Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya sita
“Kama lilivyo tamu penzi lako, basi nahitaji uniambie wapiΒ ilipo chemba ya siri iliyohifadhi pesa za Kimarekani” AlisemaΒ Chogo akiwa anavaa nguo zake, alipomaliza alikuwa badoΒ hajapata jibu kutoka kwa Selina ambaye alikuwa akitetemekaΒ kwa wogaΒ
“Ukimya wako unaashiria kuwa ni bora ufe kuliko kusema ilipoΒ Chemba si ndiyo?” Aliuliza tena Chogo, safari hiiΒ alibadilisha sura yake na kujaza hasira
“Tafadhali usiniuwe, ipo chumba namba 43” Alisema SelinaΒ . Endelea
SEHEMU YA SITA
“Hebu twende huko” Alisema Chogo kisha aliongozana na Selina,Β waliingia ndani ya Lift kisha safari ilianza kuelekea juu yaΒ Ghorofa hilo la Benki, walipofika huko Selina alimuoneshaΒ ilipo chemba, ilikuwa imefichwa nyuma ya Kioo kikubwa ambachoΒ kwa Mtu mwingine ni ngumu kujuwa kuwa eneo hilo kulikuwaΒ kumehifadhiwa Mabilioni ya Dola za Kimarekani ambazoΒ zilitokana na mauzo ya Siri ya Madini ambayo Rais na WaziriΒ Mkuu walifanya Biashara hiyo kisiriΒ
“Fungua” Alisema Chogo, Selina alibonyeza mahali kisha kiooΒ kilijivuta pembeni, kulikuwa na mlango wa Umeme eneo hilo,Β palitakiwa kuingizwa namba za siri, Selina aliingiza namba zaΒ siri na Mlango huo ulifunguka, Chogo hakuamini macho yake,Β kwa mara ya kwanza katika Maisha yake alishuhudia kiasiΒ kikubwa cha pesa, chumba kilijaa pesa nyingi za kimarekaniΒ
“Woww!!” Alisema Chogo akionesha kufurahi sana, alimfuataΒ Selina na kumpiga busu kama ishara ya furaha baada yaΒ kukutana na kiasi hicho ambacho ndicho kilichowafanya waitekeΒ Benki hiyo na baadhi ya Miji na kambi za Jeshi.Β
“Nakuwa Bilionea muda siyo mrefu Selina, ilikuwa ni ndoto yaΒ Maisha yangu kuja kuwa Bilionea mkubwa Afrika” Alisema ChogoΒ huku akiruka kwa furaha kisha aliendelea kusemaΒ
“Hatimaye Baba yangu atalala kwa amani baada ya kuhakikishaΒ nasomba kiasi hiki cha pesa” Aliposema hivi Selina alipataΒ shahuku ya Kumuuliza ChogoΒ
“Baba yako atalala kwa amani? Anahusiana vipi na pesa hizi?”Β Alihoji huku akiwa anautazama mgongo wa Chogo, alipogeukaΒ alimpa jibu SelinaΒ
“Miaka mingi nikiwa na umri wa miaka 10, Baba yangu alikuwaΒ akifanya kazi kwenye mgodi wa Melerani, alipokuwa akichimbaΒ alikutana na Jiwe kubwa sana la dini, alienda kuwaambiaΒ viongozi wa mgodi huo ambao walielekea pamoja chiniΒ kuliangalia, walipothibitisha kuwa Jiwe hilo lilikuwa ni diniΒ lenye thamani kubwa sana walimuuwa Baba yangu kisha walitoaΒ taarifa kuwa amefukiwa na kifusi, niliishi maisha magumuΒ sana. Nilimuaga Mama kuwa naenda Mjini , bahati mbayaΒ nilipata ajali ya gari, kitu pekee kilichonisaidia nilirushwaΒ dirishani na kutumbukia kwenye maporomoko, wengine woteΒ walikufa kwenye ajali hiyo, aliyenisaidia alikuwa ni rafikiΒ wa Baba yangu ambaye alinieleza kila kilichotokea, Mama yanguΒ pia alikufa kwa presha baada ya kusikia kuwa nimepata ajali.Β Sikuwa na sababu ya kurudi Arusha, yule rafiki wa Baba aliniambia napaswa kulipa kisasi kwa kila kilichomfika BabaΒ yangu”Β
