Ilipoishia 

Angalau eneo Hilo lilikua na taa, nilitembea haraka haraka Hadi nilipofika  nyumbani, ila nilikua naogopa sana kuingia ndani, nikapata wazo la  kumuamsha Mama Amida nimuombe nilale nyumbani kwake Hadi  Asubuhi. 

Niligonga mlango wake kwa nguvu huku nikimtaka anifungulie haraka,  chozi lilianza kunitoka. Nilikua nageuka huku na kule, mara haraka Mama  Amida alinifungulia, nilimsukuma nikaingia Hadi ndani Kisha  nikamwambia aufunge mlango haraka, akafanya hivyo haraka bila kujua ni  kwanini nilimtaka aufunge mlango, Kisha akanigeukia 

“Saida, Kuna tatizo gani?” aliniuliza, chozi lilikua linanibubujika tu.  Akanishika mkono na kunipeleka chumbani kwake Kisha akaniambia nikae  kwenye kiti.  

 Hukusoma SEHEMU  ZILIZOPITA?  Isome Kwa KUGUSA HAPA…... SEHEMU YA KWANZA , SEHEMU YA PILI  ,  SEHEMU YA TATU Kisha Endelea 

SEHEMU YA NNE

“Una shida gani saida mbona unanitisha, Usiku huu umetokea wapi wewe  Mtoto?” kiukweli sikuweza kujibu chochote maana nilizidiwa na woga kiasi  kwamba hata mdomo Wangu uligoma kusema chochote kile. Alinielewa,  istoshe yeye ni Mtu mzima akaniambia nipande kitandani tutaongea  Asubuhi, nilipandwa kitandani nikajikaza Chali. Alikua akiishi peke yake  baada ya Mume wake kufariki, Mtoto wake alikua akilala chumba kingine  na Msichana wa kazi. 

Sikupata hata lepe la Usingizi Hadi kulipo pambazuka. Mama Amida  aliniambia nimpe majibu ya maswali yake, akili kidogo ilikua imetulia  lakini nilifikiria kua siwezi kumweleza chochote kinachoendelea 

“Saida, naomba unijibu ulipatwa na Nini?” Aliniuliza kwa msistizo. 

“Samahani, nilikua nafukuzwa na wezi” nilimpa jibu la uwongo huku  nikiwa Nina aibu machoni pangu kwa kusema Uwongo kwa Mtu ambaye  nilikua namchukulia kama Mama yangu. 

“Wezi?” 

“Ndiyo” 

“Ulikua unatokea wapi muda ule?”  

“Nilienda kwa rafiki yangu lakini nakuahidi haitajirudia tena”  “Mmh! Haya” 

“Pia Asante kwa msaada wako”

“Usijali Saida, muda wowote” alisema Mama Amida lakini sura yake  ilionesha Wazi kua alikua ameshanishtukia kua nilikua nasema Uwongo  lakini hakutaka kukuza mambo, nilimuacha akiwa amekaa kwenye kiti  chumbani kwake. Niliondoka nikaelekea nyumbani, safari hii niliingia  ndani sababu nilihitaji kubadilisha nguo lakini pia kuvaa viatu. 

Nilioga haraka haraka Kisha nikabadilisha nguo nikatoka, nikakaa nje ya  nyumba. Nyumba yetu nilikua naiyona kama Kituo Cha Polisi, niliogopa  hata kukaa ndani 

Nikampigia simu Veronica, akaniambia kua alishaongea na Meneja hivyo  niende kwao Mabibo halafu Ndiyo twende kwa Mganga. Katika Hali  ambayo nilikua nayo ilikua rahisi kwangu kukubali Kila ninachoambiwa ili  tu nipate ahueni, kwa jinsi nilivyoongea na Veronica ilionekana hakupata  kashikashi yoyote Usiku hivyo Mlengwa nilikua ni Mimi. 

Basi niliondoka nyumbani nikaelekea kituo Cha Daladala, nikaingia kwenye  daladala Kisha safari ya kuelekea Mabibo ilianza.  

Nilimtazama Kila Mtu kwenye lile daladala kama vile nilikua kondakta,  lakini nilikua mwoga sana sababu nilishajua Maisha yangu yalikua hatarini.  Nilikua mwingi wa kushtuka shtuka. 

Hadi tunafika Mabibo nilikua nimegeuza shingo yangu mara nyingi sana  kuangalia huku na kule. Veronica alinipokea akanipeleka Hadi nyumbani  kwao, ilikua ni mara ya kwanza nafika kwao pia nakutana na Mama yake.  Tuliongea mengi huku Mama yake akitupatia stori za hapa na pale zenye  

kufanana na mkasa wetu, akatupatia uhakika kua utapatikana muafaka bila  wasiwasi wowote ule 

Maneno yake yalikua ni faraja pekee niliyohitaji Maishani mwangu kwa  wakati ule, nilihitaji kutiwa moyo kama alivyofanya Mama yake Veronica,  akatuandalia chai tukanywa huku tukipiga stori.  

Baada ya kumaliza akatuambia twende sasa kwa Mganga maeneo ya  Mburahati. Tulielekea kituo Cha daladala tukapanda magari ya Mburahati,  nilikua najisikia amani sana sababu nilihisi nipo salama zaidi. 

Tulipofika Mburahati, akatupeleka nyumbani kwa Mganga.  Akatuhakikishia kua ni Mganga kiboko sana kutokea Liwale, ana uwezo  mkubwa sana. 

“Msijali, hii Dunia isikieni tu ila Ina mambo mengi sana Wanangu” alisema  Mama yake Veronica akiwa amesimama mbele ya nyumba Moja ya 

kizamani. Namna alivyokua anaongea nasi ni kama vile kapteni wa Timu ya  Mpira vile 

Tuliachia tabasamu kwa pamoja, nisiseme Uwongo ila nilikua mwenye  amani zaidi nilipokua namsikiliza Mama yake Veronica. Alikua amevalia  gauni Jekundu na Ushungi. 

“Hili limekwisha, twendeni” 

“Sawa Mama” tulisema kwa pamoja Kisha tulitazamana halafu tukamfuata  Mama Veronica ndani. Namna alivyoingia ni kama vile alikua ni mwenye  kuja sana kwa huyo Mganga. Tuliingia Uwani, Kisha tulisogea Hadi  mlangoni kwenye chumba kimoja hivi ambacho kilikua na pazia nyekundu  iliyokua ikipepea mlangoni. 

“Baba Masinde” aliita Mama Veronica huku akigonga Mlango.  “Karibu” ilisikika sauti nzito ya kukwaruza.  

“Nipo na wageni Baba” alisema tena Mama Veronica. 

“Ingieni hakuna shida” alisema, Kisha Mama Veronica alitangulia ndani.  Nilianza kuogopa kidogo lakini nilihitaji kua na amani ya Maisha yangu, ili  nipate amani ya Maisha yangu ni lazima niyaondoe mauzauza kwenye  Maisha yangu, njia pekee ilikua ni kupewa tiba kwa Mganga.  

Tulivua viatu pale nje Kisha tuliingia ndani, tulipokelewa na harufu za  ajabu ajabu sana, binafsi ilinibidi nivumilie tu kwasababu nilikua Nina  shida lakini harufu hii ilinikumbusha Maisha ya Rukwa kule nyumbani kwa  Mzee Mwinyi Mkuu.  

Mganga huyo alitukaribisha tukae kwenye mkeka, chumba kilikua na  mandhari zote za Uganga, hata mavazi ya huyo Mzee yalikua yakiganga pia.  Basi tukasalimiana naye lakini Mama yake Veronica alisalimiana naye kwa  shahuku kubwa sana. 

“Baba, kama nilivyokwambia kwenye simu wakati natoka nyumbani, huyu  ni Binti yangu anaitwa Veronica na huyu ni rafiki yake. Chonde Mzee  wangu wasaidie hawa Vijana” alisema Mama yake Veronica. Yule Mganga  akatuangalia kwa jicho lililo kimya, hakusema chochote. 

Ilipofika zamu ya kuniangalia aliniangalia sana tena kwa muda mrefu Hadi  nikawa na hofu. Alitumia dakika Moja ananiangalia tu, nilitamani  kumuuliza kwanini alinitazama kwa muda mrefu. 

“Hebu Mama tuongee nje” alisema yule Mganga Kisha yeye na Mama  Veronica walitoka mle chumbani. Nilimsogelea Veronica nikamuuliza  kwanini yule Mganga aliniangalia sana?  

“Nitajuaje sasa Saida, Mimi sijui haya mambo ni vile tu Mama amesistiza”  alisema Kisha aliegemea Ukuta.  

“Yaani moyo unanienda mbio sana, naogopa mno” Nilisema, nilijikuta  nikiwa mwoga mno.  

Baada ya dakika Moja mlango ulifunguliwa Kisha Mganga na Mama  Veronica walirudi ndani, nilizidi kutetemeka kwa hofu. 

Kilicho chochea hofu yangu ni jicho la Mama Veronica, alikua akiniangalia  kwa jicho Kali sana lisilo na Upendo kabisa.  

Palikua kimya sana, si Mama Veronica wala Mganga aliyesema chochote.  Nilitamani kulia maana niliona Wazi kua Kuna kitu hakipo sawa kwangu,  halafu Mganga na Mama Veronica walitazamana Kisha Mganga  akajikoholesha Kisha akasema kwa sauti yake kavu. 

“Binti” alimtazama Veronica. 

“Wewe hauna shida yoyote sababu umeingizwa kwenye Mchezo  usioufahamu. Ila wewe Binti….” Alinitazama kwa jicho Kali sana huku  akininyooshea kidole. 

“Mimi?” niliuliza huku nikigusa kifua changu. 

“Ndiyo….wewe ni mchafu sana” alisema yule Mganga, hata Veronica  alishangaa. Alinitazama kwa Mshangao sana huku akionekana kua na kiu  ya kutaka kujua sababu ya maneno Yale makali kutoka kwa Mganga. 

Mganga alikua akiongea huku mate yakinirukia kutokana na mkazo wa  maneno aliokua nao. 

“Kwanini unasema hivyo?” 

“Wewe ni Mchawi, wewe Binti ni Malkia wa wachawi.” Alisema yule  Mganga, Jamani moyo ulinidunda kwa Kasi sana Hadi nikahisi kuchoka  mwili mzima, pua zilikua kama zinauma kwa Kila pumzi niliyoivuta. 

Maneno ya Mganga yalikua yakiuchona sana moyo Wangu, nilihisi kabisa  sindano ndogo ikipita na kuniumiza ndani ya Moyo Wangu, Hadi chozi  lilinilenga, sikuwahi kuambiwa Mimi Mchawi hata siku Moja tangu  Kuzaliwa kwangu

Wakati ambao nilihitaji msaada Ndiyo wakati ambao nilianza kuitwa  Mchawi, nawezaje kua Mchawi bila Mimi mwenyewe kujua? Tena Nina  cheo Cha Umalkia? 

“Usijilize hapa, wewe Ndiyo chanzo Cha kumuingiza Mwanangu kwenye  Giza. Umeharibu Maisha ya Binti yangu Mjaa Laana wewe” alisema Mama  yake Veronica kwa sauti Kali sana, alipaza sauti kwa hasira dhidi yangu.  Shutuma hizi zote ziliniacha njia panda maana akili yangu haikuweza  kuelewa lolote lile. 

