Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Nane-08)
    Stori Mpya

    Nyumba Juu Ya Kaburi (Sehemu Ya Nane-08)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaMay 3, 2025Updated:May 3, 202537 Comments10 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 07

    Hatimaye Mama yangu aliungana na Zena na Caren kwenye makazi ya milele. Kilichokua  kimebakia kwangu kilikua fumbo kubwa, hakuna aliyejua kuhusu ile nyumba yenye kaburi na  jini anayeuwa. 

    Sikutaka kumwambia yeyote, moyo wangu ulijawa na kisasi. Sikuuona umuhimu wa kuendelea  kuishi ikiwa nimepoteza Wapendwa wangu kwa usiri wangu. Baba alifikishwa Mahakamani siku  Nne baada ya kumzika Mama, alikiri mbele ya Mahakama kua alitenda Mauwaji hayo kwa  mikono yake kwa kile alichokiita wivu wa Mapenzi. Endelea

    SEHEMU YA NANE

    Baba alivikwa kofia ya Muuwaji, alisemwa na kutukanwa kila kona. Hatimaye alihukumiwa  Miaka 13 jela ka kosa hilo, kutokana na Umri wake ilikua rahisi kusema alikua anamalizia  Maisha yaliyobakia akiwa gerezani. Siku moja nilimtembelea gerezani, sikuwahi kuzungumza  naye tangu tulipoachana siku ile ya kifo cha Mama kule Hospitali. 

    Japo alikua gerezani lakini Baba alitabasamu mbele yangu na kuniita

    “Mwanangu Celin” kisha alinikumbatia kwa hisia ya furaha sana ya kuniona, alinishika mabega  yangu akaniambia 

    “Siku moja utakua Mama, utakua na Watoto ndipo utajuwa nini Maana ya kua Mzazi. Sijali ni  shida kiasi gani nitazipata Mwanangu lakini furaha yangu ni kukuona ukitabasamu siku zote,  ukiwa huru kama kijana na kutimiza ndoto zako” Nilifumba macho kwa hisia ya maumivu  makali ya moyo, maneno ya Baba siyo tu yaliniumiza bali yalinifundisha nini Maana ya kuwa Mzazi. 

    “Usilie Celin, Mimi Baba yako nitakuombea kila dakika iendayo, kamwe sitakuacha Upotee.  Wewe ni Jasiri Celin, unaweza kulimaliza hili, hata kama hautanitoa hapa lakini utapigana hii  vita na kulipa kisasi cha Wazazi wako, rudisha ile nyumba mikononi mwako, ni jasho langu  nililolipigania Ujana wangu wote” nilishusha pumzi zangu, Baba alikua akizungumza maneno  katili sana lakini yalikua yakinipa ujasiri na kunikumbusha kua nimebakia peke yangu nje ya  Dunia yake, nje ya Dunia ya Mama yangu. 

    “Pale chumbani kwangu kuna kabati dogo, nimehifadhi kadi yangu ya Benki. Kuna pesa ya  kukusaidia Binti yangu, namba ya siri ni Mwaka wako wa kuzaliwa. Usirudi hapa hadi uwe  umelipa kisasi, umerudisha kila kitu. Ikiwa umeshindwa basi nenda mbali na Dunia yangu  Celin” alisema Baba kisha alinionesha sura katili sana, akageuka na kuondoka akiongozwa na  Askari magereza. Aliniacha nikiwa nimesimama 

    Baba yangu hakuniaga, aliondoka mbele ya macho yangu mithiri ya Barafu juani, aliniachia kazi  nzito sana. Nilimshukuru Mungu kwa baraka ya uzima na uhuru, nilirudi nyumbani kwa  mjomba. 

    Jioni nilimueleza Mjomba wangu kua ninarudi nyumbani, alikua na wasiwasi na maswali mengi  lakini nilimueleza jambo moja kua, siwezi kuikimbia nyumba yetu. Huzuni zitanifuata na  zitaondoka zenyewe, Mjomba Mgina aliniruhusu nirudi nyumbani japo alijua nitaishi peke  yangu.  

    Kesho yake Asubuhi nilikodi Bajaji ili nirudi nyumbani, moyo wangu ulipasuka, ulikosa Uwoga  tena, nilijua naenda kwenye nyumba ya namna gani. Nikiwa ndani ya Bajaji safari ikiwa  imeanza, nilianza kuihisi hali ya tofauti sana ambayo mara kadhaa niwapo hatarini huwa naihisi. 

    Kichwa kilianza kua kizito ghafla tu, masikio yalikua yakipiga kelele mithiri ya filimbi  ikipulizwa ndani ya sikio langu. Mwili ulikua ukinisisimka sana, nikamuuliza dereva wa Bajaji 

    “Unaihisi hali ya tofauti?” akacheka kidogo akaniuliza 

    “Hali ipi hiyo?” swali lake lilikua ni jibu tosha kua alikua katika hali ya kawaida tu wala  hakuhisi kama ninavyohisi, nilijiinamia huku nikiwa nimeziba masikio yangu. Bajaji ilikua  ikiendelea na safari, mara nilianza kusikia Honi ya Bajaji ikipigwa sana na yule dereva,  nilistajaabu.

    Wakati nanyanyua kichwa changu niangalie mbele nilisikia sauti moja ya kishindo, nikajigonga  mahali na kuumia. Bajaji ilikua imetumbukia mtaroni. Halafu yule dereva akawa wa kwanza  kutoka kisha akanitoa na Mimi kwenye bajaji iliyolala mtaroni upande, nilimuliza 

    “Imekuwaje?” nilikua na maumivu makali kwenye kiwiko cha mkono wa kulia, yule dereva  akaniambia 

    “Nilimwona Bibi mmoja akiwa amesimama barabarani, nilipojaribu kumkwepa ndio tumepata  ajali” nilivyosikia tu kuhusu Bibi, nikajua ni yule jini ananiwinda animalize. Sikutaka kuuliza  chochote tena, nikamlipa pesa yake ya safari hata kama hatukufika mwisho wa safari, kisha  nilichukua begi langu la mgongoni nikaanza kutembea kando ya Barabara. 

    Kichwa kilikua na mawazo tele, nilijitahidi sana kujiambia kila kitu kitakua sawa lakini nilikua  ndani ya vita kali ya Mimi na Mimi, nilijua ninachojiambia kilikua kigumu sana lakini  niliendelea kujiaminisha huku nikitembea. Akili yangu ilihama kabisa nikaanza kuwaza mambo  mengine ya Kutisha, ghafla nilisikia honi ya pikipiki nyuma yangu. 

    Ile nageuka tu naiyona Pikipiki ikija kwa kasi ikielekezwa kwangu, macho yalinitoka.  Nilikubaliana na akili yangu kuwa siwezi kuikwepa na ilikua hatua chache kunifikia, nilifumba  macho yangu nisione namna mwili wangu utakavyovamiwa na ile pikipiki. Ghafla nilihisi  kuvutwa nikajikuta pembeni ile pikipiki ikapita kama Mshale wa masafa marefu. 

    Nilishtuka sana, mkono wa Mtu mwingine ulikua umenishikilia. Niligeuka haraka kumtazama  aliyenisaidia nikakutana na yule Mwanaume aliyekufa na kuzikwa ndani ya nyumba yetu.  Nilishtuka sana lakini akanipa ishara ya kutulia, kiukweli moyo wangu ulikua unaenda mbio  sana. Macho yalinitoka nikiwa ninahema na kumeza mate kupitia koo langu kavu.  

    “Shiii‼ usiogope Celin” alianza kusema kisha aliniambia nimfuate, nilisimama nikiwa  ninamwangalia akitembea. Nilijiuliza maswali mengi ya haraka lakini jibu nililolipata ni  kumfwata maana ndiye Mtu pekee anayeweza kunisaidia. 

