Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home Β» Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Pili (02)
    Hadithi

    Pumzi Ya Mwisho Sehemu Ya Pili (02)

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaOctober 12, 2024Updated:October 28, 202416 Comments8 Mins Read6K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia “Jacklin Mwanangu sijapata pesa kama unaweza kusubiria hadiΒ  jioni sawa” Alisema MamaΒ 

    “Usijali Mama nitarudi tu” Nilisema, sikuwa na pesa ya nauliΒ  ya kurudia nyumbani alafu mvua ilikuwa ikinyesha sana,Β  kulikuwa na hali ya radi pia, nilifikiria kama OsmanΒ  angelinikuta pale nje ingeleta picha mbaya zaidi, nilifikiriaΒ  pia ile pesa niliyompa kwa hasira, nilijilaumu sana kwaΒ  kiburi changu. Basi niliingia kwenye mvua, nilivua viatuΒ  vyangu. EndeleaΒ 

    Kumbe yule Mdada msaidizi wa Osman alikuwa akiniangalia tu,Β  alienda kumwambia Osman, nilitembea kwenye mvua nikiwaΒ  natetemeka, kufika nyumbani kwetu kwa mguu ni zaidi ya masaaΒ  matatu. Kwa jinsi mvua ilivyokuwa ikinyesha ilionesha waziΒ  kuwa isingelinyamaza kwa muda huo, basi niliendelea kutembea.Β  Osman alipopata taarifa kuwa natembea kwenye Mvua aliachaΒ  kazi zake, alichukua Mwamvuli akaingia kwenye gari yakeΒ  akaanza kunifukuziaΒ 

    Ilifika mahali baridi lilinizidia, nilitembea kwa maumivuΒ  makali huku nikimfikiria sana Mosses, kwanini hakunitumiaΒ  hiyo pesa? Kwanini alikuwa hapokei simu zangu, nilijikutaΒ  nikilia njiani sababu moyo wangu nilimpa Mosses, niliulaumuΒ Β umasikini ambao Baba yangu alituachia, nilimlaumu MunguΒ  kwanini alimchukua Baba wakati akiwa masikini?

    Mara nilisikia Honi ya gari, niliipisha ipite lakiniΒ  haikufanya hivyo, alikuwa ni Osman. Nilipogundua ni yeyeΒ  niliondoa mikono yangu kifuani, nilitabasamu ili asione kamaΒ  kutembea kwenye mvua kumetokana na kutokuwa na hela bali niΒ  mazoezi tuu. Alishusha kioo akaniambiaΒ 

    “Ingia kwenye gari nikusogeze Jacklin” Alisema kwa busara naΒ  hekima ya hali ya juu sana, pesa alizonazo Osman hakustahiliΒ  kuninyenyekea namna ileΒ 

    “Hapana nafurahia maajabu ya Mungu” Nilisema huku nikiwaΒ  napiga hatua huku Osman akiendesha taratibu.Β 

    “Hapana mvua ni kubwa sana Jacklin, twende nikupeleke kwenu”Β  Alisema tena OsmanΒ 

    “Usijali Osman, nitachukua Tax mbele, nafurahia mvua kwanza”Β  Nilisema nikiwa nimeshikilia viatu vyangu mkononi, Basi OsmanΒ  alifunga kioo ili aondoke zake, kiukweli hali yangu haikuwaΒ  nzuri, lile baridi lilinitesa sana, njaa ilikuwa ikinikwanguaΒ  vibaya mno, nilijikuta nikianguka kwenye mvua.Β 

    β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’β€’Β 

    Nilipokuja kurudisha fahamu zangu nilijikuta nikiwaΒ  Hospitali, Osman alikuwa amekaa kitandani, Mama yangu alikuwaΒ  pembeni yanguΒ 

    “Mama!” Nilimuita MamaΒ 

    “Jacklin Mwanangu, nesi Mwanangu ameamka” Alisema Mama,Β  alinifanya nitabasamu sana, Upendo wa Mama ulikuwa Mkuu sanaΒ  kwangu, niligeuza macho na kumtazama OsmanΒ 

    “Asante sana Osman” Nilisema nikiwa natabasamu japoΒ  nilipoteza fahamu ila nilijuwa tu aliyenisaidia alikuwa niΒ  Osman, kabla hajanijibu Chochote nesi alikuja kwa ajili yaΒ  kuangalia hali yangu, Osman alimwambia MamaΒ 

    “Naomba tuongee kidogo Mama” Basi Mama na Osman walitoka hukuΒ  Daktari akiwa ananiangalia kwa makini na kiniuliza baadhi yaΒ  Maswali ili kujuwa nilikuwa najisikiaje.Β 

    Osman alionekana kuwa mwenye msongo wa mawazo, alimuulizaΒ  MamaΒ 

    “Huyu ni Binti yako wa kumzaa?” Mama alitabasamu kishaΒ  alimjibu Osman

    “Ndiyo, ndiye Mtoto pekee ninayemtegemea, nakushukuru sanaΒ  Baba japo sijakufahamu maana umenipigia tu simu na kunielezaΒ  kuhusu hali ya Binti yangu, kwa jinsi nilivyokuwaΒ  nimechanganikiwa wala sikuwa na muda wa kukuuliza” AlisemaΒ  MamaΒ 

    “Naitwa Osman, Mimi ndiye mmiliki wa kampuni ambayo BintiΒ  yako alikuja kuomba kazi” Alijitambulisha Osman kwa MamaΒ  yanguΒ 

    “Ooh! Asante sana Baba” Alisema MamaΒ 

    “Sasa Mama! Pamoja kwamba hali ya Binti yako unaiyona ipoΒ  sawa lakini kuna tatizo kubwa sana katika mwili wake,Β  inaoneka figo zake zote mbili hazifanyi kazi ipasavyo,Β  inatakiwa kubadilishwa, kama zitapatikana mbili au moja iliyoΒ  imara sana” Alisema Osman, Mama alishindwa hata kusimamaΒ  aliomba akae kwanza, akiwa kama Mama alichanganikiwa sanaΒ  kusikia nina tatizo la figo zanguΒ 

    “Unasemaje?” Aliuliza Mama akiwa anakaribia kuanza kuliaΒ 

    “Ndiyo maana Mama nimekuita hapa iliniweze kuzungumza na weweΒ  kuhusu hali ya Jacklin, ana siku 30 za kufanyiwa matibabu”Β  alisema OsmanΒ 

    “Sasa mimi na umasikini huu nitaweza vipi Baba yangu? MunguΒ  kwanini ananipa mtihani mzito kiasi hiki niimemkosea niniΒ  Mimi?” Alisema Mama akiwa analia, Osman aliketi na kumwambiaΒ  MamaΒ 

    “Mimi nina safari ya kwenda Dubai kesho, gharama zoteΒ  nitazifanya. Mnapaswa kutafuta Mtu wa kumtolea figo Jacklin”Β  Alisema Osman, angalau Mama alifuta mchozi wakeΒ 

    “Nitakuunganisha na daktari Bingwa wa hii Hospitali,Β  mtasaidiana itakapopatikana hata moja imsaidie Binti yako”Β  Alisema Osman, Mama alimtazama Osman akamwambiaΒ 

    “Wewe ni Binadamu mwenye moyo wa peke yako Mwanangu, MunguΒ  azidi kukubariki kwenye kila hatua” Alisema MamaΒ 

    “Ila Mama naomba hili liwe siri yako, Jacklin hapaswi kujuwaΒ  kama ana tatizo la figo sababu akijuwa inaweza leta shidaΒ  zaidi” Alisema Osman, walipomaliza kuzungunza walirudiΒ  wodini, walinikuta nikiwa ninafakamia vyakula maana njaaΒ  niliyokuwa nikiisikia haikuwa ya kawaida, sura zaoΒ  hazikuonesha dalili ya tatizo lolote lileΒ 

    “Jacklin!” Aliniita Mama kisha aliketi kitandani

    “Kama kuna Binadamu ana roho nzuri katika hii Dunia basi huyuΒ  Kijana ni namba moja, namshukuru kwa kuokoa Maisha yako”Β  Alisema Mama kisha alitabasamu, kumbe Osman alikuwaΒ  amewasiliana na Mosses na kumwambia kuwa nilikuwa nina umwaΒ  sababu namba ya Mosses nilisave kama Mume wangu, alikuja mudaΒ  huo, alinikumbatia na kunipiga busu mbele ya Mama na Osman,Β  Mama alishangaa sana sabahu alikuwa hamfahamu MossesΒ 

    “Mama!! Huyu anaitwa Mosses, ni..ni…ni” nilishindwaΒ  kumtambulisha Mosses mbele ya Mama na Osman, Basi muda huoΒ  huo Osman aliaga na kuondoka zakeΒ 

    “Mama huyu ni Mchumba wangu anaitwa Mosses…..Mosses huyu niΒ  Mama yangu” Nilijitahidi hadi kumtambulisha Mosses kwa MamaΒ  yangu, japo niliona Mama hakufurahia ila alijikaza tuΒ 

    “Oooh!! Sawa, basi mpate muda wa kuongea Mimi naenda kwaΒ  daktari” Alisema Mama, kumbe alikuwa anataka kumuwahi OsmanΒ  nje, kweli alimkimbilia Osman kabla hata hajapanda kwenyeΒ  gari akamuita, alipomfikia alimwambia OsmanΒ 

