Ilipoishia Nzena (Kijiji Kilicholaaniwa) sehemu ya nane
“Nakufahamu Zahoro, wewe ndiye jibu la Laana hii. Uliiona kabla haijaingia pia utaiona ikiondoka, huwezi kunielewa kwasasa lakini nitakueleza zaidi. Nifuate” alisema Mwanamke huyo, Bado aliacha maswali mengi sana kichwani kwa Zahoro. Taratibu Zahoro alianza kutembea kwa kuchechemea kutokana na majeraha ya Mguu aliyoyapta
Alitembea kidogo Kisha alianguka tena kutokana na kizunguzungu kilichosababishwa na njaa Kali na kiu. Anna akambeba Zahoro na kuondoka naye hapo.
SEHEMU YA TISA
Giza liingiapo Mzimu wa Bibi Lugumi huacha kufanya kazi ya Mauwaji. Kijiji Cha Nzena kilikua kimeharibiwa sana, Kila mahali ulionekana moshi ukifuka. Sauti za kutisha, Bundi walikua wakilia Usiku huo.
Ndani ya pango Moja, Zahoro alikua amelala juu ya jiwe, jasho jingi lilikua likimtoka. Kando yake alikuwepo Anna pamoja na Upendo. Naaam‼ yule Upendo aliyepotea
machoni mwa Zahoro wakati ule alikua mikononi mwa Mwanamke huyo wasiye mfahamu aliyejiita Mwokozi.
Usingizi mzito ulikua kichwani kwa Zahoro, ndoto ya kutisha ilianza kupita taratibu mithiri ya picha Mjongeo. Ndoto hiyo ilimfanya Zahoro kuhangaika, Anna akamwambia Upendo
“Kama atakumbuka anachokiota atatoa jibu la namna ya kuondoka hapa salama” alisema akiwa anamwangalia sana Zahoro, wakati huo Kibatari kilikua kinawaka huku kikisombwa sombwa na Upepo wa hapa na pale. Jasho jingi liliendelea kumvuja Zahoro, Kisha Ndoto yake ilianza kama filamu ya kutisha sana.
Ndoto ya Zahoro.
Zahoro alianza kuona Msitu wa kutisha sana, uliofungamana na Barafu Kali lililoganda na kufanya Msitu kua na rangi nyeupe. Hali hiyo iliashiria kua pasingelikua na Kiumbe kilicho hai kutokana na Baridi Kali.
Katika Hali isiyo ya kawaida alianza kuwaona Watoto wawili wa Miaka Nane, Mtoto mmoja alikua Msichana na mwingine ni Mvulana. Watoto hao walivalia mavazi ya thamani mfano wa Watoto wa kifalme
Mtoto Mmoja akasimama Kisha akamwambia mwenzake.
“Tucheze Mchezo wa Kujificha kwenye Barafu” aliyesema alikua ni Msichana, yule Mvulana akakubali haraka sana Kisha akamwambia yule Msichana.
“Utajificha Kisha nitakutafuta, nikikuona nakuuwa” alisema akiwa anatabasamu. Kisha yule wa Kike akakubali haraka sana kua akionwa basi atauawa na yule Mtoto wa Kiume.
Eneo Hilo lilikua lenye baridi Kali sana lakini Watoto hao wala hawakutetemeka kwa baridi. Siku zilienda, majira yaliondoka Watoto hao wawili waliendelea kutafutana, Hadi walipofikisha umri wa ujana Bado walikua Msituni angali wanatafuna.
Kila mmoja hakuweza kuiona njia ya kurejea nyumbani. Upanga wa Mwanaume ulianza kupata kutu Kisha kwa hasira aliamua Kujichinja mwenyewe kutokana na kushindwa kumpata yule wa kike.
Kijana wa Kiume wakati anatapatapa pale chini ndipo sura yake halisi ilipoonekana, alikua ni Zahoro, alipojichinja TU yule wa kike alitokea Kisha akamwambia Zahoro
“Nilipaswa kufa ili utoke hapa Msituni urudi nyumbani, umekosea sana” Kauli hii ilikua inajirudia sana tena kwa sauti ya Juu sana, kadili yule Mwanamke alivyokua anairudia Kauli hii ndipo sura yake halisi ilipo onekana, alikua ni Upendo
Pale pale Zahoro akashtuka kutoka Usingizi mzito, hewa ilikua nzito sana kwake akajikuta akikaa kwa lazima ili aivute hewa. Macho yalimtoka, akavuta hewa nzito ya lazima ili kuurudisha uhai wake, akajikuta akihema haraka haraka huku akiangaza huku na kule
Alimwona Anna Kisha alimwona Upendo, alishusha pumzi huku taratibu Hali yake ikianza kukaa sawa. Kitu Cha Kwanza alipewa chakula ili aimalize njaa yake, alifakamia chakula bila kuuliza swali lolote lile kwani alikua na njaa isiyo mithirika.
