Ilipoishia 

“Saida Amka ule chakula, Amka Mwanangu. Amkaaa usilaleee” Mara ghafla  nikajikuta nikizinduka kutoka kwenye Yale mawazo. Nilijikuta nipo pale  pale kitandani nikiwa Nimekaa, nilikumbuka ni kweli Mama yangu  aliniambia nikihisi njaa niende Mezani nikale 

Basi nilihema, ndoto za Kutisha zilikua Sehemu ya Maisha yangu. Wakati  mwingine niliota ndoto nikiwa nimekaa tena nikiwa macho kabisa, hayo  Ndiyo Yalikua Maisha yangu baada ya kuponea chupuchupu kule Rukwa. 

Basi, nilinyanyuka taratibu nikaelekea sebuleni, nilikua nikitembea taratibu  sana. Nilipofika sebuleni nilikikuta chakula kikiwa hapo, nilifunua Hotipoti.  Nilijiandalia chakula Kisha Niliketi, nilianza zoezi la kufungua kichwa  changu chenye vidonda vya Ukimya .   Hukusoma? Isome Kwa KUGUSA HAPA Kisha Endelea

SEHEMU YA PILI

Nilikua nahisi maumivu makali sana Hadi pale nilipofanikiwa, ngozi ya  midomo yangu ilikua imegandana sababu ya Ukimya wangu, hata kula  yangu nilikua na uwezo wa kukaa siku tatu bila kula chochote kile Hadi pale  nitakapojisikia. Hii Hali ni Bora uendelee kuisoma kutoka kwangu lakini  isikukute. 

Nilianza kula taratibu, huku macho yangu yakiutazama mlango wa chumba  Cha Mama yangu. Mlango ulikua Wazi, siyo kawaida ya Mama yangu  kabisa yaani aingie chumbani halafu asiufunge mlango wake? Hapana. 

Niliendelea kula huku nikiendelea kuutazama sana ule mlango bila hata  kupepesa macho yangu.  

Moyo Wangu ulianza kwenda Mbio, sikuelewa ni kwanini. Basi niliacha  kula Kisha nilinyanyuka na kuanza kutembea kuelekea Mlangoni kwa  Mama yangu. 

Taratibu nilikua naendelea kukanyaga sakafu iliyojaa baridi huku nafsi  yangu ikiniambia nitarajie kuona kitu kisicho Cha Kawaida. Nilimeza mate  Kisha nilisimama mlangoni, halafu niliufungua zaidi ule mlango. Sauti ya  Bawaba ilisikika kuashiria kua mlango ulikua ukipitia mateso ya  kufunguliwa kwa nguvu.

Nilikosa pumzi kwa nilichokiona, nilihema kwa kukatishia. Macho  yalinitoka nikimtazama Mama yangu aliyekua akining’inia kwenye kenchi,  mtandio ulikua umeibana shingo yake, Mama yangu alikua amejinyonga 

Chozi lilianza kunibubujika, nikajikuta nikipiga goti huku nikifungua  mdomo Wangu kwa mara ya kwanza na kumwita 

“Mama….Mamaaa…Mamaa” niliita kwa sauti ya chini huku Kila  nilivyoendelea kuita ndivyo sauti yangu ilivyotoka vizuri kabisa. 

Niliangua kilio kilichowafanya majirani waingie ndani, taratibu za kuutoa  mwili wa Mama yangu zilifanyika.  

Nililia sana, ilikua ndiyo mara ya kwanza Watu wanaisikia sauti yangu  baada ya Miaka mitano kupita, Kila aliyeisikia sauti yangu alishangaa sana  kuona nilikua ninaweza kuongea 

Mama aliacha Ujumbe juu ya meza uliosomwa na Mjumbe, alisema 

“MWANANGU SAIDA, USIHUZUNIKE WALA USILIE KWASABABU  NISINGELIWEZA KUENDELEA KUISHI NIKIKUONA WEWE KATIKA  HALI HIYO. UMEGUSA MAISHA YANGU, UMEGUSA HISIA YANGU.  HATA KAMA SITAKUA KARIBU NA WEWE LAKINI NAFSI YANGU  HAITAKUACHA” huo ndio ulikua Ujumbe wa Mama yangu 

Kumbe Mama alijinyonga kwasababu yangu, nilizidi kulia na kujilaumu ni  kwanini sikufungua kinywa changu na kuzungumza pale alipokuja  chumbani kuniita kwa ajili ya chakula, nilijilaumu kwasababu hakusikia  tena sauti yangu.  

Alianza Baba kufa kwa ajili yangu, Kaka Hamidu, Mjomba Kambona Kisha  Mama yangu. Hii iliniumiza sana, sababu ya haya yote ni Salehe na Mzee  Mwinyimkuu.  

Taratibu za Mazishi ya Mama yangu zilipangwa, ndugu walikuja kutoka  Sehemu tofauti tofauti. Kila aliyekuja alishangaa kuniona nilikua nikitoa  sauti ya kilio, walishanikatia tamaa na kuamini nilikua Bubu.  

Siku iliyofuata, Mama yangu kipenzi alizikwa. Baada ya mazishi, ndugu  walijadili kuhusu Mimi. Kutokana na Hali yangu walinitaka nikaishi Kibaha  kwa Shangazi yangu lakini nilikataa. Walinisihi sana kua isingelikua busara  kuishi mwenyewe, niliwaambia kua ningependa niishi peke yangu 

Ushawishi wao haukufua dafu kwangu kwani nilikua tayari nimedhamiria,  sikutaka kusikia habari za kwenda Kibaha au kunipa Mtu wa kuishi naye, 

nilisimamia msimamo wangu Hadi dakika za mwisho Kila mmoja  alikubaliana na Mimi japo kwa shingo Upande. 

Msiba ulipoisha walianza kuondoka mmoja mmoja Hadi wote  walipomalizika na kuniacha Mimi na nyumba yangu. Nyumba ilikua kimya  sana, niliachiwa pesa na ndugu zangu sababu nilikua Sina kazi. 

Nilipata Matibabu ya Mdomo Wangu, nilipona kabisa. Nilianza kuishi kwa  kujipenda, nikanawiri vizuri sana. Nilivaa vizuri, niliacha Tabia ya kukaa  mwenyewe, mara nyingi nilikua nazungumza na Watu. 

Kila aliyeniona mwanzo alishangaa sana kuniona nimekua Saida yule  waliyemjua, Saida aliyewavutia wengi kwa kujisitiri na kujifunza.  Nilikubaliana na Hali halisi kua Maisha yaliyopita yalikua mabaya lakini  yalishapita 

Kitu kimoja ambacho kilibakia kwangu ni chuki dhidi ya Wanaume,  sikuhitaji mahusiano na Wanaume, Alichonifanya Salehe hakikutoka kabisa  akilini Mwangu.  

Nilianza Maisha mapya yaliyojaa amani ndani yangu, hata zile ndoto za  Kutisha zilipotea. Nilikula na kulala vizuri bila wasiwasi, Miezi ilipita, kifo  Cha Mama yangu kilibadili kabisa Maisha yangu 

Bahati nzuri nilipata kazi kwenye sheli Moja pale pale Magomeni.  Nilijipatia pesa ya kukidhi mahitaji yangu, Sikuhangaika kuhusu pesa ya  kula, wala matumizi yangu Binafsi. 

** 

Siku Moja ilikua mishale kama ya Saa Moja hivi Usiku, nilikua kazini  nahudumia Wateja. Mara ilikuja gari Moja nyeusi, siikumbuki ilikua gari  gani. Ilipofika, nilijua ni mteja wa mafuta 

Lakini Cha ajabu, kilishushwa kioo tu Kisha ukatoka mkono. Sikumwona  aliyekua ndani sababu alizima taa za ndani halafu hata kioo chenyewe  hakukishusha chote, kingine nilikua na hekaheka na haraka. 

Nilipewa karatasi Moja. Kisha gari iliondoka, nilistaajabu sana lakini kabla  hata sijaisoma ile karatasi walikuja Wateja wengine hivyo nikaanza  kuwahudumia. Nilipomalizana na wale Wateja, niliitoa ile karatasi Mfukoni 

Niliketi kwenye kiti ili niangalie kilikua kimeandikwa nini, nilipoiangalia  nilikutana na maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa yakisema 

“SAIDA BADO UNA DENI NA SISI” 

“MH!” Niliguna, nikalikumbuka ile gari, ilikua gari ya kifahari. Nikajiuliza  Nina deni kwao kwa kipi, sikuwahi kumkopa Mtu pesa pia sikua na ukaribu  na Watu wenye pesa.  

Nikanyanyuka na kumfuata Mdada mmoja ambaye naye alikua akifanya  kazi pale kwenye kituo Cha kuuza mafuta, nikampatia ile karatasi.  Alipoisoma akaniangalia Kisha akaniuliza 

“Eeh shoga yangu, deni Hilo ilikuaje?” 

“Hata Mimi nashangaa kuambiwa nadaiwa halafu sikumbuki ni deni gani” “Mh! Kua makini tu Saida, wasije kua watoa Figo hao. Mjini hapa Ohooo‼”  

“Weee Mimi mwenyewe Mtoto wa Mjini” nilisema Kisha nilirudi kwenye  pampu yangu nikawa nahudumia Wateja. 

Japo nilimwonesha yule Mdada kua Sina hofu ila moyoni mwangu nilikua  Nina wasiwasi sana, Kila nilipofikiria sikupata jibu la swali langu Hadi  nilipoondoka na kurudi nyumbani, nilikumbuka Kauli ya yule Dada kua  huwenda ni Watoto Figo. 

Basi nikahakikisha nafunga milango vizuri, nikaoga Kisha nikala chips  nilizonunua Barabarani. Nilijikuta nimekua mwoga ghafla tu. Nilipomaliza  kula nilienda Moja kwa moja chumbani kulala, nilikua nimehama  chumbani kwangu nikawa nalala chumbani kwa Marehemu Mama yangu. 

Nilijifunika shuka gubi-gubi, nilijilazimisha sana Usingizi. Hali ya hofu  ilinitawala sana, kilichonipa wasiwasi zaidi ni kutajwa kwa jina langu  kwenye ile karatasi, niliulazimisha Usingizi Hadi uliponiteka. 

Nilishtuka asubuhi mapema, nikajiandaa Kisha nikaelekea kazini.  Nikamsimulia yule Mdada aliyekua akiitwa Veronica 

“Basi nenda polisi ukatoe taarifa Saida” alinishauri, lakini nilifikiria  nikaona anachokisema kipo sahihi. 

“Nitaenda mchana Wacha kwanza nifanye kazi za Watu hizi.” Nilimwambia  Veronica Kisha nikaendelea kufanya kazi huku nikisubiria Mchana niende  kituo Cha polisi kutoa taarifa.  

Ilipofika saa Nne asubuhi, alikuja Kichaa mmoja wakati huo Wateja walikua  wamekata. Alinitazama sana yule Kichaa Hadi niliogopa, nikampatia  Shilingi mia Tano ili aondoke lakini hakuondoka alikua akinitazama sana  

Nikamwita Veronica, alipokuja akajaribu kumfukuza yule Kichaa ambaye  alikua na nywele ndefu zilizotawaliwa na Uchafu, alikua amebeba Begi 

chakavu, alivalia suruali chakavu. Alikua akitutazama kwa hasira halafu  akasema 

“Wewe utakufa kwasababu unaingilia Maisha ya Watu” alimnyooshea  kidole Veronica.  

“Wewe fala nini, atakufa Mama Yako. Wewe jifanye chizi Mimi ni chizi zaidi  Yako” akasema Veronica kwa hasira, sote tulimchukulia kama chizi wa  kawaida tu. Halafu akaniangalia Mimi akaniambia 

“Watakuja kukuchukua kwasababu hawajamalizana na wewe Saida”  nilishtuka sana, sikuwahi kumwona kabla yule Kichaa lakini alilitaja jina  langu kuonesha kua alichokisema alikua anakimaanisha. Kisha alimtazama  Veronica akamwambia 

“Kimbelembele kimekuponza” Kisha aliondoka zake, namna alivyokua  akizungumza alionekana siyo Kichaa kama alivyoonekana. Veronica  alinitazama huku nikiuwona uso wa Uwoga ukimtawala. 

“Saida, twende Polisi. Wanaanzaga hivi hivi hawa halafu waje kufanya  matukio” Hata Mimi nilikua naogopa sana, tukamwita Meneja  tukamsimulia. Akaturuhusu twende Polisi kutoa taarifa ya vitisho  tulivyopewa na Watu tusio wafahamu.  

Tulibadilisha zile Sare za kazi, tukavalia nguo za kawaida Kisha tukaondoka  ili twende Polisi. Kutoka kazini kuelekea Kituo Cha Polisi siyo mbali sana,  tuliamua tutembee kwa Miguu, Njiani tulikua Tukizungumza kwa mkazo  kua Watu wale huwenda ni Majambazi walikua wakisoma ramani au ni  Watoa Figo 

Tulipokaribia kituo Cha Polisi, tulimwona yule Kichaa akitoka kituoni.  Alikua akishusha ngazi, Mimi nilikua wa kwanza kumwona Kisha  nikamwambia Veronica 

Tulisimama tukimtazama namna alivyokua alishusha ngazi, Kisha  tulitazamana kwa Mshangao mkubwa. Mtu tuliyekua tunaenda kumshitaki  alikua akitoka kituoni tena akiwa amevalia nguo zile zile za kuchakaa.  Mioyo yetu ilianza kwenda Mbio 

“Sasa tufanyaje Veronica?” nilimwuliza huku kijasho Cha hofu kikianza  kunitoka. Nilikua ninahema sana. 

“Saida, si unaona? Yule siyo Kichaa na ukitaka kuamini jiulize kwanini  alienda kituo Cha Polisi?” aliniuliza Veronica akiwa amenishika bega, mara  alisimama yule Kichaa Kisha aligeuza shingo kutazama tulipokua 

tumesimama. Nikamvuta Veronica tukajificha nyuma ya gari Moja lililokua  limepaki nje ya kituo Cha Polisi 

Tukawa tunamchungulia, alitazama sana pale tulipokua tumesimama,  Kisha aliondoka zake akipitia upande mwingine ambao ulikua na geti la  kutokea, sisi tulikua upande wa geti la kuingilia pale kituo Cha Polisi. 

“Mama yangu!” Nilisema huku nikishika Sehemu ulipo moyo Wangu,  nilikua nimeishiwa nguvu sababu ya Mshituko. Veronica akanyanyua  kichwa kumtazama akamwona akiondoka

Nini Kitaendelea? Usikose SEHEMU YA TATU Sasa ( Comments ziwe nyingi) 

SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPA 

SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINI 

SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPA 

SOMA KISASI CHANGU HAPA  

SOMA RIWAYA YA MSALA HAPA

JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa 

Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx  Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx Niliolewa Na Mtu Nisiyemjua xx

 

Leave A Reply

Exit mobile version