Ilipoishia “Alinivuta haraka sana kama vile Mtu aliyekua akijua anachokifanya, akili haikutaka kuendelea kufikiria, macho yalikataa kumtazama yule Mtu, sikujua alikua ni Askari au alikua ni Mtu wa aina gani, kitu pekee nilichokabakiwa nacho kwenye mboni za macho yangu ni Mgongo wake wenye makovu kadhaa.ย
Endelea Na Simulizi Hii Ya MSALA SEASON 2
SEHEMU YA KUMI NA MBILIย
โShit, unasemaje?โ Alihoji Rais Mbelwa, mbele yake alisimama IGP Hassan Kitulo.
โMasaa matatu sasa hawajafanikiwa kuupata mwili wake, inaonekana kuna Mtu amemsaidia na kumficha kwa siri ndani ya Msitu. Kibaya zaidi ni katika Msitu wa Magoroto MuhezaMkoani Tangaโ alisema IGP huku sura yake ikimea woga wa hali ya juu
โMshenzi weweโ akasema Rais Mbelwa kisha akamtandika kofi IGP Hassan Kitulo โElizabeth haijulikani kama kafa au yupo hai, Mtu pekee anayeweza kusema ilipo M21 mmempoteza kirahisi sanaโ alisema Rais kisha akashushia na mvinyo mkali ambao ulikua ukimsaidia kusukuma siku, kilikua ni kipindi kigumu kwao, hakuna aliyejua Benjamin alipotea vipi Msituni.
Msitu wa Magoroto ni miongoni mwa Misitu yenye maajabu, Msitu wa kutisha ambao watalii kadhaa waliwahi kutoweka na wasijulikane mahali ambapo walipo hadi hivi leo, watalii hao walitokea Uturuki. Kwa kipindi hicho Rais aliyekua madarakani alishirikiana na Serikali ya Uturuki kuwatafuta lakini hawakuonekana tena, zaidi ya Askari sitini waliotumwa Msituni walitoweka, Msitu huo ukapewa jina la Msitu wa ajabu, hakuna Binadamu anayeishi huko, inaaminika kuwa Mizimu na Majini ndiyo wanaoishi huko.
โMkuu operesheni ya kuhakikisha anapatikana imeshaanza kwa Helkopta kuzunguka juu ya Msitu na kumulika taa, nina imani chini ya Masaa ishirini na nne Benjamin atakua amepatikanaโ akasema IGP. Rais Mbelwa aliumamisha meno yake asijue aseme nini, alikua amechanganikiwa vya kutosha.
Usiku ulikua tayari umeingia, Rais akapoa kidogo kisha akatupa macho yake ukutani. โUna Masaa 24 tu ya kuendelea kuwa IGP, Kama hutompata yule Mwanaharamu basi acha kazi ukiwa huko hukoโ alisema kwa hasira huku akishupaza shingo yake ndefu iliyopambwa kwa cheni ya silva inayongโaa.
IGP akatoa heshima kwa Rais Mbelwa kisha akaondoka Ikulu, muda huo huo Rais Mbelwa akaelekea kwenye moja ya chumba kilichopo mita kadhaa kutoka Ofisini kwake, alipoingia humo akaufunga Mlango kwa funguo huku akitembea kwa jazba.
Ndani ya chumba alikuwemo Mke wake aliyepigika vya kutosha, alikua akimwagika damu usoni akiwa sakafuni, jicho moja lilikua limevimba, nywele zake zikiwa Tim-tim.
โWewe ndiye Chanzo, umeuza ramani ya Ikulu si ndiyo?โ alisema Rais Mbelwa kwa hasira akiwa amemwinua Mke wake, alikua ameshikilia nywele zake kisha akampa ngumi ya uso
โUtaniuwa, lakini kifo na Maisha yangu vitaandika Historia mpya ya Tanzaniaโ alisema huku akitoa udenda ulioambatana na damu nzito sana โKama unafikiria umeshinda basi nikwambie kuwa hiki ni kipindi cha pili cha mchezo, wanaharamu wote unaoshirikiana nao nitawatia nguvuni, huo utakua mwisho wakoโ alisema Rais Mbelwa kisha akamsukumiza Mke wake na kumgongesha ukutani kisha kwa hasira akaondoka ndani ya chumba hicho.
Masaa 72 yaliyopita ( Kabla ya Kizaa zaa )
Gauni fupi lenye kuwakawaka lilikua likisindikizwa na Dereva mmoja kuelekea ndani ya gari, walinzi wa kutosha wakiwa wanawatazama. Msichana Elizabeth aligeuka na kuitazama Ikulu ya Tanzania kisha moyoni akajisemea
โMoto ukishawaka, mtauzima kwa kazi sanaโ akatabasamu kisha akazama ndani ya gari, akaufungua mkoba wake, ndani mlikua na Flashi moja ya chuma, Mke wa Rais ndiye aliyeiweka kwenye mkoba wa Elizabeth. Ndani ya mkoba pia kulikua na karatasi, aliigeuza na kuanza kuisoma
โBinti, najua una jukumu zito sana lakini huna budi. Nimefanya yote sababu ya mateso ninayoyapitia, nimekubali kuvujisha taarifa nyeti ili Rais atoke madarakani, tambua kuwa endapo utashindwa basi vifo vyetu havitakua na Maanaโ ulikua ni ujumbe mfupi ambao Mke wa Rais aliuweka ndani ya Mkoba wa Elizabeth.
Msichana Elizabeth alimeza funda zito la mate kisha akakumbuka jinsi alivyokutana na Mke wa Rais kwa mara ya kwanza.
