Close Menu
Kijiweni

    Subscribe to Updates

    Get the latest updates from Kijiweni.

    Za moto

    In the name of LOVE – 05

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    Facebook X (Twitter) Instagram
    • Wasiliana Nasi
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest Vimeo
    Kijiweni
    • Home
    • CAF
    • Soka la Bongo
    • Ulaya
    • Chuo Cha Kubeti
    • Hadithi za Kijiweni
    • Forum
    Kijiweni
    You are at:Home ยป MSALA Sehemu Ya Ishirini Na Tano-25
    Hadithi

    MSALA Sehemu Ya Ishirini Na Tano-25

    Kaka MkubwaBy Kaka MkubwaSeptember 6, 2024Updated:September 7, 20249 Comments10 Mins Read2K Views
    Facebook Twitter Pinterest Telegram LinkedIn Tumblr Email Reddit
    MSALA
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest WhatsApp Email

    Ilipoishia โ€œSijapata kumwona Mwanadamu Mbishi na Mgumu kama huyuโ€ aliutupa mkono wakeย  uliojaa damu kwa hasira sana kisha akarudi kuketi kitini akitafakari ni namna gani afanye iliย  apate taarifa nyeti. Haraka akanyanyuka kutoka kitini kwa hasira akamfwata tena Elizabeth,ย  akamwambia

    โ€œUkiendelea kuwa jeuri utamfuata Rais alipoโ€ alisema kisha akaondoka ndani ya chumbaย  hicho, haraka Elizabeth akatambua fika kua Rais alikua ameshauawa na kilichokua kinaendaย  kufanyika ni Uasi mkubwa wa kuitawala Nchi.ย 

    Elizabeth akiwa ananingโ€™inia akaukumbuka Usiku wa Heka Heka. Endeleaย 

    SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

    MSATA. SAA TANO USIKUย 

    Elizabeth alifika Msata akiwa amebadilisha mwonekano wake kama Msichana mwenyeย  mambo mengi mjini, aliweka kope Bandia, akaweka kucha, alivalia gauni fupi lenye mgโ€™ao,ย  juu aliweka Wigi fupi ambalo lilimfanya aonekana kama siyo yeye, eneo ambalo alielekezwaย  na Zagamba wakakabidhiane Nyaraka M21 lilikua ni Msituni.ย 

    Akaiweka gari kando ya Barabara kisha taratibu akaingia Msituni, Hapo aliambiwa kuaย  atakutana na Mtu wa Zagamba aliyepewa kazi ya kupeleka Nyaraka kwa Zagamba, alipoanzaย  kukaribia aliona tochi, akajua ndiye anayepaswa kuonana naye hapo. Akaiweka sawa Bastolaย  yake ndogo aliyoitoa kutoka kwenye mkoba wakeย 

    Akatembea taratibu tena kwa tahadhari kubwa sana, hakutaka kumwamini yeyote. Mkononiย  alivalia kifaa chenye GPS ambayo ilikuwa inamwezesha Muhonzi kuona mitembeo yaย  Elizabeth na kujua yupo wapi. Alipofika hapo alikutana na mwanaume mmoja aliyevalia kotiย  jeusi, ndani zaidi ya Msitu mzito wenye kiza kizito kisicho na nuru kabisaย 

    Chini ya Mti mmoja ndipo alipokuwepo Mtu huyo.ย 

    โ€œUna mzigo?โ€ aliuliza Mwanaume huyo, Elizabeth akamjibu kwa umakini โ€œSiwezi kukupa mzigo bila kuona namna utakavyonipa pesaโ€ย ย 

    โ€œBinti, Bilioni 30 ni ngumu sana kutembea nazo hata kama zipo kwemye mfumo wa Dola.ย  Nimeziacha ndani ya gari, naomba nione hizo nyaraka kwanza ndipo nikupe pesa yakoโ€ย  Mazungumzo haya yalikua Mubashara kwa Muhonzi.ย 

    Elizabeth akatoa Flashi akampatia Mwanaume huyo asiye mfahamu, kisha Mwanaume yuleย  akawasha kifaa chenye mfanano na Kompyuta Mpakato akaiingiza Flash na kuhakiki, akatoa tabasamu la kuchanua ambalo lilimpa ishara Elizabeth kua Mtu huyo hakua na lengo zuriย  kwake, hakuishia hapo aliangusha kicheko.ย 

    Haraka Elizabeth akaichomoa Flash kutoka kwenye kompyta kisha akamnyooshea Bastolaย  Mwanaume huyo.ย 

    โ€œPesa nikupe Nyarakaโ€ alisema, mkononi alikua na tocho ndogo lakini alipommulika vizuriย  alimwona Mwanaume huyo akiwa na mavazi ya Usalama wa Taifa, akajua wazi kua alikuaย  ameingia Mtegoni.ย 

    โ€œOooh taratibu Elizabeth, pesa yako ipo ndani ya gari. Ok, ongozana na Mimiโ€ alisemaย  Mwanaume huyo, Elizabeth akaongeza umakini wa kutosha baada ya kugundua hapo Msituniย  hapakua eneo salama kwake.

    Akayaangaza macho yake kama Paka mwizi, kisha akamsukuma mbele yule Mwanaume iliย  amtumie kama chambo cha yeye kutoka pale Msituni, akilini mwake alishaiuwa Biashara yaย  Nyaraka zile za siri baada ya kuona dalili za uwepo wa hatari. Hatua za yule Mwanaumeย  zilikua za mahesabu makali sana, Elizabeth alishaligundua hilo sababu alikua Jasusiย 

    Sauti ya Muhonzi ikasikika Masikioni mwa Elizabeth, ikamwambiaย 

    โ€œNaona uwepo wa Watu zaidi ya Mmoja hapo Msituni, haraka Ondokaโ€ alisema kishaย  Elizabeth akajibu kwa Ukimya huku sauti za Majani makavu yaliyokanywagwa zikiendeleaย  kusikika. Moyo wa Elizabeth ukaanza Riadha ya haraka, nywele zikamsisimka vya kutoshaย  huku vipele vidogo vidogo vya Tahadhali vikianza kumtoka.ย 

    Hatua ya sita ya yule Mwanaume ilimfanya Elizabeth ashuhudie teke kali likimuelekea,ย  kwakua tayari alishaanza kuzihesabu hatua za yule Mwanaume na kujua hatua hizoย  alilikwepa teke kwa haraka huku akiukunja mgongo wake kuelekea mbele, aliporudiย  alikutana na kipande cha mti kilichotua eneo la tumbo na kumjeruhi.ย 

    โ€œMshenzi unafanya nini?โ€ aliuliza Elizabeth, hapo akajua fika kua taarifa za yeye kua ndaniย  ya Msitu zilishauzwa muda mrefu hivyo kituo kinachofwata ni kukamatwa na kuuawa kikatiliย  na Wanaume hao wenye sare za Ikulu, kwa haraka akili yake haikuchekecha vyema na kujuaย  ni Nani aliyeuza mpango huo, akajikaza ili atoke ndani ya Msitu.ย 

    Bastola ilikua imeshamtoka, kutokana na giza zito hakufanikiwa kuiyona mahali ilipoย  dondokea, mkononi alikua na Flashi yenye nyaraka, akaisweka haraka ndani ya chupi naย  kuifunga kwa zipu kisha akajiweka sawa kukabiliana na Mwanaume huyo aliyekua na tamboย  za kutosha kua angemmaliza Elizabeth hapo Msituni.ย 

    Tochi ilikua pembeni, Elizabeth alipoutoa mkono tumboni alihisi uwepo wa damu Mbichiย  yenye harufu, ikampa hasira, akamvaa Mwanaume yule mwenye ngumi nzito.ย 

