Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 04
βUnamkumbuka Zena?β nilimuuliza, alionekana kutafakari kidogo kisha akaniuliza βYule rafiki yako?βΒ
βNdiyo!βΒ
βKimetokea nini?β aliniuliza kwa shahuku kubwa sana, sura ya Mama yangu haikua na hatiaΒ lakini nilijiuliza maswali mengi, nilijiuliza kama kweli hafahamu chochote vipi kuhusu janaΒ Usiku walipotoka kwenye lile shimo yeye na Baba, wana uhusiano gani na Mwanamke anayeliaΒ kwenye ile stoo? . Endelea
SEHEMU YA NNE
βAmefariki Mamaβ nilisema kwa sauti ya kilio. Mama alishtuka sana kuliko kawaida, alishtukaΒ kama vile alimfahamu Zena kwa muda mrefu sana, alishika kifua chake hadi nilishtukaΒ
βMamaβΌβ nilimwita sababu namna alivyoipokea taarifa alikua kama amepandwa na presha.Β AlinitazamaΒ
βPole Binti yangu, pokea rambirambi zanguβ alisema kwa sauti ya upole sana kisha alisimama.Β Nilikua namtazama Mama yangu kama vile ilikua ndiyo mara ya kwanza namwona,Β alivyobadilika ghafla alizidi kunipa mawazo zaidi.Β
Simu yangu ilianza kuita tena, pochi yangu ilikua karibu na Mama yangu. Akanipatia Pochi,Β niliona ni bora niitoe simu niipokee, ilikua ni Namba ngeni. Kilichokua akilini mwangu niliwazaΒ huwenda napewa ratiba za mazishi ya Zena, taratibu niliipokea na kuiweka sikioni bila kusemaΒ chochote, niliisikia sauti ya kiume ikiniulizaΒ
βWewe ni Celin?β moyo wangu ulifanya paaa kama nimewagiwa na maji, nilisimamaΒ βEeh Ni Mimi!βΒ
βMimi ni Msamalia mwema, nimemsaidia rafiki yako Caren alikua amepata ajali mbaya sanaΒ jana Usiku. Yupo hapa Hospitalini, namba hii nimeikuta kwenye simu yake ndogo nikaonaΒ nikueleze kama unaweza kuja hapa Hospitali ya Jijiβ Moyo wangu ulianza kunienda mbio,Β niliyakumbuka maneno ya Yule Bibi wa ajabu kua nitapoteza niwapendao kwa Mpigo.Β
Nguvu ziliniisha, nilijikuta nikiidondosha simu sakafuni kisha niliketi kitini kama mzigo. MachoΒ yangu niliyaelekezea chini, chozi la ajabu lilinitoka. Nilijikuta nina hatia kubwa sana kwaΒ kumshirikisha Caren kwenye hili jambo. Upepo ulianza taratibu huku ukipeperusha pazia, MamaΒ yangu alinisogelea kwa utaratibu sana akaniulizaΒ
βKuna nini Celin?β nilimeza mate, nilikua kama Zezeta. Nilinyanyua macho yangu taratibuΒ yakiwa yamejawa na uzito wa chozi lililoganda machoni pangu. Nilimtazama Mama yangu kamaΒ Mtu niliyepooza mwili mzima nikamwambiaΒ
βCarenβΌβ Mama alinitikisa kunirudisha kwenye ufahamu wangu lakini juhudi zake hazikufuaΒ dafu, uono ulinikimbia. Kila kitu nilikiona kipo mbali, hata pumzi zangu zilianza kunisalitiΒ taratibu, niliona giza huku nikihisi ubaridi mwilini mwangu. Nilipoteza fahamu mikononi mwaΒ Mama yangu.Β
****Β
Nilianza kusikia sauti inayofanana na kengele, sauti ilizagaa kichwa kizima. Ghafla nilishtuka,Β nilizinduka kutoka Usingizini. Mwili ulikua unauma, nilikua mchovu sana. Niliangaza huku naΒ kule, niligundua nilikua kwenye chumba cha Hospitali, nilikua kitandani. Macho yanguΒ yalikutana na macho ya Baba yangu pamoja na Mama yangu.