Nilimeza mate kwa Uchungu huku chozi likitiririka mashavuni mwangu,  nilijiinamia nikiwa ninalia kwa sauti ya Ukimya. Haki ya Mungu  nilimkumbuka sana Mama yangu, yeye ndiye Mtu pekee ambaye angeweza  kunishika bega na kuniambia nisiwe na wasiwasi lakini hakuwepo kwenye  Dunia yangu. 

“Mama Veronica, hebu subiri kwanza” alisema yule Mganga akimtuliza  Mama Veronica, kwa jinsi ambavyo alikua amekasirika angenishika na  kunigalagaza, nilisogea pembeni kwa kujiburuza kwa kutumia Makalio  yangu. Muda wote huo Veronica alikua kimya akinitazama kwa Mshangao  

mkubwa sana, licha ya kumwonesha sura yangu ya hatia lakini alionekana  kutaka kusema jambo zito sana ambalo lilikua limemkaa moyoni. 

“Kwanini mnanituhumu kwa kitu ambacho sikijui Mimi?” niliuliza huku  nikiwa ninalia, nilikua nimepandwa na hisia ya hasira na huzuni kwa  wakati mmoja. 

“Usichokifahamu ni kipi? Sasa chochote kinakachomkuta Veronica kuanzia  sasa ni juu Yako. Utalipa nakwambia” alisema Mama Veronica Kisha  aliondoka pale chumbani kwa hasira akiliburuza gauni lake kuelekea nje 

“Yanayosemwa ni kweli Saida?” aliniuliza Veronica huku naye akisema kwa  sauti iliyojaa kilio. Nilimtazama nikatikisa kichwa Kisha nikamwambia 

“Ningewezaje kuigiza wakati wote ikiwa nafahamu Kila kitu Veronica. Sijui  chochote kinachosemwa hapa, nipo njia panda sielewi” nilisema, Veronica  alitikisa kichwa chake. Hakua na imani tena na Mimi, alisimama Kisha  chozi likawa linamdondoka akaniambia 

“Ikiwa Maisha yangu yataharibika kwasababu Yako sitakusamehe Saida”  alisema Kisha naye aliondoka zake pale ndani, walituacha Mimi na  Mganga. 

“Ondoka hapa sitaki Matatizo” alisema yule Mganga, alikaza macho yake  kwangu. Msaada uliokua karibu kwangu ulianza kwenda mbali, nilikua na 

maswali mengi sana kichwani kama nitawezaje kuishi kwenye Dunia isiyo  na Majibu, Dunia inayobadilika kwa haraka sana kwangu 

Nilipepesa kope zangu, ni kama niliyaambia machozi yangu yamwagike.  Yalimwagika bila hata kizuizi, kulia pekee ndicho kitu nilichoweza kufanya  Mimi Saida 

“Kwanini unasema Uwongo?” nilimuuliza yule Mganga, akakaza sura yake  kwangu Kisha akaniambia 

“Ondoka hapa haraka sana sitaki Matatizo na wenyewe” 

“Wenyewe, ni akina Nani hao?” nilimuuliza huku chozi likinibubujika.  Akanyanyuka haraka Kisha akanishika mkono na kunitoa pale chumbani.  

“Ole wako urudi hapa, nisikuone” alisema kwa hasira yule Mganga Kisha  alifunga mlango. Nilijiinamia na kuanza kulia kwa Uchungu sana, sikua na  Cha kufanya tena zaidi ya kuvaa viatu vyangu na kuondoka pale. 

Hapakua na yeyote pale nje si Veronica wala Mama yake. Nilifuta chozi  langu, nikavaa viatu vyangu Kisha pole pole niliondoka pale Uwani Hadi  nje, nilipofika nje nilisikia sauti za yowe 

Hazikua mbali kutoka niliposimama, nilipozisikiliza vizuri hazikua yowe za  Mwizi Bali ni tukio la Kusikitisha kwa namna ambavyo sauti zilikua  zikisema. Nilitembea haraka kwenda kuangalia maana nyumba ya Mganga  ilikua kando ya Barabara. 