“Alinisafirisha na kunipeleka Colombia, niliishi huko naΒ kufundishwa biashara ya uuzaji wa madawa ya kulevya, jinsi yaΒ kutumia silaha na mapigano, baadaye nilirudi Tanzania naΒ kutengeneza kundi la ESS, lengo ni kusomba pesa zoteΒ zilizotokana na Mauzo ya Madini ambazo Rais na Waziri MkuuΒ waliifanya Biashara kwa siri sana, wewe ukiwa unalifahamuΒ hilo Selina.” aliposema hivi Selina aliinamia Chini, ChogoΒ alikuwa akiongea kwa Uchungu sana lakini kwa namnaΒ alivyoelezea ilionesha wazi kuwa Chogo alidanganywa na MzeeΒ Shomari ili Mzee Shomari afanikishe lengo fulani, kupitiaΒ ugaidi huo tayari alishasomba madini kwenye migodi mingi NaΒ kilichokuwa kimebakia ni hicho kiasi kikubwa cha pesa ambachoΒ endapo kitachukuliwa basi alipanga kuwauwa Diana na ChogoΒ kisha atimke zake Uholanzi kwa rafiki yake.Β
“Pole sana, lakini kufanya hivi huoni kama unahatarishaΒ Maisha yako zaidi?” Aliuliza SelinaΒ
“Maisha yangu yalishakuwa kwenye hatari baada ya Baba yanguΒ kufariki huko Mgodini, nilifanya kazi za hatari pale ArushaΒ nikiwa bado shule, nani alijali?” Alisema Chogo kisha alikaaΒ juu ya pesaΒ
“Unahisi unaweza ukatoka hapa ukiwa salama?” Aliuliza SelinaΒ
“Baada ya Masaa 24 nitatoka hapa nikiwa na kiasi hiki chaΒ pesa” Alisema Chogo.Β
Ndani ya Makao makuu ya Kitengo cha Usalama wa Taifa hukoΒ Kigamboni, Mzee Shayo alikuwa ameketi akisubiria simu yaΒ Faudhia, hakuwa na taarifa yoyote iliyomhusu Faudhia maanaΒ mara ya mwisho walipeana majukumu ya kufanya kwa kila mmojaΒ wakati Faudhia akirudi Arusha Mzee Shayo akienda gereza laΒ Segerea huko Tabata.Β
Wakati Mzee Shayo anamtafakari Faudhia, huyo Faudhia alikuwaΒ akihangaika namna ya kulifungua Brifkesi lile, kila nambaΒ waliyoingiza haikufungua Brifkesi hilo, Faudhia alimtaka yuleΒ Mdada kusimamisha gari, kisha alishuka na kutafuta jiweΒ kubwa, alipasua ile Brifkesi, ndani yake kulikuwa na karatasiΒ zilizoandikwa ” MPANGO ESS”Β
Haraka Faudhia alichukua kila kitu na kurudi ndani ya gari,Β alimwambia yule Mdada kuwa aendeshe mwendo wa kasi huku yeyeΒ akisoma karatasi hizo ambazo zilionesha kuwa mpango wote waΒ Ugaidi ulisukwa humo ndiyo maana ulienda kufukiwa ndani yaΒ shimo walilodai kuwa ni kaburi la Martin Gimbo, hivyo basiΒ mpango wa kundi la ESS ulipangwa muda mrefu hata kabla YaΒ hiyo ajali ya kutengenezwa ya Martin Gimbo.Β
Karatasi hizo zilikuwa na siri nzito za mipango yote ya MzeeΒ Shomari Nchini Tanzania, kwanza karatasi hizo zilisema niΒ wapi Mzee Shomari ataweka kambi yaani kule kwenye jengo laΒ China Plaza, pili jinsi madini yatakavyokuwa yanaibwa naΒ kupelekwa Nje ya Nchi, tatu jinsi watavyokiondoa kiasiΒ kikubwa cha pesa ndani ya Benki kuu, Nne jinsi alivyowatumiaΒ askari jeshi kupandikiza mabomu katika kambi zote TanzaniaΒ kisha akawa na rimoti ya kuongoza mabomu hayo ndiyo maanaΒ jeshi hawakuweza kutoka na kwenda kuzuia Ugaidi kwa hofu yaΒ kambi zao kulipuliwa, Tano jinsi alivyo tengeneza ajali yaΒ Basi na kumpata Chogo kisha kumjaza chuki na maneno yaΒ kupandikiza ili aichukie Nchi yake, lengo likiwa kumsadiaΒ yeye Mzee Shomari kufanya Ugaidi na kuiba alivyokusudiaΒ Tanzania.Β
