Ilipoishia SEASON 1
Kwasasa nimerudishwa kwetu Dar-es-salaam, niko Magomeni. Maisha yangu yamekuwa ya Ukimya sana, Sijazungumza tena tokea siku ile nilipozungumza kwa mara ya mwisho Rukwa, sijaandika chochote na wala sitaki kusema chochote kile ila kupitia mkasa huu nataka ujifunze.
Kamwe kwenye Maisha yako usiolewe au kuowa Mtu usiye mfahamu, Dunia ni Kichaka cha Mateso. Wasichana wengi wanayapitia mateso niliyoyapitia, wengi wanauawa, wengi wanapata ugonjwa wa akili. Hata wanaume wapo waliopoteza kila kitu, Siku nikifungua kinywa changu nitawasimulia mengi, kwasasa naishia hapa, naweka kalamu yangu chini. Endelea na SEHEMU YA KWANZA YA SEASON 2 Hapa
SEHEMU YA KWANZA
MIAKA MITANO BAADAYE
Nilikua nimesimama mbele ya Kioo nikijitazama. Nilimeza funda zito la mate, nilikua nimevalia gauni la harusi lenye kufanana na lile nililolivaa siku naolewa na Salehe. Sikuwahi kulisahau gauni hili, lilibakia kua kumbukumbu yangu. Sura ya Salehe ilikua kichwani mwangu, sikuwahi kumwona wala kumsikia tena tokea wakati ule aliponiaga kua ameagizwa na Baba yake.
Sura ya Mzee Mwinyi Mkuu ilikua ikipita machoni pangu Kila dakika, mateso niliyoyapata yalitengeneza kovu moyoni mwangu. Niliitazama miguu yangu, ilikua Haina vidole, yalibakia makovu ya Maisha.
Nilidondosha chozi langu taratibu, nilikua katika maumivu ya kihisia ambayo yalikua yakiendelea kunitesa kwa Miaka mitano.
Midomo yangu ilikua imechanika kwasababu tokea wakati ule sikuwahi kuongea chochote tena, Mama yangu alikua akiendelea kunitunza nikiishi kama Bubu, hakuwahi kuisikia tena sauti yangu zaidi ya kuliona chozi langu.
Nilijikuta nikilia kwa Uchungu, nilikumbuka namna usichana wangu ulivyoondolewa na Misukule ya Mzee Mwinyi Mkuu nilipatwa na hasira sana. Mara Mlango ulisukumwa, aliingia Mama yangu
“Saida” aliita Mama, alisogea nilipokua nimesimama. Mama yangu alikua mwingi wa huzuni, alimpoteza Mume wake kwasababu yangu. Hata moyo wake ulikua na kovu la maumivu, kama Mama alikua amepoteza Watu wawili aliowapenda sana, alimpoteza Mume wake lakini alinipoteza Mimi pia kwasababu nilikua kimya muda wote.
“Mwanangu, yaliyotokea yameshatokea. Miaka mitano imepita sasa, huna sababu ya kuendelea kukumbuka tena” alisema Mama Kisha alinitaka nikae kitandani, nilikaa taratibu huku chozi likiwa linanidondoka.
“Afya Yako sasa imeimarika lakini muda wote upo chumbani tu, huzungumzi Saida” alisema Mama, chozi lilidondoka machoni pake.
Nilizidi kuumia sana Mimi, Mama yangu alikua mpweke sana na mwenye huzuni, alikonda kwa mawazo.
Nilimtazama Mama yangu, nilitamani kusema jambo lakini moyo Wangu uliniambia napaswa kuendelea kua kimya, sikua Bubu lakini sikutaka kuongea chochote kile, sauti yangu ilikua chozi langu pekee.
“Saida, Mama Yako nakulilia na kukuombea Kila dakika ili urudi kua sawa kama zamani. Wewe ni Mtu pekee uliyebakia kwenye Maisha yangu, Mimi Mama Yako Sina mwingine zaidi Yako wewe.” Alisema Mama, niliondoa macho yangu kwake, sikutaka kabisa kumtazama Mama yangu sababu ningeendelea kuumia
Mama alifuta chozi lake Kisha akaniambia
“Ukihisi njaa, chakula kipo Mezani. Naenda chumbani” alisema Mama Kisha alinyanyuka taratibu akifuta chozi lake. Alipofika mlangoni aligeuka na kunitazama, Kisha aliondoka na kuufunga mlango.
Nililia sana Mimi Saida, moyo uliniuma sana sababu kama nitatoa japo sauti yangu basi nitaweza kumpa tabasamu Mama yangu lakini nilijiapiza kua sitazungumza tena katika Maisha yangu yote. Saikolojia yangu ilijaa mateso makali, nilishuhudia mengi yaliyonifanya nipoteze uwezo wa kujiamini na kujithamini kama Binadamu.
Sikujipenda tena, niliishi kwasababu Mungu hakutaka kuichukua pumzi yake, lakini Dunia ilinifundisha kuchoka, sikutamani kuendelea kuishi. Nilikua naishi nikisubiria siku Moja kifo kinichukue nikapumzike mbele ya safari.
**
Masaa yalienda sana, Mchana uliondoka Bado nilikua nimekaa pale pale kitandani nikilitazama dirisha namna lilivyokua likibadilisha mwanga wake. Jioni iliingia kwa Kasi sana, jua halikuwepo tena dirishani pangu, chozi lilikua likiendelea kunibubujika bila kupumzika.
Ghafla nikajikuta nikihisi moyo Wangu ukidunda kwa Kasi kama vile nilikua nazinduka kutoka kwenye Usingizi. Nilikua nasikia sauti ya Mtoto akilia kando yangu, nilianza kuhema kwa Kasi sana
Nilikua nimezungukwa na Watu wengi waliovalia nguo nyeupe tena wakionekana kua walikua wenye haraka sana kama vile walikua wakinishughulikia.
“Niacheee, Washenzi nyie. Wachawi haooo” nilijikuta nikipiga yowe Kali sana. Mara nilichomwa sindano, nikapoteza uwezo wa kufikiria pia nguvu ziliniisha nikajikuta nikiona Giza zito halafu Usingizi ukaiteka akili yangu.
Nikiwa Usingizini, nilianza kuhisi nilikua ninaitwa. Sauti ya Mama yangu ilikua ikipita masikioni mwangu kwa mtindo wa kunong’ona. Mama alikua akiniambia
“Saida Amka ule chakula, Amka Mwanangu. Amkaaa usilaleee” Mara ghafla nikajikuta nikizinduka kutoka kwenye Yale mawazo. Nilijikuta nipo pale pale kitandani nikiwa Nimekaa, nilikumbuka ni kweli Mama yangu aliniambia nikihisi njaa niende Mezani nikale
Basi nilihema, ndoto za Kutisha zilikua Sehemu ya Maisha yangu. Wakati mwingine niliota ndoto nikiwa nimekaa tena nikiwa macho kabisa, hayo Ndiyo Yalikua Maisha yangu baada ya kuponea chupuchupu kule Rukwa.
Basi, nilinyanyuka taratibu nikaelekea sebuleni, nilikua nikitembea taratibu sana. Nilipofika sebuleni nilikikuta chakula kikiwa hapo, nilifunua Hotipoti. Nilijiandalia chakula Kisha Niliketi, nilianza zoezi la kufungua kichwa changu chenye vidonda vya Ukimya
Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA PILI Sasa
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx
