Niliomba niletewe Binti yangu pale Gerezani, Mama SofiaΒ alimleta Moyo. Nilimkumbatia Mwanangu hadi nikahisi farajaΒ iliyo pitiliza.Β
“Umeongea na Wakili vizuri?” aliniuliza Mama Sofia,Β nilimtazama na kumwambiaΒ
“Ndio”Β
“Matumaini yangu utakuwa huru Veronica” Alisema, MudaΒ ulipoisha Mama Sofia aliondoka na binti yangu aliyeitwa Moyo.Β
Nilibakia pale kwenye kiza, Maaskari walinichukua naΒ kunirudisha kwenye chumba changu! Nilikuwa nikiishi kwenyeΒ chumba cha peke yangu kutokana na kesi ya mauwaji iliyokuwaΒ ikinikabili, Moyoni nilijisema kuwaΒ
“Sipaswi kuwa huru” niliketi kwenye pembe ya kile chumbaΒ kilichojaa wadudu wadogo wadogo, chini kulikuwa na majiΒ yaliyomwagika, niliyamwaga mwenyewe kwasababu sikupenda kula.Β Kuna wakati niliwahi kumwambia Askari aliyekuwa akinihudumiaΒ kuwaΒ
“Niletee sumu nife, sipendi kuendelea kukaa hapa”Β
“Veronica, Bado hii kesi ni mbichi sana. Subiria hukumu yakoΒ , Kama Mahakama ikikukuta hauna hatia? unataka kufa ili bintiΒ yako alie kwa uchungu?” aliniulizaΒ
“Usiwaze kufa, hakuna anayeijua kesho yako” alisema naΒ kuondoka zake.Β
Sikuona umuhimu wa kuendelea kuwa hai tena nikiwa paleΒ gerezani kama Mahabusu niliyekuwa nasubiria siku ya hukumu yaΒ kesi yangu ya Mauwaji
“Ni kweli umemuuwa Mama yako Mzazi?” yule Wakili alirudi tenaΒ kuutaka ushahidi ili ajuwe namna ya kunitetea, Wakili huyuΒ aliajiliwa na Mama Sofia ambaye alikuwa jirani yangu mwema,Β alipenda kuniona nikishinda ile kesiΒ
“Nikikwambia nilimuuwa utaiambia nini Mahakama? UtaidanganyaΒ kuwa sijauwa?”Β
“Ukiniambia ukweli nitajua jinsi ya kukuweka huru Veronica”Β
“Uhuru sio kitu ninachokitaka kwasasa, naitaka haki tu”Β nilisema kisha nilikaa kimya sikutaka kuendelea kuzungumzaΒ nae hadi Muda ulipoisha nilirudishwa tena kwenye kile chumba.Β
Yule Wakili alimpelekea taarifa Mama Sofia, Mama huyu alikuwaΒ tajiri sana. Alikuwa jirani yangu kule Mbezi Luis nilipokuwaΒ ninaishiΒ
“Ninavyomjuwa Veronica hawezi kumuuwa Mama yake Mzazi Jacob”Β alisema akimuelekeza yule Wakili..Β
“Veronica ni mpole, mcheshi na mtaratibu sana…kusemaΒ amemuuwa Mama yake hilo haliwezekani kabisa”Β
“Unafikiria nitafanya nini na hataki kuzungumza kabisa,Β amekaa kimya?”Β
“Veronica sema ukweli, angalia ulivyodhohofu…Mwanao analiaΒ na kukuulizia utarudi lini, hivi ni kweli hutaki kuishi tenaΒ na binti yako Moyo?” Mama Sofia aliongea Baada yaΒ kunitembelea, ni kweli nilikuwa nimekondeana sana, MwiliΒ ulidhohofu mno, Afya yangu ilikuwa mbaya!Β
Mawazo yalipelekea nidhohofike namna ile, kingine niΒ mazingira ya pale ambayo hayakuwa rafiki kabisa kwangu!Β
“Mahakama itatenda haki kwangu Mama Sofia, Mungu ndiyeΒ anayejua kilichojificha” nilisema kwasababu sikupenda kabisaΒ kuzungumzia jambo lile lililotikisa vichwa vya Watu wengiΒ sana.Β
“Kwanini hutaki kusema kama kweli umeuwa au haujauwaΒ Veronica?” Alihoji lakini sikumpa majibu kila alipokuja yeyeΒ au Wakili wa ile kesi.Β
Tukio hili lilitokea Mwaka 2009, lilizua gumzo kubwa, hakunaΒ aliyeamini kama kweli Nimemuuwa Mama yangu. Ni kweli nilikuwaΒ nimemuuwa Mama yangu Mzazi na chanzo cha tukio hili alikuwaΒ ni Mume wangu aliyitwa Jonas.
