Nikiwa kama mdau wa michezo hasa Mpira wa Miguu, nashauri Serikali kufanya haya ili kuboresha kiwango cha mpira nchini, na hata ushiriki wetu kwenye mashindano yajayo ya AFCON,2027 yatakayo fanyika nchini kwa kushirikiana na wenzetu wa Kenya na Uganda.
- Tutafute Kocha wa daraja la juu wa soka ambaye analifahamu soka la Africa na dunia kwa ujumla. Yule ambaye rekodi yake haina shaka yoyote.Nampendekeza kocha wa zamani wa Zambia na Ivory Coast ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Ufaransa , Herve Renard ,tukishindwa huyo twende na kocha wa zamani wa Aly Ahly ya Egypt/Mamelody Pitso Mosimane au Mkongo Florent Ibenge, bila kusahau suala la timu kukaa kambini muda mrefu,miezi 6 itapendeza zaidi.
- Kwa maendeleo ya muda mrefu tuchukue makocha hata 10 vijana na wale wa makamo wapelekwe nchi za Ulaya hasa Ujerumani, kwa mafunzo ya soka {Burundi walishafanya hili)..napendekeza makocha wafuatao wapate hiyo fursa, Zuberi Katwila, Selemani Matola, Minziro, Mecky Mexime, Mbwana Makata, Edward Augustino, Pawasa, huyo kocha wa sasa Prison yaani Ahmad Ally, Julio, na wengine kadiri Serikali itakavyoona inafaa ila kwa kuanzia tunaweza tupeleke Makocha 10, na wakirudi wapewe timu za taifa na hata vilabu kwa malengo maalumu. Kuhusu gharama tunaweza OMBA ufadhili kwa wenzetu wa Ujerumani kama ambavyo nchi nyingi zimekua zikifanya
3.Tuboreshe chuo cha Michezo cha Malya Mwanza,na hawa watakaopelekwa Ujerumani wanaweza kuwa Wakufunzi hata wa muda kule chuo cha Michezo Malya,
SOMA ZAIDI: Ni Wakati Wa Simba Kumuamini Kocha Mzawa?



