Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2025

    AFCON

    Ratiba ya kusisimua ya 16 Bora yakamilika AFCON Morocco 2025

    Hapa MSUVA Pale MPENJA Ofa Kibao Kutoka LEONBET

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home » Ni Yanga Sc Vs USM Alger I Fainali CAF Confederation Cup
    Africa | CAF

    Ni Yanga Sc Vs USM Alger I Fainali CAF Confederation Cup

    David MohamedBy David MohamedMay 18, 20231 Comment2 Mins Read
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    HISTORIA Imeandikwa!.

    Ndivyo unaweza kusema baada ya klabu ya Yanga kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza ikiwa ugenini katika Uwanja wa Royal Bafokeng, mjini, Rustenburg nchini Afrika Kusini.

    Naam!

    Yanga imetinga fainali hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kushinda mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali dhidi ya Marumo Gallants kwa mabao 2-1, na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-1, kwani katika mchezo wa kwanza ikishinda 2-0, nyumbani uwanja wa Benjamin Mkapa.

    Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na washambuliaji Fiston Mayele dakika ya 45 na Kennedy Musonda aliyetupia dakika ya 61.

    Katika nafasi nyingine, Mshambuliaji wa Yanga, Mayele amefikisha mabao sita katika michuano hiyo msimu huu na kuwa sawa na mshambuliaji wa Marumo, Ranga Chivaviro aliyefunga bao moja la kufutia machozi. Mastaa wa Yanga waiocheza mechi na kuweka historia ya kuhusika moja kwa moja kwenye kuivusha timu kutoka nusu fainali hadi fainali ni Kipa Djigui Diarra.

    Mabeki, Dickson Job, Shomari Kibwana, Bakari Mwamnyeto, na Ibrahim Hamad ‘Bacca’.

    Viungo ni Yanick Bangala, Kharid Aucho/Stephane Aziz Kii, na Mudathir Yahya huku mawinga wakiwa Tuisila Kisinda/Jesus Moloko, na Farid Mussa.

    Washambuliaji waliocheza leo ni Mayele, Kennedy Musonda na Clement Mzize.

    Yanga itakutana na USM Alger katika mchezo wa fainali. Ikumbukwe fainali zitachezwa mechi mbili nyumbani na ugenini na Yanga itaanzia nyumbani uwanja wa Benjamin Mkapa.

    1 Comment

    1. 66b chính thức on December 26, 2025 3:22 am

      Không giống với các trang web không rõ nguồn gốc, 66b chính thức đầu tư nghiêm túc vào hệ thống quản lý rủi ro và bảo vệ người dùng. Tất cả các giao dịch tài chính đều được mã hóa, đồng thời nền tảng cung cấp công cụ tự kiểm soát cho người chơi như giới hạn đặt cược và tính năng tự loại trừ. TONY12-24

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Stori Mpya January 31, 2026

    Matokeo Ya Kidato Cha Nne 2025

    NECTA yatangaza matokeo ya Kidato cha Nne 2025, kiwango cha ufaulu chafikia asilimia 94.98 Baraza…

    AFCON

    Ratiba ya kusisimua ya 16 Bora yakamilika AFCON Morocco 2025

    Hapa MSUVA Pale MPENJA Ofa Kibao Kutoka LEONBET

    In the name of LOVE – 12

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2026 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.