Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Pili (02)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Pili (02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 12, 2024Updated:October 28, 202415 Comments8 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Jacklin Mwanangu sijapata pesa kama unaweza kusubiria hadiย  jioni sawa” Alisema Mamaย 

    “Usijali Mama nitarudi tu” Nilisema, sikuwa na pesa ya nauliย  ya kurudia nyumbani alafu mvua ilikuwa ikinyesha sana,ย  kulikuwa na hali ya radi pia, nilifikiria kama Osmanย  angelinikuta pale nje ingeleta picha mbaya zaidi, nilifikiriaย  pia ile pesa niliyompa kwa hasira, nilijilaumu sana kwaย  kiburi changu. Basi niliingia kwenye mvua, nilivua viatuย  vyangu. Endeleaย 

    Kumbe yule Mdada msaidizi wa Osman alikuwa akiniangalia tu,ย  alienda kumwambia Osman, nilitembea kwenye mvua nikiwaย  natetemeka, kufika nyumbani kwetu kwa mguu ni zaidi ya masaaย  matatu. Kwa jinsi mvua ilivyokuwa ikinyesha ilionesha waziย  kuwa isingelinyamaza kwa muda huo, basi niliendelea kutembea.ย  Osman alipopata taarifa kuwa natembea kwenye Mvua aliachaย  kazi zake, alichukua Mwamvuli akaingia kwenye gari yakeย  akaanza kunifukuziaย 

    Ilifika mahali baridi lilinizidia, nilitembea kwa maumivuย  makali huku nikimfikiria sana Mosses, kwanini hakunitumiaย  hiyo pesa? Kwanini alikuwa hapokei simu zangu, nilijikutaย  nikilia njiani sababu moyo wangu nilimpa Mosses, niliulaumuย ย umasikini ambao Baba yangu alituachia, nilimlaumu Munguย  kwanini alimchukua Baba wakati akiwa masikini?

    Mara nilisikia Honi ya gari, niliipisha ipite lakiniย  haikufanya hivyo, alikuwa ni Osman. Nilipogundua ni yeyeย  niliondoa mikono yangu kifuani, nilitabasamu ili asione kamaย  kutembea kwenye mvua kumetokana na kutokuwa na hela bali niย  mazoezi tuu. Alishusha kioo akaniambiaย 

    “Ingia kwenye gari nikusogeze Jacklin” Alisema kwa busara naย  hekima ya hali ya juu sana, pesa alizonazo Osman hakustahiliย  kuninyenyekea namna ileย 

    “Hapana nafurahia maajabu ya Mungu” Nilisema huku nikiwaย  napiga hatua huku Osman akiendesha taratibu.ย 

    “Hapana mvua ni kubwa sana Jacklin, twende nikupeleke kwenu”ย  Alisema tena Osmanย 

    “Usijali Osman, nitachukua Tax mbele, nafurahia mvua kwanza”ย  Nilisema nikiwa nimeshikilia viatu vyangu mkononi, Basi Osmanย  alifunga kioo ili aondoke zake, kiukweli hali yangu haikuwaย  nzuri, lile baridi lilinitesa sana, njaa ilikuwa ikinikwanguaย  vibaya mno, nilijikuta nikianguka kwenye mvua.ย 

    โ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขโ€ขย 

    Nilipokuja kurudisha fahamu zangu nilijikuta nikiwaย  Hospitali, Osman alikuwa amekaa kitandani, Mama yangu alikuwaย  pembeni yanguย 

    “Mama!” Nilimuita Mamaย 

    “Jacklin Mwanangu, nesi Mwanangu ameamka” Alisema Mama,ย  alinifanya nitabasamu sana, Upendo wa Mama ulikuwa Mkuu sanaย  kwangu, niligeuza macho na kumtazama Osmanย 

    “Asante sana Osman” Nilisema nikiwa natabasamu japoย  nilipoteza fahamu ila nilijuwa tu aliyenisaidia alikuwa niย  Osman, kabla hajanijibu Chochote nesi alikuja kwa ajili yaย  kuangalia hali yangu, Osman alimwambia Mamaย 

    “Naomba tuongee kidogo Mama” Basi Mama na Osman walitoka hukuย  Daktari akiwa ananiangalia kwa makini na kiniuliza baadhi yaย  Maswali ili kujuwa nilikuwa najisikiaje.ย 