    Alinisogeza mahali nikiwa nimebeba begi langu la Mgongoni,alisimama mbele ya gari moja  akaniambia 

    “Ingia kwenye gari nitakupeleka” niliikunbuka ile gari, ni ile ambayo siku ya kwanza tunaonana  alinipakia kisha alitoweka nayo. Alinisistiza kwa ishara ya mkono kua niingie ndani ya gari,  nilijiuliza mara mbili mbili kabla ya kufungua mlango wa gari na kuingia ndani ya gari,  nilipofunga mlango alianza kusema 

    “Amedhamiria akumalize, ameshaiona hatari kwako” alisema kwa sauti iliyojaa vituo vituo huku  akiwa anadadisi nje ya gari kupitia kioo. 

    “Kama wewe Kaka yangu una nguvu za ajabu kwanini usipambane naye, mimi sina nguvu ya  aina yoyote ile” nilisema, alinitazama kisha baada ya sekunde kama kumi na tano hivi 

    akaniambia “Nimekuchagua sababu una ujasiri ndani yako, unafikiria wamepita wapangaji  wangapi kwenye ile nyumba? Wote wamekufa vifo vinavyofanana” 

    “Nani anaimiliki na kwanini anaipangisha wakati ni nyumba iliyojaa mauzauza?” 

    “Yule jini ndiye anayeimiliki baada ya kumuuwa Baba yetu. Kila anayepangishwa pale anaishia  kufa kifo kibaya sana, hakuna aliyewahi hata kupata muda wa kuchunguza chochote kile,  walikufa kikatili sana. Sijui wewe ni Binadamu wa aina gani ambaye uliweza kuichunguza ile  nyumba. Yule jini amekua akijigeuza kwenye sura ya Baba na kutafuta dalali kwa ajili ya kuiuza  au kuipangisha lakini wote walifia mle” alisema huku akitumia mikono yake kumaanisha  alichokua anakisema 

    “Bahati nzuri ni kwamba pana uvumi mkubwa wa watu kupotea ndani ya ile nyumba, lakini kwa  yeyote anayefwatilia hukuiona cha Mtema kuni.” Alisema kisha aliwasha gari, safari ilianza. Aliniacha na maswali mengi sana kichwani kwangu, sikujua niseme nini na nini Nnyamaze 

    “Nimepoteza kila kitu maishani, sina thamani. Mimi ni chanzo cha maafa yote, laiti kama  nisingeliikubali ile nyumba pasingelitokea maafa yoyote yale” nilisema huku nikitokwa na  machozi. Yule Mwanaume aliyeniambia kua ni Mfu alikua akiendesha lile gari kwa mwendo wa  kawaida. 

    “Usijali Celin, giza totoro ni ishara ya mapambazuko. Kila kitu kitakuwa sawa” aliniambia 

    “Hata kama kila kitu kitakaa sawa sitaweza kumrejesha Mama yangu, sitaweza kumtoa Baba  yangu jela, pia siwezi kuwarudisha Zena na Caren. Nimepoteza furaha, nimebakia kopo tupu”  nilizidi kutokwa na Machozi huku nikiitumia mikono yangu kufuta chozi langu. 

    “Kila jambo hutokea kwa sababu Celin, Mungu alikuleta hapa ili umalize kila kitu” aliendelea  kusema, maneno yake yalijaa faraja lakini nafsi yangu ilitawaliwa na kutu ya kutosha kiasi  kwamba nilihitaji tumaini zaidi ya maneno matupu.  

    “Sijui naanzia wapi namalizia wapi, napambana vipi?” nilimuuliza, akanijibu  

    “Nitakueleza namna ya kufumbua hili fumbo Celin, kwasababu una hiyo shanga mkononi,  hawezi kukudhuru kwa chochote labda amtumie Binadamu kama alivyofanya kuwatumia wazazi  wako kukudhuru wewe. Unatakiwa kwenda kwenye chumba ambacho sauti ya Dada yangu huwa  inasikika, hakikisha unakaa humo hadi mlango ufunguke, ukiweza kuingia ndani ya shimo  ndimo lilimo kaburi la Dada yangu. Mwambie Haji amekutuma umsaidie kutoka ndani ya lile  kaburi, ukiweza kumtoa ndio mwarobaini wa hili tatizo Celin, tutaunganisha nguvu zetu na  kummaliza yule jini, tutakuachia nyumba kwa amani na utaishi kwa amani zaidi bila tatizo  lolote” alisema. 

    Haikua rahisi kuingia ndani ya nyumba ile, niliyoyaona kwa yule jini yalinifanya niingiwe na  hofu kubwa, alikua akiniwinda sana aniuwe lakini nilikua nanusurika. 

    “Najua una hofu lakini gharama ya kumtoa Dada yangu ni ndogo zaidi ya utakachofanyiwa na  yule Jini, atakuandama Maisha yako yote wewe na kizazi chako. Hamtaishi kwa amani hadi  atakapo hakikisha amekumaliza Celin, vaa ujasiri. Mimi siwezi kurudi ndani ya ile nyumba,  nguvu kubwa inanizuia Mimi kukanyaga ile ardhi na siwezi kupambana nayo, wewe unaweza  kuingia ndani ya ile nyumba sababu ni Binadamu” alizidi kunipa moyo na ujasiri niweze  kiifanya kazi ngumu iliyo mbele yangu. 

    Alipokaribia karibu na nyumbani alisimamisha gari mita kadhaa akaniambia 

    “Hapa ndiyo mwisho wangu, siwezi kusogea zaidi na kama nitakua mbishi basi nafsi yangu  itaangamia na huu mpango hautafanya kazi tena. Nenda Celin, unaweza” alisema kwa ujasiri na  hamasa ya hali ya juu sana. Nilihema kwa nguvu ili nijiandae kuteremka ndani ya gari 

    Nilifungua kioo, palikua kimya. Nilisadiki maneno ya huyu Mfu kua yule jini alikua anauwa  Watu wa nyumba jirani. Upepo wa taratibu ulikua unasomba majani makavu yaliyoanguka  barabarani, alinitazama tena akanipa ishara ya kichwa kua niende. Niliteremka kutoka ndani ya  gari nikiwa nina hofu sana, nilimaliza miguu yote. Mwili wangu ilikua nje ya lile gari la maajabu  ambalo baada ya Mimi kushuka lilipotea tena katika mazingira tatanishi. 

    Safari hii sikushtuka tena sababu nilishaambiwa mengi, nilitembea taratibu kama Mtu mwenye  vidonda mapajani, akili yangu ilitaka kwenda lakini moyo wangu ulikua ukidunda kwa hofu  huku ukiniambia nirudi naelekea kwenye hatari. 

    Nilitembea hivyo hivyo huku picha halisi ya namna nilivyomuuwa Mama yangu ikiendelea  kupita akilini, ilinipa uchungu, nilimkumbuka Baba yangu pia. Yupo Magereza kwasababu  yangu Mimi, kauli zake za mwisho zilijirudia. Nilijipa moyo na ujasiri uliendelea kunivaa kadili  nilivyokua napiga hatua kuielekea nyumba yetu. 

    Sauti ya ajabu ya kunong’ona ilikua ikiniita jina langu, nilihisi sauti hii ikitokea kila kona. Sauti  ilikua ya yule Bibi Kizee jini, aliniita huku akicheka kwa sauti kubwa sana.  

    Sikujali vitisho vyake, nilitaka kumaliza mchezo wote ili Mama yangu apumzike kwa amani, ili  nitimize alichoniambia Baba, pia niipate nyumba ya ndoto ya Baba yangu japo alikua gerezani.  Hivyo vitu vitatu vilinisukuma hadi nililifikia geti 

    Sauti ilizidi kusambaa kila kona, haikua sauti moja pekee bali zilikua sauti nyingi, niliisikia sauti  ya Caren na Zena, nilikua nawasikia wakiniita. Niliogopa lakini sikua na sababu ya kurudi  nyuma, sikutaka hata kutazama nilipotoka ili nisije kupata woga zaidi. 

    Nilijua ilikua ni hatua muhimu sana maishani mwangu, ilikua ni hatua ya jasho na damu.  Nilipaswa kuwa askari ndani ya Uwanja wa vita, nilizidi kutetemeka, nilipolifungua geti nilihisi  hali ya utofauti kabisa 

    Palikua na ubaridi wa ajabu halafu sauti za maongezi yangu ya mwisho na Caren zilikua  zikisikika, Caren alivyokua akiniambia kua anaondoka Usiku ule. Chozi lilinivuja, nilifuta chozi 

    langu, palikua na nguvu kubwa sana iliyokua ikinivuta kuelekea ndani ya nyumba yetu. Nywele  zilikua zinahesabika kama vile zinanyonyoka. 

    Hakika nilikua katika nyakati ngumu zaidi kuwahi kupita kwenye maisha yangu. Hapakua na  yeyote pembeni yangu, nilipoinua macho baada ya kujifuta mchozi nilimwona Mama yangu  Mzazi kitu ambacho kilinishtua sana. Mtu ambaye tulimzika siku chache zilizopita alikua  amesimama mita kadhaa karibu na Bustani ya Mauwa. 

    Alikua amevalia mavazi meupe kama ambavyo inasemekana Malaika huvalia, alikua msafi sana  kiasi kwamba alikua aking’aa mithiri ya Kioo juani, halafu alikua akitabasamu sana. Macho  yalinitoka nikimtazama Mama yangu, nilijua Mama yangu amerudi kunisaidia kwenye hii vita.

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TISA

    COMMENTS ZIWE NYINGI SASA 

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896 

    Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx

    riwaya mpya riwaya za kijasusi

    37 Comments

    1. Mwanah on May 3, 2025 6:34 pm

      Maskin weee😎😎

      Reply
      • Emily on May 3, 2025 8:18 pm

        Mmmhhhh?!!

        Reply
      • Sajidu idrisa on May 4, 2025 10:01 am

        Sehem ya tisa inatok lin asee simuliz ni nzur saan

        Reply
    2. Lus twaxie on May 3, 2025 6:35 pm

      Jmn admin iweke next

      Reply
    3. Warda on May 3, 2025 6:37 pm

      Ohhh its hurts🥲🥲

      Reply
    4. Kson on May 3, 2025 7:01 pm

      Hatar sanah hii

      Reply
    5. G shirima on May 3, 2025 7:07 pm

      Malizia admin tamu sana

      Reply
    6. Neema Tesha on May 3, 2025 8:50 pm

      Aiseeeee ni maumivu sanaaa

      Reply
    7. Calvin paul on May 3, 2025 8:56 pm

      Adimini kuna buku la soda toa cha tisa

      Reply
    8. Sumaiya on May 3, 2025 9:03 pm

      Ooh mbn huzunii leta ya 9 admin

      Reply
    9. Fetty dada on May 3, 2025 9:41 pm

      Dah🤔

      Reply
    10. Çlãssïçjr_10 on May 4, 2025 3:16 am

      Mwaga ya tisa mkuu

      Reply
    11. KingzJeelay on May 4, 2025 3:54 am

      Oooooh my. God🥺🥺🥺
      Mola ampe ujasiri aumalize mtihani salama salmini🙏🏽🙏🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽

      Reply
      • Nailaty on May 5, 2025 5:11 pm

        Sehemu ya tisa jaman

        Reply
    12. KingzJeelay on May 4, 2025 3:55 am

      Kaka mkubwa eeeee 🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽🙌🏽
      Tupe ya9 chaaaaaàaaaaaaaaaaap🙌🏽🙌🏽

      Reply
    13. 🔒 Ticket; Process 1,489527 BTC. Confirm >> https://graph.org/Ticket--58146-05-02?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 🔒 on May 4, 2025 8:48 am

      1sre4a

      Reply
    14. Piana on May 4, 2025 11:18 am

      Next plz🙏

      Reply
    15. Chid boy on May 4, 2025 1:31 pm

      Noma Sana

      Reply
    16. Raymond on May 4, 2025 3:37 pm

      Vita inazidi kua nzitoo, story inazid kunoga aiseee

      Reply
    17. Yuster on May 4, 2025 9:48 pm

      Uchawi upo jmn tusimame na Mungu🙏

      Reply
    18. Pretty on May 5, 2025 12:02 am

      Next please🙏🏾

      Reply
    19. Nailaty on May 5, 2025 5:12 pm

      Tuletee sehemu ya tisa

      Reply
    20. 🔒 + 1.629600 BTC.NEXT - https://yandex.com/poll/HsemiBCtfopPhJGk2rGvc2?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 🔒 on May 19, 2025 12:14 pm

      owyijz

      Reply
    21. 🗒 + 1.402812 BTC.GET - https://yandex.com/poll/7R6WLNFoDWh6Mnt8ZoUfWA?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 🗒 on June 3, 2025 11:02 am

      gp0gsa

      Reply
    22. 🖲 Notification; Process 1,729375 bitcoin. Receive >>> https://yandex.com/poll/HsemiBCtfopPhJGk2rGvc2?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 🖲 on June 4, 2025 2:25 pm

      a8nu1n

      Reply
    23. ⌨ Notification- SENDING 1.972723 bitcoin. Withdraw =>> https://yandex.com/poll/5JjqQt7R61CTYdYVd17t6p?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& ⌨ on June 5, 2025 6:24 pm

      evpym9

      Reply
    24. 🔍 Email; Process 1,35245 BTC. Receive =>> https://yandex.com/poll/enter/BXidu5Ewa8hnAFoFznqSi9?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 🔍 on June 6, 2025 10:47 am

      z6rpeh

      Reply
    25. 🔓 Ticket: + 1,337375 BTC. Go to withdrawal > https://yandex.com/poll/enter/BXidu5Ewa8hnAFoFznqSi9?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 🔓 on June 11, 2025 5:25 am

      cs0m9n

      Reply
    26. 🗝 Reminder; + 1.760165 bitcoin. Verify =>> https://yandex.com/poll/HsemiBCtfopPhJGk2rGvc2?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 🗝 on June 15, 2025 9:54 am

      m7pu0d

      Reply
    27. 📆 + 1.528037 BTC.NEXT - https://yandex.com/poll/enter/12JSER8t8KDJewYyTprg7K?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 📆 on June 17, 2025 5:09 am

      pzhtkz

      Reply
    28. 🔓 Reminder- TRANSACTION 1,434989 BTC. Withdraw >>> https://yandex.com/poll/enter/FtVRYPu2WT9qLJ2WEoNw4E?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 🔓 on June 17, 2025 9:50 am

      h2aq45

      Reply
    29. * * * Get Free Bitcoin Now: https://www.omkarlabour.com/index.php?evz3v4 * * * hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7* ххх* on June 19, 2025 1:46 am

      76yu24

      Reply
    30. 💻 Email- TRANSFER 1,80082 BTC. Withdraw >> https://yandex.com/poll/enter/4Joc2mvUbapjsUMcMcKM3z?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 💻 on June 21, 2025 2:02 am

      9vnpie

      Reply
    31. 📬 + 1.865749 BTC.GET - https://graph.org/Payout-from-Blockchaincom-06-26?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 📬 on June 26, 2025 10:58 pm

      l7i66a

      Reply
    32. * * * Claim Free iPhone 16: http://tpk1.ru/index.php?5s7goc * * * hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7* ххх* on June 28, 2025 10:03 am

      fmij1v

      Reply
    33. 📉 Email- + 1.758388 BTC. Verify > https://graph.org/Payout-from-Blockchaincom-06-26?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 📉 on June 29, 2025 5:07 am

      xa4ywi

      Reply
    34. 📝 + 1.947486 BTC.NEXT - https://graph.org/Payout-from-Blockchaincom-06-26?hs=2c86f628f4e942bf6520c7758dc2d8e7& 📝 on June 30, 2025 7:18 am

      ddd9kl

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.