Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    ZAINABU ( 01)

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » AMRI KIEMBA : CHAMA Ni Aina Ya Wachezaji Wanaopotea, PACOME Ni Wa Kisasa Zaidi
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    AMRI KIEMBA : CHAMA Ni Aina Ya Wachezaji Wanaopotea, PACOME Ni Wa Kisasa Zaidi

    MhaririBy MhaririDecember 7, 20232 Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Mchambuzi wa soka na mchezaji mkongwe wa Tanzania, Amri Kiemba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameamua kuibuka na kutoa maoni yake kuhusu kile kinachoendelea kushindanishwa kati ya ubora wa mchezaji wa klabu ya Yanga Pacome pamoja na mchezaji wa Simba Clatous Chama.

    Kupitia kurasa zake, Kiemba ameandika

    Hivi karibuni kumekuwa na mijadala kadhaa mitandaoni kuhusiana na Wachezaji Clatous Chama wa Simba SC na Pacome Zouzoua wa Yanga, wengi wanabishana na kutaka kujua nani bora zaidi ya mwenzake.Mashabiki wengine wakienda mbali zaidi na hata kuniuliza, kama mimi ningekuwa Kocha na niko nao wote kikosini nitaanza na mchezaji gani kati ya hao wawili.

    Kwangu mimi binafsi huu ni mjadala wenye tija kwa ambao wameamua kujadili hili, mimi sioni kama hawa ni wachezaji wa aina moja kuwalinganisha, nadhani unaweza kuwashindanisha Wachezaji kutokana na nafasi wanayocheza lakini hawafanani kwa maana ya utekelezaji wao wa majukumu.

    Chama ni aina ya Wachezaji ambao kwenye soka la sasa hivi wanaanza kupotea kwa maana wale wachezaji ambao walikuwa wanacheza huru timu inapokuwa na mpira, hawa ni Wachezaji wanaoanza kupotea kwenye uchezaji wa sasa.Wakati Pacome ni mchezaji wa kisasa ambaye anaweza kufanya majukumu yote mawili kwa wakati mmoja, anaweza kuchezesha timu na anaweza kukusaidia timu kuweza kupata matokeo na anaweza kukusaidia kujilinda kama namba sita, Pacome anabadilika kutokana na eneo na vipindi.

    Kipindi ambacho timu ina mpira Pacome anaweza kuwa namba 6, 8 na anaweza kuwa namba 10, wakati timu haina mpira Pacome anaweza kuwa namba 6 halisi akazuia kama ambavyo namba 6 anafanya na pia anaweza kuwa namba 8 wa kisasa.Ukitaka kuchagua nani zaidi itabidi uchague kipengele ambacho wote wanakifanya vizuri ambacho ni uimara wao, usichukue udhaifu wa mmoja na kulinganisha, kwangu mimi kila mmoja ana ubora wake kulingana na eneo lake ambalo yuko bora zaidi.

    Pacome anaweza kumshinda Chama kwenye vitu vingi ndani ya kiwanja kimbinu kwa sababu anaendana na mchezo wa kisasa lakini Chama linapokuja suala la timu ina mpira na anatakiwa kufanya ubunifu, basi amekuwa akifanya kwa asilimia zaidi ya 80 isipokuwa kwenye kujilinda labda anatumia asilimia 20 kushuka chini, wakati Pacome anafanya kwa ubora ule ule, tukisema nani ni bora tutafute mchezaji ambaye wanaendana sifa na kuweza kupata mchezaji bora ila mimi naona wote wazuri.

    Kwako limekaaje kama mdau wa mpira wa miguu __?

    amri kiemba chama simba pacome yanga
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views
    Ligi Kuu ya NBC

    RATIBA YA LIGI KUU YA NBC MSIMU WA 2025/2026

    August 29, 202513K Views
    Don't Miss
    Hadithi March 23, 2026

    ZAINABU ( 01)

    NAITWA ZAINABU ALIYU! Hii ni Hadithi ya Maisha yangu…..!!  Mimi ni Mtoto wa kwanza kati…

    Mkeka Wa Leo Jumatatu 16/03/2026 Wa Magoli OVER 1.5

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (09)

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua

    Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua SEASON 2 (08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.