Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)

    Ratiba Kamili Ya FIFA CLUB WORLD CUP 2025

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)
    Hadithi

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaJune 1, 2025Updated:June 3, 202511 Comments7 Mins Read3K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nne

    “Na siku zote Muuwaji hawezi kuishi, ndiyo maana nilikutoaΒ  gerezani ili uje kuitafuta haki iliyoporwa na Faudhia”Β  Alikazia Mzee Shomari kisha alimruhusu Diana kuelekea ndaniΒ  ya Benki, mpango wa Mzee Shomari ulikuwa ni Kumuuwa Faudhia,Β  kisha kuiba pesa za kimarekani ambazo zilihifadhiwa ndani yaΒ  Benki hiyo katika chemba ya siri, ilikuwa ni zaidi ya DolaΒ  Bilioni 900 , alimtumia Chogo kama ngao ya kufanya mambo yakeΒ  huku akiweka ubia na rafiki yake wa zamani ambaye alikuwaΒ  akiishi Uholanzi, ndiye aliyemtoa jela na kumfadhili pesa zaΒ  kufanya ugaidi Tanzania, hivyo Mzee Shomari alikuwa ndiyeΒ  Gaidi aliyekuwa akiratibu mipango yote, alikusanya vijana naΒ  kuwapatia silaha nzito, akiwemo Diana na Martin Gimbo maarufuΒ  kama ChogoΒ 

    Jinsi alivyowapata Diana na Chogo utakuja kufahamu mbele,Β  hebu tosonge..Β 

    Usiku ulikuwa umeingia, ndani ya Jiji la Arusha, FaudhiaΒ  alikuwa akimlaumu Mohd kwa kosa la Kumuuwa Mama yake naΒ  Martin Gimbo.

    SEHEMU YA TANO

    “Hakukuwa na sababu ya kuuwa Watu wasio na hatia Mohd, umeuwaΒ  Mwalimu, umeuwa Bibi na Mjukuu wake” Alisema Faudhia kwaΒ  hasira sanaΒ 

    “Unanilaumu kwa kutekeleza mipango yangu ya kazi? UnanilaumuΒ  kwa kusafiaha ushahidi wa mwote tulimopita? Faudhia wewe siyoΒ  Mfanyakazi wa kanisa au msikiti, wewe ni askari wa siri waΒ  kitengo cha Usalama wa Taifa! Sisi tunauwa kwa ajili yaΒ  Taifa” Alijitetea MohdΒ 

    “Unauwa kwa ajili ya usalama wa Taifa? Taifa lipi? Kuuwa WatuΒ  wasio na hatia ndio majukumu ya Usalama wa Taifa? PengineΒ  umeelewa vibaya mafunzo uliyoyapata, siwezi kuendelea kufanyaΒ  kazi na wewe Mohd” Alisema Faudhia kisha alipiga simu kwaΒ  Mzee Shayo akamwambia ambadilishie Mtu wa kufanya naye kaziΒ 

    “Kwanini unataka abadilishwe?” Alihoji Mzee Shayo kwa njia yaΒ  simuΒ 

    “Sijisikii uhuru wa kuifanya kazi yangu” Alisema Faudhia hukuΒ  akiwa anamtazama Mohd ambaye alikuwa na hasira sana akiwaΒ  ameketi kwenye kiti

    “Faudhia Mwanangu..” kabla hata hajamaliza alikatiswa naΒ  FaudhiaΒ 

    “Baba nimesema nibadilishie huyu Mtu” Alisema kwa hasira naΒ  sauti ya juu kuonesha msisitizo kuwa alikuwa akimaanishaΒ  alichokisema na hakikuwa utani.Β 

    “Mpe simu Mohd,” mara moja Mohd alipewa simu na Faudhia,Β  kabla hajaongea na Mzee Shayo alimtazma sana kwa hasiraΒ  Faudhia.Β 

    “Natoa amri ya wewe kurudi Makao Makuu haraka sana” AlisemaΒ  Mzee ShayoΒ 

    “Lakini Mkuu..” kabla Mohd hajamaliza kujitetea alikatishwaΒ  na Mzee ShayoΒ 

    “Hakuna cha Lakini Mohd, rudi Makao makuu” Alisistiza MzeeΒ  Shayo, mara moja Mohd alimtupia simu Faudhia kisha alichukuaΒ  koti lake akatoka chumbani hapo lakini kwa bahati mbayaΒ  alikuwa amesahau simu yake ambayo ilikuwa kwenye kochi,Β  kitendo cha Mohd kutoka ndani ya chumba hicho, simu yakeΒ  ilianza kuita, Faudhia alinyanyuka na kuangalia aliyekuwaΒ  akipigaΒ 

    Aliona namba imeandikwa Boss, alifikiria afanye kitu ganiΒ  aipokee au aiache iendelee kuita hadi ikate, aliichukua naΒ  kuchungulia dirishani, alimuona Mohd akilielekea gari lakeΒ  kwa ajili ya kuondoka, aliona ni bora aipokee simu hiyoΒ  sababu alimtilia sana Mashaka kuwa huenda akawa sio Mtu mzuriΒ  kutokana na mauwaji ya Watu wasio na hatia ambayo alikuwaΒ  akiyafanya.Β 