Karatasi hiyo ilikuwa na michoro ya namna walivyotengenezaΒ njia ya Chini kwa chini kutokea Msikiti wa Maamur Upanga hadiΒ Benki Kuu, hivyo wangeitumia njia hiyo kuondoka na pesa bilaΒ askari kujuwa kuwa walikuwa wameshatimka, Faudhia aliendeleaΒ kusoma na kuujuwa mpango wa Mzee Shomari kuanzia A hadi Z,Β ghafla gari yao iligongwa kwa nyuma na gari moja aina yaΒ Toyota Mkonga njeΒ
Alipochungulia alimuona Diana akiwa ndani ya gari hiloΒ
“Shit!!” Alisema Faudhia akiwa tayari ameshafahamu kila kitu,Β Diana alijitahdi kutaka kuwasiliana na Mzee Shomari naΒ kumwambia kuwa mpango wao unaweza kwenda songombingo sababuΒ Faudhia ameshajuwa kila kitu lakini mawasiliano yalikuwaΒ yamekata, alichotaka kufanya Diana ni kumzuia kwanza FaudhiaΒ asifanye chochote hata kulisogelea Jiji la Dar-es-salaamΒ sababu yalibakia masaa chini ya 24 ili wamalize kazi yao.Β
Yule Mdada aliendesha kwa woga sana huku akijitahidi kukwepaΒ risasi ambazo Diana alikuwa anazimimina kwa lengo laΒ kuwazuia, Mdada alijikuta akigonga Mti baada ya kuondolewaΒ barabarani na Diana, Ukimya ulitawala sana kwenye gari yaΒ akina FaudhiaΒ
Diana alishuka kwenye gari akiwa na Bastola yake, alisogeaΒ kwa tahadhari sana kuelekea lilipo gari la akina Faudhia hukuΒ akijuwa fika kuwa haitokuwa rahisi kumnasa Faudhia kutokanaΒ na mafunzo aliyonayo. Alipofika alimkuta Yule Mdada pekee,Β hakumuona Faudhia
“Fauhdia yupo wapi?” Alihoji Diana, yule Mdada alionekanaΒ kujawa na woga, ilibidi aoneshe mahali ambapo FaudhiaΒ alikuwepo, Naam! Alikuwa nyuma ya Mti mkubwa ulio jirani naΒ eneo walilopata Ajali. Baada ya kuona ameshajulikana alipo,Β haraka Faudhia aliuwahi mkono wa Diana ambao ulikuwaΒ umeshikilia Bastola, wakawa wananyang’anyana Bastola mkononiΒ mwa Diana, hatimaye iliangukia pembeni.Β
“Diana hupaswi kufanya hivi, ningekuwa nataka kukuuwaΒ ningekuuwa tokea kule tulipokuacha, ila nilikuacha iliΒ utafakari maneno yangu!! Mzee Shomari ndiye aliyemuuwa MamaΒ yako siyo Mimi” Alisema Faudhia akiwa anamtazama Diana kwaΒ jicho lililojaa umakini sanaΒ
“Ni bora ungeniuwa pale pale Faudhia ila kuniacha hai ni kosaΒ kubwa sana, unafikiri nitapotea kwa maneno yako? LazimaΒ nilipe kisasi cha kifo cha Mama yangu” Alisema Diana kishaΒ alikaa mkao wake kwa ajili ya kupambana na Faudhia.Β
Kama kawaida yake alijirusha sambasoti na kutua karibu zaidiΒ na Faudhia, aliona pigo la ngumi lililotumwa na Faudhia,Β alikwepa kisha aliinuka na teke la mkunjo na kumpiga FaudhiaΒ begani, kisha alijifytua na kumkata ngwara Faudhia ambayeΒ alinguka chini hata hivyo haraka alijiokota. Faudhia alionaΒ ni bora apambane na rafiki yake huyo ili kuliokoa Taifa.Β
