Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Viwanja Vikubwa Vya Michezo Bara La Afrika
    Makala

    Viwanja Vikubwa Vya Michezo Bara La Afrika

    MhaririBy MhaririDecember 11, 2023Updated:May 23, 20241 Comment2 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Stade du 5 Juillet
    Uwanja wa Stade du 5 Juillet unaopatikana nchini Algera.
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ukizungumzia miundombinu ya michezo basi huwezi kuacha kutaja Bara la Afrika kwani  lina viwanja vikubwa kadhaa ambavyo huvutia idadi kubwa ya watazamaji pale yanapofanyika matukio mbalimbali ya kimichezo na burudani.

    Viwanja hivi vimejengwa katika nchi kadha wa kadha za barani Afrika na makala hii itatazama viwanja kutoka nchi kadhaa na kuangalia ukubwa wake kwa idadi ya watazamaji wanaoingia katika viwanja hivyo na tutaanza na:

    Stade Olympique de Radès – Tunisia

    Uwanja huu unapatikana nchini Tunisia na una uwezo wa kuchukua watazamaji takribani elfu sitini na tano (65,000). Ulijengwa mwaka 2001 na umekua ukitumiwa na timu ya taifa ya Tunisia lakini pia na matukio mengine ya kimichezo.

    Cairo International Stadium – Misri

    Kama ulikua hufahamu tu ni kuwa huu upo katika orodha ya dunia kikishika namba 69 kwa ukubwa duniani. Lakini pia ni miongoni mwa viwanja vikubwa barani Afrika ikiwa na uwezo wa kuchukua takribani watazamaji 75,000. Uwanja huu unatumiwa na timu ya taifa ya Misri Pamoja na mechi za vilabu barani Afrika.

    FNB Stadium (Soccer City) – Afrika Kusini

    Ni uwanja unaopatikana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini. Una uwezo wa kuingiza watazamaji takribani 94,700. Kumbukumbu kubwa kuhusu uwanja huu ni Pamoja na kutumika kwake katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2010.

    Stade 5 Juillet 1962 – Algeria

    Uwanja huu unatumika na timu ya Taifa ya Algeria na una uwezo wa kuchukua watazamaji takribani 95,000. Ulijengwa mwaka 1972 na ni miongoni mwa viwanja vikubwa vinavyopatikana nchini Algeria lakini pia umekua ukitumika katika shughuli za michezo Algeria.

    Stade Mohammed V – Morocco

    Huu unapatikana katika jiji la Casablanca nchini Morocco. Mara nyingi hutumiwa na timu ya taifa ya Morocco na mechi nyingine za ligi kuu nchini humo. Una uwezo wa kuingiza takribani watazamaji 67,000.

    Unaijua michezo nane (8) hatari zaidi duniani? Gusa hapa kusoma Makala hii sasa

    AFRICA STADIUMS

    1 Comment

    1. Pingback: YANGA Yatakiwa Kulipa Uharibifu Kwa Mkapa Kijiweni Ligi Kuu | Soka la Bongo -

    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nane  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.