Baada ya siku 21 nilirudishwa tena Mahakamani ili kusikilizaΒ kesi yangu iliyojaza waandishi wa habari, kurasa zote zaΒ Magazeti zilipambwa kwa picha yangu na maelezo juu ya tukioΒ langu la Mauwaji.Β
Hakimu alinitazama kabla ya kuanza ile kesi, jicho lakeΒ lilijaa huruma ambayo niliweza kuiona pindi nilipogongana naeΒ macho, nilimuona akitoa kitambaa chake na kufuta choziΒ lililokuwa likimbubujika. Mahakama ilizizima kusikilizaΒ atasema nini, niliweza kuzisikia pumzi zangu nilipokuwaΒ nikihema ilitokana na ukimya uliotawala pale Mahakamani.Β
Nilipotazama pembeni nilimuona Mwanangu Moyo, aliniangalia naΒ kutabasamu na kunifanya na Mimi nitabasamu.Β
Kila Mtu alikuwa kimya, wengine wakinitazama Mimi na wengineΒ wakiwa wanamtazama Hakimu aliyekuwa amejiinamia kwa zaidi yaΒ dakika 10, sikujua alikuwa akifikiria nini.Β
“Veronica!” aliniita yule Hakimu mwenye umri mkubwa, alivuaΒ miwani yake na kunitazama tenaΒ
“Abee!”Β
“Uko tayari kusema ukweli?” aliniuliza, nilikaa kimya kwaΒ dakika moja kisha nilimpa jibuΒ
“Ndio”Β
“Ilikuwaje ukamuuwa Mama yako Mzazi?” alihoji tena,Β nilimtazama Mama Sofia ambaye alinipa ishara niwe jasiriΒ niseme.Β
Alitamani kusikia nikikanusha kuwa sijamuuwa Mama yangu, WatuΒ wote wakawa bize kunitazama, waandishi wa Habari walitegaΒ karamu zao kwenye karatasi ili wapate cha kuandika kwenyeΒ Magazeti yao.Β
Nilianza kwa kigugumizi, pale pale chozi lilianzaΒ kunibubujika, midomo yangu ilikuwa ikitetemekaΒ
“Nisamehe Mwanangu Moyo” nilisema huku nikiwa ninalia,Β niliendeleaΒ
“Ni kweli nimemuuwa Mama yangu Mzazi” kauli hii iliwashtuaΒ wengi, Hakimu alionekana kuvunjika moyo kabisa aliinamishaΒ kichwa chake chini huku akijifuta Machozi.
Nilianza kueleza kilichotokea, Naitwa Veronica Moyo, najuaΒ wengi mmeshtushwa kusikia nimemuuwa Mama yangu, baada yaΒ kueleza haya naomba Mahakama inihukumu kifo.Β
MIAKA MINGI KABLA YA TUKIOΒ
Nilipofika chuoni kusomea masuala ya Utalii nilikutana naΒ Mwanaume aliyeitwa Jonas, nilitokea Kumpenda nae piaΒ alinipenda sana lakini hofu yangu ilikuwa kwenye maumbileΒ yangu, nilihofia kumwambia Jonas kuwa nimekeketwa na huoΒ ukawa udhaifu wangu katika Maisha yangu.Β
Kila nilipo kumbuka juu ya kile kitendo cha kukeketwaΒ nilijisikia vibaya sana lakini kwa kipindi chote hichoΒ nilikuwa bado sijawahi kukutana na Mwanaume na kufanya naeΒ mapenzi.Β
Jonas ni binadamu mwenye hisia kama Wanaume wengineΒ alionekana kuanza kukata tamaa kila nilipompa visingizio kuwaΒ nipo kwenye siku zangu, naogopa Mimba au tutafanya tukimalizaΒ chuo.Β
Nilimsikia rafiki yangu aliyeitwa Konzo akisema kuwa naendaΒ kumpoteza Jonas siku za usoni kwani hawezi kukaa bila kusexΒ na mimiΒ
“Ooh! amekwambia hivyo?”Β
“Ndio, anataka kujua ni kwanini humpi tendo…Mwaka wa piliΒ sasa”Β
“Sikia Konzo, naogopa Jonas atanikimbia akishakula tundaΒ langu”Β
“Hofu yako haina msingi, haishawishi kabisa Veronica au weweΒ ni msichana bado?” Aliniuliza, sikuwahi kumwambia kuwa mimiΒ ni Bikra nikaona ni vema nimwambieΒ
“Ndio, mimi ni Bikra na sijawahi kushiriki tendo na Mwanaume” “Unasema kweli? Jonas anajua?”Β
“Hajui konzo na sitaki ajue kwasasa, acha iwe siri bainaΒ yetu” Nilimueleza hivyo, kitendo cha kukeketwa kilinifanyaΒ nikose kujiamini kwasababu niliwahi kusoma majarida kadhaaΒ yanayozungumzia suala hilo kwa Wanaume, wengi wakisemaΒ Wanaume hawapendi Wanawake waliokeketwa kwa madai kuwa sioΒ Watamu.
“Sawa nitaitunza Veronica na sitamwambia Mtu hapa Chuoni”Β Alisema na kunifurahisha Konzo, siri ya kukeketwa ikabakiaΒ kwenye nafsi yangu!Β
Nilipomwambia Mama yangu Mzazi aliniambia kuwa nikionaΒ Mwanaume anasema hapendi Mwanamke aliyekeketwa basi MwanaumeΒ huyo hajui nini maana ya Mapenzi wala radha ya tendo haijuiΒ vizuriΒ
“Mama! mbona wataalam wanathibitisha kuwa kukeketwaΒ kunamfanya Mwanamke akose radha halisi?”Β
“Mtaalam gani huyo anayeshindana na mababu wa Kabila letu?Β Sayansi inakupoteza Mwanangu” Maneno ya Mama yaliniweka njiaΒ panda kwa kipindi kirefu hasa baada ya kuvunja ungoΒ
Niliishi na Mawazo ya aina mbili, Sikujua nimfuate nani katiΒ ya Mama yangu au Wataalam walioandika majarida yale. NikasemaΒ ipo siku nitaujua ukweli ingawa sikutaka kumpoteza Jonas,Β Mwanaume mzuri wa sura, alitokea kwenye maisha bora sana,Β Mcheshi na mkarimu. Alinisaidia Mambo mengi sana tukiwaΒ chuoni.Β
Alinipa robo ya pesa alizotumiwa na Wazazi wake wakati MamaΒ yangu Mzazi akinihimiza kuishi kulingana na mazingira, hakuwaΒ na uwezo wa kunisomeshaΒ
“Veronica Mwanangu! Nenda kasome huko lakini tambua kuwaΒ Maisha ni magumu mno, nitakachopata nitakituma kwako naΒ nikikosa ishi kulingana na mazingira” alisema Mama nikiwaΒ ninaenda kujiunga na Chuo Jijini Dar kutokea Arusha.Β
“Sawa Mama! nitatimiza malengo yangu na ya kwako, nitaishiΒ kama ulivyoniagiza” Jinsi alivyonilea ilikuwa ni rahisi sanaΒ kukubaliana na hali zozote za kimaisha, Baba yanguΒ alitutelekeza nikiwa mdogo, Kwa mujibu wa Mama alisema kuwaΒ Baba alikimbia madeni yaliyokuwa yakimuandama.Β
Pale chuoni kwetu wengi walinifahamu, na msemo ulikuwaΒ ukitamba sana ni ‘Tazama Pisi kali ya Arusha ile’ ulikuwa niΒ msemo uliopendwa, nilikuwa mzuri, macho makubwa yakukonyeza,Β shepu ilikuwa ya kawaida tu lakini ilitosha kunifanyaΒ nikamilike sana, Mapedeshee waliokuja kutafuta WanawakeΒ wazuri pale chuoni hawakuacha kunisumbua kila wakatiΒ waliwatuma rafiki zangu akiwemo KonzoΒ
“Una bahati sana Veronica, mabosi wanakuulizia wewe tu”Β alisema rafiki yangu Konzo, alinichekesha mno
“Sasa Bahati au usumbufu? ni kheri wewe unaishi upendavyoΒ kuliko mie ”Β
“Ningekuwa ndio wewe! ningeshapata gari maana Mabosi wakoΒ tayari kukupatia upendacho” Nilitamani sana Maisha mazuriΒ lakini ile siri ya kukeketwa niliogopa itasambaa pale chuoniΒ ndio maana nilihakikisha namkataa kila aliyenitongoza.Β
“Huyu Mwanamke anaringa sana hapa chuoni sijui anajikuta naniΒ yaani” Ni miongoni mwa kauli nilizowahi kuzisikia kutoka kwaΒ Baadhi ya Wanaume walionikataa, niliona ni bora wasemeΒ naringa kuliko ile siri ifahamike kwenye hadhara.Β
Jonas alifanya kila mtego ili nifanye nae tendo lakiniΒ nilikuwa makini kuhakikisha namaliza kwanza chuo ili hataΒ kama akijua mbele ya safari sitapata aibu kama ambayoΒ nitaipata nikiwa bado chuoni, alinitoa Out kila mara.Β
Konzo aliniletea majarida mbalimbali ili nijifunze jinsiΒ Mwanamke anavyotolewa usichana akiamini naogopa kufanyaΒ hivyo, aliniletea hadi video za ngono ili nishawishike! Ndio,Β zilinihamasisha sana na hofu yangu ikawa pale paleΒ
“Nimefanya jitihada zote Veronica, kinachokukwamisha niΒ usichana wako huo, unakosa madili ya pesa”Β
“Imeshakuwa Bwana Konzo, acha iwe hivyo hivyo wakati ukifikaΒ nitapata hayo madili”Β
“Tatizo lako wewe ni mbishi sana Veronica, jaribu usiseme tuΒ wakati…unaogopa utafikiria unataka kutolewa uhai?”Β
“Ha! ha! ha!”Β
Nilimzoea Konzo, siku moja Mwalimu Kasase aliniita ofisiniΒ kwake, alikuwa ni miongoni mwa Watu waliokuwa wakinitongozaΒ pale chuoni, nilipofika aliulizia kuhusu jibu lakeΒ nilimwambia aendelee kusubiria, alinielewa.Β
Basi Maisha ya Chuo yalikuwa matamu na ya kukera kwa wakatiΒ mmoja, kuna wakati nilisikia raha sana lakini wakati mwingineΒ nilikereka, likizo ilipofika nilirudi Arusha nikiwa msichanaΒ bado yaani Bikira. Pale nyumbani nilimkuta Mjomba yaani KakaΒ yake Mama aliyeitwa Sanga.Β
“Eeh! Veronica umekuwa Mkubwa hivi?” aliponiona aliniuliza,Β niliishia kucheka tu maana ukubwa wa Mtu unaonekana kupitiaΒ kwa wengine, mimi nilijiona nipo vile vileΒ
“Huyu Mtoto kafanana sana na Baba yake”
“Sana, hasa anavyotembea kama anarudi vile”Β
“Ha!ha!ha!” Mama aliingiza utani wake kwa kilugha cha kwetu,Β tukawa tunacheka lakini Mjomba akionekana kama kunishangaaΒ sana hadi nikawa naona aibuΒ
“Msindikize Mjomba wako Kanisani” Alisema Mama baada ya sikuΒ mbili za kuwa ArushaΒ
“Ina maana Anko Sanga hakujui kanisani Mama? siku zote hizoΒ alizokaa”Β
“Mpeleke bwana!! Hakuwa na Mtu wa kumsindikiza huko, ukirudiΒ utayarishe chakula cha Usiku”Β
Basi, tuliingia kwenye gari lake tukaanza safari ya kuelekeaΒ kanisani kwetu, palikuwa na umbali kiasi, mwendo wa KilomitaΒ 15 hadi kufika huko, palikuwa karibu na nje ya Mji wa ArushaΒ kulikuwa na hilo kanisa la Mzungu ambalo tangia nikiwa mdogoΒ nilikuwa nikisali hapo hadi nakuwa mkubwa.Β
“Kumbe ni mbali hivi?” aliniuliza tukiwa tumebakishaΒ takribani Kilomita 4, Kwa mbali mlima kilimanjaro ulikuwaΒ ukionekana kwa uzuri sana, tulipishana na magari ya WataliiΒ waliokuwa wakielekea hukoΒ
“Umeshawahi kwenda kufanya utalii?” aliniuliza tena,Β nilitabasamu tu kwani sikuwahi hata kuusogelea ule mlima japoΒ nilizaliwa Arusha.Β
“Hapana Anko sijawahi kufanya utalii, ule mlima nauona kwaΒ mbali tuu” Mjomba alicheka sana akaniuliza kama ningependaΒ twende huko mlimaniΒ
“Ndio napenda”Β
“Nitaongea na Mama yako” alisema kisha tuliendelea na safariΒ ya kuelekea Kanisani, tulipofika nilimuacha akanipatia pesaΒ kama Elfu 50 hivi kisha akaniambia nisimwambie Mama MaanaΒ ataichukuaΒ
“Sitamwambia Anko”Β
“Haya natumaini mapishi yako yatakuwa Bul bul leo Veronica”Β
“Ha!ha!ha!” nilikuwa napenda sana kucheka nilikuwa siweziΒ kununa yaani, nilifurahi kisha nilipanda daladala na kurejeaΒ Nyumbani.
Β Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA PILIΒ
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β


12 Comments
Woow inakujakuja vikee π§
dadeq anko ankol π« π€£π€£
Ni nzuri sana
Woooh
Ankolllll
nzuri
Ankol tena
Ni story nzuri inapendeza
Mzuri
Anko atuachie vero wetu bwanaππ
Ankoo atuachie vero wetu bwanaππ
ryoq5t