Alivuta taswira fupi ya mafunzo aliyoyapata Mexico kishaΒ alimtazama Diana ambaye alionekana dhahiri kuwa alijawa naΒ hasira sana, alifanya kama anamfuata hivi kisha alijifyetuaΒ na kutua pembeni akajikuta anautazama mgongo wa Diana,Β alimsindikiza na teka kali ambalo lilimsomba Diana hadiΒ kwenye mti, alichukia sana Diana aliokota gongo la mti kishaΒ alilitumia kama silaha kupambana na Faudhia ambaye alikuwaΒ tayari amedhamiria kama kufa yeye au kufa Diana maanaΒ alijaribu sana kumueleza ukweli wa kilichotokea hadi MamaΒ yake akafa.Β
Faudhia alirusha ngumi mfululizo bila kupumzika, DianaΒ alijitahidi kuzizuia lakini hakufanikiwa kuzuia zoteΒ alijikuta akiruhusu ngumi kadhaa kwenye kifua chake, paleΒ pale alikohoa damu. Faudhia hakuhitaji maongezi tena baliΒ alichotaka ni kuhakikisha anatembea ndani ya muda ili awahiΒ kuzuia mpango wa Mzee Shomari. Diana kila alipojaribuΒ kumsogelea Faudhia alikunbana na kadhia ya mapigo matakatifuΒ yaliyozidi kumfanya ateme damu, Faudhia hakuwa na huruma tenaΒ na rafiki yake alijirusha na kutua mbele ya Diana kishaΒ akafanya kama anataka kukimbia alafu akajikunja na kumvaaΒ Diana eneo la shingo kisha akampa kabali ya miguu shingoni.
Hali ilianza kuwa ngumu kwa Diana alijikuta akianza kukosaΒ hewa, alipiga miguu ya Faudhia akiomba aachwe lakini tayariΒ mzimu wa kazi ulikuwa umempanda sana Faudhia, alihakikishaΒ anambana hadi alipokatisha uhai wa Diana, alipohakikisha kuwaΒ Diana ameshakufa alimuacha kisha alimwambia yule Mdada kuwaΒ wanapaswa kuondoka haraka sana, walirudi nyuma wakachukuaΒ gari ya Diana kisha waliingia Barabarani kwa ajili yaΒ kuelekea Dar-es-salaam.Β
Mdada alikuwa akiendesha gari kwa hofu huku akijikuta akiwaΒ na maswali mengi ya kumuuliza Faudhia, alianza kumuulizaΒ
“Wewe ni nani na kwanini unafuatiliwa?” Faudhia alimtazamaΒ yule Mdada kisha alimwambiaΒ
“Naitwa Faudhia, mimi ni undercover wa kitengo cha Usalama waΒ Taifa” Alijibu Faudhia kisha alionekana kusahau jamboΒ
“Wewe unaitwa Nani?” Aliuliza FaudhiaΒ
“Naitwa Matilda”Β
“Ooh!! Sawa Matilda nashukuru kukufahamu pia nashukuru kwaΒ msaada wako, kama si wewe ningelikuwa nimeshakufa” AlisemaΒ Faudhia, Matilda aliuliza tena.Β
“Na yule ni nani? Inaonekana mlikuwa mnafahamiana, kwaniΒ ulimuuwa Mama yake?” Alihoji tena Huyo MdadaΒ Β
aliyejitambulisha kama MatildaΒ
“Hapana!! Sikumuuwa Mama yake, yule anaitwa Diana ni rafikiΒ niliyesoma naye huko Mbeya, sijui hata alijiingiza vipiΒ kwenye ugaidi” Alisema Faudhia kisha alirudisha macho yakeΒ mbele, safari yao ilizidi kusonga mbeleΒ
- β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’β’Β
Ndani ya Jengo la China plaza, Mzee Shomari alikuwa bizeΒ kumtafuta Diana kwa njia ya simu lakini simu ya DianaΒ haikupokelewa, alimtafuta kwa zaidi ya masaa mawili jamboΒ ambalo lilianza kumpa wasiwasi, alipoona simu zakeΒ hazipokelewi alimpigia Chogo ndani ya Benki kuu kishaΒ akamwambiaΒ