ELIZABETH ANAKUMBUKA
โGRII!! GRII! GRII!โ Ulikua ni Mlio wa simu ulikua unasikika, ilikua ni asubuhi moja iliyojaa ukungu wa Kutosha ndani ya Jiji la Mwanza, Elizabeth alikua ndani ya Jiji hilo kwa mapumziko. Alikua ndani ya Hoteli ya nyota tano iliyo kando ya Ziwa, macho ya Msichana huyu yaliyokua yamejaa usingizi yalianza harakati ya kufunguka ili kuisaka simu yake iliyokua inaita.
Haraka aliinasa ikiwa inakaribia kudondoka kutoka juu ya meza ndogo, mtetemo uliisukuma simu mbali kidogo, alimtazama Mpigaji, haikua namba aliyoifahamu. Akiwa kwenye tafakari aipokee au laa, simu ilikata.
โAaaahhhโ alipiga muhayo, akili yake ilishaamua kuachana na Usingizi, akafikiria kuketi, mara kidogo simu iliita tena akiwa anajiweka sawa, haraka akaitupia sikioni.
โNani?โ akatupa swali mara baada ya kupokea, akapiga tena muhayo uliosindikizwa na sauti yenye uchovu, haikutosha akapepesa macho yake huku akisubiria jibu kutoka upande wa pili, ukimya ilimwogopesha kidogo, akakitazama kioo ili kuiangalia tena ile namba. โNani wewe unapiga simu hauzungumzi?โ akangโaka Elizabeth akiwa anaweka vizuri nywele zake zilizoshuka hadi upande mmoja wa jicho la kulia
โElizabethโ uliita Upande wa pili tena ilikua ni sauti ya kiume iliyoonekana kuwa makini sana.
โNdiyo, unasemaje?โ alihoji kwa tahadhari sana.
โNataka kukupa kaziโ ulisema huo upande wa pili, yalikua ni maneno ambayo alizoea kuyasikia lakini alihitaji sana Umakini ili asije ingizwa Mkenge
โKazi gani?โ
โNataka uibe faili Ikulu kwa Rais Mbelwa, nitakupa maelekezo zaidiโ Elizabeth akacheka kwa kicheko kilicho jaa kebehi ya hali ya juu sana
โHivi unajisikiliza mwenyewe, Mimi nawezaje kuiba faili Ikulu, kwanza wewe ni Nani?โ aliuliza Elizabeth, upande wa pili uliachia kicheko kidogo
โElizabeth, pesa ipo ya kutosha sema unataka kiasi gani uifanye hiyo kazi. Nitakupatia michoro yoteโ ulisema upande wa pili, Elizabeth akatuliza kichwa chake
โUna uwezo wa kutoa Mabilioni ya pesa wewe?โ aliuliza
โPesa yoyote unayoitaka utapewa kikubwa Rais atoke Madarakaniโ ukashindilia upande wa pili, Elizabeth akaona jambo hilo halikua jambo la Mzaa na Mtu huyo alidhamiria alichokua anakisema.
โKuhusu kukuamini?โ akauliza Elizabeth
โNilitegemea swali kama hili, tunaweza kuonana kwanza kabla hatujafikia makubalianoโ ulisema Upande wa pili
โOkay! Nipe muda kutafakari nitakurudiaโ alisema Elizabeth kisha alikata simu huku akiwa kwenye Bumbuwazi, kwanza akapiga simu mahali
โMuhonzi, kuna dili lakini ni dili la kifo, narudi Dar Mchana wa leoโ alisema Elizabeth kwa kujiamini kabisa mara baada ya simu kupokelewa, kisha akaikata bila kusikiliza upande wa pili kwaniย Aliiona harufu ya Utajiri.
Mishale ya saa tano ilimkuta akiwa anamaliza kuweka nguo zake ndani ya Begi lake kubwa lenye Matairi, akalikokota akiwa anafunga zipu ya begi, akalivusha mlangoni kisha kwa haraka akashuka kwa kutumia lifti kuelekea chini, kichwa chake kilikua kinawaza kitita cha pesa atakachovuna, alijiamini anaweza kufanya kazi hiyo kwa mafanikio. Nini kitaendelea? Usikose sehemu ya 13 ya MSALA ndani ya SEASON 2ย
Je, Benjamin anaokolewa au anakielekea kifo?
Hatma ya Mzee Kimaro na Elizabeth itakuaje?
AHSANTE!! Kwa kua nami katika season ya kwanza ya Riwaya ya MSALA.
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA
17 Comments
Nzuri
Tuliiiimiss jamniiii,ninmoto sanaaa
Sehemu ya 13 tunaomba admin
Unyama ni mwingi
๐ฅ
Hii script lait ingekuwa Netflix ingekuwa Bonge la movie aise hongera sana.. Inavutia sana
Nitaipataje namm ndio nafungua hii
Habari.. Ingia Hapa Kusoma Ya Kwanza mpaka ya 11 https://www.kijiweni.co.tz/tag/msala/
Uuuuuuh jaman ๐๐ cjui nimuite jn gan anaetupa hizi stor anyway ni nzuri sanaa an na anajua uyo jamaaโฅ๏ธโฅ๏ธโฅ๏ธโฅ๏ธโฅ๏ธโฅ๏ธ
Yeah ni mtunzi mzuri sana kama kufikili yuko poa
Admin sehemu ya 13 tunaiomba
Kitu kimepangwa kikapangika, tupe mzigo admin
Aweeeh tulikaa kinyonge sana, usitupooze admin 13 please ๐ฅ๐ฅ๐ฅ
kwanini ingetolewa vidio nimependa
Enyeew hii ni movie tosha hongera sana
Admn mbona masala umestopisha
yphfaf