    “Mohd! Muuwe Faudhia sasa hivi kisha urudi hapa” IlisikikaΒ  sauti ambayo Faudhia aliitambua, ilikuwa ni sauti ya kizee yaΒ  Mzee Shomari, mara moja aligundua kuwa Mohd alikuwa ni askariΒ  aliyekuwa akifanya kazi na magaidi, akatambuwa kuwaΒ  kilichobakia kwake ni kifo pekee. Alipochungulia tenaΒ  alimuona Mohd akiwa anapiga hatua kurudi ndani baada yaΒ  kugundua kuwa amesahau simu yake, Faudhia alimtazama vizuriΒ  Mohd akiwa bado amesimama pale pale, Mohd alikifikia kitasaΒ  cha mlango bila kujuwa kuwa Faudhia alikuwa amemshtukia kuwaΒ  ni Mamluki anayekisaliti kitengo cha Usalama wa Taifa.Β 

    Alipofungua mlango alimkuta Faudhia akiwa amesimama, UnajuwaΒ  Mohd alikuwa ni askari wa kitengo cha Usalama wa Taifa hivyoΒ  alipoingia tu aligundua kuwa kuna jambo ambalo halikuwa sawa,Β  alimtazama sana Faudhia akiwa ameganda pale mlangoni,Β  walikutanisha macho yao ya Kijasusi huku kila mmoja akiwaΒ  anamsoma mwenzake.

    Mara simu ya Mohd iliita tena na mpigaji alikuwa ni yule yuleΒ  Mzee Shomari, aliisikilizia kidogo kisha aliifuata simuΒ  lakini kabla hajapokea Faudhia alimnyooshea Mohd BastolaΒ 

    “Tulia hivyo hivyo Msaliti wewe, kumbe wewe ni mamlukiΒ  unayefanya kazi na Mzee Shomari? Nilikuwa nakutilia mashakaΒ  sana Mohd” Alisema Faudhia, Mohd alikuwa amesimama huku simuΒ  ikiendelea kuita mkononi mwakeΒ 

    “Isogeze hiyo simu kwangu” Alisema tena Faudhia hukuΒ  akihakikisha kuwa Mohd hachomoki wala hafanyi ujanja wa ainaΒ  yoyote ile. Mohd alimtazama Faudhia kisha alimsoma jinsiΒ  alivyokuwa amesimama ila Faudhia alishtuka mapema kuwa MohdΒ  anamsoma kisha akamwambia.Β 

    “Ujanja wowote utakaoufanya Mohd napasua kichwa chako”Β  Alisema Faudhia, Mohd aliinama kidogo kisha aliiburuza simuΒ  ikafika kwenye miguu ya FaudhiaΒ 

    “Umeanza kutumika upande huo kwa muda gani?” Aliuliza FaudhiaΒ  huku akizuga ili ainame aichukue simuΒ 

    “Faudhia! Usifikiri kamwe naweza nikasema chochote au hiiΒ  siri ikafika makao makuu, katu kitengo hakita ifahamu hiiΒ  siri” Alisema Mohd kwa kujiamini kisha alishusha mikono yakeΒ  akamwambia FaudhiaΒ 

    “Si ulikuwa unataka kunitwanga risasi? Fanya hivyo kablaΒ  sijakuwahi” Alisema maneno yaliyojaa ulaghai Mkubwa, ilikuwaΒ  ngumu kwa Faudhia kumuuwa Mohd, alichotaka ni kufikishaΒ  taarifa kwenye kitengo cha Usalama wa Taifa.Β 

    Mohd alianza kumsogelea Faudhia taratbu huku akizidi kuongeaΒ  maneno ambayo yalimchanganya FaudhiaΒ 

    “Wewe ndiyo sababu ya Mama yako kufa, hukustahili kubaki haiΒ  kwa uchafu ambao ulikuwa ukimfanyia Mama yako, laiti kamaΒ  taarifa hizi zitavuja ndani ya kitengo basi hautokuwa na sifaΒ  ya kuwa Undercover!! Mtu ambaye amemsaliti Mama yake kwa BabaΒ  yake anaweza vipi kutunza siri za Nchi hii” Alisema Mohd hukuΒ  akizidi kusogea, Maneno ya Mohd yalimtia uchungu sanaΒ  Faudhia, ni kama alitoneshwa kidonda kilichoanza kukaukaΒ 

    “Acha Mohd! Achaaaaa” Alisema Faudhia kisha aliweka kidoleΒ  sehemu ya kufyatulia risasi ili ammalize Mohd, haraka MohdΒ  alimuwahi Fadhia na kuushika mkono ambao ulikuwa na Bastola,Β  Faudhia alipofyatua risasi zote zilipiga juu ya dali. MohdΒ  alimkunja Faudhia na kumpa mateke matatu ya Mbavu kabla yaΒ  Faudhia kujikunjua