Alipomaliza kula alishushia na Maji mengi Hadi akapaliwa, Kisha akamtazama Upendo. Akamuuliza
“Ulipotelea wapi? Nilijua umeshakufa” Upendo alionesha tabasamu huku chozi likimtoka, akatikisa kichwa chake kuashiria kua alipitia magumu. Chozi lilimbubujika Upendo, Kisha Anna akamwambia Zahoro
“Nilimwokoa kutoka kifo kama nilivyofanya kwako, hamko peke yenu hapa. Mpo Watu sita mliosalia Kijiji kizima” alisema Anna, mara Watu wengine walifika hapo. Bahati nzuri kati Yao Mmoja alikua ni rafiki wa Zahoro, alimlaki kwa furaha sana Kisha alimtazama juu Hadi chini, hakuamini kama angelisalia Mtu mwingine kua mzima kutokana na Uharibifu mkubwa uliotokea Kijijini.
Zahoro akamkumbatia rafiki yake aliyeitwa Yasin.
**
Kijiji Cha Nzena kilichokua na Wakazi zaidi ya Elfu moja walibakia sita na Anna ambaye hajulikani ni Mtu kutoka wapi. Mzimu wa Bibi Lugumi ulikiangamiza Kijiji chote, ardhi nzuri iliyopendwa na kusifiwa iligeuka kua Kuzimu ndani Muda mfupi sana.
Giza nene lilikifunika Kijiji kizima, ni nyakati za Usiku pekee ambazo Mzimu wa Bibi Lugumi ulikua hauwezi kufanya Mauwaji.
Ndani ya Pango palikua kimya sana, hapakusikika sauti ya Mtu kuzungumza chochote kile. Zahoro alikua machoni pa Anna Kila dakika alikua akimtazama sana kana kwamba alikua akimchunguza. Kisha alipogeuza shingo yake akapeleka macho kwa Upendo, akamwona akiwa anasinzia
Alizungusha tena macho yake kwa Watu wengine aligundua pia walikua wakisinzia, Kisha aliendelea kumtazama Zahoro ambaye alionekana Hana hata lepe la Usingizi. Alikua kimya akionekana ni mwenye mawazo, basi taratibu Anna alinyanyuka Kisha alisogea mahali alipokua amekata Zahoro
“Nifuate, nataka kuzungumza nawe” alisema Anna Kisha alipinga hatua zake akazama kwenye Moja ya njia, Zahoro naye akanyanyuka na kumfuata Anna asijuwe mahali ambako alikua akilekea. Alijikuta akitokea juu kabisa ya mlima, alikua akikitazama Kijiji kwa uzuri japo palikua Giza lakini baadhi ya maeneo yalikua yakiwaka moto na kufuka moshi Mkubwa.
Mbele yake alikua amesimama Anna akiwa anatazama taswira ya Kijiji, Zahoro akasimama ubavuni mwa Anna huku NAYE akisindikiza macho yake mbele.
“Nilifika nje ya Kijiji kupitia njia Moja” alisema Zahoro kwa sauti ya utaratibu. Anna alimeza funda la mate lakini hakuonekana kushtuka kabisa
“Wewe ndiye ufunguo wa sote kutoka salama hapa” aliongea Anna kwa sauti ya utaratibu huku akipepesa macho yake, halafu akageuka na kumtazama Zahoro
“Kuna ndoto umeiota Zahoro, hiyo ndoto ni ufunguo wa kutoka hapa…” aliendelea kusema Anna. Kumbe wakati wanazungumza, Upendo alikua akija taratibu
Wakati Anna na Zahoro wanatoka kule ndani yeye alikua hajalala, alihitaji kusikia ni kitu gani ambacho Zahoro na Anna walihitaji kuongea kwa Siri, akabana mahali na kuanza kusikiliza.
“Kumbuka ulichokiota Zahoro, huo ndio ufunguo pekee wa sisi kutoka hapa na kurejea kwenye Dunia halisi” alisistiza sana Anna, sauti yake ilijaa Msistizo wa Hali ya Juu sana. Zahoro alionekana kuzubaa
“Lakini wewe ni Nani na umetokea wapi?” aliuliza Zahoro Kisha alisogea nyuma kidogo huku akimkazia macho Anna.
“Sikia Zahoro, Mimi hapa ni Mwokozi..”
