Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Wachambuzi Wanamuingiza Feitoto Kwenye Chuki
    Ligi Kuu | Soka la Bongo

    Wachambuzi Wanamuingiza Feitoto Kwenye Chuki

    MhaririBy MhaririJune 3, 2024Updated:June 3, 20249 Comments2 Mins Read763 Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Feitoto
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Lipo jambo hapa ambalo lazima tulizungumze, kuhusu mchezaji FEISAL SALUM na watu wa Yanga SC naamini wapo baadhi ya Wachambuzi wanamuingiza kwenye chuki bila ya yeye mwenyewe kujua.

    Kwanza, YANGA ni taasisi ambayo ni kubwa nchini lakini siyo tu hapa nje ya mipaka yetu kwaiyo siyo rahisi kwa mtu mmoja kuweza kushindana na kundi la watu wote hao.

    Kuondoka sehemu huwa haikatazwi lakini ukiendelea kutoa viashiria itaonekana ni kama una chuki na watu hao. Yanga SC ilivyomsajili Fei kutoka Singida hakuwa mchezaji maarufu lakini ukubwa wa Yanga ukampa jina mchezaji huyu na alipendwa sana ndani ya Klabu pale.

    Hili la baadhi ya Wachambuzi kukaa kando yake na kuzitumia kalamu zao kama kumtengenezea mafuta na maji siyo kitu kizuri, wapo wenye uelewa kuwa hii ni kawaida lakini wapo wengi akili zao wanazijua mwenyewe, mimi nafikiri wengemuacha Feisal Salum acheze mpira bila ya kumtengenezea chuki kama hizo.

    Yuko wapi BERNARD MORRISON ambaye naye alitengenezewa mambo kama hayo baadae ni kama ameuzika mpira wake. Kalamu zinaweza zikawa zinaandika lakini bila ya kutambua zinabomoa kwa kiasi kikubwa sana.

    Ushauri wangu kwa FEISAL SALUM Ligi zimemalizika ni muda sasa wa yeye kujitenga na hao ambao ni kama wameamua kuzicheza vita zao na Yanga kupitia mgongo wake kwani asipokuwa makini watamuingiza katika maisha magumu ya soka. TANZANIA yetu wote hii kwaiyo tunatakiwa kuwa makini sana.

    SOMA ZAIDI: Azam vs Yanga Tutegemee Fainali Ya Namna Hii Hapa

    azam vs yanga feitoto yanga wachezaji yanga sc

    9 Comments

    1. Slavius nguvumali on June 3, 2024 10:22 am

      Fei toto akazane na kazi yake mambo ya kuchanganywa aachane nayo kwasababu ukipenda kufata maneno unaweza kosa mambo mengi kwani yanga Wana kula pesa zake anazo tolea jashi

      Reply
    2. Abdulrahim on June 3, 2024 10:23 am

      Feisal anajitengenezea chuki yeye mwenyewe vitendo vyake pale anapokutana na yanga vinazua maswali Kwa mashabiki pia ni kama…. Asilimia kubwa ya mashabiki wa yanga wanatafisiri kama ni kejeli Kwa maboss wake wa Zamani

      Reply
    3. Phosser on June 3, 2024 10:34 am

      Yanga pia wanamchukia na kumwonea wivu fei,,, kama co wao kuwa na midomo kama chiriku nadhan fei asingeonesha ishara ya “shut up” nadhan yanga wamuache fei na fei asiwasikilize yanga,,, focus on football zanzibar finest,,,mti wenye matunda ndio hupigwa mawe,,

      Reply
    4. Mr. Chabhilonda on June 3, 2024 10:40 am

      Fei ball player mzuri ila anachotaka kufanya ni kujiona yeye yuko juu kuliko mabingwa(yanga) ushari kwake atimize majukumu yake uwanjani asishindane na taasisi kamz yanga

      Reply
      • Alex Simion on June 3, 2024 11:06 am

        Kama ni matunda basi ni yale ambayo hayaliwi!!!

        Reply
    5. Mr. Chabhilonda on June 3, 2024 10:40 am

      Fei ball player mzuri ila anachotaka kufanya ni kujiona yeye yuko juu kuliko mabingwa(yanga) ushauri kwake atimize majukumu yake uwanjani asishindane na taasisi kamz yanga

      Reply
    6. Sang'wa jr on June 3, 2024 10:50 am

      Unatoka kweny mwanga unaenda gizan afu unataka watu wakuone 😂🤣😂 fei bhna anway kuna mda makombe yanaihtaji yangu kulko yanga kuhtaji makombe🙏🙏

      Reply
    7. [email protected] on June 3, 2024 11:13 am

      Fei anagecheza mpira na siyo kucheza na wadau wa yanga atapotea Sanaa mtu mmoja huwezi pigana Vita na watu mia.

      Reply
    8. Chris Mlangwa on June 3, 2024 12:27 pm

      Kuna muda tunapaswa kutumia akili ya kuzaliwa , fei atumie pia ili apone 🤦🏽‍♂️

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.