Ilipoishia “Upande wa pili, Muhonzi alikua akiteseka ndani ya Godauni, Zagamba alimshikilia ili aipateย Nyaraka M21 kutoka kwa Elizabeth, Alikua ndani ya chumba kimoja chenye dirisha dogoย tena liko juu sana, hewa ilikua nzito lakini kibaya zaidi alipaswa kujisaidia ndani ya Chumbaย hicho, Mikono yake ilifungwa kamba ili asifanye ujanja wowote ule.ย
Akili yake ilishashtuka mapema kua kuna lililompata Elizabeth ndiyo maana Zagamba alikuaย mwenye hasira sana, tumaini la yeye kuendelea kua hai aliliona kua finyu kabisa, akaanzaย kutafuta namna ya kujisaidia hapo ili aweze kuokoa uhai wake.
Kabla hajafanya chochote akakumbuka tukio moja… ENDELEAย
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
Ndani ya PIZA HUNTย
Muhonzi alikua chini ya Ulinzi wa walinzi wa eneo la chini la Piza Hunt, mahali ambapo Nyaraka M21 ilikua imehifadhiwa kwa Maagizo rasmi ya Rais Lucas Mbelwa, Walinzi haoย walionekana wazi kua hawakua Raia wa Tanzania, Rafudhi yao ilikua ya Kikongo. Kiswahiliย chao pekee kilimfanya Muhonzi atambue kua eneo hilo halikua eneo salama kwake.ย
Walimzunguka mara baada ya kuufungua Mlango wa eneo lenye mfanano na Maktaba, kishaย mmoja ambaye alikua mweusi tii, akiwa na Bunduki alimuuliza Muhonziย
โNi kipi kimekuleta hapa, huonekani kama Mtu wa hapaโ alimalizia kwa kumnyoosheaย Bunduki Muhonzi, jicho la Muhonzi lilimtoka Pima, alianza kumkagua Mlinzi huyo mwenyeย sare nyeusiย
โNakuuliza tena Kijana, nini kimekuleta hapa?โ safari hii aliikaza sura yake ngumu yenyeย vipere vingi, tena kwa Msisitizo alimtolea machoย
Muhonzi mkononi alikua na kisu, kiuno chake kilikua na Bastola, akaporwa vyote. Kishaย akakamatwa na kuingizwa ndani zaidi, hakuamini macho yake, aliona Madawa mengi yaย kulevya yakiwa yanawekwa kwenye mifuko, palikua na kitu mfano wa Maabara kubwa,ย ย
walinzi hawakutaka Muhonzi atazame zaidi akasukumizwa mbele hadi kwenye chumbaย kimoja.ย
Chumba hicho kilikua na meza na Kiti kimoja, pia palikua na taa iliyoshushwa karibu zaidiย na kiti na meza, akakalishwa hapo kisha yule Kiongozi wa wale Walinzi akaketi pia hukuย mikono yake akiwa ameiegemeza kwenye ile meza.ย
Walinzi wengine wakatoka na kuufunga mlango, wakabakia wawili tu ndani ya Chumbaย hicho, yule kiongozi akamtazama Muhonzi kisha akatabasamu na kuachia kicheko kidogoย
โNiambie nini kimekuleta hapa, wewe ni Nani?โ akayatupa maswali mawili kwa Mkupuo,ย Muhonzi hakujibu chochote, muda wote aliwaza namna Maisha yake yataishia mikononiย mwa Mwanaume huyo, akayaruhusu Macho yake kucheza kama piaย
Akaona wazi kua nafasi pekee ya yeye kua hai ni kujitetea hapo, Yule Mlinzi kiongoziย alipoona hajibiwi chochote akazunguka na kumfwata Muhonzi kwa hasira, akamnyanyuaย kama vile ana mnyanyua Mtoto mdogo. Haraka Muhonzi akaiyona peni kwenye mfuko waย shati la yule Mlinzi akaipigia mahesabu mazito baada ya kuona Mwanaume huyo amehamanikaย
Akanyoosha mkono haraka na kuifungua kisha akamkita nayo eneo la shingo, alilengaย mshipa muhimu zaidi, damu nyingi zikamruka yule Mlinzi, akapepesuka na kuanguka chiniย huku akikoroma na kutapatapa, pumzi zikamkaa sawa Muhonzi akaishika shingo yakeย iliyokua imekutana na dhoruba kali muda mchache uliopita
Akaichomoa Bastola kiunoni kwa yule Mlinzi kisha akaiweka sawa, kitu cha kwanzaย alichowaza ni kupata lile faili, kama hatofanikiwa kulipata basi pengine watalikosa kabisa. Alikua na uhakika kua faili lipo ndani ya eneo hilo la chini, akaruhusu kumbukunbu zakeย zihesabu idadi ya walinzi aliowaona, walikua zaidi ya Walinzi tisa wenye silaha kali za moto.ย
Akasogea mlangoni taratibu na kuanza kuufungua mlango, akaona viatu vya kijeshi pandeย zote mbili yaani kulia na kushoto kwa ule Mlango, walinzi hao hawakushtuka kama mlangoย umefunguliwa kwa namna ambavyo Muhonzi aliufungua mlango huo kitaalam sana.ย
Akairejesha Bastola kiunoni kisha akapiga mahesabu namna ya kukabiliana nao, umbo laย Muhonzi lilikua jembamba tena dogo kiasi kwamba Mtu hawezi kufikiria kama anaweza hataย kurusha ngumi, akausogeza mguu wa kulia na kisha wa kushoto, hapo akapiga mahesabu yaย kukita shingo za Walinzi hao kwa wakati mmoja, akayapiga mahesabu yake vizuri ni sehemuย gani aziguseย
Akachomoka kama Kipanga kisha akawapiga vifuti vya maana maeneo ya shingo,ย akawazimisha wote kwa wakati mmoja kisha akawaburuza hadi ndani ya chumba naย kuwafungia humo, akatoka na kukutana na korido moja fupi lenye vyumba vitatuย vilivyokaribiana.ย
Taratibu akaanza kutembea kwenye korido hiyo iliyo tulivu sana, hakuna Mtu mwingineย aliyekutana naye ndani ya Korido hiyo hadi anafika korido nyingine , hapo akajiuliza niย kwanini pako kimya sana, akapata wazo la kufungua chumba kimoja baada ya kingine. Kilaย chumba alichokifungua kilikua kitupu.ย
Ukimya ulizidi kumzoga Muhonzi hadi akaanza kupatwa na woga, akaendelea mbele zaidiย kutafuta chumba ambacho kina hizo nyaraka za Siri, pasipo kujua kumbe tayari walinzi woteย walishapewa taarifa ya kutoka ndani ya Eneo hilo ili sumu isambazwe. Moja ya vituย ambavyo vilikua havitakiwi katika eneo hilo ni purukushani, ili kuendelea kuliweka eneo hiloย salama ilikua ni lazima waweke mfumo wa sumu ili kama kutatokea uvamizi basi harakaย wawamalize maadui zao kimya kimya.ย
Walinzi na viongozi walitoka ndani ya jengo, kisha wakawa wanasubiria maelekezo maalumย kutoka juu yaani kwa Rais ambaye alikua akilitazama tukio la uvamizi akiwa Ikulu, mkononiย alikua na kikombe cha Kahawa kilichokua kinafuka moshi.ย
Kila mmoja alikaa kimya kusubiria agizo la Rais ambaye naye alikua makini sanaย kumtazama Muhonzi kwenye kompyuta. Akayavuta mate kisha akayapitisha kooniย
โAchia sumu sasa hiviโ alisema Rais Lucas Mbelwa, mara moja wataalam wa Ulinzi wa paleย Piza Hunt waliachia Sumu iliyokua inafuka kupitia chemba za hewa, kila mmoja alikaaย kimya kuangalia namna Muhonzi atakavyoteketea, Mke wa Rais Mbelwa alikua hapoย akiangalia tukio hilo nyeti, huku akitabasamu kwasababu yeye ndiye aliyeutoa mpango waย kuibiwa kwa hizo nyaraka.ย
Ndani ya Piza Hunt, hatua za taratibu zilikua zikipigwa na Muhonzi tena kwa tahadhari yaย hali ya juu kabisa, ghafla alianza kuhisi uzito wa hewa ndani ya Jengo, akatambua kwaย haraka kua hiyo ilikua ni sumu, akataharuki, haraka akaanza kutafuta njia ya kutoka hapo.
Alipojaribu kutaka kufungua mlango aliona tayari ulikua umefungwa, akajikuta akianzaย โkuhahaโ kwa kukosa hewa safi, ndani ya dakika moja tu alianza kushindwa kupumua vizuriย akanguka chini, hapakua na hewa nyingine aliyokua akiivuta zaidi ya hiyo sumu.ย
Sasa alijiona akikikaribia kifo alichokitafuta mwenyewe, akaanza kutetemeka huku akizidiย kulegea lakini ghafla alikuja Mtu aliyefunika uso wake kwa โMaskโย
Mtu huyo alikua amevalia koti jekundu alilolitumia kuficha sura yake, akamwinua Muhonziย na kumvisha Mask iliyoanza kumpa hewa nzuri Muhonzi. Nguvu ilimpompata vizuriย akajaribu kumtazama usoni, akagundua Mtu huyo alikua Ni Elizabeth Mlacha. Akatoaย tabasamu la kuchanua, Elizabeth akageuka na kuitazama Kamera moja iliyo nyuma yao,ย alishagundua kua walikua wakifwatiliwa kupitia Kamera hiyo.ย
Rais alishtuka, wote walishtuka. Elizabeth akafunua kofia kichwani pake, akatoa ile Mask iliย waiyone sura yake, Rais akatema kahawa kwa Mshituko baada ya kumwona Mchepukoย wake, akagundua sasa kua kilichomfanya Elizabeth akawa karibu naye ni hizo faili za siri,ย papo hapo akapaza sauti Rais akiwaambia walinziย
โHakikisheni hakuna anayetoka mzimaโ alisema Rais kwa ghadhabu nzito. **ย
Elizabeth na Muhonzi wakaanza kutafuta nyakara M21 ndani ya lile jengo, ramani yote tayariย Elizabeth alishapewa na Mke wa Rais, ikawa rahisi kufika ilipo shelf maalum ya kuhifadhiaย nyaraka, kwanza wakaharibu kamera zote ili wasigundulike walipo huku wakijua fika kuaย muda mchache ujao kutakua na patashika nzito sana.ย
Elizabeth alikua na simu ambayo ndiyo iliyokua ikiwaongoza kuelekea mahaliย zilipohifadhiwa Nyaraka hizo, walipofika mlango husika walimwona Mtu mwingine akitokaย hapo, Mtu huyo alikua amevalia kofia nyeusi, alikua na Mask usoni na kwa haraka harakaย waligundua kua alikua mwanaume, mkononi alikua na Brifkesi ambalo kwa harakaย waligundua kua ndimo ilimo Nyaraka M21.ย ย
Mtu huyo alikimbia kwa haraka kuifuata korido moja ndefu, haraka Elizabeth alimfwataย huku Muhonzi akiingia kwenye chumba ambacho yule Mwanaume alitokea.ย ย
Mfukuzano ulikua mkali kwa hatua kadhaa, kisha ghafla yule Mwanaume alisimama,ย aligeuka kisha aliliweka lile Brifkesi chini, akatabasamu na kumwambia Elizabethย
โNajua umekuja kwa ajili ya Nyaraka M21, hiyo hapo lakini unapaswa kunimaliza kwanzaโย alisema kwa kujiamini sana, aliongea kwa sauti iliyojaa Bashasha kama walikua kwenyeย utani, Elizabeth akajua hapo haitokua kazi rahisi kupambana na huyo Mtu, akaangalia saaย yake.. Nini kitaendelea?ย
Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni
Lipa Namba: 57900454
Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
Mtandao: VODACOMย ย
SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย
SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย
JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa
MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA



8 Comments
Wa Kwanza hapa kwenye huu msala๐ค๐ค
Msala ni msala kweli
Ni hatariiii
,
Duuuuh ๐ฅ
Admine Mambo unayafanya yawe pambe saana yร an Ni bul bul dร ah๐ฅ๐ฅ
Msala ni msala haswaa
y4g714