Ilipoishia
“Ina maana Salehe yupo na ananifuatilia?” nilijiuliza. Nilishagundua pale hapakua salama kwangu, nikageuka ili niondoke lakini ghafla mlango ulijifunga wenyewe. Pakawa na kigiza Fulani hivi
“Nani wewe unanifungia? Fungua mlango..” nilipaza sauti yangu. Niligonga na kuvuta mlango lakini sikuambulia chochote, hakuna aliyejitokeza lakini nakumbuka ule Mlango haukufungwa kikawaida, zilitumika nguvu nisizoziona. Kufungiwa ndani ya kile chumba kulinifanya nirejeshe kumbukumbu zangu nyumbani kwa Mzee Mwinyi Mkuu.
Hukusoma SEHEMU ZILIZOPITA? Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI , SEHEMU YA TATU , SEHEMU YA NNE Kisha Endelea
SEHEMU YA TANO
Sikutaka kuyarudia Yale Maisha tena, nilipata nguvu nikawa nausukuma sana mlango lakini bila mafanikio.
Muda ulizidi kwenda hata ile miale ya jua iliyopenya mlangoni ilikua inaanza kupungua taratibu kuashiria kua jioni ilikua inaingia. Nililia sana na kumwomba Mungu wangu asiruhusu nikarudi kwenye Maisha ya Miaka mitano iliyopita.
Palikua kimya sana tofauti na mwanzo nilipokua nasikia sauti za Magari, palikua kimya sana kama vile Watu walikua wameondoka Duniani. Nilikaa chini nikiwa nimejikunyata nikisubiria Hatma yangu.
“Eeh Mungu basi simama na Mimi wakati huu. Usiruhusu nikarudi kwenye ile Dunia” nilijisemea taratibu huku nikiwa ninalia. Nilijiinamia baada ya kuona nimekosea tumaini
Zilipita dakika kadhaa, Kisha niliusikia mlango ukifunguka, nasema niliusikia sababu nilijiinamia hivyo nilichokisikia na kunifanya niamini ulikua ukifunguka ni sauti za Bawaba.
Nilinyanyua kichwa haraka sana, kweli mlango ulikua umefunguka wenyewe, hapakua na Mtu yoyote yule kusema ndiye aliyeufungua. Moyo ulinidunda sana.
Nilinyanyuka taratibu kutoka pale nilipokua nimekaa, akili yangu iliniambia kua ninapaswa kukimbia eneo Hilo haraka sana maana halikua salama kwangu.
Nilikua ninahema sana huku nikihisi mwili Wangu ukikosa nguvu kutokana na ule uwoga wa ghafla ulionijaa, ni kweli jioni ilikua imeshaingia. Jua lilikua limepoa kabisa huko nje, huwezi amini kwa muda wote niliokua ndani ya kile chumba sikupata hata wazo la kupiga simu popote pale.
Basi niliangaza huku na kule Kisha niliutosa Mguu wangu nje, ghafla nikajikuta nimekamatwa na Wanaume wawili ambao sijui walitokea wapi, nilipiga kelele waniachilie lakini walikua na nguvu sana. Walinisomba Hadi nje, hapo nikaikuta ile gari nyeusi ambayo ilikua ikinifwatilia sana.
Ilikua imesimama kwenye uchochoro wa kuelekea Barabara kuua ya lami, hawakunipa nafasi ya kufanya chochote kile. Watu wale hawakua na woga wowote maana Watu Bado walikua wakipita lakini walinichukua kwa nguvu sana na kunitia kwenye gari.
Nilijaribu kufanya purukushani lakini sikuweza kupata hata nafasi ndogo ya kuwakimbia.
Nilichoka kwa kuhangaika bila msaada nikawauliza
“Niachilieni, mnanipeleka wapi?” hakuna aliyenijibu, waliniweka Siti ya nyuma ambako mmoja aliketi upande Wangu wa kulia na mwingine upande Wangu wa kushoto. Wanaume wale waliovalia mawani myeusi walikua kimya
“Mbona hamnijibu nyiyi ni akina Nani na kwanini mmenikamata” nilisema tena kwa nguvu sana lakini sauti yangu iliishia ndani ya gari, Watu waliopita nje walikua wakiendekea na Pilika zao, hakuna aliyenisikia tena. Kwanza hata kama wangelinisikia wasingeliweza kufanya chochote sababu hata wa mwanzo hawakutoa msaada wowote kwangu.
Mara aliingia Mtu mmoja kwenye gari Kisha akaliondoa gari. Sikutaka kuchukuliwa kilaini, nilileta vurugu sana, nikadhibitiwa Kisha nikapotezewa fahamu zangu, sijui hata walifanya nini. Baada ya hapo sikujua chochote kilichokua kinaendelea, sikujua nilikua napelekwa wapi na kufanya nini lakini kitu kimoja kilichokua akili mwangu ni kua Watu hao ndio wale walioniambia kua Nina deni.
Maneno ya yule Kichaa yalitimia kua watakuja kunichukua ila sikujua Watu hao ni akina Nani, lakini niligundua hawakua Watu wa kawaida na pengine walikua Wachawi wenye nguvu sana.
