombe yakaanza bila hata kuchojoana vizuri,  tukafanya mapenzi. Japo nilikuwa nimekeketwa lakini nilisikia  raha sana siku hiyo. Niliukatikia Mjegeje wa Jonas kama Mkuna  nazi vile na uliniingia sawa sawa, alinisugua hadi nikaomba  msamaha siku hiyo.

    Tulipomaliza tulijitupa na kulala, asubuhi mapema nikawa wa  kwanza kuamka. Kichwa kilikuwa kinanipiga, shuka ilikua  imeloa damu kidogo! Sikuwa na maumivu popote pale,  nilimuamsha Jonas 

    “Siamini kama tumelala pamoja Veronica?” alisema akiwa  anajinyoosha, kila nilipomtazama nilihisi bado nina aibu nae,  akataka anifanye cha asubuhi. 

    “Hapana Jonas, nimechoka sana jana umenifanya mpaka basi” “Ha!ha!ha!” 

    “Usicheke kweli umenifanya sana hadi damu imetoka” 

    “Yaani! ndio nimeamini kuwa ulikuwa bikra, nafurahi kuwa  Mwanaume wako wa kwanza” alisema, nilimtazama huku  nikijiambia kuwa yeye ni wapili, wakwanza alikuwa Anko Sanga  ambaye sikupendelea sana kukumbuka kilichotokea kule Mlima  Kilimanjaro. 

    Angalau moyo ulikuwa umetulia, Jonas hakufanikiwa kugundua  kuwa nilikuwa nimekeketwa kwasababu tulisex tukiwa chakali (  Tumelewa Pombe ) 

    ********** 

    “Ungeniambia hamjafanya leo ningeshangaa sana, na  kusingelikuwa na njia nyingine” Konzo alisema baada ya  kumsimulia kuwa Nilifanya mapenzi na Jonas 

    “Kusema ukweli nimefurahi sana leo huwezi amini Konzo,  nimefanya mapenzi kwa mara ya kwanza” 

    “Ndio ishakuwa hiyo hairudi nyuma, akitaka unampa atakavyo” 

    Tulicheka kwa pamoja kuashiria tulikuwa tumefurahi wote kwa  kilichotokea. Nikawa nahisi raha ile ya kusex na Jonas hata  nikiwa darasani nililoa kila nilipomtazama, naye alihisi  hilo. 

    Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA NNE

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    riwaya mpya riwaya za kusisimua simulizi kijiweni simulizi za kijasusi simulizi za mapenzi soma riwaya bure

    22 Comments

    1. Bplm1664 on May 14, 2025 5:46 pm

      Yeaaah aweeeeeh

      Reply
      • Adam on May 14, 2025 8:07 pm

        Kwa Kweli Story Inaonesha Ni Nzuri

        Reply
    2. Gervase on May 14, 2025 7:34 pm

      Uncle kama uncle 🙌🙌

      Reply
      • Rajibomba on May 17, 2025 6:03 pm

        Mmmmh haya bana uncle nimshua

        Reply
        • Khamisi Edward jinyage on May 21, 2025 2:54 am

          Duh anko ni noma sana

          Reply
    3. Lilian on May 14, 2025 7:34 pm

      Oooooh

      Reply
    4. Adam on May 14, 2025 8:07 pm

      Ila Anko Sanga Siyo Mtu Ngoja nisubiri Hii story

      Reply
    5. Yusuf on May 14, 2025 8:09 pm

      Ataliii

      Reply
      • Tabu zacharia on May 15, 2025 11:12 am

        Mmh me kazi kuwekea bundle tu

        Reply
        • Rajibomba on May 17, 2025 6:04 pm

          Mmmmh haya bana uncle nimshua

          Reply
    6. Msofe on May 15, 2025 11:37 am

      Iko vizur sana hiii simulizi nimeipenda

      Reply
    7. Cathbert on May 17, 2025 7:48 am

      Mambo ya utamu

      Reply
    8. Kevin378 on May 24, 2025 10:23 am

      Cool partnership https://shorturl.fm/a0B2m

      Reply
    9. Gage3911 on May 24, 2025 12:53 pm

      Very good partnership https://shorturl.fm/9fnIC

      Reply
    10. Zoe1441 on May 25, 2025 9:15 am

      https://shorturl.fm/oYjg5

      Reply
    11. Bailey3265 on May 25, 2025 4:25 pm

      https://shorturl.fm/a0B2m

      Reply
    12. Jolene2977 on May 25, 2025 9:58 pm

      https://shorturl.fm/N6nl1

      Reply
    13. Alyssa1129 on May 26, 2025 1:50 am

      https://shorturl.fm/TbTre

      Reply
    14. Cornelius2910 on May 27, 2025 4:38 am

      https://shorturl.fm/9fnIC

      Reply
    15. Kaylee2533 on May 27, 2025 9:03 pm

      https://shorturl.fm/a0B2m

      Reply
    16. Dominique3369 on May 28, 2025 7:18 am

      https://shorturl.fm/m8ueY

      Reply
    17. Marco3629 on May 28, 2025 7:19 am

      https://shorturl.fm/FIJkD

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.