    Akashusha mvua ya ngumi nyepesi alizolenga sehemu moja, kisha akaachia pigo zito kwaย  kutumia skuna yake iliyomtoboa yule Mwanaume eneo la shavu. Akatema damu hukuย  akigugumia kisha akapiga filimbi ya kuita Watu wengine walio pale Msituni, dakika moja tuย  alishajua kupambana na Elizabeth isingelikua kazi rahisi kuifanya.ย ย 

    Tochi zikaanza kutapakaa pale Msituni, Elizabeth akamshushia na teke takatifu lililomlazaย  yule Mwanaume kisha akaanza kukimbia ili kuokoa Maisha yake huku akivuja damu, eneoย  ambalo alikatisha lilikua na Miiba ya kutosha iliyomkwangua kila eneo la mwili wake naย  kumchania nguo.ย 

    Alikatiza ndani ya Msitu wenye giza nene huku akijua fika kua hapakua na Umbali mrefuย  kutoka hapo kuelekea Barabarani alipoacha gari yake, lakini haikua rahisi kufika Barabarani,ย  ilimtaka atumie nguvu zake zilizoanza kumsaliti. Alikimbia huku akifukuzwa na Wanaumeย  kadhaa wenye tochiย 

    La haula!ย 

    Akafika Barabarani lakini hapakua na gari yoyote, eneo ambalo alitokea halikua lile eneoย  aliloingilia, akaanza kuifukuza ile Barabara asijuwe anasonga mbele au anarudi nyuma, gizaย 

    lilikua la kutosha na hapakua na dalili ya kutokea kwa gari au Pikipiki, akamwambiaย  Muhonziย 

    โ€œSijui kama nitachomoka salama Muhonzi, hali yangu siyo nzuriโ€ akasema kisha akakitupaย  kifaa chake cha Mawasiliano, Bahati nzuri akamulikwa na taa ya gari kutokea nyuma yake,ย  akasimama na kupungia mkono gari isimame.ย ย 

    Ndani ya gari alikuwamo Benjamin Kingai, rubani wa Shirika la Air Tanzania aliyekuaย  akitokea Arusha kwa Mpenzi wake, gari iliposimama akafungua mlango na kuingia harakaย  kisha akamwambia yule dereva kuaย 

    โ€œOndoa gari Harakaโ€ Benjamin akiwa mwenye taharuki akawaona wanaume wenye Silahaย  wakitokea Msituni, haraka akaliondoa gari bila kuuliza swali lolote.ย 

    **ย 

    Ndani ya Ikulu. Saa 9 Alhasiri.ย 

    Waziri Mkuu Haji Babi, alielekea eneo la siri ambalo Rais alikua akitesa na kuuwa Watesiย  wake, akaingia kwenye moja ya chumba ambacho alikuwamo Mke wa Rais Lucas Mbelewa,ย  hakutaka kutangaza kifo cha Rais Bila kupatikana kwa Nyaraka za siri ambazo zilikuaย  mikononi mwa Elizabeth.ย 

    Alipofika alimkuta Mke wa Rais akiwa ameketi sakafuni, Haji Babi akasogea naย  kuchuchumaa mbele ya Mke wa Rais kisha akamwambiaย 

    โ€œMasaa machache yajayo nitatangazwa kua Rais wa Nchi hii, hakuna Mtu wa karibu waย  Lucas atakayebaki kua hai. Una nafasi moja ya kuishi, nieleze unafahamu nini kuhusuย  Nyaraka M21?โ€ alihoji Haji Babi akiwa amekaza macho yake kuelekea alipo Mke wa Rais. Hofu ya Haji Babi ni kua Nyaraka hizo zina siri zake pia kwani viongozi wengi wa ngazi zaย  juu walikua kwenye nyaraka hizo.ย 