“Diana hapatikani kwa zaidi ya masaa mawili, maliza mchakatoΒ haraka iwezekanavyo” Alipomaliza kumpa maelekezo Chogo,Β alipiga simu Arusha kwa Mtu mwingine wa kazi kisha alimuagizaΒ kuelekea kwenye kaburi kuangalia kama mzigo utakuwaΒ umechukuliwa
Chogo alipopata maelekezo ya kuendelea na mchakato aliitaΒ vijana wake kisha aliwaambiaΒ
“Weka pesa zote ndani ya mabegi” Aliposema hivi vijana wakeΒ haraka walifungua mfuko mmoja mkubwa sana ambao ulikuwa naΒ mabegi mengi kisha zoezi la kuweka pesa lilianza mara moja.Β
Zilikuwa ni pesa nyingi mno, walishindilia kwenye mabegi hayoΒ ambayo yalikuwa makubwa na meusi, tayali gari lilikuwaΒ limeshaandaliwa ndani ya Msikiti wa Maamur kwa ajili yaΒ kubeba pesa hizo ambazo watapita nazo chini kwa chini kutokeaΒ Posta hadi Upanga.Β
Kule Ikulu, Rais alikuwa katika hali ya wasiwasi mno endapoΒ chemba ya siri ingefahamika kupitia kwa mdada ambayeΒ anajulikana kama Selina, lakini tayari Selina alikuwaΒ ameshaonesha ilipo chemba ya siri na tayari pesa zilishaanzaΒ kuchotwa huko, yeye na Waziri Mkuu walionekana kuficha kuhusuΒ biashara hiyo ya madini ambayo waliifanya kwa siri sana iliΒ baadaye pesa hizo zihamishwe kwa siri kwenda Marekani.Β
“Naomba niongee na Shayo haraka” Alisema Rais, mara mojaΒ Waziri Mkuu alipiga simu kwa mkuu wa kitengo cha Usalama waΒ Taifa ambaye hadi kufikia wakati huo hakujuwa Faudhia alikuwaΒ wapi, ni mzima au amekufa ila Faudhia alikuwa barabaraniΒ kuelekea Dar kwa ajili ya kuzuia mpango wa Mzee Shomari.Β
Mara moja simu ya Mzee Shayo ilipokelewa na maongezi kati yaΒ Mzee Shayo na Rais yalianza, Rais alisikika kwa kupoa sanaΒ tofauti na mwanzo ambapo alionesha hasira sana kwa Mzee ShayoΒ
“Shayo!!” Aliita RaisΒ
“Naam Mkuu” Aliitika Mzee ShayoΒ
Nini Kitaendelea USIKOSE SEHEMU YA NANE
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β
25 Comments
Duuh! Nilidhani Diana angemuelewa Faudhia
Halooooo Hadithi Tamu Mnoo Hiii
Daaaah jaman mnaishia kwny utam ivoo mbn but iko vzur Sanaa hii story kongole to mwandishi
Ongera sana kikweli mambo ni π₯π₯ Diana bye bye
π₯π₯π₯π₯π₯
Mambo yanazidi kuwa ya motoooπ₯π₯π₯
Daaah kwa nin diana hakutaka kumwelewa rafiki yakeππ
π₯π₯π₯
Naomba kuipata yote tafadhali nitalipia
duuu leo kifupi
Mambo ni moto
Admin kwan unatumia mfumo gan kutumia na mdaga maana cjajua kila ck kila baada ya mda gan na mda gan unatuma uwe na utalatibu ili tujue maana husomek story ni nzul ila utoaji wako haupo sawa nilipenda jinsi ulivyo kuwa unatoa simuliz ya mama niachie mume wangu nikajua itakayo kuja utaweka mfumo mzuli zaid lakin apa ume long kuliko iliyo pita
Aisee vitu vyangu hivi napenda hadi natamani episode ziungane hongera sana mtunzi
4kgbe4
Bila kuchoka π
Good ππ
mb1j7y
ksodqf
facpc6
jwfs63
9ima0b
vwe05l
gqe6qn
pwpctg
04h75d