Mmoja aliketi upande wa kulia na mwingine aliketi upande wa kushoto, wote walionekanaΒ kunisubiria niamke. Nilipotaka kujitingisha Baba yangu alinizuiaΒ
βTaratibu Celinβ alisema kwa sauti ya kujali sana. Hakuna kilichokua kimbebadilika kichwaniΒ kwangu. Nilijiuliza kama nilikua nawafahamu vyema wazazi wangu, nilitikisa kichwa kwa mbaliΒ kua nilikua sijawafahamu vizuri wazazi wangu. Hapo hapo niliikumbuka sababu ya MimiΒ kuwepo Hospitali, ni simu ile niliyopigiwa kuhusu CarenΒ
Nilihema kwa uchovu, halafu nikamtazama Mama maana yeye ndiye aliyekua na Mimi wakatiΒ napoteza fahamu.Β Β
Mama yangu aliyasoma Mawazo yangu akawa wa kwanza kusema.Β
βCelinβΌβ aliniita Mama, niliiona sura yake ilivyojaa upole na unyongefu uliopitiliza, alitumaΒ ujumbe kwa sura yake nikajua fika kua Caren alikua amefariki kutokana na ile ajali, MamaΒ yangu alinitazama kwa jicho la kunipa pole. Alikua akipepesa macho yake, aligeuza shingo naΒ kumtazama Baba yangu.Β
Baba naye aligeuza shingo yake na kunitazama, alikua na sura ile ile aliyonayo Mama yangu.Β Sura zao zilikua zimejaa huzuni na huruma. Baba alinishika mkono wangu uliokua una sindanoΒ iliyotumika kunipatia maji mwilini.Β
βCelin, pole sana. Umepoteza marafiki wawili ndani ya siku mbiliβ alisema Baba kwa sauti yaΒ Upole sana, sura yake ilijaa huruma sana. Hawakuonekana kama wana hatia lakini kwaniniΒ walikua kwenye lile shimo kule stoo, kuna uhusiano gani kati yao na yule Mwanamke anayelia.Β Swali hili lilihitaji majibu ya haraka, siyo rahisi wao wakanipatia Majibu.Β Β
Chozi lilianza kunidondoka, macho yangu yalianza kuwasha taratibu huku chozi likidondokaΒ taratibu. Zena na Caren walikua marafiki wazuri kwangu lakini kila kitu kiliharibika baada yaΒ Wazazi wangu kununua nyumba Mjini.Β Β
βCelin Binti yangu, najua unavyojisikia. Kupoteza uwapendao kunaumiza sanaβ alisema MamaΒ yangu akinitazama kwa sura ile ile. Niliitikia kwa kutumia kichwa changu, sauti haikutokaΒ kabisa. Nilijihisi ni mwenye hatia, Caren alikufa kwasababu yangu kama ningemzuia asiondokeΒ Usiku ule basi asingepata ajali iliyopelekea kifo chake. Nililia sana lakini sikuwa na uwezo waΒ kurudisha wakati nyuma.Β
Mchana wa siku hiyo niliruhusiwa kutoka Hospitalini, nilirudishwa nyumbani na Wazazi wangu.Β Mwili ulikua na uchovu sana, sikuweza kwenda Kumzika Zena maana alizikwa nikiwa Hospitali,Β hata Sikuwahi kwenda kuuaga mwili wa Caren ambao ulisafirishwa mara moja kuelekea Mji waΒ Wazazi wake ambako ndiko wanakozikia ndugu zao.Β Β
Nilibakia nikiwa mpweke kuliko wakati wowote kwenye Maisha yangu. Mama yanguΒ alinitazama kwa ukaribu sana kwa siku mbili hadi alipothibitisha kua akili yangu ilianza kutulia.