**
Nilianza kuhisi Uhai ndani yangu, pumzi zangu zilikua zinapita puani kwa shida kidogo. Nilianza kuhisi mapafu yangu yalikua yakiamka, hata macho yangu yalifunguka. Nilijikuta ndani ya chumba kimoja kitupu, chumba hicho kilikua kina harufu fulani za ajabu hasa Udi
Niliamka haraka nikaanza kuangaza huku na kule. Kila nilivyokua nakikiangalia vizuri chumba kile nilianza kukikumbuka. Masikini Mimi Saida nilikua nimerudishwa Rukwa kwa mara nyingine, nilianza kutokwa na Machozi hasa nilipozikumbuka zile Kuta zenye Siri za mateso kwangu, mateso ya Miaka mitano iliyopita.
Nilikumbuka namna nilivyopona kutoka Kifo, sikutaka kuyaamini macho yangu, niliyafumba ili niyafumbue tena pengine lilikua wenge langu. Nilipofumbua tena hakuna kilichobadilika, nilikua ndani ya chumba kile kile ambacho nilibakwa na wale Misukule wa Mzee Mwinyi Mkuu.
Kabla hata sijatulia vizuri nilisikia sauti ya Mtoto Mchanga akilia, mauzauza Yale Yale yalikua yakianza kujitokeza kwangu. Nilitembea taratibu kuelekea Mlangoni, niliutekenya. Kitasa kilikubali ombi langu, mlango ukafunguka
Kuta zile zile zilikua mbele yangu, sakafu ile ile aliyoburuzwa Kaka Hamidu ilikua mbele ya Macho yangu. Nilimeza mate nikiwa ninachungulia Korido, nilipeleka macho yangu huku na kule. Hakuna kilichokua kimebadilika, mazingira yalikua Yale Yale
Ile sauti ya Mtoto kulia ilipotea Kisha nilisikia sauti ya kusukumwa kwa vyombo, sauti ilitokea kwenye chumba Cha Jiko. Basi niliutosa Mguu wangu kukanyaga Korido, sikua mgeni na nyumba hiyo niliijua vizuri kua kutoka ni jambo gumu sana.
Nilipiga hatua ndogo ndogo huku nikijishikiza ukutani, nilipofika mlango wa kuelekea Jikoni nilimkuta Msichana mmoja akichambua Mchicha. Aliponiona alinitazama bila kusema chochote lakini alikua na bandeji mguuni
Alikua akipitia Yale niliyoyapitia Mimi, nilipepesa macho yangu huku hofu ikiwa kubwa sana kwangu. Nilimsogelea yule Msichana Kisha nikamsalia
“Mambo” hakujibu, aliendelea kuchambua Mchicha, Bandeji yake ilikua imetapakaa Damu.
“Samahani nakusalimia” Nilisema tena, yule Msichana hata hakuhangaika kusema chochote, alikaa kimya akiendelea kuchambua Mchicha kama vile alikua hajanisikia. Niliemeza funda zito la mate, nilishusha na pumzi zangu
Nilitoka pale jikoni baada ya kukosa majibu. Hakuna Sehemu ya nyumba ile ya Mzee Mwinyi Mkuu ambayo nilikua siijui, nilizifahamu Kuta zote na kumbukumbu zake. Kila nilipokua ninapiga hatua nilikumbuka mateso makali niliyoyapitia
Nilitoka nyumba kubwa nikawa naelekea mlango wa kutoka ndani ya Nyumba. Kila kitu kilikua vile vile, kilichobadilika ni kwamba ilikua ni mara yangu ya pili naingia ndani ya Nyumba hii. Nilitembea taratibu Hadi nilipofika mlangoni, nikajaribu kuufungua Mlango, ulifunguka bila shida yoyote.
Nikayatupa macho yangu mbele, mazingira Yale Yale niliyoyaacha Miaka mitano iliyopita yalikua vile vile. Watoto walikua wakicheza eneo la Wazi kama zamani, kando Yao alikuwepo Mama anayetengeneza vitumbua na chapati, alikua kwenye foleni kubwa sana.
Nilimkumbuka yule Mama ambaye dakika za mwisho nilibadilishiwa na kuwekewa Mama mwingine kabisa.
“Mama Ashura” nililikumbuka jina lake, niligeuka nyuma Kisha nilipiga hatua zangu kuelekea kwa Mama Ashura, nilitembea taratibu sana huku nikiwaza mambo mengi kichwani kwangu. Kwanza nilijiuliza ni kwanini nilirudishwa Rukwa, kwanini nimeachwa huru? Sikupata majibu ya
maswali yangu
Nilipofika kwa Mama Ashura, nilimsalimia kwa adabu sana. Niliamini angenikumbuka lakini aliipokea salamu yangu kama Mtu asiyenifahamu. Nilitabasamu nikamuuliza kama ananikumbuka
“Hapana, Ndiyo kwanza nakuona Leo” alisema Mama Ashura huku akiendelea kutengeneza chapati.