“Sasa kama ni Mwokozi kwanini usituokoe badala ya kusema kuhusu ndoto?”
“Tatizo lako haujui upo wapi, hapa ni Kuzimu Zahoro, Mimi mmenikuta huku nimekaa kwa zaidi ya Miaka 30 nikisubiria sababu ya kurudi Duniani kuishi kama Binadamu Wengine. Na ili sisi tutoke ni lazima kuna Mtu abakie huku, niambie umeota kuhusu nini?” aliuliza tena Anna.
Akamfanya Zahoro awaze mara mbili mbili kama alipaswa kumwamini Anna, akakuna nywele za kichwa chake kama ishara ya kutafakari Kisha akajiambia kua kama kusimulia alichokiota kutawafanya kurejea Dunia, basi atamsimulia. Taratibu akasema
“Nimeota kuhusu Watoto wawili lakini wenye sura yangu na Upendo. Wakiwa Msituni, wakicheza Mchezo wa Kujificha” alisema Kisha alisita kidogo akageuka nyuma kule alikojibana Upendo, haraka Upendo akajificha. Zahoro hakufanikiwa kuona chochote, pengine alihisi uwepo wa Mtu Kisha aliendelea
“Mtoto wa Kiume akaahidi kumuuwa yule wa Kike endapo atampata. Ahadi yake ilichukua Miaka mingi bila mafanikio ya kumwona wa kike. Waliendelea kutafutana bila kurudi nyumbani kwao kwa Miaka Kenda Hadi wakawa wakubwa, yule Mwanaume akaona ni Bora ajiuwe kwa kushindwa kutekeleza ahadi yake kwa hakufanikiwa kuona njia ya kutokea.”
“Enhee, ikawaje?”
“Alijichinja kwa kutumia Upanga, akiwa chini ndipo yule Mwanamke akatokea na kumlaumu sana akimwambia kua hakupaswa kujiuwa badala yake alipaswa kumuuwa wa kike ili apate njia ya kuondoka Msituni” Macho yakamtoka Anna Kisha tabasamu likajaa usoni pake, akaangaza huku na kule akamwambia Zahoro
“Tafsiri ya ndoto Yako ni kwamba ili tutoke hapa unapaswa kumtoa kafara Upendo” alisema, maneno haya yalimshtua sana Zahoro. Akamtazama Anna akamuuliza
“Una akili wewe?” Aliuliza kwa hamaki Zahoro kama Mtu aliyepandwa na shetani wa ghafla, mazungumzo Yao yalimuumiza sana Upendo. Alipokua amejificha alitokwa na chozi. Alinyongea mwili pamoja na akili yake, alihisi kuuumia sana kihisia, lakini yeye ndiye njia ya wengine kua salama.
Kilio Cha chini chini kilikua kinamtoka Upendo akiwa amejificha, aliendelea kusikiliza
“Niliusubiria wakati kama huu Zahoro, ni lazima utende kwa kufuata ndoto Yako. Hauwezi kuangamiza walio wengi kwa ajili ya kumnusuru Mmoja. Upendo hatokufa Bali ataishi huku kama nilivyoishi Mimi huku akisubiria wakati wake ufike akomboe wengine” alisema Anna huku akimshika mikono Zahoro, alizungumza kwa sauti ya kuomba sana.
Maneno haya yalikua mwiba moyoni mwa Upendo, aliamua kurudi ndani ya pango. Hakutaka kuendelea kuumiza moyo wake kwa kusikiliza kile ambacho Anna alikua akimwambia Zahoro. Taratibu kama Mbwa aliyemwagiwa Maji alijilaza juu ya jiwe ndani ya pango huku akikitazama kibatari, macho yake yalikua yakitiririsha chozi.
Nje, Zahoro alikua njia panda. Kumwamini Anna NDIYO chaguo pekee lakini kuondoa Uhai wa Upendo haikuingia akilini mwake. Alikumbuka nyakati ngumu alizopita na Upendo, jinsi walivyokutana na kuanza safari ya pamoja ya matumaini, jinsi alivyo mlinda mara kadhaa kutoka kifo.
Alijikuta akichuchumaa, mkono mmoja akiwa ameshikilia mwamba wa jiwe la Mlima. Huku mkono mwingine akipikicha macho yake, alihisi kuguswa begani Kisha aliambiwa na Anna.
“Sitakulazimisha Zahoro, utachagua mwenyewe kama ni kuondoka au kubakia hapa kwa muda mrefu” Kisha aliondoka hapo na kurejea ndani ya pango.