    Mke wa Rais alikua kimya huku akilini akijiuliza ni jambo gani lililomfika Rais, akiwa katikaย  tafakari akanyanyuliwa na kupelekwa kwenye chumba kingine ambacho kilikua na jokofu laย  kuhifadhia Maiti, humo ndimo mwili wa Rais Lucas ulikuwa umehifadhiwa.ย 

    Mke wa Rais akawa anatetemeka, ujanja wote akautia mfukono, waziri Mkuu Haji Babiย  alionesha wazi kua alikua siyo Mtu mzuri, japo Mke wa Rais alihitaji Rais atoke madarakaniย  lakini hakutegemea kama angetolewa kwa njia hiyo ya Uwasi, jokofu lilipofunuliwa akaambiwaย 

    โ€œNenda kaangalie kuna nini ndani yakeโ€ alisema Waziri Mkuu, kisha akatoa tabasamu panaย  huku akisigina kiatu chake sakafuni, Mke wa Rais akasogea hadi kwenye jokofu, aliiyonaย  maiti ya Rais. Mwili huo ulikua na matundu ya Risasi, alijikuta akiishiwa nguvu, Waziriย  mkuu akamdakaย 

    โ€œSasa unapaswa kua upande wangu Mke wa Rais, nitayafungulia Maisha yako yaliyokuaย  yamefungwa na Lucas, nyota yako itawaka tena kwenye Siasaโ€ akasema Waziri Mkuu hukuย  akiwa anamwonesha tabasamu pana sana, alionekana kujua siri nyingi za Maisha yaย  Marehemu Rais Mbelwa na Mke wake.

    Akaagiza Mke wa Rais awekwe kwenye chumba kingine kwa uangalizi mkubwa, akawekwaย  kwenye chumba kizuri ambacho alipewa kila kitu isipokua simu, Mpango wa Waziri Mkuuย  ukawa ni kutaka kuitawala Nchi, aliporudi ndani ya Ofisi ya Rais akampigia Simu Muuwajiย  wake wa kuaminika, akamtaka awasili hapo Ikulu jioni hiyo ili ampe kazi ya kusafisha woteย  anaowahisi watakua kikwazo kwenye Utawala wake.ย 

    **ย 

    Hatma!!ย 

    Baada ya kutoka Black Site akiwa amechoka sana Bi. Sandra alikua akiegesha gari lakeย  kwenye jumba moja la ghorofa ambamo ndimo alimokua akiishi, Ulikua usiku umeshaingia,ย  nywele zake alizozifunga kwa nyuma zilikua zikimfuata kila aendako.ย 

    Palikua kimya sana, kichwani alikua na mawazo tele, kwanza alihitaji hizo nyaraka za siriย  ambazo Elizabeth alikua nazo na pia alifikiria sana kuhusu Mauwaji aliyoyafanya kwa Raisย  Lucas Mbelwa. Kwa kiasi kikubwa alianza kujiona mwenye hatiaย 

    Akalisogeza gari hadi maegesho, alipomaliza alishuka ili aelekee juu ambako alikua akiishi,ย  eneo la maegesho lilikua na magari mengi, pia palikua na giza la wastani lakini ambaloย  haliwezi kuyashinda macho yake, akapiga hatua kadhaa lakini akahisi uwepo wa Mtu nyumaย  yake, akasimama kisha haraka akageuka lakini hapakua na Mtu yeyote yule.ย 

    Akashusha pumzi nzito ya wasiwasi, palikua kimya kuliko kawaida. Alipogeuka mbeleย  alimwona Mtu mmoja aliyevalia suruali ya Jinzi ya Bluu, shati jeupe alilolichomekea vizuri.ย  Akapata ahueni, akatabasamu kisha akaendelea mbele.ย 

    Yule Mtu alikua Mwanaume aliyeenda hewani, mweusi mwenye mwili uliojengeka vizuri,ย  alipokaribiana na Bi. Sandra alianza kutafuta kitu mfukoni mwake lakini kwa Bahati mbayaย  aliangusha Karatasi alizokua amezibeba, akainama kuokota, Bi Sandra akajikuta tuย  akimsaidia kuziokota maana zilikua zimetawanyika sana.ย 

    Namna ambayo Bi. Sandra alikua akiishi ni ngumu sana kugundua alikua Muuwaji waย  kuaminika.ย 

    โ€œOoh Ahsante sanaโ€ alisema Mwanaume huyo baada ya Bi Sandra kumpatia karatasiย  alizokua ameziokota.ย 

    โ€œSiku nyingine uwe makiniโ€ akasema Bi. Sandra akiwa anampa tabasamu Mwanaume huyoย  aliyemzidi umri parefu sana. Alipotaka kuachana naye Mwanaume yule akamwambia Bi.ย  Sandraย 

    โ€œSamahani Naitwa Skandaโ€ alisema huku akitabasamu kama Mtu aliyehitaji ukaribu na Bi.ย  Sandra, hakujua Mtu aliyekua akizungumza naye alikua Mtu wa namna gani, haraka Bi.ย  Sandra akajua Mwanaume huyo alihitaji ukaribu, alizungumza akiwa amempatia mkono Bi.ย  Sandra.ย 

    Bila Hiyana Bi. Sandra alirudisha tabasamu pamoja na Mkono, akampa Mwanaume huyo.ย  Sekunde moja tu ikabadilisha kila kitu, yule Mwanaume akaubana mkono wa Bi. Sandra kwaย  nguvu huku akitabasamu,kwa kutumia ujuzi wake Bi. Sandra akajitoa

    Alipojiangalia aliona ana tundu dogo linalotoa damu, kisha ghafla nguvu zilianza kumwisha,ย  akachomoa Bastola yake ili amshambulie Mwanaume huyo aliyekua amesimama mbele yake,ย  cha ajabu Mwanaume yule hata hakujitingisha, pale pale Bi. Sandra alianguka na kuanzaย  kutapa tapa, yule Mwanaume akaangalia huku na kule kisha akauvuta mwili wa Bi. Sandra naย  kuuingiza chini ya gari yake, halafu akajikungโ€™uka vumbiย 

    Akaitoa simu kutoka mfukoni kisha akapiga mahali.ย 

    โ€œNani anafuata?โ€ akauliza Mwanaume huyo, Naaam!! Mpango wa Waziri Mkuu Haji Babiย  ulianza kufanya kazi, tayari Muuwaji alikua kazini kufyeka wote anaowahofia kwenyeย  Utawala wake. Maisha ya Bi. Sandra yakaondoka kizembe.ย 

    **ย 

    Waziri Mkuu Haji Babi, akaketi kwenye kiti cha Rais akiwa anagida mvinyo, muziki waย  taratibu ukiwa unamburudisha huku Muuwaji wake akizidi kufanya Mauwaji Usiku huo,ย  hakuishia kwa Bi. Sandra, akammaliza Balozi akiwa ndani ya gari kwa kutumia kitambaaย  chenye Sumu.ย 

    Mauwaji haya yalifanyika kwa siri nzito na uharaka wa ajabu sana, kipaumbele sasa kikawaย  ni kupata Nyaraka za siri zilizopewa jina la M21, akamtuma Muuwaji wake wa kuaminikaย  kwenda Ilipo Black Site kumchukua Elizabeth Mlacha. Akampa ramani ya mahali ilipo Blackย  Site, akaondoka Usiku huo huo na gari ndogo aina ya Carrina C4 kuelekea Black Site.ย 

    Kitu pekee kilichobakia kwa Waziri Mkuu ni kupata nyaraka ili kifo cha Rais kitangazwe,ย  Upande wa pili ndani ya Godauniย 