“Mimi Saida, tuliwahi kuzungumza Miaka mitano iliyopita” Nilisema. Yule Mama aliniangalia Kisha akaniambia hanikumbuki, niliangalia Yale mazingira nikaona Watu walikua wakituangalia hivyo sikutaka kumkumbusha chochote. Niliketi pembeni nikisubiria foleni ya chapati iishe huku macho yangu yakiitazama sana nyumba ya Mzee Mwinyi Mkuu.
Macho yangu yalikua kama ya Digidigi hivi, sikutaka kuacha kumwangalia Mama Ashura lakini wakati huo huo nikiwa makini kule nyumbani kwa Mzee Mwinyi Mkuu. Zikapita kama dakika saba hivi ndipo nilipoliona gari Moja likifika pale kwa Mzee Mwinyimkuu. Umakini ukahama kutoka kwa Mama Ashura nikawa naliangalia sana lile gari lililolisimama mbele ya nyumba ya Mzee Mwinyimkuu.
Niliona Watu wa ajabu sana ambao sikutarajia, Watu hao walikua wamevalia mashuka meupe pia Usoni walikua wamejipaka Unga mweupe. Namna walivyo walifanana sana na Misukule, gari ile aina ya Noah nyeusi ilishusha Hao Watu kama Nane hivi
Nilishtuka sana Kisha nikamwangalia Mtu mmoja aliye kando yangu, naye alikua akiangalia kule kule, nikajua sikua peke yangu ambaye nilikua nikiwaona wale Watu.
Sikujua kama naye alikua akiona kama nionavyo Mimi au ilikua kwangu tu, mapigo yangu ya Moyo yalikua yakienda mbio sana.
Namna walivyo wale Watu walifanana sana na Misukule kutokana na mionekano Yao. Baada ya wote kushuka na kuelekea ndani, Mtu mmoja ambaye kwa mbali sikumwona vizuri akasogea pale Kisha akawa anaongea na Mwanaume mmoja aliyekua amesimama
Nilihisi kama alikua akimwonesha mahali nilipo, moyo ulinienda mbio. Hakika alikua akinionesha kidole Mimi japo sikujua alikua akimwambia nini yule Mtu.
Nilitamani kukimbia lakini nilikumbuka kua baada ya kutekwa kule Mburahati nililetwa huku Rukwa ndani ya Nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Watu walioniteka hawakunidhuru kwa chochote kile, tena waliacha mlango
Wazi hivyo kwa haraka niliamini kama hawakunifungia mle maana yake walikua na jambo la tofauti dhidi yangu
Nilijiambia kwa Ujasiri sana “Saida umekimbia sana, sasa kua jasiri” sauti kutoka ndani ya nafsi yangu iliniambia kwa Ujasiri sana, niliendelea kukaa pale pale huku wengine wakiwa wanaendelea na shughuli zao bila hata kujali kuhusu Mimi. Hata yule Mtu aliyekua akiangalia nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu alikua naye anaendelea na mambo yake.
Nilivuta pumzi zangu nikajiambia kua hata kama Dunia itakua imefika mwisho kwa Upande Wangu ni Bora iwe hivyo lakini siwezi kuendelea kukimbia tena, halafu Hali ya hasira iliniingia kutokana na mateso makali niliyoyakumbuka niliyokua nikiyapata nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu.
Nilimkumbuka sana Mama yangu, kidogo chozi lilianza kunitoka lakini nililizuia. Nilipofuta chozi nilirudisha macho yangu kule kwa Mzee Mwinyimkuu, nikamwona yule Mtu aliyekua akioneshwa nilipo alikua akija upande huu nilipo, nilijua alikua akinifuata Mimi hivyo sikuogopa wala nini.
Yule Mtu alitembea haraka haraka Hadi alipofika nilipo, nilimtazama kwa macho makavu bila kumwonesha wasiwasi. Alisimama hatua kadhaa Kisha alinionesha ishara ya kuniita. Niliangalia huku na kule, hapakua na yeyote yule aliyekua akiniangalia wala hata kumwangalia yule jamaa.
Nilisimama, halafu nikaelekea alipo. Akaniambia kwa sauti ya chini
“Samahani, unaitwa” alisema huku akionesha kidole kule kwa Mzee Mwinyimkuu, hapakua na yeyote tena kule isipokua lile gari lililoleta Misukule. Nami nilikifuata kidole chake nikaangalia kule halafu nikarudisha macho yangu kwa yule Jamaa
“Nani ananiita?” niliuliza kwa Ujasiri sana japo kwa ndani nilikua mwoga lakini sikuruhusu yule Mtu anielewe, nilimkazia macho yangu huku nikichezesha Mguu mmoja.
“Bosi”
“Bosi?”
“Ndiyo”
Nilitazama huku na kule Kisha nikamwambia
“Sawa” Nilisema tu lakini nilikua naogopa sana. Tayari hatma ya Veronica ilitimia, kilichobakia kilikua ni Mimi kulipa Hilo deni ambalo niliambiwa ninadaiwa. Akili yangu iliniambia ni Bora niende hata kama nitateseka na kufia huko. Nini Kitaendelea? Usikose sehemu ya SITA
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx
