Ilipoishia “Siku nyingine sitofikiria mara mbili nini cha kukufanya, ulistahili zaidi ya hapaβ alisema kisha aligeuka aondoke lakini akapata hisia fulani iliyomwongoza kugeuka na kumtazama Mzee huyo aliyekua akitetemeka huku mara kadhaa akikodolea macho ndani.
Naye IGP akapeleka macho ndani ya Kijumba hicho, macho ya Elizabeth yakagongana na macho ya IGP Hassan Kitulo, lakini IGP alikua hajamwona Elizabeth ila macho yote aliyatupa kwenye viroba, akapiga hatua dhaifu kuelekea mlangoni, aliyakaza macho yake, kisha alipapasa kiunoni pake akatoa Bastola.Β
EndeleaΒ
SEHEMU YA NANE
Naye Elizabeth akaiweka sawa Bastola yake baada ya kuona IGP alidhamiria kusogea mbele akiwa kimya. IGP hakukwepesha wala kupepesa kope za macho yake akiviangalia vile viroba, yule Mzee alipoona hivyo akaamua kumtoa IGP kwenye reli.
βSamahani kwa hilo, unajua hofu imetutanda sababu hatujui ni kitu gani kinafanyika hapa Kijijiniβ alisema yule Mzee, angalau aliweza kumfanya IGP amtazame yeye, haraka Elizabeth alihama eneo la viroba na kuingia chumbani.
βUnataka kufanya nini? Hebu ongoza ndaniβ alisema kwa kukaza sauti, IGP alisema tena kwa hasira wakati huo mmoja wa askari alifika hapo kumpa taarifa IGP
βSonga ndani haraka, angusha vile virobaβ alisema akiwa amekaza sauti, hakuna kati yao aliyeweza kugundua kua Elizabeth alishahama haraka sana, Mke wa yule Mzee alijishika kichwa maana alishajua huo ndiyo mwisho wa Binti yao kama ambavyo Elizabeth aliwaahidi kama Polisi watamshtukia.
Yule Mzee alifika kwemye viroba wakati huo IGP akiwa ameielekeza Bastola yake vilivyo, moja ya sifa ya IGP Hassan Kitulo ni ulengaji, aliielekeza vyema Bastola yake, Mzee alipofika hapo alishusha pumzi kuu baada ya kukuta patupu, angalau alipata nguvu ya kufanya ambacho IGP alikua akikitaka
Aliviangusha kwa mbwembwe, palikua patupu hata IGP alishashusha Bastola yake na kuirejesha kiunoni
βKuna nini?β alimgeukia yule Polisi aliyefika hapo, alimtazama kwa makini
βHajapatikana popote ndani ya makazi hayaβ alisema, IGP akaitazama ile familia kisha akaondoka na yule Polisi aliyekuja. Wale wazee wakakimbilia chumbani, wakamkuta Elizabeth akiwa anachomoka chini ya Kitanda, akawakabidhi Binti yao Halafu akawaambia
βAhsante kwa kunisaidiaβ alisema kisha aliketi kitandani, yule Mzee alimtazama Elizabeth, akiwa kama Mzazi alimtazama Msichana huyo kwa jicho la huruma sana, moyoni alijua hakua Mtu mbaya maana angelikua mbaya katu asingeli mshukuru Mzee huyo.
βKwanini wanakutafuta kwa nguvu kubwa kiasi hiki Binti, huonekani kama Mtu mbayaβ aliuliza kwa upole sana Mzee yule. Elizabeth aliingiza mkono wake kwenye chupi kisha alitoa Flashi ndogo akawaambia
βWanaitafuta hii, kama nitakua salama hadi mwisho basi Rais atalazimika kuikimbia Nchi, anatumia nguvu kubwa kuhakikisha anaipata hii, ili waipate ni lazima waniuwe kwanzaβ alisema Elizabeth kisha aliirejesha ile Flashi mahali alipoitoa.
βUnataka tukupe msaada gani?β aliuliza Mzee yule tena aliuliza kama Mtu aliyeamua kutaka kumsaidia Elizabeth
βNahitaji kutoka ndani ya Kijiji hiki nifike picha ya ndege, huko nitapata Msaada ninaoutaka, sioni kama mnaweza kunisaidia kwa lolote lileβ alisema Elizabeth, yule Mzee alisimama kisha alielekea kwenye Begi moja akalisogeza pembeni, chini palikua na Mbao kadhaa fupi, akageuka kumtazama Ekizabeth kisha akaziondoa zile mbao
βNjooβ alimwita Elizabeth, haraka alisogea hapo, alichokiona alijikuta akimtazama zaidi Mzee huyo tena alimtazama kwa Mshangao, Elizabeth alichuchumaa ili kuangalia kwa ukaribu zaidi. Palikua na shimo dogo lililochimbwa na kusimikwa simenti, ndani yake palikua na Boksi lenye silaha nzito za moto
Pale pale Elizabeth alimnyooshea Bastola yule Mzee
βWewe ni Nani?β alihoji Elizabeth.
βUsihamaki nataka kukusaidia kuondoka hapa Mwambisiβ alisema yule Mzee kisha akamwambia
βMimi ni mstaafu wa jeshi, hizi ni miongoni mwa silaha nilizozitunza kwa kipindi chote, nilikimbia Uwanja wa vita wakati wa vita ya kumwondoa Idi Amin, tangu hapo nimekua na hizi silaha, nazitumia kuwindiaβ alisema Mzee huyo, Elizabeth alimeza funda zito la mate kisha akapeleka mkono kwenye boksi hilo huku mate yakimtoka kwani alishajua kua silaha hizo ndizo zitakazo msaidia kuondoka hapo Mwambisi.
Palikua na M2 Carabaine, AK47 na Risasi za kutosha, alitabasamu.
**
Hekaheka Ikulu, simu ya dharura.
Simu ya Mezani ilikua ikiita mfululizo, Rais Lucas Mbelwa alikua kitini akionekana kukerwa zaidi na simu hiyo. Alikua ameloana jasho akiwa kwenye kiti kikubwa Ofisini kwake, shingo yake ndefu ilimeza mate mengi yaliyopita kwa shida sana, alilegeza tai yake huku akipepesa macho yake
Nywele zake alizozitia karikiti zilikua Tim-tim, pumzi nzito iliusindikiza mkono wake hadi kwenye simu ya Mezani, akaipokea kwa kuiweka sikioni moja kwa moja na kuanza kutupa maneno makali, halafu akamalizia
βAsipokamatwa tumeishaβ alisema kisha aliikata simu hiyo, mara waliingia Wanaume wawili waliovalia suti nyeusi, waliketi bila kukaribishwa huku wakionekana kua na hali kama aliyonayo Rais Mbelwa, Mmoja aliitwa Ignas Zakaria, huyu alikua Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, mwingine ni Balozi Juma Nguvumbili, huyu ni Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia
βTunafanya nini Mkuu, hali inazidi kua mbaya.
Tunaelekea siku nzima isiyo na mafanikio, huyu Kirusi ni tatizo kwetuβ alisema Balozi Juma Nguvumbili akiwa anagonga meza, Rais Mbelwa alikua amejiinamia, hapo hapo Waziri Ignas Zakaria akatoa wazo
βKama yupo ndani ya kile Kijiji basi hakuna budi kutuma kikosi kwa ajili ya kusafisha Kijiji chote, afie ndani yakeβ wazo la Waziri liliungwa mkono na Balozi ambaye alihanikiza
βMkuu tuma kikosi kazi kwa ajili ya kusafisha kila kitu kule, IGP pekee apewe taarifa, hili tukio lifanywe kua ni ugaidi na tutapindisha maelezo ili picha kubwa iwe Ugaidi, japo Polisi wengi watauawa lakini kirusi kitakua kimeshaondokaβ alisema, Rais alizisugua nywele zake alizozidi kuzitibua
Alhema kama vile anakimbizwa, macho yake yalikua mekundu shauri ya kutafakari kwa muda mrefu bila kupata jibu
βVipi kuhusu wana Kijiji?β aliuliza Rais.
βMkuu tunafyeka wote kisha kikosi kazi nacho kinafyekwa na kikosi maalumβ alisema Balozi, haraka Rais bila kujiuliza mara mbili alinyanyua simu yake na kumpigia IGP Hassan Kitulo aondoke Kijijini hapo haraka sana Halafu akanyanyua simu kwenda kikosi fulani kwa ajili ya kufyeka kijiji kizima wakati huo huo alipiga simu ya dharura kule BLACK SITE na kuagiza Makomandoo kwa ajili ya kufyeka kikosi maalum ambacho kitafyeka Kijiji kizima.Β
Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya Tisa ya MSALA hapa KIJIWENI
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost KISASI CHANGU Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMΒ Β
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAΒ
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIΒ
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALAΒ Β
21 Comments
π π kikosi kazi kunafyekwa na kikosi maalum then kikosi maalum kinamalizwa na makomandoπππ
Atari
So poa kiongozi
Ni hatariiii nakukubali sana mwandishiii
Admin mbona fupi sana jmnπ₯Ί
Refusha kidogo basi ama post hata sehemu nne kwa sikuπ
Game ndani ya game πni π₯π₯.
Naona kabisa sehemu ya 9 ni vita kali sana kama kwenye picha ya rambo au anorld.
Duh,, admin weka iwe ndefu bas
Daaah admin iwe ndefu kidogo‘‘‘‘,ni nzuri sana umetisha
Nice
Mambo ni π₯π₯
Sema muwe mnaitoa kwa wakati
Makomando watafuekwa na baroz na wazili Kisha hao wawili watafuekwa na raisi rais hata chukua mda sana atakufa kwa plesha kwasababu ya ile frashi kufika katika vyombo vya habari mwisho
Duh! Fyeka kijiji kizima
Daaah Riwaya ya moto Sana hii ama kweli huu Ni msalaπ
Ni motooooooooooπ₯π₯π₯
π₯π₯noumah sana admin silaha adimuπ«π«
Wananguee tuwe tunakumbuka kumpongeza adimini kwachochote
9 iko wap
zkw3ap
xfo39t