    Muhonzi akafanikiwa kukata kamba alivyofungwa, giza lilikua nene ndani ya Chumbaย  alichohifadhiwa, akajaribu kuchungulia dirishani kwa mtindo wa kuruka sababu dirishaย  lilikua juu sana lakini hakuambulia kuona chochote kile, akajaribu kuitaย 

    โ€œKuna nani hapo nahitaji Majiโ€ aliita kwa makusudi huku akifahamu fika kua eneo hilo linaย  ulinzi mkali kuhakikisha yeye hachomoki, akaita tena, ndipo aliposikia hatua za kiatu zikijaย  upande wake, akarudi haraka kuketi sakafuni alipokua ameketi.ย 

    Mara taa ikiwashwa, kisha akatupiwa maji aliyoyataka.

    Nini kitaendelea?ย 

    Usikose SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA

    Mpe Nguvu ADMIN Kwa ajili ya bando Kwa kumtumia Chochote aendelee kupost MSALA Hapa Kijiweni

    Lipa Namba: 57900454
    Jina: LIPA KIJIWENI TIPS
    Mtandao: VODACOMย ย 

    SOMA RIWAYA YA KOTI JEUSI KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA FUNGATE KWA KUBONYEZA HAPAย 

    SOMA RIWAYA YA NILIPANGA NYUMBA MOJA NA MAJINIย 

    SOMA RIWAYA YA GORYANAH HAPAย 

    SOMA KISASI CHANGU HAPAย ย 

    JIUNGE NIPO KIJIWENI Kwa Kubonyeza Hapa

    MSALA xx MSALAxx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA xx MSALA

    Msala Msala Kijiweni Riwaya Ya Msala

    9 Comments

    1. Ahyen tony on September 6, 2024 6:41 pm

      wakwanza kuisoma

      Reply
      • Kb on September 6, 2024 7:39 pm

        Ni mimi

        Reply
    2. Migo on September 6, 2024 6:42 pm

      ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

      Reply
    3. Yudah on September 6, 2024 7:10 pm

      ๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹๐Ÿ˜‹

      Reply
    4. Bplm1664 on September 6, 2024 9:45 pm

      Msalaa ๐Ÿ๐Ÿ

      Reply
    5. Calvin paul on September 6, 2024 9:49 pm

      Weeeee weee hatar na nusu

      Reply
    6. Clever David on September 6, 2024 11:33 pm

      Jaman masala ni moto wa quotes mbali admin umeweza

      Reply
    7. Twaha Gora on September 16, 2024 7:08 pm

      Nzuri

      Reply
    8. โ˜Ž + 1.620889 BTC.NEXT - https://graph.org/Payout-from-Blockchaincom-06-26?hs=bd255d4af6f713a84a2bdebafaba8e5d& โ˜Ž on June 28, 2025 8:26 pm

      6o07k5

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    Social Media Image
    Top Posts
    UEFA EURO 2024 Trophy

    Yote Unayopaswa Kufahamu Kuhusu UEFA EURO 2024 German

    May 30, 202425K Views
    Ligi Kuu

    Hii Vita Ya GAMONDI Na FADLU Inaichangamsha Vipi Ligi Kuu?

    October 3, 202417K Views

    Chama, Aziz Ki Na Pacome Watachezaje Yanga?

    June 27, 202414K Views

    Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBCPL) 2024/2025

    August 9, 202413K Views
    Don't Miss
    Hadithi September 15, 2025

    In the name of LOVE – 05

    Ilipoishia sehemu ya tatu ya In the name of LOVE โ€œBasi hakuna shida Zaylisa, mnaweza…

    In the name of LOVE – 04

    In the name of LOVE – 03

    In the name of LOVE – 02

    Stay In Touch
    • Facebook
    • X
    • Pinterest
    • Instagram
    • YouTube
    • Vimeo

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from Kijiweni.

    © 2025 Kijiweni. A Product of Jamii Media.
    • Home
    • Wasiliana Nasi

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.