Alimwacha Zahoro akiyapitia mawimbi makubwa ya mawazo, akajilaza juu ya jiwe huku akilitazama anga. Aliitumia mikono yake kama Mto wa kulalia huku moyo wake ukisema yote aliyoambiwa yalikua ni magumu sana kwake kuyatimiza.
**
Asubuhi ilimkuta Zahoro akiwa Bado juu ya jiwe amelala Usingizi wa Pono, alikua Sehemu ya Wazi ambayo nguvu za ajabu za Mzimu wa Bibi Lugumi zingeweza kumfuata hapo. Alikua amelala Chali, jua lilikua Bado halijainuka vizuri na kummulika pengine angeweza kushtuka.
Wakati huo Upendo alikua akimtazama Zahoro akiwa amejibana kwenye njia ya kuingilia pangoni, upepo wa taratibu ulikua unaanza huku sauti ya Mzimu wa Bibi Lugumi ikianza kusikika.
Japo aliyasikia maneno Yale ya Usiku uliopita lakini alimwonea huruma sana Zahoro, moyo wake ukamwambia akamwamshe. Mwili wake ulikua unazidi kusisimka kwa woga lakini miguu yake taratibu ilianza safari ya kunyata kumwelekea Zahoro
Mara akavutwa na kurudishwa nyuma Kisha akazibwa mdomo wake, alipogeuzwa alimwona Anna. Akapewa ishara ya kua kimya, pole pole Anna akasogea mbele huku akipiga mahesabu namna ya kumfikia Zahoro na kumwamsha hapo.
Matawi ya Miti ilianza kucheza kutokana na ule Upepo, huku sauti ikianza kuja karibu zaidi.
Anna akachomoa Upanga wake Kisha akasogea taratibu kuelekea alipo Zahoro, alipaswa kumlinda sababu ndiye njia pekee ya wao kutoka salama hapo. Sauti ilizidikupaa huku
upepo uliobeba majani ukianza kumzonga Zahoro, rabsha zikamwamsha na kujikuta kwenye Hali asiyo ielewa.
Katikati ya Upepo wenye majani makavu huku Sauti asiyoweza kuisahau iliendelea kusikika na kumkumbusha kua anapaswa kutoisikia lakini alikua kwenye taharuki nzito sana. Haraka Anna akakimbilia ili amsaidie lakini Hali ilionesha Wazi kua alikua ameshachelewa.
Hakua na nguvu ya kuuzuia Upepo wala kupambana nao, ni yeye pekee ambaye hakuweza kudhurika na sauti ya Kifo ya Bibi Lugumi. Chozi lilimtoka Anna akiangalia namna upepo mithiri ya Kimbunga ulivyozingira eneo ambalo Zahoro alikuwepo.
Hata Upendo pamoja na wale wengine wanne nao walikua wakihuzunika sana na kushindwa kuuzuia chozi lao.
Mioyoni mwao waliamini pasingelikua na uhai kwa Zahoro kutokana na Upepo ule Mkali sana, Kisha ulianza kupungua taratibu Hadi pale walipoweza kuuona mwili wa Zahoro ukiwa chini. Haraka wote walikimbilia hapo, walijitahidi sana kumwamsha Zahoro lakini ilionekana Wazi kua ulikua ni mwili mtupu.
Damu zilikua zikimtoka Zahoro kama ilivyo kawaida ya vifo vya Wanakijiji wote, hakuna ambaye hakuangusha kilio kumlilia Zahoro, wote walilia kwa Uchungu sana. Mtu pekee ambaye alilia zaidi alikua ni Anna ambaye kwa mujibu wa SIMULIZI yake
Yeye aliiishi Kuzimu kwa Miaka Mingi zaidi ya Thelathini huku akisubiria sababu ya yeye kurejea Duniani lakini aliona ndoto zake zikiwa zimekufa rasmi, Mtu pekee anayeweza kuijua njia ya kutoka hapo ni Zahoro kupitia ile ndoto yake.
Ghafla uso wa Upendo uliacha kuonesha majonzi, akafuta chozi lake huku akimtazama Anna aliyekua alijitahidi kumwamsha Zahoro. Ilionekana kua ni ngumu kwa Zahoro kurejea, alikua tayari ameshakufa.
Upendo akamsogelea haraka Anna na kuuchomoa Upanga wa Anna, wote walishtuka wasijue Upendo alikusudia nini. Upendo alianza kurejea nyuma pole pole huku Upanga akiwa ameuelekeza mbele akiashiria kua asiwepo yeyote wa Kumzuia, kwamba alichokusudia alitaka kitimie.
“Unafanya nini wewe?” alihoji Anna kwa sauti ya kuchanganikiwa sana huku chozi likiwa limeacha kutoka
“Tafadhali usinizuie, Nimesikia Kila kitu mlichozungumza na Zahoro Jana Usiku. Mimi ni kizuizi Cha nyinyi kutoka salama hapa” alisema Upendo kwa sauti iliyojaa kilio, Bado Upanga ulikua thabiti mikononi mwake akiwa anazidi kusogea nyuma akiuelekea ukingo wa Mlima huo, Anna alikua wa Kwanza kuona mahali ambapo Upendo alikua akielekea.
“Upendo hakuna kitakacho badilika kuanzia sasa, huna sababu ya kufanya chochote kwasababu tayari Zahoro ameshakufa” alisema kwa maumivu makali sana Anna, taratibu Upendo alianza kuushusha Upanga wake
Macho yake akayaelekeza kwa Zahoro aliyekua chini, Kisha akamtazama Anna akamwambia
“Ikiwa alijaribu kujiuwa baada ya kunikosa kwenye ile ndoto, basi naamini kifo changu ni salama yake…” yalikua ni maneno ya haraka yakifuatiwa na Uamuzi wa kupeleka Upanga shingoni pake Kisha Damu ikaruka, Ukingo wa Mlima ukamsomba Upendo na kumpeleka chini ya Mlima.
“Hapanaaaaa‼! Upendo” alisema Anna kwa sauti ya Juu lakini mbele yake palikua patupu, hapakua na Upendo. Haraka akakimbilia kwenye Ukingo wa Mlima na kuchungulia chini akamwona Upendo akiwa amejipigiza kwenye mwamba huku Damu nyingi ikimtoka. Alilia sana Anna, alikua amewapoteza Watu wawili muhimu sana kwenye Maisha yake. Ndio Ufunguo pekeee
Majonzi yalitawala, wote walionekana kuifahamu Hadithi hii ikawafanya wavunjike mioyoni Yao. Walikaa chini huku machozi yakiwatoka
Lakini wakaisikia sauti iliyowashtua sana ikiwauliza
“Kuna nini?” wote waligeuka, hawakuamini. Zahoro alikua amesimama akijipangusa Damu akionekana ni Mtu aliyeondoka na kurejea akiwa hafahamu kilichokua kimeendelea.
Yasin alikua wa Kwanza kumsogelea Zahoro huku chozi likimbubujika, alimpapasa ili kuhakiki kama alikua mzima. Alipogundua kua alikua salama alimkumbatia kwa hisia nzito sana, pale pale Anna naye alifika.
Naye akamkumbatia Zahoro kwa hisia Kali sana. Ilionekana Kila kitu kilikua kimefika mwisho lakini tumaini jipya likarejea ghafla.
Hata Zahoro alilia kwa Uchungu sana aliposimuliwa kilichotokea na kumfika Upendo, alikua amejitoa sadaka ili yeye aishi. Wote walisimama wakikiangalia Kijiji Cha Nzena namna kilivyokua kinafuka Moshi, sauti ya Bibi Lugumi ilikua ikisikika ikiwaambia
“Hakuna atakayetoka akiwa hai, hii ni ahadi yangu kwenu. Kifo chenu ni pumziko salama la Masumbuko, niliwalaani na vizazi kwa vizazi. Mnastahili kifo” sauti hiyo ilisema huku ikizidi kupaa na kwenda mbali zaidi. Hapakua tena na tumaini la Wao kuondoka Salama tena kwasababu tayari Upendo ambaye pia ndiye funguo alikua ameshafariki.
Je, Ndiyo mwisho wao?
Watasubiria kwa Miaka Mingapi ili kupata sababu ya kurejea Dunia halisi?
MWISHO WA SEASON 1, USIKOSE SEASON 2. Unaitaka Lini?
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa Hapa
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896
Kijiji Kijiji
17 Comments
Season 2 ianze ijumaa
Kumbe Kuna season tena waisha bs ijumaa
Season 2 Ijumaa boss ianze mana ni moto wa bati, ni mwendo mpera mpera
leo
Ijumaaa jmn please
Ijumaa ianze season 2 imekuwa moto maskini zahoro upendo wake umeshaondoka
https://shorturl.fm/2uiUR
Good story
ianze. Leo
https://shorturl.fm/gLRJ0
Nzuri sana
Safi sana
https://shorturl.fm/2EAjd
So delicious story inatoa stress Kwa uraiiin duuu nipe namba ya mtunz japo apate ya maji
https://shorturl.fm/P8Yiq
https://shorturl.fm/31FvM
https://shorturl.fm/tPPpn