    “Baba upo sawa?” Aliuliza MamaΒ 

    “Ndiyo Mama nipo sawa, naenda kuendelea na kazi” AlisemaΒ  Osman, ila Mama alihisi kuna jambo lipo ndani ya Osman kwaΒ  jinsi alivyoaga pale wodini.Β 

    “Nakuomba Mwanamgu, msaidie Jacklin apone na Mungu atakulipaΒ  zaidi” Alisema Mama, Osman alimsogelea Mama akamwambiaΒ 

    “Ni jukumu nililokuahidi Mama, Mwanao atarudi kuwa sawa tuΒ  wala usijali, hii hapa ni kadi yangu ya Biashara” alimpatiaΒ  Mama kadi yenye mawasiliano yake, Osman aliingia kwenye gariΒ  yake na kuondoka.Β 

    Mosses alikuwa ndiyo Mwanaume niliyempenda sana katika MaishaΒ  yangu, ndiye aliyenitoa usichana wangu, nilimuulizaΒ 

    “Kwanini ulikuwa haupokei simu yangu?”Β 

    “Samahani Mke wangu, unajuwa muda ule nilipatwa na dharuraΒ  nikaenda kumuona Mdogo wangu alikuwa ana tatizo” AlisemaΒ  MossesΒ 

    “Ooh pole sana, anaendeleaje”Β 

    “Yupo sawa, hivi huyu jamaa aliyekuwa amekaa hapa ni nani?Β  Mbona baada ya kukupiga busu aliaga?” Aliuliza Mosses

    “Mmmh! Jamani Mosses, ni rafiki tu, ndiye aliyenisaidia”Β  nilimjibu Mosses, kitu kilichokuwa kikinivutia zaidi kwaΒ  Mosses ni wivu wake kwangu, yaani nisisimame na Mwanaume auΒ  kuongea nayeΒ 

    “Anhaa! Sasa sitaki hayo mazoea na huyo jamaa sawa?” AlisemaΒ 

    “Mmmh! Sawa” Nilimjibu, Mama aliporudi alitukuta tukiwaΒ  tumemaliza mazungumzo, basi alimuita Mosses pembeni naΒ  kumueleza kilichokuwa kikinisibu sababu alikuwa Mtu wangu waΒ  karibu sana.Β 

    Mosses alipoambiwa hivi kuwa nina tatizo la Figo alimuulizaΒ  MamaΒ 

    “Mama unajuwa matibabu ya Figo yana gharama kubwa sana naΒ  kama hivyo umesema yanahitajika ndani ya siku 30 tu,Β  itakuwaje?Β 

    “Sasa unafikiria nitafanya nini Kijana? Japo yupoΒ  aliyejitokeza kugharamia matibabu ila hatuwezi kumuachia yeyeΒ  kila kitu ndiyo maana nimekueleza na wewe ili nione kwaΒ  upande wako utajitoa vipi maana Jacklin ni wako wewe” MamaΒ  alisema, maneno ya Mama yalijaa uchunguzi sanaΒ 

    “Mama naomba siku moja ya kutafakari kisha nitakupa mrejeshoΒ  wa nini ambacho mimi nitafanya, ila nakuahidi kuwa tupoΒ  pamoja” Alisema Mosses, basi siku hiyo niliruhusiwa kurudiΒ  nyumbani ila nilikuwa nahisi maumivu kiasi fulani kwenyeΒ  mbavu zangu, jinsi Mama alivyokuwa akinifanyia kila kituΒ  ilinitia shaka sana nilimwambiaΒ 

    “Mama Mimi nipo sawa huna haja ya kunifanyia kila kitu” “Nafanya sababu nakupenda Jacklin” alisema MamaΒ 

    “Najuwa kuwa unanipenda lakini nilianguka sababu ya baridi tuΒ  Mama hakuna kingine, nipo sawa” Mama hakusema chochote kileΒ  kuhusu tatizo nililokuwa nalo la figo, siku iliyofuata OsmanΒ  alienda Dubai kama alivyomwambia Mama.Β 

    Usiku wa siku hiyo, kilikuwa kipindi cha mvua hivyo kulikuwaΒ  na baridi sana, Mama alikuja na kuniambia kuwa Osman alikuwaΒ  ameshaondoka, ilinishangaza sana namna ambavyo Osman na MamaΒ  awalikuwa karibu kiasi hicho hadi kuanza kujuwa kuhusu safariΒ Β 

    za Osman, nilicheka kwanzaΒ 

    “Mmh! Mama nawe, yote hayo umeyajuaje? “

    “Si kaniambia mwenyewe jana kule Hospitali, alafu JacklinΒ  ngoja nikuulize swali, unamuonaje Osman?”Β 

    “Mh! Mama hebu liweke vizuri hilo Swali, namuonaje kivipiΒ  tena?”Β 

    “Hujausoma Moyo wake? Hujahisi kitu ndani ya moyo wa yuleΒ  Kijana?”Β 

    “Sasa Mama naanzaje kuusoma moyo wa Mtu ambaye sina ukaribuΒ  naye? Alafu hata kama akiwa na kitu moyoni mwake mimi tayariΒ  nina Mtu wangu..”Β 

    “Sijamaanisha eti uwe naye hapana ila nimekuuliza tuuΒ  Jacklin, anaonekana ana upendo sana yule Kijana” MamaΒ  aliendelea kusema mafumbo ila niliijuwa nia yakeΒ 

    “Yaani Mama kisa tu ana hela basi umechanganikiwa kiasiΒ  hicho, kweli umasikini mbaya sana Mama, ila usijali siku siyoΒ  nyingi nitaanza kazi nitakufanyia kila kitu, sawa Mama?”Β 

    “Mmh! Sawa” Mama alisema kisha aliondoka zake ila aliniachaΒ  na jambo la kufikiria ndani ya akili yangu, nilikumbukaΒ  kitendo chake cha kuondoka pale wodini baada ya MossesΒ  kuingia, ila ni yeye ndiye aliyempigia simu Mosses baada yaΒ  kuchukua namba kwenye simu yangu.Β Β 

    Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Tatu Ya PUMZI YA MWISHO

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost RIWAYA Mpya Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAΒ 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAΒ Β 

    SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

     

    Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ  Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xx Pumzi Ya Mwisho xxΒ 

     

    Pumzi ya mwisho

    16 Comments

    1. Tumpe on October 12, 2024 7:23 pm

      Dooohhh πŸ₯΄huyu moses apotelee mbali bhn abaki OsmanπŸ˜‚

      Reply
      • Tuddy on October 12, 2024 7:47 pm

        πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™Œkivumbi

        Reply
      • Charz jr😎 on October 13, 2024 10:54 am

        Hii inanikumbusha kuna tamthiliya moja ya mfadhili …kiswahil Advance level

        Reply
    2. Lus twaxie on October 12, 2024 8:26 pm

      Mm limoses nshaanza kuliona n jau …awe n Osman tu

      Reply
      • Rickford on October 13, 2024 12:03 pm

        Lus unapenda ela wewπŸ˜‚

        Reply
    3. ALLY YUSUFU on October 12, 2024 9:30 pm

      sidhani kama moses atapatikana tena kwenye simu

      Reply
    4. Nelca on October 12, 2024 9:42 pm

      Huyo Moses ayeyukiee juani

      Reply
    5. Henderson on October 12, 2024 10:15 pm

      Ef 5 tu alizima itakuwa kuchangia FigoπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ’”

      Reply
    6. G shirima on October 12, 2024 11:45 pm

      Dada wa wap uyu mbona achangamkii fursa

      Reply
    7. Karimu on October 13, 2024 7:31 am

      Aah uhondo huu natamani usiishe hongera Kwa kaz mzuri πŸ™Œ

      Reply
    8. Sabiti Mussa23 on October 13, 2024 7:45 am

      Ongeza kidogo urefu wa liwaya mtunzi tunaenjoy sana.. πŸ™ŒπŸΏ

      Reply
    9. Charz jr😎 on October 13, 2024 10:55 am

      I SEE MFADHILI ON ONE AND TWO😁😁

      Reply
    10. Mgote on October 13, 2024 11:52 am

      Mwandishi ungekuwa mcheza mpr.. bc tungekuita pele..

      Reply
      • Selestin on October 14, 2024 11:18 am

        https://whatsapp.com/channel/0029VarTsGt1t90TiJVyWi0J

        Reply
    11. DAUD DEOGRATIAS on October 16, 2024 5:38 am

      Osman anaenda kuchukuwa mzigo kupitia ushawishi wa mama

      Reply
    12. πŸ—‚ Email; SENDING 1.849976 BTC. Verify > https://graph.org/Payout-from-Blockchaincom-06-26?hs=8129b2dc21ae5edb74ddfb3b9fa33bf0& πŸ—‚ on June 28, 2025 8:26 pm

      a7kbsc

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi July 12, 2025

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-02

    Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya kwanzaΒ  β€œBaba” aliita Zahoro, Mzee Miroshi alimtazama Zahoro bila…

    Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa)-01

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Tisa-09)

    Return Of Faudhia ( Sehemu Ya Nane-08)

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.