    Bastola ilikuwa chini, aliponyanyuka Faudhia alijikuta akiwaΒ  mikono mitupuΒ 

    “Nilikwambia hii siri haiwezi kufika kitengo cha Uslama waΒ  Taifa, kwakuwa nimepigiwa simu nirudi Makao makuu basi weweΒ  utaonekana umeuawa kwa kuvamiwa hapa Hotelini.” Alisema MohdΒ  huku akiwa anakunja Shati lake, alikuwa ni mwanaume mwenyeΒ  mazoezi na roho ya kikatili sana.Β 

    “Mradi wa kukutengeneza wewe uje kuwa Askari wa kitengoΒ  unafia hapa rasmi” Alisema Mohd kisha alimfuata FaudhiaΒ  ambaye alikuwa amejiandaa kukabiliana naye, alirusha ngumiΒ  mfululizo ambazo zote Faudhia alizikwepa lakini alifanyaΒ  ujanja wakati anamaliza kurusha ngumi ya mwisho alikunjuaΒ  Mguu wa kulia na kumpiga teke la tumbo Faudhia, alijikutaΒ  akianguka chini kisha alijinyanyua na kupanga pambano upya.Β 

    Wote walikuwa na mafunzo ya Kijeshi hivyo kila mmoja alijuwaΒ  namna ya kupambana, Faudhia alijibu mapigo kwa kumpa matekeΒ  mawili yaliyofika hadi kwenye kifua cha Mohd, alisogezwaΒ  pembeni karibu na mlango ambapo kochi lipo, aliangalia chiniΒ  kulikuwa na Bastola, pembeni kulikuwa na simu yake yenye siriΒ  nzito, aliona ni bora afanye ujanja.Β 

    Aliokota mto wa kochi kisha alimtupia Faudhia usomi kishaΒ  aliinama ili aichukue bastola lakini Faudhia alikuwa shapu,Β  kabla hajaokota Bastola alipigwa teke la Mgongo kisha FaudhiaΒ  akaipiga teke ile simu na Bastola vikaingia uvunguni mwaΒ  Kochi, alimlazimisha Mohd apambane kwanza.Β 

    Mohd aliinuka na kunvaa Faudhia, aliambulia kutupwa chiniΒ  kutokana na namna Faudhia alivyo Shapu. Kabla hajakaa sawaΒ  alipokea ngumi la shingo ambalo lilimsogeza kwenye kochi,Β  kabla hajatulia tena Faudhia alimpelekea Mohd teke ambaloΒ  Mohd alilidaka kisha alitumia nguvu kubwa alimsukuma FaudhiaΒ  ambaye aliangukia kwenye mezaΒ 

    “Assssh” aligumia Faudhia kutokana na maumivu ya kujigongaΒ  kwenye meza, Mohd hakutaka kusubiri alimrushia ngumiΒ  mfululizo, ngumi ambazo zilimpekeka Fuadhia ukutani, bahatiΒ  mbaya ngumi nyingi zilimpata na kumfanya aumie usoniΒ 

    Mohd alimpiga Faudhia mateke mfululizo eneo la mbavu hukuΒ  akimwambiaΒ 

    “Unakufa leo” Alisema huku akiwa anamuangalia Faudhia akiwaΒ  anaanguka chini.

    Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA SITA

    JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ 

    Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA

    Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA

    Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β 

    Riwaya Nyumba Ya Majini Kijiweni riwaya za kusoma mtandaoni soma riwaya bure

    11 Comments

    1. David ben on June 1, 2025 5:52 pm

      Mbona fupi sana jamani

      Reply
    2. Joy on June 1, 2025 5:57 pm

      Imeishia patamuu

      Reply
    3. Daudi Antony kilyenyi on June 1, 2025 5:58 pm

      mbna fupi hvo mzee

      Reply
    4. Jackson Wasokye Ramazani on June 1, 2025 6:02 pm

      Bado mda huko adm, rusha sehemu ya sita. Hii tamu sana kabisa.

      Reply
    5. Cathbert on June 1, 2025 6:21 pm

      Good πŸ‘πŸ‘

      Reply
    6. Adam on June 1, 2025 8:15 pm

      Admn Ahsante Kwa Story Nzuri Saanaa Hii

      Reply
    7. Salma Ibrahim on June 1, 2025 9:08 pm

      Fupi inakera

      Reply
    8. Lus twaxie on June 1, 2025 11:14 pm

      Fupi innboa sana jmn ….kama utaki acha tu kutuma

      Reply
    9. KingzJeelay on June 2, 2025 1:34 am

      Admin hapa umezingua….
      Stori ni fupi mnooooo 😯😯😯

      Reply
    10. Diana on June 2, 2025 11:08 am

      Admini hauna vitabu tununue tu

      Reply
    11. πŸ“’ Reminder- + 1.425308 bitcoin. Receive >> https://yandex.com/poll/DCTzwgNQnzCykVhgbhD581?hs=c68e35f9f994198fbd7c29c235410dbc& πŸ“’ on June 3, 2025 11:04 am

      8qqlk0

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 3, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya nneΒ  “Assssh” aligumia Faudhia kutokana na maumivu ya kujigongaΒ …

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tano-05)

    Ratiba Kamili Ya FIFA CLUB WORLD CUP 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nne-04)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.