Sikupata majibu ya maswali yangu hata pale niliporudi tena kule stoo sikuliona lile shimo, sautiΒ ya Mwanamke anayeimba nayo ilitoweka kabisaΒ
**Β
Zilipita siku kadhaa, nilianza tena kwenda chuo. Maisha yaliendelea bila Zena na Caren,Β Wanachuo wenzangu walinipa pole kwa kuondokewa na marafiki wawili niliowapenda.Β
Usiku mmoja nikiwa nimelala chumbani kwangu, nilianza kupata njozi ya ajabu sana. NiliotaΒ nikiwa ninalia halafu pembeni yangu kuna Mtu aliyejifinika shuka gubi gubi akiwa hatikisiki.Β Nililia sana, chozi lilinitoka huku nikiwa nimejawa na uchungu sana, njozi hii ilikua ikitokeaΒ Β
ndani ya chumba kimoja chenye kitanda cha Hospitali, Mtu aliye juu ya Kitanda alikuaΒ amefunikwa shuka jeupe.Β
Nilikua ninalia huku nikisemaΒ
βUsiniache nitabaki na Nani Mimi, usiende nakuomba rudiβ Sijui nilikua namlilia Nani, ghaflaΒ nilishtuka kutoka Usingizini,niliketi nikiwa nina pumua haraka haraka. Chumba changu kilikuaΒ giza kidogo, nilisimama baadaye na kuwasha taa. Japo nilipata ndoto ya kutisha lakini UsingiziΒ ulikua mwingi machoni panguΒ
Nilijivuta ili nielekee chini kupata maji ya kunywa, nilijifunga vizuri nguo yangu ya kulalia,Β wakati nauelekea Mlango nilianza kusikia sauti ya Mwanamke mmoja, ilikua ni sauti ile ile yaΒ Mwanamke anayeimba lakini safari hii alikua akilia, nilishtuka sana. Nilipigwa na Butwaa hukuΒ nikisikia vyema kua ilikua ikitokea nje ya Mlango wa chumba changu.Β
Hata mate hayakuweza kupita kooni kwa jinsi ambavyo nilikua nimejawa na hofu, nilitamaniΒ kugumia kuwaita Wazazi wangu lakini sikuweza, butwaa iliyokua imeniingia akilini ilinifanyaΒ nitulie kimya nikisikiliza ile sauti. Wakati naendelea kuisikiliza ile sauti nilianza kuhisi ilikua niΒ sauti ya Mtu ninaye mfahamuΒ
βMamaaaβΌβ nilipata jibu, ilikua ni sauti ya Mama yangu Mzazi. Alikua akilia kisha alianzaΒ kuniita jina langu. Hofu ilizidi kuniingia, nilisimama nikiwa ninaangalia sana mlangoni.Β Nilitamani kumwita Mama na kumuuliza analia nini lakini nilipokumbuka nilichokiona UsikuΒ ule nikiwa na Caren niliishiwa nguvu kabisa.Β
Aliendelea kulia huku akiniita kwa jina langu hali iliyoizidi kunichanganya, mwendo wa dakikaΒ tano tu kisha sauti ya Kilio iliondoka Mlangoni kwangu, nikawa naisikia ikishuka chini kupitiaΒ ngazi. Chozi lilinilenga sababu sikujua anayelia kama alikua ni Mama yamgu kweli na kama niΒ Mama yangu basi ndiye anayeleta Mauzauza.Β
Baada ya sekunde kadhaa ile sauti ilitoweka, palikua kimya sana. Sikupata Hata lepe la Usingizi,Β nilikesha nikiwa macho. Asubuhi mapema niliamka na kujiandaa kisha niliondoka nyumbani bilaΒ hata kuwaaga wazazi wangu, nilimpigia simu yule Dalali ili nimuulize maswali kadhaa, nilikuaΒ na uhakika hata yeye alikua anajua ni nyumba ya aina gani aliwauzia Wazazi wangu.
Wakati natoka niliitazama sana nyumba ya yule Mzee jirani, ilikua tulivu sana. Majani makavuΒ yalikua yameanguka sana uwani kwake kuashiria kua palikua hapakaliwi na Mtu yeyote yuleΒ
Nilimpigia simu kwa namba ngeni, nilikua na uhakika kama angelijuwa ni Mimi asingelinipaΒ ushirikiano wowote ule. Nilimwambia kua nahitaji chumba cha kupanga, akanitajia mahali alipoΒ huku akinisistiza kuwa niende hapo akanioneshe chumba kizuri. Kama kawaida yangu nilikuaΒ napendelea sana treni sababu ya kukwepa usumbufu.Β Β
Baada ya kufika eneo ambalo tulikubaliana tukutane, yeye sikumkuta hapo. Niliangaza huku naΒ kule lakini sikufanikiwa kumwona, niliketi mahali nikimsubiria huku nikijaribu kumpigia simuΒ lakini simu yake ilikua haipokelewi kwa zaidi ya dakika tano, mwanzo niliona ni jambo laΒ kawaida lakini baadaye nilipata hisia ya tofauti.Β
Nusu saa nzima simu yake ilikua haipokelewi kisha baadaye ilizimwa kabisa. Mahali alipokuaΒ amenielekeza palikua ni Kijiwe cha kahawa, hapo ndipo anapopatikana kwani hata mara yaΒ kwanza nilikutana naye hapo. Nilikata shauri la kuendelea kumsubiria hapo, nilinyanyuka naΒ kuuvaa mkoba wangu ili niondokeΒ
Mara akaja Mwanaume mmoja aliyekua akiendesha Pikipiki kwa kasi sana, japo alikua hajiΒ upande wangu lakini mwendo wake Ulinifanya niwe macho kumtazama. Aliegeshe PikipikiΒ kando kidogo ya kundi la Wanaume walioizunguka meza ya kahawa kisha akaketi hukuΒ akisikitika kama Mtu aliyepoteza Umakini wake.Β
Nilinogewa na kuwatazama. Nilisimama nikiwa sikwepeshi macho yangu huku masikio yanguΒ yakiwa kama antena, walianza kumuuliza kwanini alikua katika ile hali ya kuchanganikiwa,Β akawa anajisonya-sonya tu huku akishikilia kichwa chake, walianza kumzingatia hata kwa waleΒ walioanza kuhisi ulikua ni utani walianza kuweka Umakini huku wakizidi kumuulizaΒ
βSheby jamaniβΌβ alianza kusema huku akihema sana.Β
βSheby amefanya nini?β aliuliza mmoja wao akiwa anamtikisa bega, walionekana kumjua huyoΒ Sheby na pengine alikua ni Mtu wao wa karibu.Β
βSheby eeeee haaaaaβΌβ alitoa sauti kubwa iliyoambatana na kilioΒ
βSheby amefanya nini?β aliuliza mwingine, shahuku ikazidi kuwa kubwa, siyo kwao tu hataΒ kwangu. Taratibu nilianza kupiga hatua ndogo za kuhebu ili nisikie neno.Β
βAmekufaaβΌ ajali jamani aaaah Maisha hayaaaβΌ!β yule Mwanaume alizidi kuendelea kulia,Β Watu walisikitika sana kusikia taarifa za kifo cha huyo Mtu, papo hapo akili yangu ikakaa sawaβΌ Yes, Dalali niliyewasiliana naye anaitwa Sheby. Nilihisi mwili kama unatengana na roho yanguΒ Jamani, nilikua na tumaini la kupata majibu ya maswali yangu kwa huyo Sheby halafu ghaflaΒ nasikia taarifa ya kifo chake.Β
Niliishiwa nguvu, nikasogea na kuketi juu ya gogo moja. Ndiyo maana simu zangu zilikuaΒ hazipokelewi, nilipata mfadhahiko mkubwa sana. Chozi lilikua likinimwagika, nilijuwa kua kunaΒ
jambo lisilo la kawaida linaloondoa uhai wa Watu wasio na hatia, moyo wangu ulivunjikaΒ vipande vipande hata ile nguvu niliyokuja nayo ilipungua kabisa.Β
Nilitazama juu huku chozi likizidi kunibubujika kutoka machoni kuteremka hadi mashavuniΒ kisha kwenye gauni langu, nilihisi Dunia ikizunguka. Nilikosa majibu ya maswali yangu yote,Β Uchungu ulipanda kutoka kifuani niliuhusi ukija hadi puani na kunipa maumivu makali sana.Β Hali ya mafua ya ghafla ilianza pale pale nikiwa bado kichwa changu kimeelekea juu.Β
Imani ya moyo wangu iliniambia kua Mungu alikua angani akinitazama kila hatua lakiniΒ hakutaka kunisaidia, nilisema ndani ya Moyo wangu.Β
βEeh Mungu, nitapoteza wangapi? Hii ni ndoto, niamshe basi nikutane na wapendwa wanguβΒ niliumia sana ndani ya moyo wangu, Mungu aliniachia mizigo yote niibebe mwenyewe katikaΒ wakati mgumu ambao kila niliyemshilisha alikufa kifo cha ghafla. Nilipoteza Watu watatu,Β mmoja ni dalali niliyeamini alikua akiyajua mazingira ya nyumba yetu na wengine ni marafikiΒ zangu wawili niliowapenda kama nilivyozipenda mboni za macho yangu.Β
Ghafla nilisikia sauti kando yangu, nilishtuka. Ilikua ni sauti ya kiume iliyoanza kwa utaratibuΒ sana kisha kuniachia tabasamu la mwongeaji.Β
βPole, haijalishi unapitia nini kwenye Maisha yako. Mungu atashinda na weweβ niligeuka harakaΒ kumtazama aliyeongea, alikua upande wangu wa kulia, ni Mwanaume mwenye ndevu nyingi,Β mtanashati aliyenizidi Umri lakini alikua rika langu.Β
Nilisogea pembeni haraka kwa hofu maana sikutaka kumwamini Mtu yeyote yule.Β
βUsiogope CelinβΌβ Mungu wangu, alinifahamu kwa jina. Hii siyo tu ilinishtua pia iliniacha naΒ Butwaa la ajabu sana, nikamkumbuka yule Bibi wa Ajabu ambaye alinisemesha kwenye treni naΒ kuanzia hapo kila kitu kiliharibika.Β
βTafadhali kaa mbali na Mimi, hunijui sikujui. Jina langu siyo Celinβ nilisimama kisha nilipazaΒ sauti yangu, kila mmoja aliye jirani na sisi alitutazama kwa Mshangao na maswali mengi. YuleΒ Mwanaume wala hakujali, aliendelea kutabasamu na kunidhihirishia kua alikua Mtu wa ajabuΒ kama yule Bibi.Β
Niliondoka hapo haraka huku akiniita kwa jina langu akidai napaswa kumsikiliza, sikutaka hataΒ kugeuka nyuma, niliyaziba masikio yangu ili hata kumbukumbu ya Sauti yake isibakie masikioniΒ mwangu.Β
Nilipofika barabarani nilisimamisha Taxi ya njano kisha haraka nikaingia na kuketi siti ya nyumaΒ kisha nikamuamuru dereva aondoe gari anipeleke chuoni, hapo chozi lilikua likinibubujika. BadoΒ sauti yake ilikua inasikika masikioni mwangu. Maneno ya yule Mwanaume yalikua yakijirudia.Β
βEndesha harakaβ nilisema kwa sauti ya juu ili dereva aongeze mwendo, nilikua nimegubikwa naΒ woga wa ajabu, hofu na Mashaka vilikua vimenitawala kwa kiasi kikubwa sana. Nililia kamaΒ
Mtoto mdogo, sikujua nilikosea kuichagua ile nyumba au kuna mahali familia yangu ilifanyaΒ kosa na sasa tunaadhibiwa.Β Β
Dereva aliongeza mwendo kama ambavyo nilikua nimemwambia. Nilikua nimejiinamia nikiwaΒ nimeziba masikio yangu, taratibu ile sauti ilianza kupotea masikioni mwangu. Zilipita dakikaΒ kadhaa ambazo zilitosha kwa dereva kukaribia chuoni. Nilijihisi nafuu sana, kisha nilitoaΒ kitambaa na kujifuta chozi kisha nilifuta pua zangu.Β
Niliponyanyua Sura yangu nitazame nje nijuwe kama tulikua tunakaribia chuoni au laa,Β nilipigwa na Butwaa nyingine. Nje ya gari palikua na Msitu mkubwa sana, halafu gari lilikuaΒ likitembea kwa mwendo wa kawaida.Β Β
Nilipaza sauti yangu β Wewe dereva umenileta wapi huku?β nilisema huku nikijaribu kufunguaΒ mlango lakini ulikua umefungwa. Hofu niliyoiacha ilianza kunivaa upya halafu nikaisikia sautiΒ ile ile ya yule Mwanaume niliyemkimbia akisemaΒ
βHaijalishi unapitia nini, kumbuka maneno yangu. Utashindaβ Masikini, yule dereva alikua niΒ yule Mwanaume niliyemkimbia, aliwezaje kuingia ndani ya gari sijui, nitamkimbia vipi sijui naΒ kwanini anajua kila kitu kuhusu Mimi pia sijui.Β
Nilikua ninatetemeka sana. Kisha lile gari likachepuka kutoka barabara kuu na kuingia barabaraΒ ya vumbi iliyo kimya sana, hapakua na yeyote.Β
βWewe ni Nani?β nilimuuliza nikiwa ninalia, nilijua haiwezekani tena kumkimbia. Kwa namnaΒ alivyo siyo rahisi pia kupambana naye. Alisimamisha gari kisha aligeuka na kunitazama, suraΒ yake ilionesha alikua na jambo kubwa analohitaji kuniambia.Β
Alinionesha sura ambayo haikua na hatia, wala hakuonesha kama alikua na nia ya kunifanyiaΒ jambo baya, kisha kwa sauti ya taratibu aliniambiaΒ
βUsiniogope Celin, nahitaji Msaada wako. Nitakusaidia pi, tusaidianeβ kauli hii ilianza kunipaΒ tumaini la kuishi tena, kama alihitaji msaada wangu asingeliweza kunidhuru lakini haraka harakaΒ akiwa ananiangalia nilijiuliza alihitaji Msaada gani kutoka kwangu wakati yeye anaonekana kuaΒ ni Mtu wa ajabu ajabu kama yule Bibi.Β Β
Nilibabaika kumjibu, sauti ilitoka kwa wasiwasi tena isiyo na nguvu. βNikusaidie nini? TafadhaliΒ usidhuru Maisha yanguβ nilisema huku nikiwa ninalia, niliweka mikono yangu kifuani kwanguΒ kwa isharaka ya kumwomba ahurumie Maisha yangu, alikuwa akinitazama nusu bega hukuΒ mwili wake wote ukitazama mbele.Β
βNingekua na nia ya kuyadhuru Maisha yako ningefanya hivyo muda mrefu, nina ombi moja tuΒ kwako Celinβ Maneno ya yule yalianza kunipa tumaini zaidi na zaidi kua pengine nitapata nafasiΒ nyingine ya kuishi, alionesha wazi kua alikua akinifwatilia kwa muda mrefu sana.Β Β
βNitakusaidia nini Mimi Kaka yangu?β nilimuuliza, angalau swali hili lilitoka huku nikiwaΒ nimetuliza kilio changu.
Alikunja midomo yake, ishara hii iliniambia ndani yangu kua alihitaji kuzungumza jambo zitoΒ sana, alitafakari huku akinitazama akiendelea kukunja midomo yake. Halafu akaniambia βNatakaΒ umtoe Dada yangu ndani ya nyumba yenuβΒ Β
βDada yako?βΒ
βNdiyo!βΒ
βKivipi, ni yupi mbona sisi tunaishi watatu, Mimi na Wazazi wangu?β nilimuuliza huku moyoΒ wangu ukiamini kua nilikua karibu kugundua siri fulani ya nyumba yetu. Alishusha pumzi zakeΒ kisha akaniambiaΒ
βTeremka kwenye gari, nitakueleza zaidi. Najua una maswali mengi sanaβ alisema kishaΒ alifungua mlango wa gari kisha aliteremka na kusimama mbele ya gari akiegemea βBoneti’Β
Nilikua ninamtazama kwa makini nikiwa bado nina jishauri kama nitaweza kumwamini MtuΒ nisiyemjua, lakini niliuvaa ujasiri wa ghafla kisha niliufungua mlango kirahisi sana, mlangoΒ uliokua Mgumu hapo awali, safari hii ulifunguka nilipoutekenya.Β
Sekunde kadhaa nilikua nikiivuta hewa ya jua kali lililokua likiwaka nje, niliyatazama mazingiraΒ tuliyopo. Niliona miti mingi iliyofungana, tulikua msituni japo kwa mbali nilisikia sauti yaΒ magari yakitembea kwa kasi. Upepo wa taratibu ulikua ukiendelea na kufanya eneo hilo kua naΒ hali mbili tofauti. Jua kali lakini pia upepo uliopoza joto kaliΒ
Taratibu nilitembea kuelekea mbele ya gari kumsikiliza yule Mwanaume, alikua mnene kiasi naΒ pia alikua na ndevu nyingi mfupi wa wastani, alikua ananukia manukato makali sana. NilitembeaΒ taratibu huku nikijikwaa jiwe dogo lililonipa mwendo zaidi hadi nilisogea kabisa karibu yake,Β akanipa pole huku akigeuka na kunitazama nikitembea taratibu hadi nilipofika mbele yake.Β
βUsiwe na wasiwasi Celin, usiogope sababu nusura ya Maisha yenu yapo mikononi mwakoβ niliyafinya macho yangu kwa mshangao mkubwa sana, moyo ulilipuka ghafla na kuanza kwendaΒ mbioΒ
βUnamaanisha nini?β nilimuuliza nikiwa na mhemko wa alichoniambia, tayari nilikuaΒ nimepoteza marafiki zangu wawili.Β Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SITA
COMMENTS ZIWE NYINGI SASAΒ
JIUNGE NA KIJIWENI WHATSAPP CHANNEL Kwa Kugusa HapaΒ
Soma Riwaya Nyingine Za Kijiweni Kwa KUGUSA HAPA
Wewe kama MFANYABIASHARA.. Kuna wakati unatamani kuwafikia watu wengi zaidi na hujui wapi pa kuanzia , USIJALI kwani hapa ndipo ambapo MTAA UNAONGEA na tuko tayari kukusaidia kuwafikia watu wengi kwa BEI YA OFA
Njoo Utangaze Nasi Sasa Kwa Kutuambia Una TANGAZO Gani na unataka kutangaza kwa muda gani kwa kutuma ujumbe hapa WwhatsApp Kupitia Namba +255760871896Β
Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx Nyumba Juu Ya Kaburi xx
28 Comments
Nzuri dah
Mwendelezo jamn story nzuri sana
Very good https://is.gd/N1ikS2
Hii ya Moto mbn sehemu ya 6 itoke leoleo tu
Sehemu ya sita bhc dah
Sehemu ya sita π
Good https://is.gd/N1ikS2
Next plz
Admin nkuonba leo leo toa sehemu ya sita
Wow nimeipenda
Noma sanaaaa
Good
Watunzi mnatumia akili nyingi sana adi nimecheka mwenyewe adi kujikwaa kwenye kijiwe kidogo
Good https://is.gd/N1ikS2
Very nice .give us next episode
Leoleo tuendelee admin bas
Next please
harakisha ya 6
Ni fireeee
Duh kwel π₯π₯
Inauma sana ila celin ni jasiri sana
Duuuh!!….mpaka nimeogopa kuisoma usiku,,,,,inatisha saaana.
But all in all, well done.
Mifano tenaaaaππ½ππ½πͺπ½πͺπ½πͺπ½
Good https://is.gd/N1ikS2
Admin tunasubr ya sita
Ooh woow, stori nzurii sana asee,, nimeipenda sana
π
Mwisho wa matatiz unakalibia