    Osman alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo, alimuulizaย  Mamaย 

    “Huyu ni Binti yako wa kumzaa?” Mama alitabasamu kishaย  alimjibu Osman

    “Ndiyo, ndiye Mtoto pekee ninayemtegemea, nakushukuru sanaย  Baba japo sijakufahamu maana umenipigia tu simu na kunielezaย  kuhusu hali ya Binti yangu, kwa jinsi nilivyokuwaย  nimechanganikiwa wala sikuwa na muda wa kukuuliza” Alisemaย  Mamaย 

    “Naitwa Osman, Mimi ndiye mmiliki wa kampuni ambayo Bintiย  yako alikuja kuomba kazi” Alijitambulisha Osman kwa Mamaย  yanguย 

    “Ooh! Asante sana Baba” Alisema Mamaย 

    “Sasa Mama! Pamoja kwamba hali ya Binti yako unaiyona ipoย  sawa lakini kuna tatizo kubwa sana katika mwili wake,ย  inaoneka figo zake zote mbili hazifanyi kazi ipasavyo,ย  inatakiwa kubadilishwa, kama zitapatikana mbili au moja iliyoย  imara sana” Alisema Osman, Mama alishindwa hata kusimamaย  aliomba akae kwanza, akiwa kama Mama alichanganikiwa sanaย  kusikia nina tatizo la figo zanguย 

    “Unasemaje?” Aliuliza Mama akiwa anakaribia kuanza kuliaย 

    “Ndiyo maana Mama nimekuita hapa iliniweze kuzungumza na weweย  kuhusu hali ya Jacklin, ana siku 30 za kufanyiwa matibabu”ย  alisema Osmanย 

    “Sasa mimi na umasikini huu nitaweza vipi Baba yangu? Munguย  kwanini ananipa mtihani mzito kiasi hiki niimemkosea niniย  Mimi?” Alisema Mama akiwa analia, Osman aliketi na kumwambiaย  Mamaย 

    “Mimi nina safari ya kwenda Dubai kesho, gharama zoteย  nitazifanya. Mnapaswa kutafuta Mtu wa kumtolea figo Jacklin”ย  Alisema Osman, angalau Mama alifuta mchozi wakeย 

    “Nitakuunganisha na daktari Bingwa wa hii Hospitali,ย  mtasaidiana itakapopatikana hata moja imsaidie Binti yako”ย  Alisema Osman, Mama alimtazama Osman akamwambiaย 

    “Wewe ni Binadamu mwenye moyo wa peke yako Mwanangu, Munguย  azidi kukubariki kwenye kila hatua” Alisema Mamaย 

    “Ila Mama naomba hili liwe siri yako, Jacklin hapaswi kujuwaย  kama ana tatizo la figo sababu akijuwa inaweza leta shidaย  zaidi” Alisema Osman, walipomaliza kuzungunza walirudiย  wodini, walinikuta nikiwa ninafakamia vyakula maana njaaย  niliyokuwa nikiisikia haikuwa ya kawaida, sura zaoย  hazikuonesha dalili ya tatizo lolote lileย 

    “Jacklin!” Aliniita Mama kisha aliketi kitandani

    “Kama kuna Binadamu ana roho nzuri katika hii Dunia basi huyuย  Kijana ni namba moja, namshukuru kwa kuokoa Maisha yako”ย  Alisema Mama kisha alitabasamu, kumbe Osman alikuwaย  amewasiliana na Mosses na kumwambia kuwa nilikuwa nina umwaย  sababu namba ya Mosses nilisave kama Mume wangu, alikuja mudaย  huo, alinikumbatia na kunipiga busu mbele ya Mama na Osman,ย  Mama alishangaa sana sabahu alikuwa hamfahamu Mossesย 

    “Mama!! Huyu anaitwa Mosses, ni..ni…ni” nilishindwaย  kumtambulisha Mosses mbele ya Mama na Osman, Basi muda huoย  huo Osman aliaga na kuondoka zakeย 

    “Mama huyu ni Mchumba wangu anaitwa Mosses…..Mosses huyu niย  Mama yangu” Nilijitahidi hadi kumtambulisha Mosses kwa Mamaย  yangu, japo niliona Mama hakufurahia ila alijikaza tuย 

    “Oooh!! Sawa, basi mpate muda wa kuongea Mimi naenda kwaย  daktari” Alisema Mama, kumbe alikuwa anataka kumuwahi Osmanย  nje, kweli alimkimbilia Osman kabla hata hajapanda kwenyeย  gari akamuita, alipomfikia alimwambia Osmanย 

    “Baba upo sawa?” Aliuliza Mamaย 

    “Ndiyo Mama nipo sawa, naenda kuendelea na kazi” Alisemaย  Osman, ila Mama alihisi kuna jambo lipo ndani ya Osman kwaย  jinsi alivyoaga pale wodini.ย 

    “Nakuomba Mwanamgu, msaidie Jacklin apone na Mungu atakulipaย  zaidi” Alisema Mama, Osman alimsogelea Mama akamwambiaย 

    “Ni jukumu nililokuahidi Mama, Mwanao atarudi kuwa sawa tuย  wala usijali, hii hapa ni kadi yangu ya Biashara” alimpatiaย  Mama kadi yenye mawasiliano yake, Osman aliingia kwenye gariย  yake na kuondoka.ย 

    Mosses alikuwa ndiyo Mwanaume niliyempenda sana katika Maishaย  yangu, ndiye aliyenitoa usichana wangu, nilimuulizaย 

    “Kwanini ulikuwa haupokei simu yangu?”ย 

    “Samahani Mke wangu, unajuwa muda ule nilipatwa na dharuraย  nikaenda kumuona Mdogo wangu alikuwa ana tatizo” Alisemaย  Mossesย 

    “Ooh pole sana, anaendeleaje”ย 

    “Yupo sawa, hivi huyu jamaa aliyekuwa amekaa hapa ni nani?ย  Mbona baada ya kukupiga busu aliaga?” Aliuliza Mosses

    “Mmmh! Jamani Mosses, ni rafiki tu, ndiye aliyenisaidia”ย  nilimjibu Mosses, kitu kilichokuwa kikinivutia zaidi kwaย  Mosses ni wivu wake kwangu, yaani nisisimame na Mwanaume auย  kuongea nayeย 

    “Anhaa! Sasa sitaki hayo mazoea na huyo jamaa sawa?” Alisemaย 

    “Mmmh! Sawa” Nilimjibu, Mama aliporudi alitukuta tukiwaย  tumemaliza mazungumzo, basi alimuita Mosses pembeni naย  kumueleza kilichokuwa kikinisibu sababu alikuwa Mtu wangu waย  karibu sana.ย 

    Mosses alipoambiwa hivi kuwa nina tatizo la Figo alimuulizaย  Mamaย 

    “Mama unajuwa matibabu ya Figo yana gharama kubwa sana naย  kama hivyo umesema yanahitajika ndani ya siku 30 tu,ย  itakuwaje?ย 

    “Sasa unafikiria nitafanya nini Kijana? Japo yupoย  aliyejitokeza kugharamia matibabu ila hatuwezi kumuachia yeyeย  kila kitu ndiyo maana nimekueleza na wewe ili nione kwaย  upande wako utajitoa vipi maana Jacklin ni wako wewe” Mamaย  alisema, maneno ya Mama yalijaa uchunguzi sanaย 

    “Mama naomba siku moja ya kutafakari kisha nitakupa mrejeshoย  wa nini ambacho mimi nitafanya, ila nakuahidi kuwa tupoย  pamoja” Alisema Mosses, basi siku hiyo niliruhusiwa kurudiย  nyumbani ila nilikuwa nahisi maumivu kiasi fulani kwenyeย  mbavu zangu, jinsi Mama alivyokuwa akinifanyia kila kituย  ilinitia shaka sana nilimwambiaย 

    “Mama Mimi nipo sawa huna haja ya kunifanyia kila kitu” “Nafanya sababu nakupenda Jacklin” alisema Mamaย 

    “Najuwa kuwa unanipenda lakini nilianguka sababu ya baridi tuย  Mama hakuna kingine, nipo sawa” Mama hakusema chochote kileย  kuhusu tatizo nililokuwa nalo la figo, siku iliyofuata Osmanย  alienda Dubai kama alivyomwambia Mama.ย 

    Usiku wa siku hiyo, kilikuwa kipindi cha mvua hivyo kulikuwaย  na baridi sana, Mama alikuja na kuniambia kuwa Osman alikuwaย  ameshaondoka, ilinishangaza sana namna ambavyo Osman na Mamaย  awalikuwa karibu kiasi hicho hadi kuanza kujuwa kuhusu safariย ย 

    za Osman, nilicheka kwanzaย 

    “Mmh! Mama nawe, yote hayo umeyajuaje? “

    “Si kaniambia mwenyewe jana kule Hospitali, alafu Jacklinย  ngoja nikuulize swali, unamuonaje Osman?”ย 

    “Mh! Mama hebu liweke vizuri hilo Swali, namuonaje kivipiย  tena?”ย 

    “Hujausoma Moyo wake? Hujahisi kitu ndani ya moyo wa yuleย  Kijana?”ย 

    “Sasa Mama naanzaje kuusoma moyo wa Mtu ambaye sina ukaribuย  naye? Alafu hata kama akiwa na kitu moyoni mwake mimi tayariย  nina Mtu wangu..”ย 

    “Sijamaanisha eti uwe naye hapana ila nimekuuliza tuuย  Jacklin, anaonekana ana upendo sana yule Kijana” Mamaย  aliendelea kusema mafumbo ila niliijuwa nia yakeย 

    “Yaani Mama kisa tu ana hela basi umechanganikiwa kiasiย  hicho, kweli umasikini mbaya sana Mama, ila usijali siku siyoย  nyingi nitaanza kazi nitakufanyia kila kitu, sawa Mama?”ย 

    “Mmh! Sawa” Mama alisema kisha aliondoka zake ila aliniachaย  na jambo la kufikiria ndani ya akili yangu, nilikumbukaย  kitendo chake cha kuondoka pale wodini baada ya Mossesย  kuingia, ila ni yeye ndiye aliyempigia simu Mosses baada yaย  kuchukua namba kwenye simu yangu.ย ย 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Tatu Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxย 

     

    Pumzi ya mwisho

    15 Comments

    1. Tumpe on October 12, 2024 7:23 pm

      Dooohhh ๐Ÿฅดhuyu moses apotelee mbali bhn abaki Osman๐Ÿ˜‚

      Reply
      • Tuddy on October 12, 2024 7:47 pm

        ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ™Œkivumbi

        Reply
      • Charz jr๐Ÿ˜Ž on October 13, 2024 10:54 am

        Hii inanikumbusha kuna tamthiliya moja ya mfadhili …kiswahil Advance level

        Reply
    2. Lus twaxie on October 12, 2024 8:26 pm

      Mm limoses nshaanza kuliona n jau …awe n Osman tu

      Reply
      • Rickford on October 13, 2024 12:03 pm

        Lus unapenda ela wew๐Ÿ˜‚

        Reply
    3. ALLY YUSUFU on October 12, 2024 9:30 pm

      sidhani kama moses atapatikana tena kwenye simu

      Reply
    4. Nelca on October 12, 2024 9:42 pm

      Huyo Moses ayeyukiee juani

      Reply
    5. Henderson on October 12, 2024 10:15 pm

      Ef 5 tu alizima itakuwa kuchangia Figo๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ’”

      Reply
    6. G shirima on October 12, 2024 11:45 pm

      Dada wa wap uyu mbona achangamkii fursa

      Reply
    7. Karimu on October 13, 2024 7:31 am

      Aah uhondo huu natamani usiishe hongera Kwa kaz mzuri ๐Ÿ™Œ

      Reply
    8. Sabiti Mussa23 on October 13, 2024 7:45 am

      Ongeza kidogo urefu wa liwaya mtunzi tunaenjoy sana.. ๐Ÿ™Œ๐Ÿฟ

      Reply
    9. Charz jr๐Ÿ˜Ž on October 13, 2024 10:55 am

      I SEE MFADHILI ON ONE AND TWO๐Ÿ˜๐Ÿ˜

      Reply
    10. Mgote on October 13, 2024 11:52 am

      Mwandishi ungekuwa mcheza mpr.. bc tungekuita pele..

      Reply
      • Selestin on October 14, 2024 11:18 am

        https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J

        Reply
    11. DAUD DEOGRATIAS on October 16, 2024 5:38 am

      Osman anaenda kuchukuwa mzigo kupitia ushawishi wa mama

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi June 9, 2025

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Ilipoishia Return of Faudhia sehemu ya naneย  “Safi” sauti ya pili nayo ilisema kutokea chumba…

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Saba-07)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Sita-06)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.