Nilipofika niliona Watu wengi sana, baadhi walikua wamejishika vichwa  vyao. Nilijiuliza mwenyewe bila kupata majibu, nikamalizia kufuta chozi  langu Kisha nikamuuliza Mtu mmoja aliyekua amesimama kando 

“Eti Kuna nini pale?”  

“Ajali, wewe acha tu hujaona” 

“Ajali?” 

“Ndiyo, Kuna Watu wameangukiwa na Kotena. Sura zao hata hazitamaniki”  nilishtuka sana huku moyo ukinienda mbio, nikasogea karibu. Ndiyo  kwanza walikua wakiiondoa Miili, nilipepesa macho yangu kwa Mshangao  mkubwa sana, japo sura zao hazikutambuliwa ila nguo zao zilikua machoni  pangu 

Nilitamani nikae chini maana hata nguvu ziliniisha, Veronica na Mama  yake walikua Ndiyo walioangukiwa na Kontena. Chozi lilinitoka kama 

mwendawazimu, nikatikisa kichwa changu Kisha nikatimua mbio kuelekea  kwa yule Mganga kumpa taarifa. 

Hata kama hakunihitaji tena ila alipaswa kujua kua Mama Veronica na  Mwanae walikua wamesha fariki. Niliusukuma mlango wa kuingilia Uwani  Kisha niligonga sana mlango wa yule Mganga.  

Sikukaribishwa, nikahisi labda atakua amenuna. Nikafikiria kuondoka  lakini nikaona ni Bora nimwambie tu.  

“Mama Veronica na Mwanaye wamepata ajali hapo nje” nilipaza sauti Kisha  nilisubiria jibu lake lakini palikua kimya kabisa. Nikaona ni Bora  niusukume ule Mlango, nilivuta nguvu lakini niliposukuma ulikua rahisi  kufunguka. Nikajikuta nimeingia ndani ya chumba Cha Mganga 

Hapakua na yoyote yule, niliangaza huku na kule lakini sikumwona, ila  wakati nataka kuondoka niliona kitu Cha kushangaza sana. Nilisogea  taratibu nikachuchumaa ili nikiangalie kitu nilichokiona kikanishangaza 

Kilikua ni Picha yangu, nikiwa nimevalia gauni JEUSI, nakumbuka picha  hiyo nilipiga baada ya kufunga ndoa na Salehe Miaka mitano iliyopita.  Nilipigwa nyumbani kwetu wakati tunajiandaa kuondoka kuelekea Hotelini  kulala ili kesho yake tuanze safari ya kuelekea Rukwa 

Mtu pekee aliyekua na picha hii alikua ni Salehe, ndiye aliyenipiga picha  kwa kutumia simu yake. Tokea kipindi kile sikuwahi kuiona hii picha, sasa  nikajiuliza iliwezaje kufika pale kwa yule Mganga? Aliyeipeleka ile picha  alikua ni Nani?  

“Ina maana Salehe yupo na ananifuatilia?” nilijiuliza. Nilishagundua pale  hapakua salama kwangu, nikageuka ili niondoke lakini ghafla mlango  ulijifunga wenyewe. Pakawa na kigiza Fulani hivi 

“Nani wewe unanifungia? Fungua mlango..” nilipaza sauti yangu. Niligonga  na kuvuta mlango lakini sikuambulia chochote, hakuna aliyejitokeza lakini  nakumbuka ule Mlango haukufungwa kikawaida, zilitumika nguvu  nisizoziona. Kufungiwa ndani ya kile chumba kulinifanya nirejeshe  kumbukumbu zangu nyumbani kwa Mzee Mwinyi Mkuu. 

Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TANO Sasa ( Comments ziwe nyingi) 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx  Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

Leave A Reply

Exit mobile version