Niliomba niletewe Binti yangu pale Gerezani, Mama Sofiaย alimleta Moyo. Nilimkumbatia Mwanangu hadi nikahisi farajaย iliyo pitiliza.ย
“Umeongea na Wakili vizuri?” aliniuliza Mama Sofia,ย nilimtazama na kumwambiaย
“Ndio”ย
“Matumaini yangu utakuwa huru Veronica” Alisema, Mudaย ulipoisha Mama Sofia aliondoka na binti yangu aliyeitwa Moyo.ย
Nilibakia pale kwenye kiza, Maaskari walinichukua naย kunirudisha kwenye chumba changu! Nilikuwa nikiishi kwenyeย chumba cha peke yangu kutokana na kesi ya mauwaji iliyokuwaย ikinikabili, Moyoni nilijisema kuwaย
“Sipaswi kuwa huru” niliketi kwenye pembe ya kile chumbaย kilichojaa wadudu wadogo wadogo, chini kulikuwa na majiย yaliyomwagika, niliyamwaga mwenyewe kwasababu sikupenda kula.ย Kuna wakati niliwahi kumwambia Askari aliyekuwa akinihudumiaย kuwaย
“Niletee sumu nife, sipendi kuendelea kukaa hapa”ย
“Veronica, Bado hii kesi ni mbichi sana. Subiria hukumu yakoย , Kama Mahakama ikikukuta hauna hatia? unataka kufa ili bintiย yako alie kwa uchungu?” aliniulizaย
“Usiwaze kufa, hakuna anayeijua kesho yako” alisema naย kuondoka zake.ย
Sikuona umuhimu wa kuendelea kuwa hai tena nikiwa paleย gerezani kama Mahabusu niliyekuwa nasubiria siku ya hukumu yaย kesi yangu ya Mauwaji
“Ni kweli umemuuwa Mama yako Mzazi?” yule Wakili alirudi tenaย kuutaka ushahidi ili ajuwe namna ya kunitetea, Wakili huyuย aliajiliwa na Mama Sofia ambaye alikuwa jirani yangu mwema,ย alipenda kuniona nikishinda ile kesiย
“Nikikwambia nilimuuwa utaiambia nini Mahakama? Utaidanganyaย kuwa sijauwa?”ย
“Ukiniambia ukweli nitajua jinsi ya kukuweka huru Veronica”ย
“Uhuru sio kitu ninachokitaka kwasasa, naitaka haki tu”ย nilisema kisha nilikaa kimya sikutaka kuendelea kuzungumzaย nae hadi Muda ulipoisha nilirudishwa tena kwenye kile chumba.ย
Yule Wakili alimpelekea taarifa Mama Sofia, Mama huyu alikuwaย tajiri sana. Alikuwa jirani yangu kule Mbezi Luis nilipokuwaย ninaishiย
“Ninavyomjuwa Veronica hawezi kumuuwa Mama yake Mzazi Jacob”ย alisema akimuelekeza yule Wakili..ย
“Veronica ni mpole, mcheshi na mtaratibu sana…kusemaย amemuuwa Mama yake hilo haliwezekani kabisa”ย
“Unafikiria nitafanya nini na hataki kuzungumza kabisa,ย amekaa kimya?”ย
“Veronica sema ukweli, angalia ulivyodhohofu…Mwanao analiaย na kukuulizia utarudi lini, hivi ni kweli hutaki kuishi tenaย na binti yako Moyo?” Mama Sofia aliongea Baada yaย kunitembelea, ni kweli nilikuwa nimekondeana sana, Mwiliย ulidhohofu mno, Afya yangu ilikuwa mbaya!ย
Mawazo yalipelekea nidhohofike namna ile, kingine niย mazingira ya pale ambayo hayakuwa rafiki kabisa kwangu!ย
“Mahakama itatenda haki kwangu Mama Sofia, Mungu ndiyeย anayejua kilichojificha” nilisema kwasababu sikupenda kabisaย kuzungumzia jambo lile lililotikisa vichwa vya Watu wengiย sana.ย
“Kwanini hutaki kusema kama kweli umeuwa au haujauwaย Veronica?” Alihoji lakini sikumpa majibu kila alipokuja yeyeย au Wakili wa ile kesi.ย
Tukio hili lilitokea Mwaka 2009, lilizua gumzo kubwa, hakunaย aliyeamini kama kweli Nimemuuwa Mama yangu. Ni kweli nilikuwaย nimemuuwa Mama yangu Mzazi na chanzo cha tukio hili alikuwaย ni Mume wangu aliyitwa Jonas.
Baada ya siku 21 nilirudishwa tena Mahakamani ili kusikilizaย kesi yangu iliyojaza waandishi wa habari, kurasa zote zaย Magazeti zilipambwa kwa picha yangu na maelezo juu ya tukioย langu la Mauwaji.ย
Hakimu alinitazama kabla ya kuanza ile kesi, jicho lakeย lilijaa huruma ambayo niliweza kuiona pindi nilipogongana naeย macho, nilimuona akitoa kitambaa chake na kufuta choziย lililokuwa likimbubujika. Mahakama ilizizima kusikilizaย atasema nini, niliweza kuzisikia pumzi zangu nilipokuwaย nikihema ilitokana na ukimya uliotawala pale Mahakamani.ย
Nilipotazama pembeni nilimuona Mwanangu Moyo, aliniangalia naย kutabasamu na kunifanya na Mimi nitabasamu.ย
Kila Mtu alikuwa kimya, wengine wakinitazama Mimi na wengineย wakiwa wanamtazama Hakimu aliyekuwa amejiinamia kwa zaidi yaย dakika 10, sikujua alikuwa akifikiria nini.ย
“Veronica!” aliniita yule Hakimu mwenye umri mkubwa, alivuaย miwani yake na kunitazama tenaย
“Abee!”ย
“Uko tayari kusema ukweli?” aliniuliza, nilikaa kimya kwaย dakika moja kisha nilimpa jibuย
“Ndio”ย
“Ilikuwaje ukamuuwa Mama yako Mzazi?” alihoji tena,ย nilimtazama Mama Sofia ambaye alinipa ishara niwe jasiriย niseme.ย
Alitamani kusikia nikikanusha kuwa sijamuuwa Mama yangu, Watuย wote wakawa bize kunitazama, waandishi wa Habari walitegaย karamu zao kwenye karatasi ili wapate cha kuandika kwenyeย Magazeti yao.ย
Nilianza kwa kigugumizi, pale pale chozi lilianzaย kunibubujika, midomo yangu ilikuwa ikitetemekaย
“Nisamehe Mwanangu Moyo” nilisema huku nikiwa ninalia,ย niliendeleaย
“Ni kweli nimemuuwa Mama yangu Mzazi” kauli hii iliwashtuaย wengi, Hakimu alionekana kuvunjika moyo kabisa aliinamishaย kichwa chake chini huku akijifuta Machozi.
Nilianza kueleza kilichotokea, Naitwa Veronica Moyo, najuaย wengi mmeshtushwa kusikia nimemuuwa Mama yangu, baada yaย kueleza haya naomba Mahakama inihukumu kifo.ย
MIAKA MINGI KABLA YA TUKIOย
Nilipofika chuoni kusomea masuala ya Utalii nilikutana naย Mwanaume aliyeitwa Jonas, nilitokea Kumpenda nae piaย alinipenda sana lakini hofu yangu ilikuwa kwenye maumbileย yangu, nilihofia kumwambia Jonas kuwa nimekeketwa na huoย ukawa udhaifu wangu katika Maisha yangu.ย
Kila nilipo kumbuka juu ya kile kitendo cha kukeketwaย nilijisikia vibaya sana lakini kwa kipindi chote hichoย nilikuwa bado sijawahi kukutana na Mwanaume na kufanya naeย mapenzi.ย
Jonas ni binadamu mwenye hisia kama Wanaume wengineย alionekana kuanza kukata tamaa kila nilipompa visingizio kuwaย nipo kwenye siku zangu, naogopa Mimba au tutafanya tukimalizaย chuo.ย
Nilimsikia rafiki yangu aliyeitwa Konzo akisema kuwa naendaย kumpoteza Jonas siku za usoni kwani hawezi kukaa bila kusexย na mimiย
“Ooh! amekwambia hivyo?”ย
“Ndio, anataka kujua ni kwanini humpi tendo…Mwaka wa piliย sasa”ย
“Sikia Konzo, naogopa Jonas atanikimbia akishakula tundaย langu”ย
“Hofu yako haina msingi, haishawishi kabisa Veronica au weweย ni msichana bado?” Aliniuliza, sikuwahi kumwambia kuwa mimiย ni Bikra nikaona ni vema nimwambieย
“Ndio, mimi ni Bikra na sijawahi kushiriki tendo na Mwanaume” “Unasema kweli? Jonas anajua?”ย
“Hajui konzo na sitaki ajue kwasasa, acha iwe siri bainaย yetu” Nilimueleza hivyo, kitendo cha kukeketwa kilinifanyaย nikose kujiamini kwasababu niliwahi kusoma majarida kadhaaย yanayozungumzia suala hilo kwa Wanaume, wengi wakisemaย Wanaume hawapendi Wanawake waliokeketwa kwa madai kuwa sioย Watamu.
“Sawa nitaitunza Veronica na sitamwambia Mtu hapa Chuoni”ย Alisema na kunifurahisha Konzo, siri ya kukeketwa ikabakiaย kwenye nafsi yangu!ย
Nilipomwambia Mama yangu Mzazi aliniambia kuwa nikionaย Mwanaume anasema hapendi Mwanamke aliyekeketwa basi Mwanaumeย huyo hajui nini maana ya Mapenzi wala radha ya tendo haijuiย vizuriย
“Mama! mbona wataalam wanathibitisha kuwa kukeketwaย kunamfanya Mwanamke akose radha halisi?”ย
“Mtaalam gani huyo anayeshindana na mababu wa Kabila letu?ย Sayansi inakupoteza Mwanangu” Maneno ya Mama yaliniweka njiaย panda kwa kipindi kirefu hasa baada ya kuvunja ungoย
Niliishi na Mawazo ya aina mbili, Sikujua nimfuate nani katiย ya Mama yangu au Wataalam walioandika majarida yale. Nikasemaย ipo siku nitaujua ukweli ingawa sikutaka kumpoteza Jonas,ย Mwanaume mzuri wa sura, alitokea kwenye maisha bora sana,ย Mcheshi na mkarimu. Alinisaidia Mambo mengi sana tukiwaย chuoni.ย
Alinipa robo ya pesa alizotumiwa na Wazazi wake wakati Mamaย yangu Mzazi akinihimiza kuishi kulingana na mazingira, hakuwaย na uwezo wa kunisomeshaย
“Veronica Mwanangu! Nenda kasome huko lakini tambua kuwaย Maisha ni magumu mno, nitakachopata nitakituma kwako naย nikikosa ishi kulingana na mazingira” alisema Mama nikiwaย ninaenda kujiunga na Chuo Jijini Dar kutokea Arusha.ย
“Sawa Mama! nitatimiza malengo yangu na ya kwako, nitaishiย kama ulivyoniagiza” Jinsi alivyonilea ilikuwa ni rahisi sanaย kukubaliana na hali zozote za kimaisha, Baba yanguย alitutelekeza nikiwa mdogo, Kwa mujibu wa Mama alisema kuwaย Baba alikimbia madeni yaliyokuwa yakimuandama.ย
Pale chuoni kwetu wengi walinifahamu, na msemo ulikuwaย ukitamba sana ni ‘Tazama Pisi kali ya Arusha ile’ ulikuwa niย msemo uliopendwa, nilikuwa mzuri, macho makubwa yakukonyeza,ย shepu ilikuwa ya kawaida tu lakini ilitosha kunifanyaย nikamilike sana, Mapedeshee waliokuja kutafuta Wanawakeย wazuri pale chuoni hawakuacha kunisumbua kila wakatiย waliwatuma rafiki zangu akiwemo Konzoย
“Una bahati sana Veronica, mabosi wanakuulizia wewe tu”ย alisema rafiki yangu Konzo, alinichekesha mno
“Sasa Bahati au usumbufu? ni kheri wewe unaishi upendavyoย kuliko mie ”ย
“Ningekuwa ndio wewe! ningeshapata gari maana Mabosi wakoย tayari kukupatia upendacho” Nilitamani sana Maisha mazuriย lakini ile siri ya kukeketwa niliogopa itasambaa pale chuoniย ndio maana nilihakikisha namkataa kila aliyenitongoza.ย
“Huyu Mwanamke anaringa sana hapa chuoni sijui anajikuta naniย yaani” Ni miongoni mwa kauli nilizowahi kuzisikia kutoka kwaย Baadhi ya Wanaume walionikataa, niliona ni bora wasemeย naringa kuliko ile siri ifahamike kwenye hadhara.ย
Jonas alifanya kila mtego ili nifanye nae tendo lakiniย nilikuwa makini kuhakikisha namaliza kwanza chuo ili hataย kama akijua mbele ya safari sitapata aibu kama ambayoย nitaipata nikiwa bado chuoni, alinitoa Out kila mara.ย
Konzo aliniletea majarida mbalimbali ili nijifunze jinsiย Mwanamke anavyotolewa usichana akiamini naogopa kufanyaย hivyo, aliniletea hadi video za ngono ili nishawishike! Ndio,ย zilinihamasisha sana na hofu yangu ikawa pale paleย
“Nimefanya jitihada zote Veronica, kinachokukwamisha niย usichana wako huo, unakosa madili ya pesa”ย
“Imeshakuwa Bwana Konzo, acha iwe hivyo hivyo wakati ukifikaย nitapata hayo madili”ย
“Tatizo lako wewe ni mbishi sana Veronica, jaribu usiseme tuย wakati…unaogopa utafikiria unataka kutolewa uhai?”ย
“Ha! ha! ha!”ย
Nilimzoea Konzo, siku moja Mwalimu Kasase aliniita ofisiniย kwake, alikuwa ni miongoni mwa Watu waliokuwa wakinitongozaย pale chuoni, nilipofika aliulizia kuhusu jibu lakeย nilimwambia aendelee kusubiria, alinielewa.ย
Basi Maisha ya Chuo yalikuwa matamu na ya kukera kwa wakatiย mmoja, kuna wakati nilisikia raha sana lakini wakati mwingineย nilikereka, likizo ilipofika nilirudi Arusha nikiwa msichanaย bado yaani Bikira. Pale nyumbani nilimkuta Mjomba yaani Kakaย yake Mama aliyeitwa Sanga.ย
“Eeh! Veronica umekuwa Mkubwa hivi?” aliponiona aliniuliza,ย niliishia kucheka tu maana ukubwa wa Mtu unaonekana kupitiaย kwa wengine, mimi nilijiona nipo vile vileย
“Huyu Mtoto kafanana sana na Baba yake”
“Sana, hasa anavyotembea kama anarudi vile”ย
“Ha!ha!ha!” Mama aliingiza utani wake kwa kilugha cha kwetu,ย tukawa tunacheka lakini Mjomba akionekana kama kunishangaaย sana hadi nikawa naona aibuย
“Msindikize Mjomba wako Kanisani” Alisema Mama baada ya sikuย mbili za kuwa Arushaย
“Ina maana Anko Sanga hakujui kanisani Mama? siku zote hizoย alizokaa”ย
“Mpeleke bwana!! Hakuwa na Mtu wa kumsindikiza huko, ukirudiย utayarishe chakula cha Usiku”ย
Basi, tuliingia kwenye gari lake tukaanza safari ya kuelekeaย kanisani kwetu, palikuwa na umbali kiasi, mwendo wa Kilomitaย 15 hadi kufika huko, palikuwa karibu na nje ya Mji wa Arushaย kulikuwa na hilo kanisa la Mzungu ambalo tangia nikiwa mdogoย nilikuwa nikisali hapo hadi nakuwa mkubwa.ย
“Kumbe ni mbali hivi?” aliniuliza tukiwa tumebakishaย takribani Kilomita 4, Kwa mbali mlima kilimanjaro ulikuwaย ukionekana kwa uzuri sana, tulipishana na magari ya Wataliiย waliokuwa wakielekea hukoย
“Umeshawahi kwenda kufanya utalii?” aliniuliza tena,ย nilitabasamu tu kwani sikuwahi hata kuusogelea ule mlima japoย nilizaliwa Arusha.ย
“Hapana Anko sijawahi kufanya utalii, ule mlima nauona kwaย mbali tuu” Mjomba alicheka sana akaniuliza kama ningependaย twende huko mlimaniย
“Ndio napenda”ย
“Nitaongea na Mama yako” alisema kisha tuliendelea na safariย ya kuelekea Kanisani, tulipofika nilimuacha akanipatia pesaย kama Elfu 50 hivi kisha akaniambia nisimwambie Mama Maanaย ataichukuaย
“Sitamwambia Anko”ย
“Haya natumaini mapishi yako yatakuwa Bul bul leo Veronica”ย
“Ha!ha!ha!” nilikuwa napenda sana kucheka nilikuwa siweziย kununa yaani, nilifurahi kisha nilipanda daladala na kurejeaย Nyumbani.
ย Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA PILIย
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapaย
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896ย
12 Comments
Woow inakujakuja vikee ๐ง
dadeq anko ankol ๐ซ ๐คฃ๐คฃ
Ni nzuri sana
Woooh
Ankolllll
nzuri
Ankol tena
Ni story nzuri inapendeza
Mzuri
Anko atuachie vero wetu bwana๐๐
Ankoo atuachie vero wetu bwana๐๐
ryoq5t